*AFANDE MILLAN๐* *57&58
Daaah basi mwanangu ibraaa ndo akanipanga hivyo kwamba, nitafuta mama yoyote uku pemba , awe anaongea na zena ,akijifanya ni mama yangu ili impe amani zena , nikaona sio suala mana siwez kumdanganya kila siku zena ni atastuka tu au atahisi kitu ,mi kuna mama flan hivi, anaitwa mama tawfiq, uyu mama tawfiq huwa anaishi kalibu na nyumbani kabisa ,yani ni jilani tu na nyumbani ,na ni mama ambae ni nimemzoe sna, na uyu mwanae tawfiq mimi alikuwa ni mshikaji wangu mkubwa mnoo uku nyumbani na nimekua nae kabisa , ila uyo tawfiq ni alifariki bwana tulipomaliza form four tu ๐ญ๐ญ๐ญ, jamaa akafalikigi ila bado mama yake ,mi naongea nae sana , na nikija uku huwa lazima nikamsalimie, ni kama mama yangu kabisa, yote sababu nilikuwa ni rafiki sana na mwanae na uyu mama huwa ananichukulia mm kama mwanae kabisaa, sasa basi nikaona asa apa niendee kwa mama tawfiq nikamsalimie na niongee nae hii issue yangu, basi bwana kweli mimi moja kwa moja nikaludi mpaka mitaa ya home, ila sikuenda nyumbani ata ,nikafiki kwa mama tawfiq, ahaaaa uyu mama aliponiona alinifurahia sana, yani alifurahi mnooo, akanmbia jamani baba umekuja lini, ahaa nikasema mama mimi ndo kwanza nimekuja jana na leo nikaona nije kukusalimia
Basi mama tawfiq akatoa mkekaa, na tukatandika uwani kwake tukakaa , tukaanza kusalimina vizuri, akawa ananiuliza naendeleaje na za masiku mingi, mana mm huwa siludigo myumbani ovyo ovyo kabisaa, nikasema nipo njema mama na naendelea vizuri, sijuh wewe apa, na yeye akanmbia kiwa anaendelea vizuri sana, basi akanmbia hongera sana , nasikia familia imekuolea mke , nikasema ndio mama, akanmbia lakini na nyie vijana mnajishau sana, millan ungeoa lini sasa, yani familia imekungojea uoe mpka wamechoka wamekuolea, nikasema acha tu mama, mam tawfiq akanmbia lakin jalia ni binti mzuri sana, asie na shidaa, yani mzuri mno yule mtoto wa tabia na kila kitu, kwaiyo naamini ata wazazi wako waliliona hilo kwake na ata mimi naamini umepata mkwe mzuri na mwema
โ
Nikasema ni kweli anaonekana hivyo mama ila mama mimi nilishakuwa nimepata mwanamke uko dar, na tunapendana sana , na ana mtoto mmoja nimemzalisha na ana mimba yangu tena kwa sasa ,na uyo mwanamke ndo mimi ndo ninayempemda na ndo nilopanga kumuoa, kwaiyo mama ,hizi habari za kwamba nimeolewa mimi zimenistukiza sana ,na nimekuja kuzijulia apa , kiukweli sikua nimelizia kabisa juu ya uyu mke, mama tawfiq akanmbia pole sana kijana wangu, daah basi wasikilize wazazi, lakini pia wewe ni muislamu unaweza ukawaoa wote, yani ukawa na wake wawili, nikasema sawa maam, lakini uyu mwenzangu wa dar sijamueleza lolote juu ya yanaoyoendeea uku kwetu, mama tawfiq akasema hapana usimuelezee kwa sasa utamuumiza sana , apo ukiludi dar ndo ukamueleze, nikamwambia sasa mama, uyo wa dar anataka sana kuongea na mama ,na kama unavyomua mama yangu daah hawezi kukubali mana yeye anamtaka jalia tu, na nilipojalibu kumueleza habari za uyu mwengine ,kanmbia hamgaki kabisaa , na hamtambui, sasa naomba unisadie kuongea na zena mama, ili tu apate amani ,ya kwamba kaonge na mama yangu mzazi, na kwetu kakubalika, mi mambo mengine ntaenda kumuelezea mwenyewe nitakapoludi dar
Mama tawfiq akasema wala usijali mwanangu, mimi ni mama yako kabisaaa, wala hakuna shida, nipe niongee nae, daah nilifurahi, na harka nikampigia zena na zena akapokea simu, nikasema zena aaya nipo na mama naomba uongee nae sasa, zena akanmbia sawa, mimi sasa nikampa mama tawfiq simu akaanza kuongea na zena, daaah mi nilitulia kimya, niliona maam tawfiq ana play part vuzuri mnoo, anamuliz amaswali kweli kweli, kwamba kwenu wapi, una miaka mimgali , unafanya biashara gani, yani maswali yote amabyo nna uwakika ata mama yangu mzazi ni lazima angemuuliza zena, baada ya apo niliona mama tawfiq anafurahia tu kuongea na zena, na akawa anaulizia mpaka mtoto wangu, yanji mm mwenyewe nilipata amani kabisaa, na baada ya apo sasa, mama tawfiq akaagana na zena, kisha akakata simu akanipatia simu yangu, mama tawfiq akanambia ata uyu anaonekana ni mwanamke mzuri sana, na anaongea vizur na muelewa mnoo, nimempenda kweli, mi nikabaki natabasamu tu, mama tawfiq akasema kanambia anaitwa zena
Nikasema yaa anaitwa zena mama, ndo mwanamke amabe nampenda sana mm mam, mama tawfiq akanmbia pole sana lakini shida ni wewe ungeoa mapema aya ata yasingekukuta mwananagu, daah basi baada ya apo story nyengine zikaendelea na nikongea sana na mama tawfiq ,sikutaka kuwahi kuludi nyumbani kabisaa, mi nilitulia pale mpka chakura cha mchana nikala pale, niliposhiba sasa , nikasema mama tawfiq mimi leo nipo nipo apa ,ntaenda jioni home ,akanmbia wala usijali kabisa mwanangu, na pale kwake si kuna kafensi na miti mimngi, mi nikajilaza kwenye mkeka uku miti innipepea nikapiga usingizi pale, yote si nakimbia nyumbani , mana dah naenda kukutana na jalia na mdomo wa mama mi sikutaka ata, basi nikapiga usingizi pale mpka jioni saaa 12 ,ndo nikaamka nikamuaga mama tawfiq, nikatoa na chochote kutu nikampa yule mama, akapokea na akanishukuru sana , mimi sikukaaa tena ndo taratibu nikaanza kulejea nyumbani, nimefika home nakutana na broo barazanai, akanmbia ulikuwa wapi dogo, na nakupigia ukawa hupokei simu, ni kweli niliona simu zake ,ila sikutaka kupokea mna namjua mtu wa amri amri sana uyu, nikasema kazini nilipewa oders za kuja kufanya uku, so nilikuwa nimeenda kufanya baazi ya kazi ,kaka akaningalia sana kisha akacheka akaniuliza we si umepewa likizo hizo kazi wanakupaje dogo, mi.nikabaki kimya ,kaka akanmbia mkeo anakungoja ndani, na hongera kw akumkuta mwali mkeo,
Ahaa mimi wala.sikujibu kitu nikaingia ndani, nikamkuta mama yupo sebleni, nikasogea apo nikamsalimia mama, akaniitikia ,akanambianmbona umechelewa na nilikueleza kuwa wakwe zako wanakuja, nikasema mama kazi ni muhimu sana kwangu, nilikuwa na kazi nyingi zikanibana nikaona nimalizane nazo kwanza , ila si ntawaona tu hakuna shida na nataka kujua ni kwa mda gani ntakuwa uku, mma akanmbia mpaka umalize saba na mkeo ndo mtaenda ,nikasema sawa , basi nikainuka nikaingia chumbani kwangu ,nikamkuta jalia anaongea na simu na mama yake, aliponiona akasema ahaa mam ndo ameludi apa mume wangu, naona mma yake aliomba kuongea na mimi, nikapewa simu, daah sikuwa na jinsi nikamsalimia yu mama mkwe, basi hakuwa na jipaya zaidi ya kunisalimia na kunisihi sijiuh nikaishi na mwanae kwa mapenzi na wema mana anaelewa kuwa mtoto wake hana shida kabisaa, na yuko vizuri tu, mi nikasema sawa mama nimekuelewa na nitajitahidi kuhishi na jalia vizuri, apo akiri inawaza nataishi nae vp uyu mwanamke ,akiri na moyo kama utkuwa kwa zena acheni kabisaa, basi baada ya kuongea na yule mam, mi nikaenda kuoga, nilipotoka, nikakuta jalia kashajiandaa kunipa penzi ila nilimwambia leo hapana nimechoka sana nahitaji kupumzika , na nikajitupa kitandani, uku nachezea simu, yangu na nilikuwa nachart na.zena, basi bwana mi ata achakura cha usiku sikutaka kula kichwa hakikuwa sawa, nikamuaga zena kwenye charting na nikapumzika
Na ayo ndo yalikuwa maisha yangu kwa siku zote nilizokuwa uku pemba, ila sas mpka tunamaliza saba na jalia nilimgusa mala 2, ni mtundu sana na kama kufundishwa aliyashikilia ila mood sina mwanaume ,yani nilifanya nae mala 2 tu, kila siku namwambia sina mood, na kuna siku usiku natoka nje kuongea na zena, na zena akawa akitaka kuongea na mama naenda kwa mama tawfiq, anaongea nae na ndo ikawa hivyooo mpaka sasa ikafika siku ya kuondoka yani kuludi dar , mama akatuaga na akatutakila barka tele, ila sasa nikawa naludi na broo, kwaiyo uku dar sis tutliludi watatu yani.mm na mke wangu jalia , na brooo, mana kakayangu mm anakaa uku uku dar ,mdogo wetu wa mwisho ni dr ndo yuko pemba, apo mm sijamueleza chochote zena kuwa naludi dar, mana ibraa alinambia nisimwambie kitu ,mpka.nifike dar tuseti mipango kwanza, basi bwana tulitoka pemba mapema.sana na mpka saa 8 mchana tukaingi bandanrini, kaka akakodi tax kisha akatupeleka mpaka kwangu, yani kama kaambiwa vile, ahaaa ila.sikuwa na kauli mbele ya broo nikatulia kimya kama.sipo mbwa mm, basi baada ya kufika home. Mi.nikafungua milango, nikamkalibisha ndani jalia sas, jalia alifurahi sana kufika kwangu na akanmbia asante sana na nimempapenda sna kwako , nikawaambia sawa nashukuru, na broo akaingia mpaka sebleni kisha sasa akasemaaa........
๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni