NAKUPENDA BILA MIPAKA 36 - 45
:36
Sijapenda kabisa, binti alisema wanapika kwao, ina maana wewe huli kabisa huko nje kwasababu una uwezo au ni kwasababu gani. Kumbuka na wewe hapa umeajiriwa kwaajili yangu, kwanini haujali hisia zangu.”
Nikaona eenh kumbe mama ana maanisha, nikasikia dokta anasema “lakini mama sikujua kama una hamu namna hiyo na maandazi. Sio kwamba hutakiwi kula lakini kwa usalama wako mama yangu.
Kama unapenda sana bora tuone hapa wanapika kwa usafi. Nisamehe mama, sikujua nitakukwaza na unajua hutakiwi kukwazika si ndiyo mama.”
Nikaona nisije sutwa mie nikaondoka zangu. Sijui waliongea nini zaidi ila baada ya dakika kadhaa dokta alitoka amekasirika hata macho yake naona kabisa amekasirika.
Halafu alinitazama na kunipa Ishara nimfuate. Nilimfuata kwa hofu, alikuwa anaelekea chumba changu cha kubadilisha. Nilipofika alisimama kwa hasira akanitazama akisema “umemwambia nini mama?”
Nilimtazama na kusema “sio kitu dokta, aliulizia maandazi nikamwambia sijabeba.”
Alishusha pumzi na kusema “Nazwi upo hapa kikazi. Fuata kilicho kuleta.
Habari za umbea maneno na mgonjwa wangu sitaki sijui unanielewa. Yule ni mgonjwa hatakiwi kusumbuliwa unanielewa binti. Umekuja kufanya kazi sio kugombanisha watu.”
Nikamtazama na kusema “nimekuelewa dokta ndiyo nipo nafuata kilicho nileta.”
Akanitazama, akanipandisha, akanishusha halafu akanisonya akawa anatoka. Eenh mimi hapo nasema “ya leo kali, ya moto haswa sasa kwani nimekosea wapi. Mboba jeuri sana huyu dada.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:37
Nilijikuta najisikia tu vibaya hata ile hali ya kazi nayo ikanitoka. Nikawa sasa sina la kufanya natakiwa kurudi tu chumbani kwa mama.
Niliporudi, nikawa sio yule mchangamfu tena ingawa nikawa najitahidi sasa. Nilianza kumuweka mama sawa. Nikamvalisha nguo nzuri na kusema “umependeza sana mama.”
Alinitazama tu ni wazi aligundua sipo sawa, nilitabasamu na kukusanya pale nguo na kuweka kitanda safi kabisa. Baada ya hapo nikamrudisha mama kitandani vizuri na kuweka kiti mwendo mahali pake.
Baada ya hapo nikawa naendelea na mambo mengine na hapo dokta aliingia. Alipoingia alisema kwa furaha “sasa mama kuna sindano inabidi nikuchome ndiyo niende.”
Nipo hapo naendelea na kazi, yule mama alisema “usijali binti yangu, Nazwi atanichoma wewe kaendelee tu na kazi.”
Niligeuka kutazama, unajua jicho nimepigwa, nilipigwa jicho ambalo sijawahi kupigwa, alinitazama kwa jicho la ukali na uchungu. Ikabidi nijifanye najali mambo yangu tu kwa maana haya yanaendelea hapa hayanihusu ndewe wala sikio(hayanihusu kwelikweli).
Nilisikia Dokta ananiita kama hajachukia vile, hapo kama naona moyoni anavyosema “huyu nesi ananichukulia nafasi yangu kwa mama.”
Nikaitikia kwa adabu “abee dokta.”
Nikafika pale na yeye alinipa maelekezo juu ya hiyo Sindano, halafu akamuaga mama kwa upendo kisha alipogeuka na kunikata mimi hilo jicho, mpaka naogopa. Aliondoka zake.Nami nikashusha pumzi nikijiongelesha pale ili tu mama asijue lolote linaendelea pale.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:38
Mama alinitazama akisema “mwanangu unachoma sindano vizuri sana, akinichoma yeye hapa nitaumwa mkono wiki zima unichome mwanangu.”
Nilitabasamu tu.
Nilimchoma mama sindano, akanitazama akisema “sasa je umenichoma hata sijui kama umenichoma. Nashukuru sana mwanangu.”
Nilimtazama na kusema “usijali mama, nitakuchoma mara zote nitakazo kuwa hapa.”
Mama alitabasamu tu, nikaendelea na mambo yangu. Basi nikahakikisha mama anakuwa sawa.
Nilihakikisha amekula vizuri, amepata dawa zake, yeye alikuwa anafurahia. Sasa wakati tumemaliza kila kitu mama alinitazama na kuniuliza “Upo sawa mwanangu?”
Nilimtazama na kusema “nipo sawa mama wala usijali.”
Alinitazama na kusema “amekufokea na kukutisha eenh?”
Nilitabasamu na kusema “hapana mama, ni sawa kila kitu kipo sawa.”
Huyu mama alitikisa kichwa na kusema “Unajua mwanangu nikuambie kitu?”
Nilimtazama na kusema “niambie mama yangu.”
Alitabasamu na kusema “hakuna kitu kizuri kwenye haya maisha kama unyenyekevu na hekima. Vitu hivi unaweza kuona ni vya kawaida sana hata havina maana na mbaya zaidi hivi vitu huwezi kuigiza hata ukijaribu ni kwa siki chache sana.
Unajua ni ngumu kwasababu vitu hivi vinaleta neema nyingi sana kwenye maisha yetu. Neema nzuri za kupendeza machoni pa watu na Mungu. Lakini mbaya zaidi watu wengi hawana hivi vitu.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:39
Wote hatufanani kila mmoja ameumbwa kwa namna yake na hii ndiyo inatufanya tuwe tofauti. Usijali kuhusu Dokta.Chochote akikuambia usiweke moyoni kabisa, ni mtu wa kujiona yupo sawa muda wote. Ni binti yangu wa muda mrefu sana, namfahamu hanisumbui akili.”
Nilitabasamu na kusema “nimekuelewa sana mama. Nashukuru sana kwa maneno yako mazuri. Lakini mimi nipo salama kabisa.Nakuahidi sitasumbuka kabisa.”
Akatabasamu na kusema “sasa kesho ole wako usilete maandazi. Nitakasirika. Sitakula kabisa. Nakuambia.”
Nilicheka nikisema “mama jamani, nitakuletea usijali.”
Mama alitabasamu na kusema “nilale kidogo sasa.”
Nilimtazama na kusema “ni kweli mama, pumzika kidogo.”
Basi nilisogea kwa mama na kumlaza vizuri halafu nikawa natoka sasa kwenda kupeleka sahani kwa dada Maria.
Aliponiona alitabasamu, nikamuuliza “dada Maria mbona tabasamu hivyo kuna nini?”
Alinitazama na kusema “Mdogo wangu, natamani ungekuwepo jana. Boss aliponiuliza kuhusu wewe na utendaji wako kazi.”
Nilimtazama na kusema “eenh ikawaje?”
Alitabasamu na kuendelea “kitendo cha kusema mama amekula asubuhi, amekula mchana na jioni hajaamini. Unajua amebaki anatabasamu, akaenda kwa mama yake kuzungumza naye wametumia muda kweli. Alifurahi sana.”
Nilitabasamu nikisema “weee usiniambie, ina maana huwa hafurahi?”
Dada Maria akasema “weee, hivi unaona ile sura ndugu yangu au unaongea tu hapa. Ananuna balaa.”
Nikacheka, halafu akatazama huku na kule akisema “vipi dokta naye.”
Nilishusha pumzi sikutaka mengi nikasema “mambo ya kazi tu.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:40
Alitabasamu akisema “namfahamu vizuri, Na wivu balaa. Dokta utasema hapa ndiyo kwao. Anavyompenda Boss sasa humwambii kitu, unajua nini sasa. Boss hata muda naye hana.
Basi yeye pale ndiyo aonekana anamtunza sana mama, mara hivi mara vile si unajua tena aonekane ana jali eenh. Kwahiyo kuwa mvulimivu maana mwenzako kwa jino na ukucha (kwa kila njia)anatamani aolewe hapa.”
Nilimtazama Da maria nikisema “wee usiniambie!”
Alicheka akisema “ndiyo hivyo mdogo wangu.”
Nikashusha tena pumzi ndefuu ili nipate afua.
Akanitazama na kusema “Kiukweli jana Boss alifurahi sana. Mimi pia tunashukuru sana. Tafadhali usimzingatie huyo Bi mzuri.”
Nikatabasamu na kusema “dada Maria lakini.”
Tukacheka tu.
Basi nikaweka vitu jikoni nikiwa na amani kabisa.Nikarudi zangu sehemu yangu ya kazi kuhakikisha namalizia kila kitu. Nilikuwa nafanya kila kitu vizuri sana. Nikafua nguo za mama.
Nikamuweka safi kabisa na baada ya hapo mama alipata chakula cha jioni, na bado alipata na dawa. Sasa ile jioni aliniuliza “Nazwi mwanangu umejiandaa vipi kuhusu suala letu.”
Nikamtazama na kumuuliza “suala letu, suala lipi tena mama?”
Alitabasamu na kusema “ushasahau jamani, kuhusu kusali.”
Nikatabasamu na kusema “mama jamani, nakumbuka. Na jana tu nimefikiria. Nitajifunza, nitakaa karibu na Mungu nakuahidi.”
Alinitazama na kusema “mama yako lazima atakuwa anajivunia sana wewe. Ni binti mzuri sana. Mwanangu, ukitaka kuishi siku nyingi, maisha marefu sana na furaha kuwa karibu na Mungu.”
Nilimtazama na Kumuuliza “ina maana wewe mama unampenda sana Mungu.”
Alinitazama akaniambia “ninampenda mwanangu, sio mara zote nakuwa karibu naye. Upo wakati kwasababu ya maumivu, mateso ya magonjwa na mambo mengi ya maisha nakaa mbali naye.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:41
Lakini Mungu ana mambo mengi sana. Ukiwa karibu naye na ukijiweka kwake hakuachi upotee kirahisi. Mara zote hunifuata popote pale na kunirudisha kwake. Unajua mimi peke yangu ndiyo naamini hivi. Mwanangu kipenzi wakati mwingine anachoka na kuniona napoteza muda.
Na kabla ndugu zangu walikuwa wananichukua na kunipeleka kwa waganga eenh wakati huo hali ilikuwa mbaya zaidi. Siku moja niliona namkosea tu Mungu leo huku kesho kule. Niliamua kusimama na Mungu ndiyo kupata hii nafuu hata sasa nipo hapa. Unajua nilikuwa siongei kabisa.”
Nilimtazama na kusema “ooh jamani mama, kumbe umeteseka sana.”
Akasema kwa upole “ndiyo maana sasa nakuambia, kaa karibu na Mungu utajiepusha na mengi sana.”
Nilimtazama Kisha nikatazama saa ya ukutani.
Huyu mama aliniuliza “umechoka kukaa hapa?”
Nilimtazama na kusema “nawezaje mama ikiwa unanipa elimu nzuri namna hii. Kusema kweli mama, Nina hofu sana kuhusu mtoto wangu.”
Alinitazama na kusema “hii ndiyo nguvu ya mama. Muda nao umeenda naona dokta wako hajafika mpaka sasa ili ukamuone. Kachukue simu yako emu.”
Nilishusha pumzi, na haraka nikainuka na kufuata simu yangu Kisha nikarudi chumbani kwa mama. Nilikuta simu imeita sana. Alikuwa ni mama yangu.
Halafu akanitumia ujumbe “mwanangu ilikuwa ni homa. Tumepumzishwa hapa jirani na nyumbani. Lakini sio muda natoka.”
Ujumbe ulikuwa ni wa saa 12.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:43
Muda huu ilikuwa inaenda saa mbili. Nilipiga hakupokea. Mama mgonjwa akauliza “eenh kuna nini?”
Nikamwambia mama huyu “walimpumzisha lakini saa 12 alisema wanajiandaa kutoka.”
Akaniambia kwa upole “Tulia sasa, mama anajua anachosema. Kila kitu kitakuwa sawa.”
Nilikaa kwa upole, wakati huo Dokta aliingia, niliinuka na kumsalimia akawa anatabasamu huku akimchangakia mama.
Na mama naye anamjibu vizuri tu. Kisha aliniuliza Mimi kuhusu maendeleo ya mama. Vile namjibu tu simu yangu iliita. Mungu wangu, dokta aliacha alichokuwa anafanya akanitazama na kuniuliza “Nazwi Ina maana hukuelewa?, unawezaje muhudumia mama na ukiwa busy na simu yako. Chuo ulichosoma ndiyo walikufundisha hivyo?”
Nilimtazama kwa upole na kusema “nisamehe sana Dokta. Sitarudia tena.”
Akanitazama na kusema “nachukia sana kuombwa msamaha, unajua kwanini?, watu kukosea makusudi na Kisha kuomba msamaha. Msamaha bila mabadiliko sio msamaha.”
Yaani mpaka nakosa la kusema hapo ni simu tu imeita, hata mama alisema “Nazwi Binti yangu, Mimi ndiyo nilimruhusu atumie simu Baada ya kuona mnachelewa kurudi na ameacha mtoto anaumwa.”
Alishusha pumzi, alinitazama na kusema “mama yangu, usijali lazima nimuelekeze.”
Mama alinitazama, Kisha alimtazama akisema “taratibu sawa mwanangu.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:44
Alitabasamu na kusema “Unaweza kwenda kubadili sasa umuwahi mtoto.”
Haraka nilitoka, Nilifika kwa chumba cha kubadili nikashusha pumzi na kujiambia “Siku ya Leo aiseee.”
Nikampigia simu mama yangu. Mama alipokea akisema “mwanangu ondoa hofu tushatoka nipo naye hapa nyumbani. Alikuwa anacheza cheza saizi naona tena amelala. Vipi bado tu.”
Nikasema kwa upole “ndiyo natoka mama.”
Akaniambia kwa upole “jitahidi uwahi Labda akikuona atafurahi.”
Nilitabasamu, na haraka nilianza kubadili nguo zangu.
Baada ya kumaliza Mimi nikaenda chumbani kwa mama.
Nilipofika nilikuta mama, dokta na Mr Gallen. Nikasalimia “Shikamoo Boss.”
Alinitazama na kusema “marahaba.”
Sikutaka maneno mengi, nilisema “mama uwe na mzuri, Mimi naenda.”
Mama alinitazama na alisema “usisahau ulichoniahidi na sasa kesho ukija uje nayo si ndiyo?”
Nilitabasamu, Mr Gallen akawa haelewi, Dokta ananitazama kwa dharau Mimi hata najali sasa. Nikasema “nakuahidi mama.”
Mama alisema “kesho uwahi mwanangu.Uwe na mwema msalimie sana mama.”
Nilitabasamu na kuanza kuondoka.
Natoka huku nasema kimoyomoyo “huyo Mr Gallen ndiyo alifurahi mbona sioni hiyo furaha.”
Wakati najisemesha Dada Maria akasema “nesi ndiyo unaondoka?”
Nikatabasamu na kusema “Uwe na usiku mwema dada.”
Akaniambia kwa upole “Amen mdogo wangu, usiku mwema.”
Basi vile natoka na muamala ushasoma nikawa na furaha kwelikweli. Nilianza safari huku Naomba Mungu mwanangu asiwe tu amelala.
Safari haikuwa rahisi nilichelewa kweli kufika, Ila kwa bahati nilikuta mama yake Dee na Dee wapo nyumbani na Dee anambembeleza mwanangu alikuwa analia. Nilipofika tu nikamchukua mwanangu huku nikimbembeleza, alikuwa Hana raha lakini homa ilikuwa imeshuka.
Basi nikasalimia huku nabembeleza mwishowe Priya alilala. Mama na rafiki yake walikuwa nje Mimi nikasema “mama wacha nilale naye tu Leo.”
Mama alinitazama akitabasamu na kusema “ni sawa mwanangu.”
Nikaingia chumbani, mama alinifuata na kuniambia aliazima pesa mahali hivyo tunadaiwa nikasema “sawa mama hakuna shida.”
Wakati anatoka na Dee aliingia.Nilisema “Karibu kipenzi, Asante kwa kumsaidia mama.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:45
Akatabasamu akisema “niliposikia anaumwa hatujaweza kukaa nyumbani. Vipi lakini upo sawa?”
Nilimtazama na kusema “nimechoka, nimepata tu kazi na mwanangu anaanza kuumwa kweli?”
Alinitazama na kusema “rafiki yangu Mungu akikupa Neema anakupa na majukumu yake. Kwahiyo usijisikie vibaya furahia vipi angeumwa huna mia.”
Nilisema kwa upole “usiseme hivyo.”
Akanitazama akisema “nakujua wewe, shida nini?”
Nilimtazama na kusema “Acha tu si huyo Dokta Leo Ana foka bila hata sababu yaani hata simuelewi. Naona ananipa wakati mgumu kweli.”
Rafiki yangu akasema “unajua hawa watu wenye pesa wana matatizo sana. Usiwe karibu naye sana, Fuata vile anataka kaa naye mbali muhimu kazi yako.”
Nilishusha pumzi, Mara ujumbe ukaingia kwa simu. Alikuwa dokta kabale, alichokiandika sasa rafiki yangu hapo ananitazama kaandika “kesho usije kazini nitakuwepo mwenyewe mpaka nitakapo kujulisha.”
Dorice akaniuliza “kuna nini tena?”
Nikajisemea “Kumekucha shooo, huyu dokta Kama chawi.”
Basi Nikampa simu Dorice akaanza kusoma Kama Hana meno vile “kejo usije kazhini nitakuwepo mpaka nitakapo kujulisha.”
Nikacheka na kusema “Ana hekaheka.”
Dorice akasema “au ana mtaka boss huyu?”
Nikacheka nikisema “haswaaaa nacho kasema dada wa kazi.”
Tukacheka sana huku Dorice akisema “ana hofu utamchukua au, mbona kazi anayo na mama tunaye tunatamba naye.”
Nikacheka na kusema “rafiki yangu huyo boss na ukauzu ule, ule utu uzima ingawa mzuri Ila apambane sio kuniharibia ugali.”
Dorice sasa alivyonijibu “Una kichaaa?, utu uzima upi, hata ubaba bado, uanko tu atushindwe akitupenda hatumchukui?”
Nilimtazama Dee kwa jicho Fulani halafu, 😂😂😂sijui mpoje siku hizi hamlike wala comment Nisameheni basi mlike na mkomenti kesho nipost😂😂😂
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni