Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*
Gonga94 · Stories

*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.

*______________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*

Utaniita shemeji ☺️aisee hii simulizi sijui nikae mkao gani ili niilete kwa usahihi bila kukwama wala kupunguza radha😊.

Ila hii kitu imenionesha kuwa kweli watoto wa elfu mbili wameshindikana yaani hawataki msiala na mioyo yao kabisa , we ukimwaga ugari wao watamwaga mboga 😃.
Na ukijifanya chizi wao wanakuonesha kuwa wao ni machizi pro 😃kiufupi hiki kizazi hakina mda wakupoteza kucheka na kima wao ni shwaaa twende mbele😀.

Haya acha nimlete mrembo wetu ambae amapendezwa kuleta kisa chake ili tupate kujifunza kupitia mapito yake , sasa kwa tetesi na akili za hawa watoto wa elfu 2000 tutapata cha kujifunza kweli ?

Au ndo tutaishia kusonya tu😊, haya tuanze na story yetu , binti mrembo huyu anasema " kwa majina naitwa Wardah Abdallah, leo bwana nimekuja kushare story yangu story ambayo inakwenda kugusa sehemu nyingi sana za maisha ya vijana hasa kwenye engo ya mahusiano.

Kabla sijaanza story yangu naomba niulize hivi kuna shetani gani alie mkali kumpita mwanamke alie umizwa na kuamua kulipiza kisasi? .

Kama yupo niambiwe maana mwanamke anapo amua kulipa kisasi baada ya kufanyiwa ukatili ama usaliti huwa ni moto wa kuotea mbali ,au je kuna mtu anaeweza kusimamisha kisasi hicho ?.

Niseme tu hakuna ila siku zote mwanamke anapoa amua kulipa kisasi basi jua shetani mwenyewe hukaa pembeni na kujifunza kutoka kwake ☺️.

basi bwana story yangu inaanzia siku ya alhamis siku hii nilikuwa njiani nikisafiri kutoka Bukoba kuelekea dar es salaam.

Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kutoka nje ya mkoa wangu ,na nakumbuka kwa miaka mingi nilikuwa kutamani sana kufika katika jiji la dar es salaam .

Lakini leo hii nalielekea jiji nikiwa na moyo ulijawa na huzuni kuu😔 , na hii ni kwasababu ninaenda kinyume cha matakwa yangu 😔.

Yes haikuwa mpango wangu kufika katika jiji hilo nikiwa hivi nilivyo , mara zote niliota na kutamani kuingia katika jiji hili kama mwanafunzi mpya wa chuo kikukuu cha dar es salaam (udsm)

Lakini ule msemo wa mbuzi wa masikini hazai umenivaa na kuleta maana kwenye maisha yangu 😪 ,ndoto yangu imekufa huku njia nzangu zikijaa miiba na kiza kinene kiasi cha kufanya nisione mbele😔😔 ..

Wardah nilietamani kuwa msomi mkubwa na mfano wa kuigwa kwenye jamii yangu leo naenda kuishi kwenye nyumba ya mtu nikiwa kama kijakazi 😪aah hii sio sawa.

Haya sio maisha niliyotamani kuishi 😪 kuishi kama kijakazi eti house maid no hii sio sawa kabisa , lakini sasa nitafanya nini wakati dunia imeamua kunibadilishia hatma??😪.

Yes sina chaguo lingine zaidi ya kukubali hili huenda Mungu anamakusudi yake , lakini kama aishivyo Mungu wallah nitapambana hadi hatua ya mwisho ilimradi tu niishi ndoto zangu.

Gari (bus) lilianza safari macho yangu yakawa bize kutazama nje, moyo wangu uliuma mno kuona nikiiacha Ardhi ya nyumbani kinyume cha matakwa yangu😔.

Jamani sijalazimishwa na mtu kwenda kufanya kazi za ndani,ila ugumu wa maisha ya familia yangu umenilazimu kufanya hivi.

Na maamuzi haya nimeyatoa roho ikiwa inauma mnoo huku nikiamini kuwa nitakwenda kubadili maisha ya familia yangu japo kwa asilimia chache.😔😔

Basi safari iliendelea njia nzima nilikuwa kimya sikuongea wala kushuka sehemu ambazo tuliambiwa tukapate chakula , maana sikuwa na hela yoyote mkononi.

Na sio kwamba mwenyeji wangu alinitumia nauli bila pesa ya kutumia njiani no alituma ila sikuona faida ya mimi kula njiani ile hali nyumbani hawana hata senti ya zamani.

So nilikubali kusafiri kutoka Bukoba to dar pasipo kula kitu ili wao wale , hata hivyo kushinda au kulala bila kula si kitu kigeni kwangu so hili ni jambo dogo sana kwangu.

Basi masaa yalienda usiku ukaingia nikaja kuingia dar kesho yake asubuhi maana kipindi hicho magari yalikuwa hayajaanza safari za usiku .

Hivyo asubuhi tulifika nikamfuata konda na kuomba amtafute mwenyeji wangu (maana waliongea kabla ya safari na kukubaliana kuwa tukifika awape taarifa )

Hakuwa na neno akapiga na kuwajulisha kweli baada ya mda aliekuwa mwenyeji wangu akafika , macho yangu yalitua kwenye mapaja maupe yaliyokuwa wazi.

Nakushangaa kwanini amevaa nguo fupi iliyomuacha wazi kiasi kile 😶, kwa uchangamfu alinisalimia mwenyewe nikaitikia na kumpa shikamoo akagoma kuipokea.

Madai bado mdogo na nikweli kwa muonekano alikuwa binti ndio lakini hakuwa na udogo wakushindwa kupokea salamu yangu labda tuseme watu wa dar hawapendi shikamoo🥲.

Basi bwana baada ya salamu alinambia nibebe nguo zangu ambazo zilikuwa kwenye shangazi kaja lililochoka nikabeba tukaongozana hadi kwenye gari , kufika akafungua mlango upande wa dereva akaingia na kukaa.

Nilibaki nimesimama maana sikujua hata huo mlango unafunguliwaje , nae kuniona nimesimama alishusha kioo na kuniuliza " we vipi mbona umesimama kama sanamu ingia tondoke "

Kwa unyenyekevu wa hali ya juu nikamwambia " samahani sijui kufungua mlango "

Akashangaa nakusema "Khaaa😮! hujui kufungua mlango dada mkubwa hivyo !!!jamani kweli ushamba mzigo " aliongea akashuka na kuja kunifungulia .

Sasa baada ya kufungua mlango nikataka niweke shangazi kaja langu ila kabla sijafanya hivyo alinizuia na kusema .

"Weka huko nyuma usije kunichafulia gari langu " nilijibu sawa na kusogea akafungua buti nikaweka shangazi kaja lile na kupanda nyuma kama alivyo nitaka kisha safari ya kuelekea kunako makazi yao

SEHEMU YA 02

SONGA NAYO...............

Safari ilichukua mda wa saa moja tukawa tayari nje ya jengo ambalo kwa wakati huo niliona kama kasri la kiarabu, honi ilipigwa haikuchukua mda geti likafunguliwa .

Bila kuchelewa akaingiza gari ndani akaenda yalipo maegesho akasimama na kunambia nishuke ,mie bila kuongea neno nikashuka na yeye akashuka .

Sasa baada ya kushuka mlinzi alikuja akitaka kunipokea kwa sauti ya ukali bidada yule akamwambia "eeeee wewe umeambiwa au kutumwa mbona unakuwa na kiherehere namna hiyo?.

Lione janaume zima kujifyatua akili tu embu toa tumbo lako hapa,, lione kama zombi😒 "

Masikini kaka wawatu alinywea na kurudi nyuma huku akikuna kichwa , tukaingia ndani kufika nikakuta mwanamama akiwa amekaa sebleni huku akioshwa miguu na kijana mmoja hivi.

Basi Dada aliekuja kunipokea akamwambia " haya mama mtu wako huyu hapa nadhani sina deni na wewe tena "

Aliongea na kutaka kuondoka ila akasimama baada ya mama yake kusema " wewe huyu mtu ndo tumeletewa kama mfanyakazi mbona mweusi hivi ?"

Binti akamjibu " eee we nae mama ushaanza,, sasa unataka mweupe uliona wapi Bukoba akatoka mtu mweupe 😒" aliongea huku akiniangalia kwa kuninyali.

Mama mtu akajibu " Aah hata kama bwana sasa huyu siatafanya wanangu wakose amani maana wakimuangalia watahisi wamekaa na msukule maana sio kwa weusi huo.

Na vipi kuhusu hilo juba maana ndo limekufanya uonekana kama umetoka kufunzwa uchawi embu sogea hapa nikuone vizuri huenda ukawa bora zaidi ya nikuonavyo."

Aliongea na kunielekeza nisogee nami bila kuongea nikasogea hapo macho yanaangalia chini , moyoni nilikuwa namwambia Mungu nisaidie nisianze kulia .

Maana sikufurahishwa na maneno yao hata kidogo, ndio me mweusi na najua kabisa me mweusi ila ndo nini kunisema kwa dharau hivyo .

Tena ndo nimefika yaani hata neno karibu hakuna 😥,kweli kuna watu naviatu na viatu wenyewe ndo hawa na sijui nitaishije maana dakika za mwanzoni tayari nishaonjeshwa joto la meno.

Basi mtoto wa mzee Abdallah mie nikasogea alipo akanambia "eee wewe sijakwambia uje mbele yangu embu rudi nyuma😡, khaa jamani yaani unanuka kwani una mwezi mzima hujaoga binti au ulikuwa mtengeneza ugolo?🤧

Haya chuchumaa hapo maana naogopa hata kukwambia ukae kwenye makochi yangu usije tia kunguni bure."

Nilirudi nyuma na kuchuchumaa kama alivyo sema kisha akaniuliza" mh unaitwa nani na una miaka mingapi?? "

Kwa sauti ya upole nikamjibu " naitwa Wardah Abdallah nina miaka 18"

"Oh afadhali sheria haitanihukumu ,mh unajua kilichokuleta huku?"

"Ndio "

"Vizuri ,sasa kabla ya yote kitu ambacho sikitaki kukiona hata siku moja ni kukuona ukivaa hayo masantula yako sijui ndo mnaita majuba .

Yaani usije kujaribu kuvaa iwe ndani wala nje sawa!?"

Neno hataki kuona nimevaa Juba lilinishangaza nikamuangalia kama vile sijamuelewa na kumuuliza " samahani una maanisha nikae kichwa wazi??"

Akasema "ndio na sio kuvaa Juba tu kiufupi mavazi yako sijaelewa kwa hiyo utavaa vile nitakavyo mimi " aliongea na kumuita mlinzi akaja na kumwambia.

"Embu chukua hilo fuko lake ukachome vitu vyote huko nje ,maana linatishia amani na kwakuliangalia tu halikosi kuwa kunguni,, sasa kabla hawajaanza kutoka litiwe moto haraka ""

Aliongea haraka nikainuka na kulishikilia shangazi kaja langu nikataka kuomba wasichome nguo zangu ila kabla sijaongea aliniwahi na kunambia .

"We mtoto wewe tulia kama unanyolewa chini ,hapa kwangu kauli yangu ni sheria isiyo pingwa na yeyote unanielewa?.

Embua achia gunia lako hilo ,na wewe ole wako nije nikute hata nyuzi iliyobakia unguza vyoote "

Aliongea kwa ukali sana nikajikuta naachia taratibu, mlinzi akachukua na kwenda nazo nje , nilishindwa kujizuia machozi yakanitoka mama yule kuona hivyo akacheka cheko la kishangingi na kusema.

"Ona hili bwege!! Wewe yaani unatoa chozi kisa mitambala iliyojaa chawa ? Embu acha ujinga binti hizo nguo zimechomwa kwasababu hazina hadhi sawa na nyumba yangu.

Na kwa maana hiyo unapewa nguo zenye hadhi sawa na nyumba yangu sawa ,? Eeh futa michozi yako hiyo usije kuniletea nuksi buree "

Bila kuongea nilifuta machozi akamuita mmama ambae alikuwa jikoni akiandaa chakula na kumwambia anipeleke chumbani .

Na akinifikisha huko ahakikishe navua nguo nilizo vaa ili nazenyewe zikachomwe ,mama yule alifanya kama alivyo ambiwa tulifika chumbani akanambia vua .

Nami bila kubisha nikavua akanipa kanga nikajifunga kisha akaondoka nikabaki nimesimama nisielewe nifanye nini maana sikupewa hata maelezo wala kuoneshwa bafu .

Nilisimama huku macho yangu yakizunguka kuangalia mazingira ya chumba kile ,taratibu nikasogea dirishani na kushuhudia nguo zangu zikichomwa moto😥.

Ukweli nilijiskia vibaya sana , nguo zangu nilizikapata kwa tabu leo kirahisi wanazichoma moto bila kujua nilipambana kiasi gani ili kuzipata .😔😔

Machozi yalinitoka nikawa nakazi ya kufuta na kurudisha mafua ndani huku macho yakiangalia namna zinavyo teketea, mara mlango ukafunguliwa haraka nikajiweka sawa na kugeuka.

Nikashtuka kuona mwanaume ambae kwa haraka haraka umri wake ulikuwa ni kati ya 20 __25 ,kaka yule aliniangalia kwa macho yaliyojaa uchu huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.

Alisimama na kukuna kidevu huku akitoa ulimi nje kama paka alieona maziwa 😥😥.

Toka nimezaliwa sikuwahi kusimama mbele ya mwanaume nikiwa nimefunga kanga tu ,hivyo kitendo cha kumuona kaka yule mbele yangu nilishtuka na kukimbilia kwenye pazia nikajifunika ili kuustili mwili wangu.

Ajabu kaka yule alizidi kutabasamu na kunifuata kwa mwendo mdogo mdogo, nilitoa macho huku mapigo ya moyo yakianza kwenda kwa kasi sana .


(Ndo nabakwa au 😥)

SEHEMU YA 03

SONGA NAYO...............

Aliendelea kupiga hatua hadi akafika nilipo taratibu akanyoosha mkono na kutaka kushika pazia nililotumia kujifunika 😥😥, nilitetemeka kwa hofu sana nikataka kumwambia asinifanyie ubaya.😥

Lakin kabla sijafungua kinywa changu kuongea mlango ulifunguliwa na kumfanya ageuke kwa mshtuko.

Mama alietumwa kunileta chumban ndie alikuwa amefungua mlango, akashangaa kumuona kijana yule mle ndani na kumuuliza" we Alvin unafanya nini humu chumbani??"

Kijana huyo ambae anafahamika kama Alvin baada ya kuulizwa hivyo alitabasamu na kumjibu " aaa shangazi nae , me nimekuja kumuangalia mgeni "

Mama yule alikunja uso kwa hasira na kumuuliza " unakuja kumuangalia chumbani kwanini usinge msubiri sebleni ??"

"Ushaanza mambo yako, sikia haina noma naondoka ,sema nini mmeleta mdada mrembo sa sijui mmepango kunifanya nikae nyumbani!?"

"Wewe ondoka bwana na hii tabia ife leo"

'"Sawa " aliondoka,, mama yule akanipatia nguo aliyokuja nayo na kunionesha bafu lilipo nikaoga kisha nikavaa na kwenda sebleni kwaajili ya kupata chakula.

Nilikula na baada ya hapo nikashukuru kwa chakula kisha nikaelekezwa majukumu yangu na bila kupoteza mda nikaanza kazi.

Mda ulienda ilipofika jioni boss wangu pamoja na yule dada aliekuja kunipokea wakatoka , aina ya mavazi waliyovaa iliniacha mdomo wazi.

Maana sio kwa nguo zile na hawakuwa na wasi wasi hata kidogo ndo kwaanza walikuwa bize kusifiana kuwa wamependeza.

Basi niliendelea na majukumu yangu huku masaa yakisogea taratibu, usiku ukaingia tukapata chakula kisha yule mama alienionesha chumba mda ule ambae anaitwa madam Vero .

Nae alijiandaa na kuvaa nguo fupi kuliko hata walizovaa boss wangu na binti yake, kisha akaondoka na kuniacha na watoto .

Kwakua nilikuwa nimechoka sana na safari nikapanda kitandani na kulala , sikujua walirudi sangap ila nilikuja kuamka asubuhi na kukuta wote wakiwa sebleni.

Pembeni yao kulikuwa na chupa za pombe ambazo hazikuwa na kitu ndani yake , niliangalia namna walivyo lala kihasara hasara nikawapita na kuingia jikoni .

Nikawaandalia watoto chai wakanywa na walipo maliza nikawaandaa wakaenda shule ,mimi nikabaki nafanya usafi wa ndani.

Mda ulienda ilipofika saa tano waliolala sebleni ndo wakaamka na kunywa chai kisha wakaoga na kuanza kupiga story.

Story walizokuwa wakipiga zilinifanya nikabaki nawaangilia huku kichwa kikijaa maswali mengi juu yao , kwanza zilikuwa story za aibu kuongea mbele za watu.

Lakini wao walikuwa wakuongea bila hata aibu, niliendelea kufanya kazi zangu huku masikio yote yakiwa kwao kusikia yale wanayoongea.

Mda ulienda nikapika chakula cha mchana na kuweka mezani , kwakua nilishaambiwa siruhusiwi kula au kukaa meza moja nawao nilijikokota hadi jikoni .

Nikapakua chakula changu na kukaa chini nikaanza kula , mara nikaitwa na boss haraka nikainuka na kwenda ,,kufika akanambia nimletee glass ya maji.


Nami bila kuchelewa nikageuka ili niende nikachukue hiyo glass alohitaji ajabu akanisimamisha kwa mshangao sana akasema " Da Vero hili ndo lile gauni ambalo halikukutosha ama??"

Aunt Vero kuulizwa hivyo aliinua uso na kuniangalia kisha akajibu " ndio kulikoni kwani kuna shida?"

"No hakuna ila nashangaa limemkaa vizuri, alafu kumbe Mungu alikuumba vizuri kabisa cheki huo mlima nyuma !" Aliongea huku akinisogeza na kunigeuza nyuma .

Aunt Vero pamoja na Shuu (binti wa boss) walijiangalia kwa pamoja wakacheka kisha Shuu akasema " mmmh ni kweli shundu analo ila kunafaida gani ya kuwa nakitu ambacho hujui matumizi yake.

Sanasana anaonekana kabeba uchafu tu😏 "

Alivyosema hivyo boss akajibu " aaah hapa hatuongelei matumizi ila uumbaji "

Aunt Vero akasema " ni kweli bhna bidada amabarikiwa haswa na huyu siku akijua kuoga walai Shuu utakuwa nyuma yake mita mia"

Shuu kuambiwa hivyo alisonya na kusema " nyooo huyu mshamba ndo anizidi mimi ? We kweli huna macho ,embu niangalie vizuri,, mtoto nimeumbwa siku ya mapuziko .

Sina doa wala kipengele chochote yaani kila mahali niko fresh 😇"

Aunt Vero akicheka na kusema " awaapi yaani pamoja na kwamba una rangi moja mwili mzima bado haikupi max za kumpita Warda, we muangalie vizuri. "

Aliongea na kuinuka akaja nilipo akawa anaongea kwa kumuonesha vitendo" Shuu ona hili shundu halina mabonde bonde hata kidogo, ona kiuno kilivyo jitenga , unaona hapa kama hana tumbo vile


Achana na tumbo sasa unaona chuchu kitu ni saa tano na nusu , haya angalia unywele yaani hapa hajui cha steaming wala leaving conditioner ila unaona mkia ulipo?.

Achana na hayo ona ngozi inavyo tereza nikukumbushe hapa mafuta hayajui sasa nambie akisema leo atengenezwe na kujaliwa utamfikia?

Au unataka kusema weusi wake utamfanya ayaage mashindano ? Na kabla ya kujibu nikwambia tu hii rangi yake ndio maana hali ya neno black is beauty.

Aka rangi adimu maana zingine zoote unaweza nunua dukani ila hii hakuna sehemu yoyote utayaenda ukauziwa ,hii ni pure nature iliyotoka moja kwa moja kwa sir God.

Sasa endelea kujiona mzuri ila jua hapa hufui dafu sawa bidada "

Maneno ya Aunt Vero yalimkera sana Shuu akapiga ngumu kwenye meza kwa hasira na kusema " kwa hiyo mmeleta mtu ilimnishindanishe nae au ??"

Aunt Vero alicheka na kusema "akuuu hakuna anaetaka kukushindanisha ila unaambiwa ukweli huyu humfikiii hata robo dada "

Kwa hasira Shuu alisonya na kusema " huna lolote unampaisha kwasababu anatoka kwenu ila hana chakunishinda mshamba tu huyo"

"Ushamba nakubali ndio anao ila kwa uzuri dada humfikii😆na ninakwambiaga Bukoba haijwahi kutoa pisi mbovu, yaani siku zote utakuta binti anakitu special kama sio sura basi shundu.

Na kama Sio shundu basi rangi ama guu sasa huyu Mungu aliweka umakini wake woote yaani bila presha akatoa kitu hicho aaah napenda mambo kama haya bwana 😋😆"

Shuu alichukia zaidi na kutaka kususa chakula ,mama yake akamtuliza na kunambia " we nae mbona bado umesimama kama jinga embu kalete nilicho kutuma huko"

Bila kuongea nilienda jikoni nikachukua glass na kumpelekea kisha nikarudi kukaa jikoni nikala chakula changu pale hadi nikamaliza.

Na kwakua walikuwa bado wanakula nikaamua kuosha vyombo nilivyotumia huku nikisubiri wamalize , uzuri haikuchukua mda wakamaliza .
Nikatoka na kwenda kutoa vyombo, kufika nakuta boss pamoja na Aunt Vero wameshaondoka akawa amebaki Shuu peke yake , sikuwa na neno nikasogea na kutaka kukusanya sahani.

Mara akanishika mkono kuniuzia , niliuangalia mkono wake na kumuangalia usoni ,alikuwa na hasira sana kiasi cha macho yake kuwa mekundu .

Kichwani nikajiuliza kuna kosa nimefanya au ,,mbona kanishika na ananiangalia kwa hasira hivyo?😥, kabla sijapata hata jibu nikashangaa anauvuta mkono wangu na kuweka kwenye sahani ya miba.

Bila kupepesa macho yake pembeni aliukandamiza mkono wangu kwenye miba ile ambayo ilikaa kama ameiweka ili afanye hivyo😥, nilikunja sura yangu kwa maumivu .

Nikataka kuutoa ila akaweka mkono wake mwingine juu na kukandamiza kwa nguvu na kufanya nichomwe zaidi, kwa maumivu makali niliita "mamaa"😫 mda huo huo akaingia Alvin nakuliona tukio lile .

Aisee alikimbia haraka na kumsukimia mbali Shuu akaanguka chini kwa kishindo ,bila hata kuniangalia usoni akauchomoa mwiba ule kwa nguvu .

Nilihisi maumivu makali nikataka kupiga kelel akaniwahi na kuniwekea mkono mdomoni😥,bila kutegemea aliniangalia usoni kwa uso wa huzuni sana .

Taratibu akautoa mkono wake mdomoni kwangu na kunivutia kifuani mwake 😲,kwa sauti ya upole akanambia "Nisamehe mimi na........."🙊😲!!!


SEHEMU YA 04

SONGA NAYO...................

Sikusubiri amalize alichotaka kusema haraka nikajitoa kwake na kurudi jikoni mbio,😥 hazikupita sekunde 5 nikasikia anamfokea Shuu .

Shuu kwa hasira akamwambia " Alvin hii sio mara ya kwanza na kwambia uwe unafanya yanayo kuhusu we unajua kanifanya nini yule?"

Kwa msisitizo Alvin akasema " sitaki kujua amekufanya nini ila iwe mwanzo na mwisho kumnyanyasa mtoto wawatu ,we kama kakosea mueleze yaishe sio kuumizana .

Alafu nazijua pigo zako vizuri hiyo roho chafu uliyoibeba iko siku nitaichomoa sasa endelea 👉"

"Eti utanifanya nini !??thubutu yako uone 🤧, na kama ni demu wako muonyee mapema asipite kwenye njia zangu maana nitampasua hata aamini "

"Kabla ya kumpasua make sure unanipasua mimi kwanza kenge wewe embu toa fito zako hapa"

Shuu aliondoka huku akimsindikiza kaka yake na sonyo , Alvin alimuangalia Shuu akiondoka hadi apotea machoni mwake .

Taratibu akageuka na kukusanya vyombo vizuuri kisha akaja navyo jikoni , mda huo nilikuwa kwenye pembe nikilia nilivyo muona tu nikafuta machozi haraka na kujifanya nachukua fagio.

Alvin aliniangalia kwa huzuni na kuweka vyombo kwenye sinki ,taratibu akaanza kupiga hatua kunisogelea nikataka kumkwepa akaniwahi na kunishika mkono.

Kwa sauti iliyojaa utulivu akanambia " pole ni changamoto ,ila kuwa makini na kama itatokea shida tafadhali usiiname na kulia tu bali jitetee sawa?"

Nilitikisa kichwa kuashilia ndio na kuutoa mkono wangu kwake ,nikasogea lilipo sinki la vyombo na kuanza kuosha huku nikikwepa macho yangu kumtazama .

Alisimama akiniangalia kwa mda bila kuongea kitu, nikaona anasogea jikoni na kufunua sufuria zilizo kuwa na chakula akapakua na kusogeza kigoda akakaa na kuanza kula.

Wote tulikaa kimya sauti za vyombo na kijiko ndo zikawa zinasikika ,akala chakula chake na alivyo maliza akainuka na kuweka sahani palipo na vyombo vichafu.

Akashukuru na kupiga hatua kadhaa kutoka jikoni ila akasimama ghafla na kusema "samahan kwakuingia chumbani kwako bila kupisha hodi"

Alivyo sema hivyo niliinua uso wangu nikamuangalia na yeye akaniangalia na bila kuongeza neno akaondoka nikabaki nimesimama huku macho yakimuangalia anavyoishia .

Na taratibu nikarudisha umakini kwenye kuosha vyombo , mda ulisogea nikamaliza kazi zangu mdogo mdogo nikaingia chumbani na kufika najitupa kitandani kama mzigo.

Nililala chali macho yangu yakiangalia dali,,
Taratibu nikazama katika dimbwi la mawazo huku kumbu kumbu zangu zikinirudisha miaka mitatu nyuma.

Ambapo nilikuwa kidato cha pili , nilikumbuka namna nilivyo kuwa bize kukesha kujisomea kwa bidii mno huku ndoto zangu ni kuhakikisha nafanya vizuri kwenye masomo yangu.

Ambapo niliamini nitakapo fanya vizuri katika masomo yangu kutaniwezesha kuikomboa familia yangu kutoka katika janga la umasikini kwa asilimia 💯 .

Na Mungu hakuniacha kwani juhudi zangu zilionekana nikawa ni mtu wa kuongoza kwa kila mtihani , kitu ambacho kilikuwa kinanifurahisha sana na kufanya nione naenda kuishi maisha ya ndoto yangu.☺️

Lakini ghafla Mungu aliyageuza maisha yangu na kuniweka kwenye nafasi ngumu mnoo 😥, nafasi ambayo ilininyang'anya ndoto zangu nakunifanya niishi kwa kuugua nafsi kila iitwapo leo.

Unajua nini kilitokea? ,mmmm! Baba yangu ambae ndie alikuwa akipambana kuhakikisha watoto wake tunakula ,kuvaa na mahitaji mengine yote muhimu.

Ghafla tu alianza kuumwa ugonjwa wa ajabu sana ,ugonjwa ambao ulimfanya ashindwe kufanya kitu chochote na kuwa mtu wa kitandani.

Kitu ambacho kilinilazimu niache shule na kuanza kumuuguza pamoja na kuhangaikia mambo mengine muhimu kwetu, utakuwa unauliza itakuwaje nibebe jukumu hilo kwani mama hayupo?

Jibu ni kwamba mama yangu yupo lakini hakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwani alikuwa na matatizo ya afya ya akili ( chizi) japo uchizi wake ulikuwa ni wa mda .

Yaani kuna kipindi anacharuka na kupotea kabisa ,alafu kuna kipindi anakuwa kama ziko sawa ila ukiona anarudi kwenye hali yake ya kawaida basi jua mtakacho fanya kwa wakati huo ni kumuuguza tu.

Maana anaumwa kiasi ambacho ukimuangalia hivi unasema huyu mtu anaondoka kesho kama si leo,na akipona tu akili zinaruka tena.

Na shida hii hakuzaliwa nayo ila ilizuka ghafla tu ,,kwa maneno ya watu wanadai alirogwa na aliekuwa bibi yetu ( yaani mama wa baba yangu) japo sina hakika na hilo .

So kupitia changamoto hiyo ya mama nililazimika kubeba jukumu zima mwenyewe huku ndugu wa baba wakijiweka kando kanakwamba anae umwa si ndugu yao.

Basi maisha ya kumuuguza baba na kuendesha familia yaliendelea ,ikafikia kipindi baba hawezi hata kuinuka akawa ni wakujisaidia hapo hapo kitandani.

Bila kinyaa wala kinyongo nilimsafisha baba yangu na kumpa kila huduma aliyostahili kwa kipindi kile , ilikuwa ni ngumu lakini nilivaa ujasiri.

Sikuwahi kulia au kuonesha huzuni mbele yake, lakini niwapo mbali nae nilikuwa nalia sana ,Mungu anisamehe ilifika mda nikamuomba Mungu amchukue tu.

Maana ilifika hatua akakonda ikabaki ni mifupa mitupu yaani ukimuangalia hivi kama huna roho ngumu utalia ,, lakini Mungu akaona amchukue mama yangu na kumuacha baba .

Mnajua siku mama yangu anakufa alirudi nyumbani na mchicha fungu mbili , akanifuata jikoni ambapo nilikuwa nimejikunja huku nikilia .

Maana siku hiyo sikuwa na hela ya bonga na mda huo wadogo zangu walikuwa wakilia na kuniambia wanasikia njaa , jambo ambalo liliniumiza mnoo.

So kama kawaida yangu nikaingia jikoni na kulia huko , mama alikuja na mchicha akafika ananishika begani huku mkono mmoja akininyoshea ule mchicha.

Niliuangalia na kuinua uso wangu kumuangalia nikakuta ananiangalia huku akitabasamu, neno alilonambi ni kwamba , ""mwanangu nimewalea mboga ili msilale bila kula mkaja kufa na njaa .""

Nilishangaa maana aliongea kama mzima vile , nilitamani kuongea lakini sikuwa na neno la kusema nikaishia kumuangalia huku machozi yakinitoka .

Nae kuona vile akanishika mkono na kunikabidhi ule mchicha kisha akaondoka akicheka cheka na kuruka ruka , nilifuta machozi na kuinuka nikaingia ndani .

Nikawaambia wadogo zangu "msilale namepata mboga napika sasaiv " haraka niliwasha moto na kuanza kupika , mda huo wote mama alikuwa amekaa chini ya mti akiwa bize kuchezesha maguzi kama watoto.

Basi nilipika na nilivyo maliza nikawawekea chakula wadogo zangu ,hicho hicho nikagawa na kumpelekea baba nikaanza kumlisha .

Na alivyo tosheka nikainuka sasa niende kula na mama maana niliona walau siku hii madudu yake yalikuwa yamepoa ,so kula nae nikaona haitakuwa na shida .

Basi nikachukua chakula kidogo kilicho bakia nikatoka nacho nje na kumfuata alipo, kufika nikakuta amelala chini , nikamuita huku nikimtikisa taratibu.

Ajabu hakuitika wala hakuonesha dalili za kuwa uhai ,nilishtuka na kumtikisa kwa nguvu lakini wapi , machozi yalianza kunitoka nikamuangalia huku akili ikinambia kalala tu .😥😥

Taratibu nilisogeza kichwa kifuani mwake na kufanya kama nasikia mapigo ya moyo 😥, aisee nilihisi moyo wangu kama umechanwa chanwa na upanda mkali.

Mama yangu alikuwa tayari kashafariki, wala hayupo tena katika dunia hii 😫😫😥,


SEHEMU YA 05

SONGA NAYO......................

Nilipigwa na butwaa na kubaki nikimuangalia bila kujua nipige ukulele wa kilio au nifanyeje ? , karibu dakika zima ikapita nikiwa namuangalia tu.

Mwisho nikafungua kanga niliyo kuwa nimejifunga nikamuweka vizuri na kumfunika ,kisha nikaingia ndani kimya kimya na kuchukua kanga nyingine.

Nilijifunga nikatoka nje na kwenda kwa jirani bahati nzuri nikamkuta hivyo nikasalimia na kumpa taarifa kuwa mama yangu ameaga dunia.

Taarifa ile niliitoa nikijua itamsikitisha au kumshtua maana kabla ya mama kuwa katika hali ile alikwa rafiki yake sana ,ajabu baada ya kumueleza vile alinambia.

"Weee! Usinambie Mungu kaamua kumpumzisha? Dah kama ni kweli basi Mungu atakuwa amefanya la maana sana maana marehemu aliteseka mno.

Na kitu pekee alichohitaji ni kifo tu ili apumzike ila Mungu alizuia hilo kwa mda mrefu ,lakini kama kweli kaondoka baasi furahi binti yangu."

Nyie nilimuangalia yule mama kwa mshangao sana ,kichwani nikajiuliza maswali mengi sana lakini sikuthubutu kuongea wala kuuliza kitu katika yale yote aliyosema.

Zaidi nilitabasamu na kuondoka , sikuwa na nguvu za kwenda sehemu nyingine nilichofanya nilisogea hadi mama alipolala nikamfunua na kumfunika kawaida.

Kisha nikamuita mdogo wangu na kumwambia " Irene! kaa hapo muangalie mama maana anaweza kuamka akaondoka " mdogo wangu bila kubisha aliitikia sawa na kukaa pembeni yake.

Mimi nikaingia ndani na kuweka mazingira ya chumba vizuri, na kuweka kila kitu sawa na baada ya kumaliza nikarudi nje nikamwambia mdogo wangu tumunyenyue mama .

Ili tumpeleke ndani, akatii tukasaidizana kwa shida hivyo hivyo hadi tukafanikisha kumfikisha chumbani, ambapo baada ya kumlaza tu mdogo wangu akaniuliza.

"Dada mbona mwili wa mama unashuka joto kiasi hiki unajua nimekaa nae pale naona kila dakika zinavyo sogea ndivyo anazidi kupoa au kaanza kuumwa tena?"

Swali lake lilikuwa jepesi tu lakujibiwa kuwa amefariki lakini mdomo wangu ulikuwa mzito kutamka neno hilo mbele yake😔 ,,hivyo nikaishia kumwambia

"naomba wembe nikiokutuma jana dukani"

Akaondoka na kuniletea wembe nikamwambia "unaweza kuendelea mambo yako ila usicheze mbali " Akajibu sawa na kuondoka,,nikafunga mlango na kusogea kitandani alipo lala mama na kukaa.

Nilimuangalia kwa sekunde kadhaa hapo macho makavu wala hata dalili ya machozi haikiwepo , basi nikafungua ule wembe na kuanza kumkata kucha za mkono na miguu.

Nilivyo maliza nikamfumua mabutu yake ambayo yalikuwa yamefumuka fumuka ,,, kisha nikazichana nywele vizuri na kutoka nje ili nikachukue maji ,nikakutakana jirani nilietoka kumpa taarifa.

Alivyo niona tu akauliza "vipi mbona hakuna hata watu au hujatoa taarifa? " sikumjibu nikampita na kuchukua maji kisha nikarudi ndani , sekunde kumi nyingi akasimama katikati ya uwanja na kuanza kupiga ukunguka wa kilio huku akifungua kitenge alicho jifunga.

Sauti yake ya kilio iliita watu na ndani ya mda mfupi watu walijaa ,wakulia nje walilia wakaingia ndani wakaingia na kuomba nifungue mlango.

Bila kuitika wala kuongea na mtu niliendelea kumsafisha mama yangu hadi pale nilipomaliza ndo nikafungua mlango na kwenda chumbani aliko lala baba nikamkuta amelala pale pale nilipo muacha .

Kwa upole na utii nilikaa karibu yake na kumwambia " baba ! mama amefariki " maneno yale yalikuwa mazito kwake akaniuliza " una uhakika na unacho kisema mwanangu? ,, maana hali ya mama yako unaijua anaweza kuwa ameanza kuumwa kama ilivyo kawaida yake.."

Niliuchukua mkono wake na kumwambia " Nina uhakika na hivi ninavyo ongea na wewe tayari nimeshamuosha "

Masikini baba yangu alishindwa kujiuzia na kujikuta akilia kwa uchungu sana , nilimbembeleza na mda huo huo wakaingia wadogo zangu nao wakilia kwa uchungu mno.

Niliwatuliza lakini hakuna aliekubali kutulia ,majirani wakaja na kuwatoa wadogo zangu wote ,wengine wakabaki na baba mimi nikaanza kusadizana na watu kuanza kupanga baadhi ya vitu.

Niseme tu mwanzo wa msiba hadi mwisho wa msiba sikuumwa roho wala kulia hata kwa sekunde moja, yaani nikama niliingiliwa na roho ya ajabu sana.

Akili yangu mda wote ilikuwa kuhakikisha nasimamia kila kitu kiende sawa na mwisho tukamaliza msiba salama, sasa baada ya msiba kuisha na watu wote kurudi makwao.

Kwangu msiba ndo ukaanza aisee moyo ulijaa uchungu wa hali ya juu nikawa ni mtu wakwenda vichakani na kulilia huko,maana niliona kulia mbele ya baba na wadogo zangu kutawafanya wajisikie vibaya zaidi.

Hivyo njia pekee niliyoona sawa nikulia nikiwa mbali nao, siku zikaenda ilivyo pita wiki mbili baada ya kifo cha mama, baba nae akaondoka 💔.

Hiii nilijitahidi siku ya kwanza ila siku ya mazishi sikuwa hata na nguvu ya kusimama , nililia kuliko kawaida lakini pamoja na yote maisha mengine ilipidi yaendelee.

Hivyo msiba uliisha majukumu yangu yakaendelea kama kawaida mwezi wa kwanza ukapita na wapili tuhamia kijiji cha pili ambako ndiko alikuwa akiishi bibi yetu.

Na sababu kubwa ya sisi kuhamia huko ni kwasababu bibi alinipatia mashamba ya kulima na kwakua upande wao mazao yalikuwa yanatoka kuliko haya mashamba ya baba ikabidi twende.

Maana tegemezi kuu lililobaki kwetu ni kilimo , hivyo tukahamia huko na shughuli za shambani zikaanza kama kawaida , miaka mitatu ikakata wadogo zangu wote wawili wakapata ujauzito .

Na mbaya zaidi wanaume walio wapa ujauzito wakaingia mtini kwahiyo nikabaki na jukumu la kuwalea wao na matumbo yao hadi pale nilipopata nafasi ya kuja huku kufanya kazi .

Hivyo huko kijiji wamebaki na bibi ambae kwasasa Kawa kipofu 😔..

Basi baada ya kukumbuka mambo yote hayo nilifuta machozi na kujifunika shuka kisha nikalala.


Usiku ukapita kesho yake nikaamka mapema na kuanza majukumu yangu kama kawaida , na ilivyo fika mda wa kuandaa vitafunwa nikaacha nilichokuwa nafanya nikaingia jikoni na kuanza kuandaa.

Mara akaja Alvin na kufika ananifumba macho kwa nyuma , nilishtuka na kutoa mikono yake haraka nikataka kuongea akaniwahi na kusema.

"Samahani ni michezo tu maana naona kama umechukia ,ila naomba nikuombe kitu kama hutojali"

Sikutaka kuongea kitu nikageuka na kuendelea kufanya kazi yangu ,akaniomba tena "Wardah tafadhali naomba uwe rafiki yangu"

Nilisitisha nilichokuwa nafanya na kumuuliza " unahisi hicho ndicho kilicho nileta hapa?"

Akajibu "hapana ila bila hiki huwezi kuishi kama kwa amani na unaelewa hili,, kwa hiyo acha usumbufu na uwe rafiki yangu "

Nilimuangalia na kutabasamu kisha nikamwambia " mitego yako ni miepesi sana ,hembu kapange mbinu zingine na naomba sana usiniletee uzito katika kazi yangu sawa"

Bila papara alisogea ilipo friji akafungua na kuchukua mayai akasogea nilipo na kushika mkono wangu akaniwekea yale mayai huku akiniangalia usoni na kusema.

"Hii nyumba sio salama kama unavyoona wewe wala watu walio kuzunguka si wazuri kama ufikiliavyo , hapa salama yako ni mimi tu so huna jinsi zaidi ya kuwa karibu na mimi ili uwe salama.

Na kama huamini subiri utaona " aliongea na kuondoka huku akicheka cheko la dharau sana .🤔

ITAENDELEA
Tangazo - Distro kid Upload your music To day
Distro kid Upload your music To day
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*


*______________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*

Utaniita shemeji ☺️aisee hii simulizi sijui nikae mkao gani ili niilete kwa usahihi bila kukwama wala kupunguza radha😊.

Ila hii kitu imenionesha kuwa kweli watoto wa elfu mbili wameshindikana yaani hawataki msiala na mioyo yao kabisa , we ukimwaga ugari wao watamwaga mboga 😃.
Na ukijifanya chizi wao wanakuonesha kuwa wao ni machizi pro 😃kiufupi hiki kizazi hakina mda wakupoteza kucheka na kima wao ni shwaaa twende mbele😀.

Haya acha nimlete mrembo wetu ambae amapendezwa kuleta kisa chake ili tupate kujifunza kupitia mapito yake , sasa kwa tetesi na akili za hawa watoto wa elfu 2000 tutapata cha kujifunza...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/utaniita-shemeji-1-5

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi utaniita-shemeji
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

MY WANGU❤️ sehemu ya 88

MY WANGU❤️ sehemu ya 88

625
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 57...58💘💘

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 57...58💘💘

512
MY WANGU❤️ sehemu ya 89 na 90

MY WANGU❤️ sehemu ya 89 na 90

433
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 39 na 40

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 39 na 40

330
REAL LOVE  Chapter 13

REAL LOVE Chapter 13

150
*MY WANGU❤️* *FINAL SEASON* *91-92*

*MY WANGU❤️* *FINAL SEASON* *91-92*

66
*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*

*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*

18
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06

UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06

16
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07

UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07

12
MY WANGU❤️ sehemu ya 93

MY WANGU❤️ sehemu ya 93

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.13K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

6.88K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.68K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.06K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.47K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tatu.  👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tatu. 👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

2.41K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.3K
I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

2.3K
❤❤ MTOTO WA MKE WANGU😛😛  Sehemu ya tisa.  Sasa jamaa akaupitisha ulimi kwenye mdomo wa  hawa na hawa kaachama

❤❤ MTOTO WA MKE WANGU😛😛 Sehemu ya tisa. Sasa jamaa akaupitisha ulimi kwenye mdomo wa hawa na hawa kaachama

2.25K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya nane.  👉 Mimi Nalia ndio tayari bikra imetolewa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya nane. 👉 Mimi Nalia ndio tayari bikra imetolewa...👇

2.16K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

****

  • MY WANGU❤️ sehemu ya 93 15-02-2026 08:00

****

  • MY WANGU❤️ sehemu ya 94 na 95 15-02-2026 17:40
Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07 Post Mpya
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 07
@majario LIVE

SONGA NAYO................. Taratibu nilifuta machozi na kuinuka nikatoa vyombo na kuendelea na ratiba zingine, sasa wakati nikiwa bize na kazi Alvin akaja na kusimama pembeni yangu. Sikutaka kumsemesha ndo kwanza nikawa bize...

*MY WANGU❤️* *FINAL SEASON* *91-92* Post Mpya
*MY WANGU❤️* *FINAL SEASON* *91-92*
@majario LIVE

Basi bwana .mie nikawa busy na maisha yangu. Ile namba za yusta nilisave ila wwala hatukuwa na ushost tena. Na kama baada ya mwez niliona status yusta kapost kaolewa na...

*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5* Post Mpya
*UTANIITA SHEMEJI.* *1-5*
@majario LIVE

*______________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* Utaniita shemeji ☺️aisee hii simulizi sijui nikae mkao gani ili niilete kwa usahihi bila kukwama wala kupunguza radha😊. Ila hii kitu imenionesha kuwa kweli watoto wa elfu mbili wameshindikana...

UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06 Post Mpya
UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06
@majario LIVE

SONGA NAYO.................. Nilibaki namuangalia huku nikijiuliza ana maana gani kusema vile ?,🤔na nitakosaje amani eti kisa kutokuwa karibu yake 🤔na niukaribi gani anaoutaka kutoka kwangu na kwanini atake ukaribu na mimi?.🤔 Niliwaza...

MY WANGU❤️ sehemu ya 89 na 90 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 89 na 90
@majario LIVE

Basi bwana zayd akaendesha gali mpaka kwake . Akanmbia kumbe uyu boya bado hajaondoka na anakufatilia . Nikasema ndio mi mpaka namshangaa yani sijuh ata anataka nn. Mi simtaki bwana....

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 39 na 40 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 39 na 40
@majario LIVE

Nikasema ooh alex. Mama bwana uyo jamaa si tumesoma nae mpama form 4. Sijamzoea sana ila huwa na mazoea nae mama. We mpe tu namba zangu wla hakuna shida. Mama...

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 57...58💘💘 Post Mpya
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 57...58💘💘
@majario LIVE

Pendo🥹🥹 kwani nilikukoseaga nini mamangu?! Mbona adhabu uliyonipatia haiendani na mwonekano wako?! Kwanini ulinipatia penzi lako kama ulijua ya kwamba utaenda mbali na mimi🥹 haujui ni kwa kiasi gani...

REAL LOVE  Chapter 13 Post Mpya
REAL LOVE Chapter 13
@majario LIVE

seven aliwasha gari na kuliondoa spidi njia nzima alikuwa akilalamika tu mtu unaiona hali yako lakini unakubari tu kufanya mikazi kwahiyo unataka kulazwa tena hospitari ishindwa kuomb hata sjmu kwa jirani umpigie...

MY WANGU❤️ sehemu ya 88 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 88
@majario LIVE

Mlige akaipasua ile simu kwa hasira. Akanmbia nilijua tu . Umebadilika sana faridah kumbe una mwanume ana pesa kunizidi sio . Mie nikasema nisamehe mlige acha nikuelezee. Mlige akafoka .akasema...

🔞 Aaaaaaah..imezama🔞1-5  ( NILIVYOMF🤫LA MUHINDI) Post Mpya
🔞 Aaaaaaah..imezama🔞1-5 ( NILIVYOMF🤫LA MUHINDI)
@majario LIVE

SEHEMU YA KWANZA 😭😭 Acha nilie alafu ninyamaze duku duku langu nilimalize maana najiuliza maswali magumu sana ivi serekali inajua hawa wahindi wanatufanyisha kazi za ndani raia wa nchi hii...

REAL LOVE  Chapter 12 Post Mpya
REAL LOVE Chapter 12
@majario LIVE

kitendo cha fahima kushikwa na seven. kiliwakera sana walikasirika ghafla tu lakini fatuma hakusahau dhamira yake akatoka haraka mpaka kwa fahima na kumsaidia kumshika mkono mwingine lakini mzee fahad akamkemea kabisa "wewe...

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 38 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 38
@majario LIVE

Basi mimi nilikaa home siku 3. Nikapigiwa simu ya kwenda kusaini mkataba katika iyo bank. Na kweli nilienda nikasaini mkataba wa miaka 2. Na mshahara ulikuwa ni mrefu sana ....

MY WANGU❤️ sehemu ya 86 na 87 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 86 na 87
@majario LIVE

Daaah yani sikuwa naelewa nifurahi pale . Ama ninune. Yani nilikuwa katika hali ambayo ata siielew. Basi zayd akanishika mpaka karibu na ile gari kabisa. Akafungua milango na nikaona...

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 55...56💘💘 Post Mpya
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 55...56💘💘
@majario LIVE

Nilitoka kule ndani kwa Tristan bila hata kuwaaga🙈🙈 wenyewe walikuwa wako busy kubebishana😆 nilichukua usafiri nikaenda hadi maeneo ya kule nyumbani kwa Hemed ilikuwa ni mida kama saa tano sita...

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 36 na 37 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 36 na 37
@majario LIVE

Basi bwana kuanzia apo rasmi mi nikavunja mkataba na princess kabisa. Nikawa busy na maisha yangu kabisaa. Lemi aliniulizaga we ndo unahusika na mimba ya princess nikasema hapana siusiki kivyovyote...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest