Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

BADO  NAKUPENDA  sehemu ya 1 hadi ya 4
Gonga94 · Stories

BADO NAKUPENDA sehemu ya 1 hadi ya 4

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
BADO NAKUPENDA ????????

Sehemu ya : 1

By Miss Hamida

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

Simulizi yetu inakwenda kuanzia Miaka ya nyuma kabisa kabla ya kila mtu hajaanza kumiliki simu, ambapo mtu akikupa shilingi elfu kumi ni kama amekupa laki moja, miaka ambayo hakukua na njia yoyote nzuri ya mawasiliano zaidi ya barua????.

Lakini mbali ya vyote ivo bado watu hawakuacha kupendana. Tena wakati huo mapenzi yalinoga sana kuliko hata sasa, likiwemo penzi la Magreth na Simon??.

Watu hawa wawili walijua namna ya kuitendea mioyo yao haki. Hawakukubali kuona tofauti zao za kiuchumi zikikikatisha ndoto yao ya kua pamoja.

Magreth yeye alitokea kwenye familia yenye pesa lakini Simon hakua na pesa bali alipambana kuzipata. Aliendesha taksi na kuzunguka jiji zima la Dar ili tu kujipatia riziki. Na ivyo ndivyo alivyo fanikiwa kukutana na Magreth.

Siku moja ya kukutana ilitosha kabisa kuwafanya waanze kupendana. Na walifanya siri sana sababu ya Mama yake na Magreth.

Alikua ni mama ambae hapendi kusema kitu mara mbili, na mbaya zaidi alichukia sana watu maskini! Alijitaidi sana kumlea binti yake afuate nyayo zake ila sasa baada ya Magreth kupenda mambo yalianza kubadilika….

Kwa wakati huo Magreth alikua bado anasoma chuo, baada ya kumaliza vipindi vyake alikwenda kukutana na Simon! Huko walikaa pamoja na walifanya mambo yao kwa uhuru????.

Taratibu Mama Magreth alianza kuona mwanae ana badilika. Kwanza matokeo yake ya chuo aliyaona sio mazuri! Sio kama hakufaulu, hapana! Magreth alifaulu vizuri ila sio kwa ufaulu alio utaka yeye.

Pili hakua mtu wa kushinda nyumbani, hata siku za weekends alidai kwenda chuo pasipo sababu za msingi.

Tatu, alikua na barua nyingi ambazo hakutaka mama yake azione! Alipotumiwa na Simon alizificha sehemu aliyo hisi kuna usalama ili azisome baadae.

Mpaka hapo Mama Magreth akapata uhakika kua binti yake tayari alikua na mahusiano na mwanaume. Mwanaume ambae hakua akimjua na hakuruhusu awe nae pasipo ruhusa yake.

Ilikua ni siku ya jumapili, siku ambayo Magreth hakutaka kushinda nyumbani. Alipotoka tu huku nyuma mama yake alimuita mfanyakazi.

“Magreth amesema anakwenda wapi?”????

“hajasema Mama”

“Ok! Nime gundua kuna vitu vipo tofauti humu ndani, hasa kwa Magreth! Na wewe umeliona ilo?”

“ndio Mama”????

“Nifuate”

Mama Magreth na yule mfanyakazi walifuatana mpaka chumbani kwa Magreth. Huko walianza kupekua kila mahali na mwisho walishindwa kuendelea kupekua zaidi sababu Magreth alifunga kabati lake na kuondoka na funguo.

“Vunja!” Mama Magreth alitoa amri????

“Nivu…nje mama”

“hujaelewa nini hapo?? Nimesema vunja”????

Kwa utii yule dada wa kazi alisogea kabatini na kuanza kuvunja. Hata hakuchukua mda mrefu kabati lilivunjika na mlango ukafunguka.

Mama Magreth alifurai, haraka alianza kukagua nguo za mwanae mpaka pale alipokutana na boksi kubwa lililo pambwa kwa stika nzuri za rangi nyekundu.

Alilifungua na ndani yake kulikua na barua nyingi pamoja na kadi za mapenzi. Hasira zilimkaba sana akaanza kushusha pumzi kwa mkupuo????.

Kila barua aliyo soma ilizidi kumpa kichaa kwani aligundua mwanaume aliekua kwenye mahusiano na Binti yake hakua alie mtaka yeye! Tena alikua maskini wa kutupwa, maskini ambae mlo wake ulikua mmoja kwa siku.

Alilitupa lile boksi pembeni na kuelekea sebuleni. Alipofika huko alichukua simu yake ya mezani na kupiga namba flanii alizo zishika kichwani.

“Ibrah, nahitaji umfuatilie Magreth! Nahitaji kumjua huyo mwanaume aliekua nae kwenye mahusiano” Mama Magreth aliongea kwa jazba mara baada ya simu kupokelewa

“Hakuna shida! Jambo limeisha” ????

Simu ilipokatwa Ibrah akaanza kazi ya kumfuatilia Magreth kwa ukaribu zaidi. Ndani ya wiki aligundua mengi mno kuhusu Simon kuanzia alipoishi, kijiwe chake cha kupaki taksi na hata sehemu aliyopenda kukutana na Magreth.

Baada ya kukamilisha jalada lake la upelelezi, alilikabidhi kwa Mama Magreth. Hapo sasa ndipo vita vikaanza.

Mama Magreth alicho kifanya cha kwanza alikwenda kijiweni kwa Simon na kumkanya akae mbali na binti yake. Lakini ilikua ni kazi bure maana ni kama aliwapa uhuru zaidi.

Na yeye pia akaona ni heri aongeze nguvu, tena alitumia nguvu ya pesa. Alimuahidi Simon angempa shilingi laki moja ikiwa atakubali kumuacha Magreth.

Msisahau shilingi laki moja kipindi icho ilikua ni kiasi kikubwa cha pesa. Na kwakua Simon alikua amezichoka shida zake na hali yake ya umaskini, roho ya tamaa ikaanza kumuingia.

“Laki moja ni ndogo kwako??” Mama Magreth alimuliza Simon kwa macho ya udadisi zaidi ????

“Sio ndogo”

“Laki moja itabadilisha maisha yako! Badala ya kupaki taksi kijiweni kila siku kwa wateja wa manati kwanini usianzishe biashara yako!? Tena nje kabisa ya huu mkoa??”

“Mh…” Simon aliguna????

“Labda hujajua kuhusu hili, Magreth ni binti yangu na kamwe siwezi kuruhusu hata siku moja aolewe na mtu kama wewe! Kwanza nimesha mtafutia mchumba tayari! Mchumba ambae anaweza kumhudumia kwa kila kitu! Basi kama unampenda Magreth na hutaki ateseke kwenye umaskini wako muache aende!”

Maneno yale yalimuuma sana Simon, ndio alimpenda sana Magreth na hakutaka aishi maisha magumu kama aliyo kua anaishi yeye????.

Kwaiyo alicho ona kinafaa zaidi ni kupokea kile kiasi cha pesa na kumuahidi Mama Magreth kua angeondoka siku iliyofuata asubui na mapema.

Mpaka Pale Mamaa Magreth akawa ameimaliza kazi yake pasipo kutumia nguvu kubwa. Ni kapesa kadogo tu kalitumika kumtia kunguru wake mtegoni. Kazi ikabakia kwa Magreth, ambae hakumuona mpenzi wake.

Nakuja……………

BADO NAKUPENDA ????????

Sehemu ya : 2

By Miss Hamida

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

TULIPOISHIA……….

Ni kapesa kadogo tu kalitumika kumtia kunguru wake mtegoni. Kazi ikabakia kwa Magreth, ambae hakumuona mpenzi wake.

TUENDELEE…………

Kijiweni hakuwepo, alipokua anaishi alihama na hata sehemu yao pendwa ya kukutania hakuwepo. Alihisi vibaya mno, moyo ulimchoma! Alijua kabisa mama yake alikua ana husika na lile.

Aliporudi nyumbani jioni alimfuata na kumuuliza

“Unajua ni wapi Simon alipo?” ????

“Ina nihusu nini mimi!” Mama Magreth alijibu kidharau kana kwamba hakukua na chochote alichokua anakifahamu.

“Simon hayupo! Amepotea ghafla tu! Najua unajua ni wapi alipo”????

“Sijui kwakweli! Na hata kama najua unadhani nitapoteza mda wangu kukuambia”

“Mama nampenda Simon! Unajua ni jinsi gani ninavyo hisi juu yake! Tangu Baba Afariki sijawai kupata furaha ninayo pata toka kwa Simon. Kwanini hutaki kuona furaha yangu?? Please niambie ni wapi alipo”

“Sijui!”???????

“Mama…”

“Magreth sijui! Pengine ameona hakufai” ????

“Nimekua nae kwenye mahusiano ni mwaka sasa! Namjua Simon vizuri kabisa! Ni mwanaume ambae hayumbishwi na mali wala pesa”

“Hahahhahahahahah! Unajua Magreth wewe ni mpuuzi sana! Umeacha mapenzi yakudanganye namna hii??? unasemaje eti??? Hayumbishwi na pesa??? Unajua nime mpa kiasi gani yule mjinga??? Laki moja tu na akawa tayari kukuacha! Sahau kabisa kuhusu Simon, ameona hela niya maana kukuzidi wewe”

“Sio kweli…. Sio kweli….! Sio…. Kweli”????????

“Huo ndo ukweli! Simon hayupo tena kwenye maisha yako! Ni muda wako wa kurudi chuo na uendelee na masomo”

“Hapaana…. Hapana…” Magreth alianza kulia kwa uchungu! Kutelekezwa kwake na Simon ni kitu ambacho kilimpa machungu makubwa mno????????

“Nisikilize wewe….! Msahau uyo mpuuzii mwenzako na usidhani kabisa kama ataweza kurudi tena”
Mama Magreth alimkamata mwanae kwa nguvu huku akimsisitizia????

“siwezii msahau! Nina kiumbe chake tumboni” alilipapasa tumbo lake taratibu huku akizidi kutoa machozi.

Ile habari ni habari ambayo Mama Magreth hakua akiitegemea hata kidogo. Eti binti yake alikua mjamzito na hata hakushtukia.

“Una sema nini wewe!”????

“Ndio nina mimba yake! Ina mwezi sasa”

“Magrethhhhhhhhhh!”????

“Imeshatokea! Labda kweli kachagua hela na kuniacha! Ila mimi nitaishi daima kumpenda na ipo siku atanirudia mimi na mwanangu”

Magreth aliondoka kihuzuni na kurudi chumbani kwake. Mbali na kuumizwa ila bado hakua tayari kuacha upendo wake kwa Simon upotee.

Aliendelea kusoma kwa bidii huku ujauzito ukizidi kukua. Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo alikata tamaa ya Simon kurudi.

Akawa ni mtu wa kulia tu hasa pale alipokua mwenyewe! Alitamani mno kama Simon angekua pamoja na yeye kwenye ile hali.????

Aliendelea kuvumilia hadi pale ujauzito ulipofikisha miezi tisa. Siku hiyo nyumbani kwao walikua wana sheherekea siku ya Mama yake ya kuzaliwa.

Kulifanyika sherehe kubwa sana ambayo ilihudhuriwa na watu wengi mno wenye hela zao. Na kila mtu aliefika kwenye ile sherehe alimshangaa sana Magreth.

Mwanzoni alivumilia kushangawa namna ile lakini mwishoni akachoka. Akashika gauni lake vizuri na kutoka nje kwaajili ya kupunga upepo.

Akiwa hapo ghafla aliona taksi, Taksi ambayo Mpenzi wake Simon alikua anaitumia hapo nyuma. Moyo wake ukaanza kumuenda mbio. Akiwa anazidi kujiuliza maswali kioo cha ile taksi kikashushwa.

Macho kwa macho akakutana na Simon aliekua kavimba kwa machozi. Magreth alitamani kwenda kumkumbatia lakini alishindwa. Alikua na hasira nae sana kwa kile alicho mfanyia.

“Magreth…”????

“ondoka nyumbani kwetu kabla sijakuitia mwizi”????

“Magreth”

“Simon tokaaaaa”

Simon hakutaka kusikia, aliteremka haraka toka kwenye gari na kwenda kumshika Magreth.

“Niachie!! Niachieeee”

“tafadhali nisikilizeee”

“Niachiieeee…. Niachieeee”

Walianza kuvutana huku Magreth akizidi kupiga kelele. Watu waliokua pale wakaanza kuwatazama kwa mshangao, wengine wakazipeleka zile habari kwa Mama Magreth.

Ikabidi Mama Magreth aache kila kitu na kutoka nje alipo ambiwa binti yake yupo. Alipofika huko hakufanikiwa kuwaona ila aliambiwa Simon alimkamata Magreth kwa nguvu akampakiza kwenye gari na kuondoka nae.

“Washa gari…. Washa gari harakaaa”

Mama Magreth aliongea kwa hasira huku akipanda kwenye gari lake na kuanza kufuata njia aliyo pita Simon.

Upande wa Magreth alikua na hasira sana! Alileta vurugu kwenye gari lakini haikumfanya Simon amshushe.

“Nakuchukia Simon! Nachukia kukupenda” ????

“Nakupenda Magreth na sijawai jutia kukupenda”??

“Hujawai jutia kunipenda?? Mimi najuta sana, laki moja imefanya uniache?? Na ujauzito wangu?? Unajua ni mangapi niliyo yapitia?? Watu wanani cheka na kunisema kua nimeshika ujauzito kabla ya ndoa! Unajua mama yangu alikua akini andama kiasi gani?? Nilitegemea tungekuwa wote kwenye hii hali lakini Simon ukachagua pesa kushinda mimi na mwanangu..”

“nisamee Magreth, kwa wakati huo sikua na namna! Nilikubali pesa za mama yako Kwa sababu! Zimenisaidia kuanzisha biashara na kwa sasa inafanya vizuri! Ndo maana nimekurudia wewe na mwanangu tukaishi maisha ya furaha na amani kama tulivyokua tunataka.

“Muongooooo! Muong….” Magreth alishindwa kumalizia sentesi yake kwani alianza kuhisi maumivu makali tumboni.

Naam muda wake wa kujifungua ulikua umefika.

“Simon… mtotoo…. Tumbooo” alilia kwa maumivu makali hali iliyo mfanya Simon aanze kupaniki. Alishikilia usukani kwa mkono mmoja huku mkono mwingine akijaribu kumtuliza Magreth.

Alipoteza umakini barabarani na yote ni kwa sababu kilio cha Magreth kilimchanganya akili yake.

“Nakupeleka Hospitali sasa ivi… vumiliaa mke wangu”????

Wakati anayasema hayo tayari mtoto alianza kutoka

“Simon… simam…isha Gari…..!”????

Magreth aliona kabisa anakwenda kujifungulia njiani sababu walikua mbali mno na eneo la hospitali. Aliomba Simon apaki gari pembeni ili angalau aweze kujifungua salama.

Basi Simon akawa anazidi kupaniki zaidi, alimtazama Magreth namna alivyokua anateseka akatamani kama kungekua kuna uwezekano angemsaidia maumivu.

“Angalia mbele…. Simon”????

Ile Simon anayarudisha macho yake barabarani, alishtuka kuona kuna gari iliyokua inakuja kwa kasi sana mbele yake. Tayari alikwisha toka upande wake na kuhamia upande mwingine pasipo kujua.

Haraka akakanyaga breki

Wakati ajali inatokea nae Mama Magreth pamoja na dereva wake walikua wameshafika eneo la tukio. Haraka waliwahi kwenye gari kusaidia kuwatoa maana gari lilikua limeshika moto????.

Nakuja………

BADO NAKUPENDA ????????

Sehemu ya : 3

By Miss Hamida

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

TULIPOISHIA…………

Haraka waliwahi kwenye gari kusaidia kuwatoa maana gari lilikua limeshika moto????.

TUENDELEE………..

“Anza kwanza na Magreth!! Mtoe kwanza Magreth” ????

Kwa kutii yule dereva alimtoa Magreth, kwa bahati nzuri bado alikua anapumua japo alipoteza fahamu.

“Kuna mtoto…. Kuna mtoto…” aliongea dereva huku macho yakimtoka????

“Mtoto??? Yupo wapi??”???????

Dereva alimtoa mtoto mdogo wa kike alie ungua upande mmoja wa uso wake kwa moto! Mbali na ilo alikua mzuri mwenye afya njema.

“Na vipi kuhusu Simon” Dereva akauliza

“Muache!” Mama Magreth aliongea mno kwa hasira, alikua tayari kuona anaungua kwa moto kama ndio ilikua njia pekee ya yeye kukaa mbali na binti yake

“Boss…!!”????????

“Abuu unajisahau sana?? Nimekuambia muache huko huko”????

Abuu alikubali kishingo upande, alimbeba Magreth na kumpakiza kwenye gari lao pamoja na yule mtoto wake mchanga.

Huku nyuma Mama Magreth alisimama pembeni kutazama jinsi Simon alivyokua anateketea kwa moto. Aliungua mpaka akafia pale pale. Mwishoni gari likatoa mlipuko na kumfanya abaki majivu.

“Abuu! Hako katoto sikataki nyumbani kwangu! Tafuta sehemu umtelekeze! Nilitaka auwawe ila hana hatia, sipaswi kumpa adhabu kubwa kwaajili ya makosa baba yake” ????

“Boss…” Abuu macho yalimtoka????

“Unadhani nitakubali kulea damu ya yule mpuuzi nyumbani kwangu?? Damu ya kimaskini??”????

“sawa Boss”????

“Na Kuhusu Swala la Magreth niachie mimi! Wewe kazi yako ni Simple, kamtupe huyo mtoto mbali sana na hili eneo! Na asije mtu yoyote akajua kuhusu ili, iwe ni siri baina yetu Abuu! Nakuahidi nitakulipa vizuri”

“Na polisi.. je?”???????

“Pia hao niachie”

Baada ya kukubaliana walipanda kwenye gari na kuondoka kwenye lile eneo. Abuu Alimpeleka Mama Magreth na binti yake hospitali kisha yeye akaenda kutekeleza alicho agizwa.

Lakini roho ya huruma ikamuingia. Ni watu wengi sana walikua wanatafuta watoto kwa hali na mali alafu yeye kirahisi tu akamtupe??

Alitafakari sana na mwishoni akapataa jibu. Mtaa aliokua anaishi kuna Mama Aliitwa Sabitina! Ni mama mwenye maisha duni naya upweke.

Kabla ya mume wake kufariki walikua wakijaribu sana kutafuta mtoto ila ikashindikana. Kwaiyo baada ya mume wake kufariki ikawa ngumu kwa yeye kuendelea kutafuta mtoto kwani tayari umri wake ulimtupa mkono.

Kwaiyo Abuu akaona Mama Sabitina alifaa kabisa kupewa kale kachanga. Ivo alivuta muda hadi saa kumi na moja alfajiri, akaenda mpaka kwenye kibanda cha mkaa cha Mama Sabitina akamuweka yule mtoto.

Hata Dakika tano hazikupita Mama Sabitina alifika kibandani kwake akakutana na baraka nzuri ya mtoto aliekua na kovu usoni????.

Mpaka pale Abuu akawa amemaliza kazi yake. Upande wa Mama Magreth tayari alikwisha wahonga polisi ivyo ile kesi haikuchunguzwa sana zaidi ya kufanywa kama kesi za ajali nyingine.

Kisha akamuhamishia Magreth kwenye hospitali nyinginee maana mbali ya kupata fahamu alikua kama chizi sababu ya kumpoteza mtoto pamoja na Baba mtoto.

Alihakikisha Magreth alipata kila aina ya matibabu hasa ya akili. Na palipo hitajika aliwatoa madaktari South Africa mpaka Tanzani kwaajili ya mtoto wake.

Jitihada zake zilianza kufua dafu mwishoni kwani Magreth alirudi kwenye hali yake ya kawaida ila hakuwa sahau wapendwa wake.

Baada ya hapo Mama Magreth hakutaka kurudia makosa yaliyo jitokeza mwanzoni, alimpeleka Magreth uingereza ili akasomee huko!

Hakutaka kabisa akutane na Mwanaume mwingine kama Simon ambae atamharibia maisha yake tena.

Na huko ndipo alipoishi Magreth kwa kipindi cha takribani miaka 22 pasipo kurejea Tanzania.

Turudi ndani ya jiji la Dar-es-salaam katika mtaa mmoja iviii wa changanyikeni alipo kua akiishi Mama Sabitina pamoja na binti yake Anura.

Anura sasa amekua, tena binti mchangamfu na mcheshi kweli! Hali ya maisha yao na mtaa aliokulia ulimfanya awe vile.

Angekua mnyonge sana na hali yake wangemuonea, ila kwakua ni mjanja mjanja basi watu walijifunza kumzoea.

Bado walikua wakiishi maisha duni ila ya amani! Anura aliendelea kuuza mkaa huku Mama Sabitina akifanya kazi za ndani.

Na walizoeleka sana kwa kuuza mkaa! Ile biashara Mamaa Sabitina aliianza miaka mingi sana hata kabla ya Anura kuzaliwa. Na hakua na mpango wa kufanya kazi nyingine ila alibidi afanye kazi ya ziada ili tu apate hela.

Hela iyo alipanga kumpeleka Anura chuo, akajifunze mitindo. Hio ndo ilikua ndoto kubwa ya Anura! Alikua tayari kuifanikisha kwa namna moja ama nyingine, hata kama angefanya kazi kumi kwa siku yeye alikua tayari.

Basi Wakati Mama Sabitina anakwenda kufanya kazi zake za ndani huku nyuma Anura anakwenda kibandani kuuza mkaa. Hio ndo ilikua ni ratiba yao ya kila siku.

Kama Zilivyo kua siku nyingine zote siku iyo Anura alikua na furaha sana. Baada ya Mama Sabitina kuondoka yeye alijiandaa kwa kuvaa gauni lake leupe lililo fubaa kisha akachukua kitambaa na kujifunga usoni kisha akatoka.

Kila alipokua anapita watu waligeuka kumtazama maana mbali ya kuwa na kovu la moto usoni, Anura alijaliwa shepu namba nane na mguu mzuri wa kuvalia kimini????.

“Daaah, sema nini wanangu huyu demu ni pisi ila akigeuka tu basssii” waliongea baadhi ya wahuni waliokua wamekaa kijiweni mara baada ya Anura kupita.

“utadhani Dragon anatema moto” wakaanza kucheka kwa pamoja????????.

Nakuja………..

BADO NAKUPENDA ????????

Sehemu ya : 4

By Miss Hamida

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

TULIPOISHIA……….

“utadhani Dragon anatema moto” wakaanza kucheka kwa pamoja????????.

TUENDELEE…………

“Sema ukiwa na demu wa hivi humtazami usoni, unatazama shepu tu!” ????

“Ndio! Sema aaaah!!! Kwa namna iyo bora tuendelee kudunda na akina Arafa wetu”

Wakaendelea kucheka huku macho yao yakizidi kumtazama Anura. Lakini Anura hakupenda kabisa yale maneno????.

Sio kwamba aliumia? Hapana! Alishazoea sana watu kumshangaa na ile hali yake toka mdogo ila hakupenda namna jinsi walivyo kua wanamsema kwa dharau.

Badala ya kuendelea kutembea Anura alisimama. Akafungua pochi yake akatoa manati kubwa iliyokazwa vizuri????.

Kwenye pochi yake pia kulikua na mawe! Huwa anapenda sana kujaza mawe, kama humjui Anura basi unaweza sema amejaza hela????????.

Alipotoa yale maye akayaweka vizuri kwenye manati yake kisha akageuka nyuma haraka. Hapo hapo alianza kuwapa kitu na boksi.

Na aliwalenga kichwani na machoni. Wale wahuni walipoona wanashambuliwa sana kila mtu akakimbilia kona yake. Basi Anura akacheka kweli, akarudisha manati yake kwenye pochi????.

“Leo ni siku yangu nzurii sanaa! Sipaswi kuchukia”

Alijiweka sawa na kuendelea na safari yake hadi kibandani. Alipofika alifungua banda lake, akabadilisha nguo na kuvaa nguo zake za kazi.

Akatenga magunia yake ya mkaa pamoja na makopo, akaendelea kusubiria wateja huku akiweka umakini kwenye kitabu alichokua anatumia kuchora picha za baadhi ya mitindo mbali mbali ya magauni.

Akiwa pale alifika rafiki yake mkubwa kwa jina la Scola! Hawa watu wawili walikua marafiki toka walipokua wadogo. Walipendana mno utadhani walishea tumbo.

“Ilo gauni nimelipenda” Scola aliongea huku macho yake yakiwa kwenye kitabu cha Anura

“ushaanza kuchungulia chungulia vitu vyangu” Anura alifunika kitabu chake haraka????

“Sasa nisipo ona mimi nani mwingine ataona! Unatakiwa kujiamini na mitindo yako! Unataka kuwa mwanamitindo na hauna comfidence”

“sio ivyo! Haijakamilika tu! Enheee niambie nilikua nakusubiria wewe”

“ndo nimekuja, sema sina vocha”

“Ushaanza mambo yako Scola, hata kama unayo unasemaga sasa! Sijui unaibania ibania ya nini, au mwenzangu una kijana unaongeaga nae usiku”

“heeeeee! Kijana! Acha zako Anura fanya mpango tupate vocha lasivyo itakula kwako”

“Scola nina mia tano tu”

“Hio hio inatosha au unadhani vocha inauzwa shi ngapi??”

“Basii ngoja nikalete”

Anura aliweka kitabu chake pembeni akatoka na kwenda dukani kisha baada ya dakika kadhaa akarudi na vocha akampatia Scola.

Baada ya vocha kuwekwa, Scola aliingia kwenye website iliyokua inaitwa GIVE BACK TO THE SOCIETY yani kwa kiswahili ina maana ya kuirudishia jamii.

Huko kulikua kuna orodha ya majina ya watu waliochaguliwa kama wanufaika wa iyo program ya GIVE BACK TO THE SOCIETY.

Ngoja nielezee kidogo…, shirika la GIVE HOPE ni shirika binafsi lililokua lina jishughulisha na masuala ya jamii katika sekta mbali mbali za mazingira pamoja na afya.

Na shirika hili lilikua Tanzania kwa miaka 10! Na ndipo wakaanzisha program yao waliyo iita Give Back to the Society.

Ambapo katika program hiyo walikua wanatoa matibabu buree, nikisema matibabu buree namaanisha matibabu ya magonjwa yote mpaka surgery walifanya bila malipo.

Ulichotakiwa kufanya ni kujaza fomu ya maombi na kuituma kisha Shirika litachagua watu wawili ambao watakwenda kutibiwa kwao bure????.

Na shirika hilo hufanya ivo mara moja kwa mwaka. Na karibia kila mwaka Anura alituma maombi yake. Alikua na tumaini iwapo angekubaliwa basi angekwenda kuondoka kabisa lile kovu usoni mwake.

“Mbona unasita, onyesha majina!” Anura alimshangaa Scola????

“Mimi naogopa”????

“Unaogopa nini bhana…” Anura alivuta simu ya Scola na kuangalia orodha ya majina na kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuona jina lake.

“vipi umechaguliwa??”???????

“Hapana…” alisononeka sana, alikata tamaa kabisa

“Usiwe ivyo Anura! Ipo siku watakuona na watakutibu”

“sioni kama iyo siku inakaribia! Miaka sita sasa bila mafanikio, ina maana nitaishi na hili kovu mpaka siku yangu ya mwisho?”

“Usiseme ivo, kila kitu hutokea kwa sababu, labda mda wako haujafika! Pindi utakapo fika hutojutia kusubiria” ??

“Mimi nimechoka kusemwa kila ninapo pita! Asubui nimetoka kuwapiga watu manati sababu ya maneno yao ya shombo kwangu! Nitawapiga watu mpaka lini! Natembea na manati na mawe kwenye pochi sio kwamba napenda Scola”

“Najua! Na unavumilia, basi vumilia na hili! Naamini mwakani utapata nafasi” ????

“Daah!” Anura alitoa kitambaa chake usoni na kufanya kovu lake lionekane vizuri.

Kama sio lile kovu basi Anura angekua mzuri mnoo pengine angesumbua mtaa mzima kwa uzuri wake.

“Pole Anura”

Scola alimuonea huruma, alichukua kitambaa chake na kukirudisha usoni mwake. Baada ya dakika chache huzuni ikapotea na wakaendelea kucheka kama kawaida.

Uzuri Anura sio mtu wa kukaa na huzuni kwa mda mrefu, ana huzunika dakika chache na kucheka mda mrefu!

Nakuja……..

Full 1000
Namba ya malipo 0763083437
Jina Hamida
Vodacom

Maoni

You're not logged in


Tangazo - from bangi to baby fully stories 1 to 21
from bangi to baby fully stories 1 to 21
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BADO NAKUPENDA sehemu ya 1 hadi ya 4

BADO NAKUPENDA ????????

Sehemu ya : 1

By Miss Hamida

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

Simulizi yetu inakwenda kuanzia Miaka ya nyuma kabisa kabla ya kila mtu hajaanza kumiliki simu, ambapo mtu akikupa shilingi elfu kumi ni kama amekupa laki moja, miaka ambayo hakukua na njia yoyote nzuri ya mawasiliano zaidi ya barua????.

Lakini mbali ya vyote ivo bado watu hawakuacha kupendana. Tena wakati huo mapenzi yalinoga sana kuliko hata sasa, likiwemo penzi la Magreth na Simon??.

Watu hawa wawili walijua namna ya kuitendea mioyo yao haki. Hawakukubali kuona tofauti zao za kiuchumi zikikikatisha ndoto yao ya kua pamoja.

Magreth yeye alitokea kwenye familia yenye pesa lakini Simon hakua...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/bado-nakupenda-sehemu-ya-1-hadi-ya-4

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi bado-nakupenda-sehemu-ya
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

*AFANDE MILLAN😎* *season 3*  *SEHEMU YA HAMSINI NA SITA*

*AFANDE MILLAN😎* *season 3* *SEHEMU YA HAMSINI NA SITA*

783
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 59

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 59

689
*AFANDE MILLAN😎* *57&58

*AFANDE MILLAN😎* *57&58

558
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 48.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 48.

366
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 46  na 47.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 46 na 47.

271
SASA NAKUPENDA Sehemu ya  45.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 45.

214
SHAMIRA 52 to 53

SHAMIRA 52 to 53

188
 SHAMIRA Sehemu ya 54&55

SHAMIRA Sehemu ya 54&55

138
SHAMIRA 49 to 50

SHAMIRA 49 to 50

137
SHAMIRA Sehemu ya 51

SHAMIRA Sehemu ya 51

132

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.73K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.45K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.82K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.33K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.92K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

2.87K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.71K
MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

2.7K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.64K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.58K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 59 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 59
@majario LIVE

Kaka akasema jalia apa ni kwako, na ndo kwa mumeo feel good kuwa apa , jisikie upo kwako kabisaa, na apa ndo kwa mumeo, asikutoe apa kukupeleka kokote, na...

*AFANDE MILLAN😎* *57&58 Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *57&58
@majario LIVE

Daaah basi mwanangu ibraaa ndo akanipanga hivyo kwamba, nitafuta mama yoyote uku pemba , awe anaongea na zena ,akijifanya ni mama yangu ili impe amani zena , nikaona sio suala...

*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) 7 kwa 8 Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) 7 kwa 8
@majario LIVE

MTUNZI: SMILE SHINE EP 7. Kucheki vizuri alie nikaba kumbe ni vicram, alivyoona nimetulia akaniingiza Kuna chumba jilani, sijui ata alikiandaa saa ngap, kwani we kaka unashida Gani na Mimi? Vicram alitabasam...

 SHAMIRA Sehemu ya 54&55 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 54&55
@majario LIVE

🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 Mwandishi; 0742443214 Mwanangu alifika mwaka ila ata kutembea alikuwa hawezi husna akanambia wewe uyu mtoto anaumwa ebu tumpeleke zakiemu hospitali kubwa. Mh nikasema sawa. Mtoto wangu ni karembo jamani yani...

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA & Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF Post Mpya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA & Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF
@majario LIVE

wametoa kibali rasmi cha kuthibitisha kuwa uwanja Wa Hoima City uliopo Uganda, unakidhi viwango vya kimataifa vya kuandaa mechi kubwa za soka. Uwanja huo wa kisasa uliopo katika mji wa...

*AFANDE MILLAN😎* *season 3*  *SEHEMU YA HAMSINI NA SITA* Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *season 3* *SEHEMU YA HAMSINI NA SITA*
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Daaah basi mwanangu ibraaa ndo akanipanga hivyo kwamba, nitafuta mama yoyote uku pemba , awe anaongea na zena ,akijifanya ni mama yangu ili impe amani zena , nikaona sio suala...

SHAMIRA 52 to 53 Post Mpya
SHAMIRA 52 to 53
@majario LIVE

🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 Sehemu ya 52 Mwandishi; lissa wa huru media Basi bwana kesho yake asubuh husna na aisha wkaniletea uji na viazi vya rosti nilikula vizuri mana mwanangu kana nyonya mno. Basi nilipomaliza...

MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) 6 Post Mpya
MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) 6
@majario LIVE

MTUNZI: SMILE SHINE EP 6. Kumbe alikuwa ni Kingslay, jamani kanichungulia,niliona aibu nyie dah!, upande wa Kingslay aliingia Moja Kwa Moja chumbani kwake,alijikuta hisia zimempanda Ile Ile, "uyu binti jamani ni mrembo😋,...

MY HOT PILOT ZYRO ( Rubani Wangu ) 1 to 5 Post Mpya
MY HOT PILOT ZYRO ( Rubani Wangu ) 1 to 5
@majario LIVE

(Kitabu Chote) MY HOT PILOT ZYRO ( rubani wangu 🔥) MTUNZI; SMILE SHINE EP 1. Ikiwa ni majira ya saa tatu usiku, nikiwa jijini dar, maeneo ya tabata bima, Kwa Jina naitwa milembe mzaliwa wa...

SHAMIRA Sehemu ya 51 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 51
@majario LIVE

Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi na aisha hakuchelewa sna akaleta vifaa vyangu na kadi langi la clinic pale.mimi sielewi nikawa nasema jamani nipelekeni nikazae naumwa sana. Manurse...

SHAMIRA 49 to 50 Post Mpya
SHAMIRA 49 to 50
@majario LIVE

Sehemu ya 49 Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Aisha alinishauri nitafute mwanaume mmoja nimpe mimba. Nimasema wala sina mda uo. Kwanini nikamuongopee mtu kuhusu mtoto Uyu mtotot akizaliwa .mimi...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 48. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 48.
@majario LIVE

48 MWISHOOO 🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Kesho yake mapema sana . Posa ya baraka ililetwa kwetu. Baba akaipokea nimksema mahari. Apo sasa ilibidi nimpigie adrian kua mimi naolewa.akanmbia aha sawa...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 46  na 47. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 46 na 47.
@majario LIVE

46 MPAKA 47 🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Yani nilibaki kimya namuangalia tu ata la kusema sina na wazazi wanatuangalia. Akanmbia shakira. Tusijitese mama angu. Tuanglie mioyo yetu.mimi naelewa shakira unanipenda...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya  45. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 45.
@majario LIVE

🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Na baada ya mda sasa ndo baraka akaingia. Kapoa kweli kweli na tangia zamani ana sura ya upole ndo akazidi nakwambia. Nna hasira nae...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 43  na 44. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 43 na 44.
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Aseeee kwanza apa kwenye paji nilishonwa nyuzi 6.ni ngumi iyo .yani mkono wa mwanaume tu. Msenge alijua kuniweka alama. Basi nasehemu zengine nilipata mikwaruzo. Nilivimba...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest