" Ni kweli mtoto sio wako Tristan nisamehe sana sikupanga kufanya hivi nililazimishwa na boyfriend wangu ili tupate pesa kutoka kwako "
aliongea Silvia huku amepiga magoti na alikuwa analia
" Baba wa mtoto ni nani ?"
Aliuliza Tristan
" Baba wa mtoto ni roman "
aliongea Silvia huku ameangalia chini
" Hahaha roman sikitegemea katika watu wote atakuwa ni yeye nilimuamini sana , haya potea sitaki kuiona tena sura yako karibu yangu na umfikishie huu ujumbe hiyo mpuuzi mwenzio akae mbali na mimi laa sivyo nitakachomfanya hatokaa alisahau maisha yake yote " roman ni secretary wa Tristan na alitokea kumuamini sana
Silvia alikimbia hakutaka kuchukua hata nguo Tristan alikaa chini machozi yalianza kumtoka
" Nimeachana na mwanamke niliyempenda kwasababu yao sijui kama Gabriella atanisamehe "
Tristan alichukua pombe na kuanza kunywa Zilipita week mbili nyingine ambazo zilitomiza mwezi tangia maverick aende kwenye mafunzo Tristan aliamua kumfuata baba yake Mr Edward
" Baba nisamehe sana kwa kuto kukusikiliza na kukuamini najuta kwanini sikusikiliza maneno yako sijui kama Gabriella atanisamehe "
" Usijali kuhusu Hilo Tristan Nina uhakika Gabriella atakusehe na bado anakupenda sana niachie mimi hili suala nitaongea na wazazi wake "
" Asante sana baba " Tristan alifurahi sana
Kwa upande wa Gabriella alianza kutapika kichefuchefu hakikuacha akiwa nyumbani kw Veronica alianza ghafra alikimbilia bafuni na kuanza kutapika Veronica alimfuata " Besti kwema kwani umekula nini asubuhi asubuhi "
Veronica alimshika Gabriella mkono wakaenda kukaa sitting room
"Hata Sina hamu ya kula lakini nashangaa siku hizi kila asubuhi lazima nitapike "
Gabriella aliongea kwa kulalamika huku amelaza kichwa chake kwenye bega la Veronica
" Gabriella una mimba ? "
Veronica alimuangalia Gabriella usoni
" Hahahaha Vero naona umeanza kuchanganyikiwa siku hizi naanzaje kuwa na mimba na unajua kabisa niliambiwa hospital Sina wezo wa kuzaa " Gabriella alicheka kwa uchungu
" Vipi kama walikudanganya ? Embu jiulize mwenyewe kwanini una dalili za kuwa na ujauzito na lini uliona siku zako ?" Maswali ya Vero yalimfanya Gabriella abaki na mshangao
" Vero bhana haiwezekani mimi kuwa mjamzito nilienda kabisa hospital nikiwa na Mr Edward na Tristan nakumbuka tulipima na majibu yakaja kuwa Sina uwezo wa kushika mimba "
" Sawaaa lakini bado hujajibu swali langu mwisho kuona siku zako ni lini na maverick ulikutana nae lini ?"
" Oops Yani hata nahisi kuchanganyikiwa mwezi huu sikuona siku zangu na Rick nilikutana nae mwezi uliopita "
" Hiyo ni mimba shoga angu na nakuona tu unavyozidi kunawiri siku hizi"
" Acha mambo yako bhana mimi hata siamini "
" Sasa hivi twende hospital "
" Mimi nimechoka niache nilale kidogo " Gabriella alijilaza kwenye kochi
" Twende utalala tukirudi "
Veronica alimlazimisha Gabriella mpaka alikubali walienda kupima kwenye hospital ya karibu
" Wewe ndo Gabriella Alphonse?"
Aliuliza dactari
" Ndiyo ni mimi "
alijibu Gabriella kwa wasiwasi
" Hongera ujauzito wako unawezi mmoja Sasa na siku 4 "
aliongea dactari huku anatabasamu Gabriella aliishiwa na nguvu akazimia alikuja kuamka amelazwa kwenye kitanda Cha hospital
" Kwanini nipo hapa ?" Gabriella alikaa kitandani
" Ulizimia baada ya kupewa majibu na dactari kuwa wewe ni mjamzito "
" Oh mungu wangu sijui nifanye nini?"
Gabriella alianza kulia
" Unalia nini Sasa badala ya kufurhi unaenda kuwa mama Sasa "
" Sio kama sitaki au sijapenda ila nalia kwa furaha huu ni kama ndoto kwangu siamini kama naenda kuwa mama hivi karibuni asante sana mungu wangu "
Veronica alimkumbatia Gabriella
Baada ya kuruhusiwa Veronica alimpeleka Gabriella nyumbani kwao kwani asingeweza kuendesha gari mwenyewe Gabriella na Veronica walishtuka baada ya kumuona Mr Edward akiwa na Tristan nyumbani kwa kina Gabriella tena waliongea na mr Alphonse
" Gabriella ..."
Aliita Tristan baada ya kumuona Gabriella
" Dad anafanya nini huyu hapa ?"
Gabriella alikasirika sana
" Gabriella binti yangu yaliyotokea kati yako na mume wako Tristan yanaweza kuongelewa na kuisha "
alisema Mr Alphonse
" Yeye sio mume wangu baba au umesahau kuwa alinipa talaka tena kwa kunilazimisha sitaki kumuona hapa nataka aondoke Sasa hivi " Gabriella alipanda ngazi za kuelekea vyumbani Veronica alimfuata nyuma waliingia kwenye chumba Cha Gabriella
" Gabby punguza hasira unaweza kupata shida kumbuka umebeba maisha ya kiumbe kingine tumboni kwako "
Wakiwa wanaongea hayo kumbe Tristan alikuwa mlangoni alimfuata Gabby nyuma
" Ina maana Gabriella ni mjamzito ?"
Tristan alikosa Raha aliamua kurudi sitting room lakini hakusema alichokisikia chumba kwa Gabriella
" Naumia sana Veronica kwasababu hadi baba yangu Sasa Yuko upande wao sijui hata nifanye nini kuondokana nao "
" Mimi nakushauri usimwambie mtu yoyote kwanza kuhusu ujauzito wako tusubiri huenda maverick akarudi "
" Usitake jina la huyo mshenzi mbele yangu nitajua mwenyewe nipambane vipi kuondokana Tristan na kumtunza mtoto wangu "
Veronica alimuaga Gabriella akaondoka
" Tristan kijana wangu usiwe na wasiwasi ilhali umeshalijua kosa lako na umeomba msamaha basi Gabriella atakusamehe tu na mtarudi kuwa mume na mke kama zamani " alisema Mr Alphonse
" Asante sana baba ,nitaenda kujaribu kuongea nae "
Tristan alienda chumbani kwa Gabriella
"Umekuja kufanya nini chumbani kwangu ?"
" Nataka kuongea na wewe nataka kukuomba msamaha mke wangu "
" Tristan sikutaki nenda kaendelee na maisha yako siwezi kurudiana na wewe Kuna vikwazo vingi mbele yetu toka nje "
Gabriella alifungua mlango ili Tristan aondoka
" Vikwazo vipi kama huyo mtoto uliyembeba tumboni mwako au Kuna kingine "
Gabriella alishtuka sana alifunga mlango haraka
" Umejuaje kama mimi ni mjamzito ?"
" Hilo halina umuhimu nataka tu kukwambia nitalea huyo mtoto kama mtoto wangu na umsahau baba wa huyo mtoto "
aliongea Tristan bila aibu....
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments