SASA NAKUPENDA Sehemu ya 43 na 44.
Mwandishi; lissa wa huru media
Aseeee kwanza apa kwenye paji nilishonwa nyuzi 6.ni ngumi iyo .yani mkono wa mwanaume tu. Msenge alijua kuniweka alama. Basi nasehemu zengine nilipata mikwaruzo. Nilivimba kweli.kweli. yani.nilivimba jamani. Mwili ulitutumuka kweli kweli. Baba alikuwa kimya ila.niliona ana hasira kweli.kweli. basi nilikaa hospitali siku 2. Ndo at least sasa nikawa sawa . Ata mwili nikawa nauona kama wangu sasa.na ndo nikaruhusiwa kuludi nyumbani. Hii siku ambayo niliruhusiwa wazazi hawakutaka kujua lolote kuhusu baraka na mimi kwanza .walikuwa wananiangalia mimi zaidi na afya yangu. Na ata simu kwa mda wote uo sikuwa nimezishika kabisa mimi. Yani mwili unauma kiasi cha kwamba hukumbuki kushika chochote kudadeki.nyie kuna wanaume wanapiga uwiiiiii. Usiombe ukakutana nao. Mbona utaoma dunia chungu hiii. Shoga yangu gile.akaja kuniona mana mama.alimpigia simu kumuelezea . Basi akanipa ple sana .akanmbia unajua nini. Nikasema ndio. Akanmbia yule baraka anakupenda sana kiasi cha kwamba anakuwa na hasira sana.nikasema gile mwanaume anayenipenda ndo angenipiga hivi . Amenipiga kama anataka.kuniua mimi.akanambia unajua mimi ndo niliona baraka alivyokuwa ana haha ile siku umeenda kulala kwa adrian. Ila kama ni mpigaji ata uyo mkewe ana kazi wallah. Nikasema we acha tu ndugu yangu.yani han ata aibu kaja kunipiga nyumbani kabisa looooh. Simtaki sasa.ndo anipige mpka aniue simtaki. Gile akawa ananitiliza.kisha akanmabia kuwa adrian alimtafuta kuniulizia.nikamwmabia wr mueleze naumwa nilipata ajari kidogo mambo mengine ntamuelezea mwenyewe. Akanmbia powa. Basi jioni sana ndo gile akaondoka.
Na mimi kesho yake .ndo nilitamani ata kushika simu yangu. Heee et nakuta barka nae kanitumia sms. Loooh . Et sijuh nisamehe ni hasira na wivu. Et ohhh mimi mapenzi yako yananitesa. Malaa ohhh shakira nakupenda sana. Na kila nnachokifanya ni hasira za kutokukumiliki. Yani alituma sms kibao. Nikazifuta zote kisha nikablock namba yake. Nikampigia adrian. Akaniukiza mama umepata ajali gani. Mbona gile kanmbia umepata shida.nikasema ndio nilipata ajaali ya pikpiki. Nimechanika apa kwemye paji la uso . Nikamuelezea uongo kibao nakwambia. Akanipa pole sana pale .akanmbia natamani kuja kukuona ila.sijulikani kwenu daah.nikasema ndo ufanye ujulikane sasa. We unazani tutakuwa hivi mpaka lini. Adrian akacheka.akasema si unajua tatizo ni nn kati.yetu kuwa mkristo basi nakuoa chapu.mimi. nikacheka mana uyu nae. Nikasema tutaongea hizo mada ntakapopona . Akanmbia sawa.
Basi baada ya kama week mimi nikawa sawa kabisa. Nikawa naendelea vizuri kabisa. Apo sasa ndo mzee akaniita akaniuliza kwa nini baraka alikupiga. Aseee nikasema baba mimi baraka ananitaka . Nikimkataaa ndo ananifanyia fujo. Ata saloon kwangu anakujaga kunifanyia fujo. Ndo kawaida yake ila hiii ya mwisho ndo kazidisha kanipiga.na mimi namuambiaga sikutaki sababu ni mume wa mtu. Ila yye anataka mimi.niwr kama.mchepuko wake. Na wakati mimi hilo suala nimeshalikataaa kabisa mimi. Baba akasema sawa baraka ana week hayupo dar .wala hayupo kwake ila nitamkamata tu.na ndo atanieleza mimi ni nani. Yeye si anajifanya mwanajeshi. Ngoja ntamkamata tu. Mie kimyaa. Mana baba anavyoelewana na baraka ila hii safari.ilikuwa ni noma.
Basi mie baada ya siku 2 .3 .uyo nikaingia zangu kazini kuendelea na majukumu yangu. Na ikapita week nna amani tu mana wala.sijamuona baraka ata .heee siku iyo sasa nipo busy na kazi. Si naona kaingia maua. Na wifi yake bahati. Mi.namkumbuka uyu dada japo sikuwah kuonana nae face to face. Mama alinioneshe akwenye picha. So nilivyomuona wala sikupata shida ya kumtambua kwamba uyu ndo bahati. Nikasema eeh nini wenzangu. Mana walikuja kama.kishari. maua akasema sikia nikwambia bahati uyu ndo maraya anaekuibia mumeo uyu ndo kafanya wewe umepewa taraka 3 ni uyu msenge. Anampelekesha sana kaka yangu. Aseeee awa wana nn . Yani apo nna kidonda kaka yao katoka kunidunda aya week 2 bado wamekuja na wao. Wananwambia upumbavu ata siuelewi.mimi.
Nikasema mbona wr maua sikuelewi. Uyo bahati hakutaka ata maongezi akanilukia. Akaanza kunipiga .nyie na mwenzenu nguvu sina.ila mdomo weeeeee utalala. Ntaongea kuanzia usiku mpaka kesho asubuh. Aseeeee yule dada nae sio powa . Aliniiga ngumi kama 2 hivi .nashukuru gile ndo aliiniingilia nakwambia. Na kuna wateja pale ndo wakanitoa mimi wakanieka pembeni. Teali nishaanz kulia.mana ata sielewi wallah. Basi bahati akaanza kupigana na gile. Nikamuuzia ugomvi gile na uzuri sasa gile nae sio mnyonge nae nguvu anazo weeeeee. Kikanuka tena. Heeee maua akaanza kualibu ofisi yangu. Aseee nilibaki tu namuangalia. Alipasua vioo vya ofisi nzima niliumia sana. Gile akawa anataka kumzuia ila wapi.nikaingia tu kumshika gile. Nikasema waache watakuumiza .acha wafanye wanachokitaka. Aseee wakapasua kila kitu ofisini. Mawigi gite wakayachana chana na viwembe. As if hii saloon alinijengea barka mimi. Kumbe walaaaa. Roho iliniuma sana. Walivyotosheka wakapanda boda wakasepa . Aseee nilimpigia simu mama nalia .nikawa namuelezea kilichonitokea .na baada ya mda mama akaja sasa slooon ndo anakuta vile .mama akasema aya mambo yote ni baraka ndo anasababisha naona anataka kukua mwanagu . Utu kijana anataka kukuua naona.
Nikabaki nalia tu. Basi mama akanichukua. Mana tulitaka kwenda polisi. Ila baba akasema ludini nyumbani kwanza .kwa sbabu apa kuna issues za ndugu yani ugomvi huu. Ushakuwa unahusisha ndugu. Basi mimi na mama tukaludi nyumbani tu. Na baba akawa kaludi pale mimi nalia kweli.kweli saloon yangu. Nikawa nasema baba mimi ntamfunga yule maua. Masuala yao mimi hayanihusi.mimi.nataka niende polisi. Baba akasema baraka anakuja ngoja. Nikawa nalia na apo apo .akaja baba mdogo bakari na mkewe. Yani sasa hili sula likawa la familia. Ikawa anaongojewa tu barka .ambae alisema anakuja. Apo mimi nna hasira kweli kweli. Yani mpaka natetemeka kwa hasiraaaaa nilizonazo
๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni