ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5
SEHEMU YA KWANZA
Ni majira ya jioni ikiwa ni muda mfupi tokea ametoka bafuni kuoga kwa ajiri ya kujiandaa aweze kurudi nyumbani mara baada muda wa kazi kuisha, Isabela akiwa amemaliza kujipodoa na kuvaa nguo zake alizotoka nazo nyumbani alimalizia kwa kukunja vizuri nguo za kazi na kuzihifadhi kabatini baada ya hapo akatoka na pochi yake begani kwa ajili ya kuelekea jikoni kumuaga Aunt Nina (housemaid mwenzie, mama mtu mzima aliyemkuta akifanya kazi hapo nyumbani kwa bosslady ) tofauti iliyopo ni kwamba aunt Nina yeye aliishi hapo hapo kwenye nyumba anayofanyia kazi huku Isabela yeye akienda na kurudi nyumbani
Akiwa tayari kwa kuanza safari ya kurudi nyumbani Isabela alitoka chumbani na kwenda jikoni kwa ajili ya kuagana na aunt Nina ambapo aliingia na kumkuta akimalizia kupanga panga vitu kwenye friji
"Aunt Mimi ndio naenda"
"Aah! Ushamaliza sio?"
"Eeh! Kila kitu tayari, hapa nataka niwahi nikamshikie mama kwenye biashara yake"
"aah! Ndio kule kwenye samaki.... Sawa basi wewe wahi, ila kama nilivyokwambia kesho tutakuwa na wageni, watoto wa madam wanarudi nyumbani hivyo jitahidi usichelewe"
Aliongea aunt Nina ila kutokana na haraka aliyokuwa nayo Isabela hakutaka kuhoji Wala kuongeza neno alichowaza kwa wakati huo ni kuondoka kwenda kutafuta usafiri umfikishe nyumbani
"Aah? Sawa basi aunt akija madam utaniagia"
Aliongea haraka haraka akatoka humo jikoni na kuanza kuelekea nje ya geti Kisha bila kuchelewa alifika kituoni akachukua bodaboda na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao huku akiiacha mitaa ya wenye nazo taratibu.
Kutokana na kuondoka jioni sana na ukijumlisha na umbali uliopo akajikuta akifika huko uswahilini mida ya saa mbili kasoro usiku ambapo walishika barabara ya kuelekea maeneo ya sokoni eneo ambalo mamaake anapofanyia shughuli zake za kukaanga samaki ( wakazi wa hapo wamezoea kumuita mama Isabela au mama samaki kutokana na umaarufu wake wa kuuza samaki)
"Shikamoo mama Isabela" alisalimia ila mamaake alimtazama na kuishia kucheka ๐
"Wewe Isabela unajua mjinga, Mimi nilijua nani kumbe ni wewe ndio unaniita mama Isabela๐"
"Aah! Sasa mama si ungeitika lakini" alisema huku akishuka kwenye boda boda
"Hebu acha porojo zako, sogea hapa nikuachie biashara Mimi nataka nikafanye shughuli zangu saa hizi"
Kama ilivyo kawaida alisogea hapo mezani kukabidhiwa biashara Kisha mamaake akaondoka kurudi nyumbani, Isabela akachukua nafasi ya kuwahudumia wateja, ukizingatia alivyo shapu kwenye suala la kazi na hivi wateja wanapenda wakiona msichana yupo hapo basi haikuwa shida kuwapata na walikuwa wakimiminika haswa,
Usiku huo Isabela akawa yupo kijiweni karibu kabisa na kituo Cha basi akihudumia wateja wa samaki mteja akishatoka anatoa simu na kuanza kuperuzi akichoka anakaa kutazama pilika pilika zinazoendelea hapo sokoni upande wa pili wa barabara waliokuwa upande huo walikuwa wakitazamana nalo uso kwa uso.
Na baadae wadogo zake wote watatu walifika kuja kumpa kampani Hadi pale usiku ulipozidi walifunga biashara na kurudi nyumbani kukabidhi mahesabu kwa mama Yao.
Kwa kifupi hayo ndio maisha waliyokuwa wakiishi kina Isabela kama familia maskini, wakitegemea biashara ya mama yao ya kuuza samaki na kazi ya baba Yao ya ufundi seremala jitihada ambazo ziliishia katika kuipatia familia mahitaji ya msingi tu na si vinginevyo.
.............................................................................
Muda ukiwa umesogea sana Isabela ndio ameingia chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika ghafla anakutana na ujumbe kwenye simu yake akaangalia na kukuta umetoka kwa aunt Nina
"Isabela usisahau kesho ni siku ya kuwahi tafadhali usipuuze"
" Aunt bwana Mimi nilijua Nini kumbe kuwahi kazini Sasa si alishaniambia.... Kwa hiyo hao watoto wa madam ndio wanamshughulisha kiasi hicho ๐....
eeh! Mimi kama ni hiyo Hela Bora niikose kuliko mambo ya Kusumbuana Yani usumbufu ndio sitaki kabisa nitafanya kazi kuendana na ratiba zangu sio atokee mtu anipangie kisa yupo kwao๐..."
alijiongelesha moyoni huku akiwaza kuhusu hao watoto wa boss wake ambao hakuwahi kuwaona kabla tokea aanze kazi miezi mitatu iliyopita ni kina nani? Wapoje? Wana umri gani? Je tunalingana? Hayo ndiyo maswali yaliyosumbua kichwa cha Isabela kwa muda huo
ITAENDELEA........
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA:
" Aunt bwana Mimi nilijua Nini kumbe kuwahi kazini Sasa si alishaniambia.... Kwa hiyo hao watoto wa madam ndio wanamshughulisha kiasi hicho ๐....
eeh! Mimi Bora kama ni hiyo Hela Bora niikose kuliko mambo ya Kusumbuana Yani usumbufu ndio sitaki kabisa nitafanya kazi kuendana na ratiba zangu sio atokee mtu anipangie kisa yupo kwao๐..."
alijiongelesha moyoni huku akiwaza kuhusu hao watoto wa boss wake ambao hakuwahi kuwaona kabla tokea aanze kazi miezi mitatu iliyopita ni kina nani? Wapoje? Wana umri gani? Je tunalingana? Hayo ndiyo maswali yaliyosumbua kichwa cha Isabela kwa muda huo
ENDELEA.......
Aliwaza kwa muda Fulani mwisho akapitiwa na usingizi , kesho yake akaja kushtuliwa na pilika pilika za mama Isabela akijiandaa aelekee feri kuchukua samaki,
"Kwani saa ngapi saa hizi, mbona kama mama kawahi sana"
kwa haraka aliiwahi simu yake na kuangalia muda akakuta ndio kwanza inakaribia saa kumi na moja alfajiri,
"mmh! Bado mapema sana" aliwaza huku akivuta shuka ajifunike vizuri ghafla akashtukia mamaake akiingia chumbani
"Wewe Isabela kumbe upo macho"
"Hamna mama ndio kwanza nimeshtuka saa hizi"
"Basi Mimi ndio natoka ikifika saa kumi na mbili hao watu waamke waende shule"
Alitoa maagizo mama Isabela Kisha akaondoka kwenda kutafuta usafiri wa kumpeleka feri, Isabela akaona ndio muda wa kuanza kuutafuta usingizi kwa mara nyingine hazikupita dakika akaja kupitiwa hata hakujua ni muda gani wadogo zake Miriam na Jayden waliamka kujiandaa kwenda shule.
Baada ya muda akaja kukurupuka tena jua limeshawaka tena ni kwa vile Brian amemshtua baada ya kugundua kuwa hajaamka kwenda kazini, basi alishtuliwa na sauti ya mdogo wake huyo anayemfata akawa amekurupuka kutoka nje na nakutana na Brian mlangoni
"Sister kwani Leo kazini Huendi"
"Naenda, nilijisahau kidogo"
"Basi Mimi nilihisi labda umeondoka ila nikawa sielewi elewi"
"Dah! Hata sijui nilijisahau vipi wakati niliamka mapema tu, kwani baba ameshaondoka"
"Ameshaenda muda tu, Mimi nikajua na wewe umeshaondoka kumbe upo ndani"
"Nilipitiwa, ila Acha nijiandae niondoke nitawahi tu"
Aliongea haraka na kurudi ndani kujiandaa Kisha akatoka na khanga shingoni pamoja na mswaki Ili aende akaoge mara anafika nje anakuta mazingira yameshafanyiwa usafi huku ndani sakafu imeshadekiwa kuonesha ni jinsi gani amelala sana.
Bila kupoteza muda aliingia bafuni kuoga Kisha akarudi kujiandaa haraka haraka baada ya hapo alimuaga Brian na kuondoka kuwahi kibaruani, kwa bahati nzuri kwa muda huo usafiri huwa hausumbui wengi wameshaondoka alfajiri kuelekea makazini hivyo magari ni ya kumwaga, hivyo alipata basi la haraka haraka hatimaye akafanikiwa kufika huko kwenye mitaa ya wenye fedha zao akashukia kituoni na kuanza kutembea kwenye eneo Hilo lenye utulivu wa Hali ya juu, kila nyumba imejifungia ndani ya geti ukipita kwenye barabara za mitaa ni wewe tu na magari binafsi unayopishana nayo.
Hakukuwa mbali sana na barabarani, ndani ya dakika chache akajikuta ameshafika kwenye geti la nyumba ya kifahari ya bosslady (mwanamama mwenye pesa zake mjini, kama ni pesa basi huyu mama amejikamilisha) . Kwa vile alikuwa mwenyeji haikumpa shida alifika tu na kufungua geti Kisha akaingia ndani na kukutana na mlinzi akiendelea na shughuli zake ambapo walipeana salamu ya kishkaji Kisha Isabela akapita kuelekea ndani na kupitiliza chumbani kwa aunt Nina kubadili nguo, hatimaye akatoka akiwa na mavazi rasmi ya kazi na kwenda moja kwa moja jikoni alipo aunt Nina , muda huo Aunt Nina akiwa bize na kazi zake humo jikoni ghafla akashtuliwa na salamu
"Shikamoo aunt" alisalimia Isabela na kufanya aunt Nina ageuke kumtazama
"Marahaba Isabela, ndio unaingia saa hizi, si nilikwambia uwahi wewe leo tuna wageni"
"Yani sijui hata nilipitiwa Vipi, kwa kweli unisamehe tu aunt yangu"
"aah! Mimi Sina neno, Ili mradi umekuja basi sio mbaya... nimeshakutayarishia nyama nimeiweka jikoni, wewe andaa upike pilau kwa ajili ya wageni ndio maagizo niliyopewa"
"eeh! Pilau tena!... Kwani hao watoto wa madam wameshafika!?๐"
"Ehee! Wamekuja Jana usiku, kwani hujapata taarifa"
"Nijulie wapi Mimi... Sasa Mchele nipime kiasi gani aunt, kwani hao wageni wenyewe wako wangapi?"
"Wewe ni mtaalamu Isabela, zunguka huko nyuma ukawaangalie halafu utajua upike kiasi gani".
"mmh! Basi ngoja nikawaone kwanza Nisije nikajichanganya"
Alisema huku akitoka humo jikoni na kuanza kupandisha ngazi Ili akawaangalie vizuri kupitia juu akihofia kuzunguka huko nyuma ya nyumba na watu wenyewe hawafahamu mmh! Kazi kweli kweli , basi alipandisha ngazi na kutokea upande wa nyuma ya nyumba akafanikiwa kuwaona vijana watano wako kwa chini wamekaa wakipiga stori , kwa kuwaangalia tu muonekano wao akajua hawa ndio wale wale (Koo za kitajiri)
" Kumbe ni wakaka wakubwa tu kuliko hata nilivyofikiria, Yani Bora hata nilivyokuja huku juu sijui ningetoka huko ingekuwaje"
Alijiongelesha moyoni na kugeuka kutaka kurudi ndani ghafla akajikuta akisita na kurudi kusimama hapo juu akiwatazama
"Kwani wanaongea kuhusu nini" aliwaza moyoni Ile anakaa vizuri asikilize wanachoongea ghafla akaona wamebadili lugha na kuanza kuongea kiingereza
"mmh! Acha nikafanye yanayonihusu naona hapa hapanifai Tena" aliwaza moyoni na kugeuza kurudi jikoni na kukuta aunt Nina anamalizia kumpangia viungo
"Vipi umeshawaona"
"ehee! Nimewakuta"
"Ushawahesabu na kujua unapika kiasi gani"
"Ehee! Wapo watano"
"Ok! Basi sawa, Mimi nakuachia hapa ila usisahau kutujumlisha na sisi wenyewe na mlinzi na pia madam anaweza akaja na mgeni kwa hiyo uongeze kidogo"
"Sawa aunt"
"Ok! Mimi nipo chumbani"
Aunt Nina akiwa amemaliza kutoa maagizo yake akatoka humo jikoni Sasa Isabela ndio akawa na jukumu la kuandaa chakula Cha familia nzima Yani wenyeji waliokuwepo na wageni waliokuja, haikuwa kazi rahisi, ila ilibidi ifanywe vile inavyostahili ili asilaumiwe na wageni waridhike maana hofu yake kubwa ilikuwa ni kuhusu wageni wakaka wa watu wamefunga safari kutoka nje ya nchi Kuja nyumbani kwao halafu wapikiwe vitu visivyoeleweka,
Basi akawa anaandaa huku akiwaza hili na lile ilifika muda akaanza kuwafikiria hao wakaka
"Mmh! walivyo smart vile halafu ni kama wanafanana vile au ni akili yangu tu ndio
inaniambia hivyo ๐"
"Ina maana wale wote ni watoto wa madam๐... Sasa mbona kama wanalingana!?, kwa hiyo siku zote hizo walikuwa nje ya nchi"
Alijiuliza na kujijibu mwenyewe mwisho akaona hayo hayamuhusu afanye kilichomleta akawa bize na kazi yake hatimaye msosi ukawa tayari kwa kuliwa Sasa limebaki jukumu la aunt kuja kukagua hivyo aliweka Kila kitu sawa na kutoka jikoni kwenda kumuita aunt Nina chumbani kwake
"Aunt..... Mwenzio tayari nimeshaplay part yangu" alisema huku akijilaza kitandani na kufanya aunt Nina atake kucheka ๐คฃ
"Unajua wewe Isabela una vituko, kwa hiyo ndio umeona ulale kabisa"
"๐คฃ๐คฃ aunt bwana niache mwenzio, we unafikiri mchezo kuandaa chakula Cha wageni"
"aah! Wageni wapi sema tu hujawazoea, wale kina Nick nao ni wageni"
"Aunt sema tu wewe umewazoea ndio maana unaona kawaida, Mimi mwenzio nahisi joto tu hapa"
"Wasiwasi wako tu... Kwanza hebu inuka hapo twende ukawatengee chakula muda unaenda"
Akasema huku akifungua mlango kutoka nje, ikabidi Isabela ainuke na kufatana nae huko jikoni, aunt akafikia kukagua kile na kuishia kusifia sifia hapo Kisha alimwachia Isabela jukumu la kuandaa meza wakati yeye anamalizia kupakua,
Kwa upande wake Isabela alitoka hapo na sahani zikiwa kwenye tray na kuelekea dining, akawa anatembea taratibu huku yupo bize akiangalia sahani zisidondoke bila Kujua kama Kuna watu wameshakaa hapo mezani wanamtazama anavyokuja ghafla akainua uso kuangalia mbele mara akashtuka kuona wale vijana wapo kimya wakimtazama ghafla akajikuta akihisi uoga na kuanza kutetemeka, aibu si aibu akatamani hata ageuze kurudi jikoni ila ndio alishafika na wameshamuona hana jinsi Tena ikabidi ajikaze afikishe hizo sahani, alifika tu na kuweka sahani kiuoga uoga na kuondoka haraka haraka Kwenda kuingia jikoni huku akihema kwa nguvu na kufanya Aunt Nina ashtuke
"Wewe Isabela una Nini?๐"
"Hamna kitu aunt๐"
"Hamna kitu na unahema hivyo, kwani Nini kimetokea huko nje" akahoji huku akimalizia kupanga mahotpot vizuri
"Skia, malizia kupeleka Kila kitu uje uchukue na haya mahotpot uwapelekee"
"Ila aunt twende wote unisindikize๐"
alitamka na kufanya Aunt Nina abaki akimshangaa ,
"Ila Isabela๐....ok! sawa hakijaaribika kitu beba hiyo tray twende"
Akamkabidhi tray ikiwa na glass na jagi la juisi Kisha na yeye akabeba mahotpot wakaongozana pamoja kuelekea dining, safari hii kidogo Isabela alipata ujasiri japo alikuwa kimya sana ila alifanikiwa kuwaandalia Kila kitu huku akikwepesha kumtazama mtu usoni maana alishaona hao vijana walikuwa wakimuangalia sana
Basi akawa anamalizia kuandaa kuja kutahamaki aunt Nina ameshatoka hapo dining hakujua ameondoka saa ngapi , kitendo Cha aunt Nina kutoka hapo kikafanya akose Tena ujasiri na kuanza kufanya haraka haraka akahakikisha Kila kitu Kiko sawa akageuka kuanza kuondoka ghafla akashtukia akiitwa Tena
"Isabela hebu subiri mara moja" ilikuwa sauti ya kiume iliyoita kwa ujasiri sana na kufanya Isabela ashtuke
"uuh! Nini tena๐ฅบ" alijisemesha moyoni huku akigeuka kumsikiliza
"Nahitaji unimiminie maji kwenye glass"
akasema huyo mkaka ambaye kwa muonekano tu alionekana ni mdogo kuliko wenzie, kwa upande wa Isabela akaona Isiwe tabu akachukua glass na kummiminia maji Kisha akamkabidhi huyo mkaka na kutaka kuondoka ghafla akashtukia akizuiliwa na mwingine
"Samahani na Mimi nilikuwa nahitaji matunda, naomba ukaniandalie....."
ITAENDELEA....
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA:
"Isabela hebu subiri mara moja" ilikuwa sauti ya kiume iliyoita kwa ujasiri sana na kufanya Isabela ashtuke
"uuh! Nini tena๐ฅบ" alijisemesha moyoni huku akigeuka kumsikiliza
"Nahitaji unimiminie maji kwenye glass"
akasema huyo mkaka ambaye kwa muonekano tu alionekana ni mdogo kuliko wenzie, kwa upande wa Isabela akaona Isiwe tabu akachukua glass na kummiminia maji Kisha akamkabidhi huyo mkaka na kutaka kuondoka ghafla akashtukia akizuiliwa na mwingine
"Samahani na Mimi nilikuwa nahitaji matunda, naomba ukaniandalie....."
ENDELEA......
Alitamka mkaka mwingine ambaye alionekana kama alitaka kufanana na huyu aliyeomba maji japo sio sana, kwa upande wake Isabela aliona kama usumbufu akahisi kama wanamfanyia kusudi ila hakuwa na jinsi atafanyaje na ndio jukumu lake na wao ndio maboss ikabidi arudi jikoni akaandae matunda kwa ajili ya huyo kijana mwingine
"Kusumbuana tu, mtu juisi nimeandaa kwa matunda halafu Kuna mtu bado anataka aandaliwe matunda mfyuu! "
alijiongelesha huku akiingia jikoni na kuanza kutoa matunda kwenye friji akitaka kuandaa mara akaingia aunt Nina na kukuta yuko bize akifanya hiyo kazi
"aah! Wewe Isabela hayo matunda ya Nini Tena Mimi nilijua unaandaa chakula tuweze kula"
"Wewe endelea aunt, Mimi kuna mkaka kaniagiza nimuandalie matunda"
"Kaka gani huyo kakuagiza umuandalie matunda!?๐"
"Si ni yule kakaa peke yake kule mwisho"
"ah! Atakuwa Antony huyo ndio Huwa Hali chakula bila kuwepo na matunda ..... sikia wewe achana na hiyo kazi, Kuna matunda nilishayaandaa Toka asubuhi yapo humo kwenye friji wapelekee na uwaambie kabisa aunt Nina kasema muache kunisumbua"
Aliongea kiutani utani ila Kwa upande wa Isabela aliona ni ukweli kuwa hao vijana walishaanza kumsumbua, basi ikawa nafuu kwake akafungua friji kutoa hayo matunda akapeleka mezani Kisha akawahi haraka kurudi jikoni ilipo kampani yake ambapo alikuta aunt Nina ameshamuwekea chakula kwenye sahani yeye jukumu lake likawa ni kufakamia tu.
Tofauti na ilivyo siku zote, siku hii Isabela hakukaa sana kazini na pia hakuwa na ukaribu na mtu yeyote zaidi ya aunt Nina , hivyo muda mwingi alikuwa chumbani kwa aunt wakipiga stori zao wanazozijua wenyewe Hadi pale ilipofika jioni akajiandaa na kuondoka kurudi nyumbani huku akimuachia aunt Nina jukumu la kuandaa mlo wa usiku.
Kutokana na mawazo aliyokuwa nayo siku hii hakupitia kwenye kijiwe Cha kuuza samaki alienda Moja kwa Moja nyumbani na kufikia kujilaza kitandani kwa uchovu na kuanza kuifikiria siku ya Leo ilivyoenda vibaya
"Kwa hiyo wale wote watoto wa madam, duh Mimi ndio nitakuwa napikia mibaba yote ile.... Yani wanaume watano๐, ila madam nae Sasa kawezaje kuzaa watoto wote wale kwa wakati mmoja, halafu ukiwaangalia kama wote wanalingana ๐ฅบ"
Wakati anawaza hayo ghafla akaja kushtuliwa na sauti ya mama Isabela akimuulizia huko nje akajua kwa vyovyote Kuna kazi anataka aifanye hivyo ikabidi atoke mwenyewe kumsikiliza
"Aah! Isabela kumbe muda wote nakuulizia upo humo ndani"
"Eeh! Nimerudi muda kidogo nilikuwa chumbani"
"Nilitaka uende ukanishikie kuuza samaki na wadogo zako ila pumzika tu Brian ameshaenda"
Alisema mama Isabela huku akiingia jikoni ikabidi Isabela ajiongeze kwenda kumsaidia maana hapo nyumbani kwao hakukuwa na housegirl kila mtu ni mchapakazi Hadi watoto wadogo walisaidia pale wanapoweza.
Tukiizungumzia familia ya kina Isabela iliishi maisha ya kawaida kabisa huku wadogo zake Isabela (Miriam na Jayden wakisoma shule za kawaida Miriam akiwa darasa la Tano na Jayden ndio ameanza chekechea huku Isabela na Brian wamehitimu kidato Cha nne wakiwa wamepitia mazingira hayo hayo wanayosoma wadogo Zao.
*******************************************************************
Kesho yake Isabela aliamkia kwenda kibaruani kama ilivyo ada ila tofauti na ilivyokuwa Jana, siku hii alikuta Hali ya tofauti, hapo kwenye jumba la kifahari alikuta wakaka wawili tu Yani yule aliyeomba ammiminie maji na yule mwingine aliyetaka amuandalie matunda, akatamani kujua sababu ni nini? wale wengine watatu wako wapi? ila mdomo ulikuwa mzito kuuliza kuhusu hao wakaka wengine, hakujua ni uoga wa kuongea au ni ubize aliokuwa nao siku hiyo.
Aliendelea kufanya majukumu yake kama kawaida akamaliza kazi za mchana na kuamua kwenda kupumzika chumbani kwa aunt Nina, muda huo Aunt Nina Yuko bize akikunja nguo zake zilizokuwa zimelundikwa kitandani Isabela akiwa pembeni yake Yuko bize kuwafikiria hao wakaka
"Sasa kama ni watoto wa madam kwa Nini wameondoka... Na watakuwa wameenda wapi ๐"
Aliwaza kichwani mwisho akaona ya Nini kusumbuka na watu wenyewe wapo hapa,
"Acha nikawaulize tu wasiponiambia basi kwani nitakufa"
hapo hapo alinyanyuka kitandani bila kuongea chochote akatoka nje na kwenda Hadi sebuleni kuangalia kama atamuona mtu yeyote kati ya Nickson au Antony ila hakufanikiwa kuwaona
"Sasa na wao wameenda wapi"
alijiongelesha moyoni akatoka sebuleni na kuanza kuelekea getini kwenye chumba Cha mlinzi akawaangalie huko ila kabla hajafika getini mara anamuona Antony akiwa anamtazama kupitia juu ghorofani akiwa nje ya dirisha la chumba chake Cha kulala akiangalia chini upande wa getini, kwa haraka akaghairi kwenda kwa mlinzi na kugeuza kurudi ndani ambapo alipandisha ngazi na kuanza kuelekea upande alipo Antony mara akatokeza na kumkuta Antony Bado ametulia hapo hapo akiangalia nje kabisa ya fensi basi Isabela akaanza kusogea taratibu ghafla Antony akageuka kumtazama mara moja Kisha akaendelea kuangalia nje ya geti bila kusema chochote
"Antony" aliita kiuoga uoga na kufanya Antony ageuke kumtazama, taratibu Isabela akasogea kusimama karibu yake huku akitafuta namna ya kuanza Kisha alijikaza na kuanza kuongea Kwa sauti ya upole
"Eti Antony, kwani wale ndugu zako wengine wako wapi mbona nimekuja hapa sijawaona"
alitamka kwa uoga mara Antony akageuka kumuangalia kwa mara nyingine wakajikuta wakikutanisha macho na kufanya Isabela apate uoga na kuangalia chini kwa aibu
"Ndugu zangu!?... Ndugu wapi hao ambao haujawakuta?" aliongea mara moja na kugeuka kuangalia mbele
"Si wale wakaka wengine mliokuwa nao Jana, mbona wenyewe hawapo?๐"
"Mimi sina ndugu yoyote zaidi ya Nickson"
"Kwa hiyo unataka kusema wale wengine sio ndugu zenu?๐"
Akahoji Isabela kwa mara nyingine ghafla akaona Antony amemkata jicho Kali ikabidi akae kimya๐ฅบ akijitafakari mara anamuona Antony ametoa simu yake na kuweka sikioni akaondoka mahali hapo akiongea na simu
"Ningejua hata nisingemsogelea kumuuliza, mtu mwenyewe anaonekana ana dharau๐..... Sasa nani ataniambia kuhusu wale wakaka wengine ni kina nani au nikamuulize Nickson?๐.... Bwana acha nikamuulize tu na yeye akinishushua basi kwanza kuuliza sio ujinga"
Alijiongelesha huku akitoka hapo na kuanza kuelekea kilipo chumba Cha Nickson , basi mpelelezi huyu wa kimataifa akafika Hadi kilipo chumba Cha Nickson na kusimama mlangoni akisikiliza kama kuna dalili ya mtu kwa Bahati nzuri akasikia sauti kama Kuna movie inaendelea humo ndani hapo ndipo akapata uhakika kuwa Nickson yupo ndani akagonga mlango mara moja Kisha akabaki akisubiri hazikupita dakika akashtukia mlango umefunguliwa akatokea Nickson na kumkuta Isabela amesimama hapo mlangoni ambapo Nickson aliganda kwa dakika nzima akimtazama Isabela kuanzia chini Hadi juu kama anamkagua Fulani hivi jambo lililofanya Isabela ajishtukie na kuanza kujiangalia mara Nickson akaonesha tabasamu
"Karibu Isabela, ingia, nipo nacheki movie hapa"
Alisema Nickson na kufanya Isabela auangalie Tena huo mlango na kujikuta akiganda kwa muda ikabidi Nickson amshtue tena
"Isabelaa...??"
"Abee!"
"Pita uingie Mimi nipo humu"
akasema huku akimshika mkono kumuongoza aingize humo chumbani
kidogo Isabela akajikuta akifarijika kwa kuona kumbe sio wote wenye dharau, japo ni kwa aibu aibu ila kwa mara ya kwanza alibahatika kuingia kwenye chumba Cha Nickson Moja ya kijana wa boss lady .
Kiuoga uoga akaingia humo chumbani, hakujua ni ushamba ama ni nini ila alijikuta akiganda mlangoni akikiangalia hicho chumba
"mmh! Pazuri sana..... Kumbe vyumba vyao ndio vizuri hivi๐....nahisi huko kwa madam ndio zaidi..... siku waniruhusu na Mimi nikafanye usafi kama aunt Nina"
Aliwaza Isabela ghafla akaja kushtuliwa na sauti ya watu wakipigana kwenye TV ndipo akakumbuka Kuna movie inaendelea humo ndani hivyo akageuza macho kuangalia mara anamuona Nickson akisogea kumshika mkono
"Njoo ukae Isabela, sasa utasimama Hadi saa ngapi"
"Hapana Mimi sijaja kukaa Nickson Kuna kitu nilitaka kukuuliza mara moja halafu natoka"
"Sasa si ndio ukae, utaniuliza ukiwa umesimama!?"
Akasema huku akimsogeza akae kitandani jambo lililomfanya apate ujasiri akajikuta amekaa kitandani kwa Nickson wanapiga stori bila hofu yoyote
"Kwa hiyo Nickson unataka kuniambia wale wakaka sio ndugu zenu ni marafiki tu wa Antony"
"Yah! Wale ni rafiki zake na bro, tumekuja wote juzi tulikuwa nao huko nje ya nchi tulipokuwa"
"Ila mnaishi vizuri, mtu hawezi kujua kama ni marafiki tu ..... Mimi nilidhani wote mmezaliwa pamoja"
"๐ Yani tuzaliwe pamoja tunalingana vile dah! Hiyo Kali" akaongea Nickson akitaka kucheka ikabidi na Isabela ajicheke ujinga
"Sikia Isabela, sisi tumezaliwa wawili, ameanza Antony halafu Mimi nikafata ila mtu akituona anaweza asijue mkubwa nani kwa vile hatujazidiana sana, Antony ananizidi mwaka mmoja tu na miezi kama mitano hivi"
Akaongea Nickson na kufanya Isabela azidi kushangaa, kwa kweli stori zote alizopigiwa Nickson zilikuwa mpya kwa Isabela na zilikuwa za kitajiri tu jambo lililomfurahisha sana Isabela, akajikuta ndani ya muda mfupi amemzoea Nickson amejiachia mwenyewe kwenye chumba Cha kaka wa watu hata hakumbuki Tena kama madam anaweza kumkuta humo ndani ikawa shida nyingine ndio kwanza yuko bize na movie.
Zilipita dakika wakiwa humo ndani ghafla wakashtukia kitasa kikiguswa kama mlango unataka kufunguliwa kwa haraka Isabela akawahi kusimama na kutaka kujificha kwa bahati nzuri Nickson aliona hilo akawahi kumzuia
"Usihofu uko na Mimi hakuna kitakachoharibika" alimnong'oneza kwa sauti ya chini akampa ishara atulie Kisha yeye akasogea kwenda kufungua mlango
"aah! Bro" akatamka Nickson na kufanya moyo wa Isabela umlipuke Kwa mshtuko paah!, wakati ameduwaa akishangaa ghafla akashtukia Nickson amegeuka kumtazama
"Nimeghairi Isabela, we nenda tu kaendelee na kazi zako"
"Nani Mimi!?๐"
"Yah! Kaendelee na kazi zako tu utafanya siku nyingine"
Akasema huku akimpa ishara atoke nje ikabidi Isabela aitumie hiyo fursa kutoka humo chumbani haraka japo hakuelewa Nickson ameghairi Nini na yeye anatakiwa afanye nini.... Mtihani kweli kweli, ila akatoka haraka na kupishana na Antony mlangoni yeye akawa ameingia chumbani Isabela akataka kuelekea kwa aunt Nina ghafla akasita na kujibanza karibu na mlango wa chumba Cha Nickson Ili asikie Antony ataongea Nini baada ya kumkuta humo ndani, na ni kama alijua vile haikupita hata dakika akamsikia Antony akihoji kwa sauti ya ukali
"Nick huyu Isabela amekuja kufanya nini humu ndani?๐ "
ITAENDELEA.....
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA:
"Nimeghairi Isabela, we nenda tu kaendelee na kazi zako"
"Nani Mimi!?๐"
"Yah! Kaendelee na kazi zako tu utafanya siku nyingine"
Akasema huku akimpa ishara atoke nje ikabidi Isabela aitumie hiyo fursa kutoka humo chumbani haraka japo hakuelewa Nickson ameghairi Nini na yeye anatakiwa afanye nini.... Mtihani kweli kweli, ila akatoka haraka na kupishana na Antony mlangoni yeye akawa ameingia chumbani Isabela akataka kuelekea kwa aunt Nina ghafla akasita na kujibanza karibu na mlango wa chumba Cha Nickson Ili asikie Antony ataongea Nini baada ya kumkuta humo ndani, na ni kama alijua vile haikupita hata dakika akamsikia Antony akihoji kwa sauti ya ukali
"Nick huyu Isabela amekuja kufanya nini humu ndani?๐ "
ENDELEA.....
"Aah! Nani Isabela... huyo ni Mimi nilimuita aje kunisaidia kubadili mashuka haya naona nimeyatumia sana"
Kwa kweli Isabela hakuamini kama Nickson amemtetea kirahisi hivyo hakutaka Tena kusikia wataongea nini baada ya hapo aliposikia tu wamebadili mada alitoka hapo haraka na kwenda kuingia chumbani kwa aunt Nina ambapo alimkuta aunt Nina Hana habari yoyote ndio kwanza amepitiwa na usingizi hivyo hakuona haja ya kumsumbua
Akaachana nae na kukaa kimya pembeni yake akitafakari balaa alilochokutana nacho huko chumbani kwa Nickson
"Ila yule Nickson Yuko peace sana, sio kama Antony anaringa sana yule kaka๐.... anajiona sana yule kaka .... sijui kanionaje Mimi, kwamba Nina shida sana... Ndio Nina shida ndio maana nimekuja kwao kutafuta kazi lakini sio ndio anioneshe dharau za waziwazi sijapenda kabisa tabia yake ๐ฅบ"
"Sijui hata Nini kilinisukuma Hadi nikamfata kumuongelesha๐"
Basi muda huo ikawa ni kujulaumu tu mwisho wa siku akaona aachane na hayo mambo maana hawezi badilisha awe hajamuuliza, akaona Ili kujisahaurisha atoke nje akafanye usafi wa mazingira, kweli alitoka kwenda kufanya usafi Hadi pale alipoona jua limetua akarudi kuoga na kubadili nguo Kisha nikabeba pochi yake na kumuaga Aunt Nina tayari kwa kuondoka kurudi nyumbani
"Aunt basi tutaonana siku nyingine Acha niende nyumbani nikapumzike"
"Ukapumzike na hujaagana na boss wako, sikia huwezi kuondoka kiholela hivyo Isabela wakati kesho na kesho kutwa hautokuwepo kazini, ni vizuri ukaenda kumuaga madam"
Alishauri aunt Nina na kufanya Isabela ashtuke
"Dah! Halafu kweli Acha nimuage madam kabisa"
Aliongea huku akitoka humo chumbani haraka na kwenda kumgongea madam chumbani kwake ambapo haikuchukua dakika madam akawa ametoka kumsikiliza
"Nilijua tu utakuwa ni wewe Isabela, ehee! Hii tarehe si ndio Huwa unakuwa off"
"Ndio madam naenda kupumzika nitarudi baada ya siku tatu"
"Na Vipi kuhusu mshahara wako si uliuona kwenye simu, nakumbuka nilikutumia asubuhi"
"Ehee! Iliingia, nashukuru sana madam๐"
"Sawa basi Haina shida wewe nenda kapumzike, ila uzingatie siku ya kurudi kazini"
"Asante madam"
Hatimaye alimaliza kuagana na madam bosslady mwenyewe ( mama la mama ) baada ya hapo Isabela akaanza kushuka ngazi taratibu aelekee nje kumbe muda huo Nickson ndio anapanda aelekee chumbani kwake mara anashangaa mtu anambinyia jicho๐ na kumpita, Isabela na haraka zake ukijumlisha na shauku ya kwenda kupumzika nyumbani kusema ukweli hakupata muda wa kumzingatia aliachana nae na kutoka nje ambapo alienda Moja kwa Moja kituoni kutafuta usafiri wa kumfikisha nyumbani kwao
...........................................................................................................................................................
Siku kama hii Huwa ni siku njema sana kwa Isabela pamoja na kwa familia yake kwa ujumla kwa kuwa huwa Kuna kiasi Cha Hela kimeingia ndani na pia Kuna fursa imepatikana ya kukaa na familia, basi Isabela kwa kuwa aliwahi kufika nyumbani mapema hakutaka kupoteza muda alipitia Moja kwa Moja kwa wakala kutoa hela Kisha akarudi nyumbani na kufikia kwenye geto lake na mdogo wake Miriam na kuanza kupanga bajeti kiasi gani kiende kwa mama Isabela kiasi gani abaki nacho mwenyewe akawa bize anapiga mahesabu yake huku Miriam akiwa pembeni akimtupia jicho huku akicheza game kwenye simu
"Dada kumbe umepewa hela zako" aliongea Miriam ila hakuzingatiwa ndio kwanza dadaake Yuko bize na mahesabu, ambapo haikupita dakika akashtuliwa Tena na Miriam
"Dada simu Yako inaita Kuna mtu anakupigia"
Aliongea Tena na safari hii Isabela aligeuka kumtazama ndipo akaona ni kweli simu yake inaita ambapo aliichukua kutoka kwa Miriam Ili aone ni nani amemkumbuka mara anakutana na namba mpya,
"Mmh! Nani Tena huyu, itakuwa ni wrong namba" aliiangalia akasita kupokea akihisi labda ni mtu amekosea namba hivyo akataka aiweke kitandani ila kabla hajafanya hivyo akaona Kuna sms imeingia
"Naomba upokee simu Isabela, Nickson hapa nakupigia"
wakati ameduwaa nikishangaa hiyo sms na kujiuliza Nickson kapataje namba yake ghafla simu ikaanza kuita Tena namba Ile Ile inampigia hapo hapo akaona ampokelee Ili amsikie atasemaje, basi akawa amepokea na kukaa kimya mara akasikia sauti ya Nickson akiongea kutokea upande wa pili
"Hallow Isabela"
"Nickson!?๐"
"Yah! Ni Nick hapa naongea, unajua nimeona haupokei nikaanza kupatwa na wasiwasi... Vipi lakini umefika salama?"
"Ehee! Nipo nyumbani"
"Kwa hiyo umefurahi mwenyewe kwenda likizo si ndio!?.."
"Hamna napumzika tu siku tatu Kisha nitarudi kazini kama kawaida"
"Dah! Haya bwana Isabela we pumzika ila Kaa ukijua Kuna mtu anaumia kwa ajili Yako... Ukikaa ukitulia tumia muda wako kulitafakari Hilo"
aliongea Nickson Kisha akakata simu
ITAENDELEA.....
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA:.
"Hallow Isabela"
"Nickson!?๐"
"Yah! Ni Nick hapa naongea, unajua nimeona haupokei nikaanza kupatwa na wasiwasi... Vipi lakini umefika salama?"
"Ehee! Nipo nyumbani"
"Kwa hiyo umefurahi mwenyewe kwenda likizo si ndio!?.."
"Hamna napumzika tu siku tatu Kisha nitarudi kazini kama kawaida"
"Dah! Haya bwana Isabella we pumzika ila Kaa ukijua Kuna mtu anaumia kwa ajili Yako... Ukikaa ukitulia tumia muda wako kulitafakari Hilo"
aliongea Nickson Kisha akakata simu
ENDELEA.....
mmh! Huyu Nickson katumwa na nani Tena aje aniambie huo ujinga ๐ isije kuwa wale wakaka niliowakuta nao siku ile!?... najua hawezi kuwa Antony๐"
"Au itakuwa mapepe yake tu ๐ maana Nick nae ๐๐" alijiongelesha moyoni na kuishia kucheka inaonekana Hilo jambo halikumshughulisha sana na Wala hakulipa uzito
Kwa kuwa muda uliruhusu na kesho haendi kazini akaona aitumia nafasi hiyo kwenda kijiweni hivyo mama Isabela alirudi nyumbani na Jayden, Brian yeye alikuwa ameenda kushinda na babaake kwenye shughuli zake hivyo usiku huo Isabela kawa yupo mwenyewe maeneo ya sokoni nikihudumia wateja wa samaki, ila Sasa kilichomshangaza siku hii Nickson ni Kama aliamua au kwa vile ndio mara ya kwanza amepata namba ya Isabela maana chating hazikuisha Kila mara ni kumtext na vijimaswali vya hapa na pale ili mradi tu uchokozi, mara atume vichekesho Ili mradi tu Isabela aweze kumzoea.
Basi Isabela nae ni kama alivutiwa na maongezi ya Nickson hivyo muda mwingi walikuwa wakiwasiliana kiasi kwamba hata hizo siku za mapumziko hakuziona tena alishtukia tu siku tatu zimeisha na anatakiwa kurudi kazini
"Yani hata siamini kama nimekaa siku tatu..... Nickson mpuuzi wewe umenimalizia likizo yangu ๐ ila Nickson mjinga sana jamani dah๐คฃ๐คฃ....."
Alijiongelesha na kuishia kucheka mwenyewe huku akijitazama kwenye kioo makeup yake ilivyomkaa vyema Kisha akavaa viatu vyake simple kabisa na kujipulizia kapafyum baada ya hapo akaanza kujigeuza geuza akijiangalia kwenye kioo kama yuko sawa na anaendana na wadada waishio huko anapokwenda ๐
"Nickson Leo utakoma, nakujia huko huko nikutunge jina, yani umeniita Mimi dada mkuu๐... Ila Nickson bwana sijui kawaza Nini Hadi akawa ananiita dada mkuu"
Alijiongelesha mwenyewe huku akisoma baadhi ya text zake alizomtumia akajikuta akicheka mwenyewe moyoni japo kwa wakati huo hakuelewa Nickson anamaanisha Nini
"Hebu nachelewa Mimi, nikianza kufikiria mambo ya Nickson nitakesha"
akaona aachane na hizo sms akaweka simu kwenye pochi Kisha akafunga mlango na kuichomeka funguo panapostahili baada ya hapo hakutaka kupoteza muda safari Moja kwa Moja kituoni kwenda kutafuta usafiri
Ndani ya saa Moja tayari alishafika kwenye nyumba ya boss lady, ambapo hakuacha kusalimiana na mlinzi (kaka Enock) basi Isabela alisalimiana na kaka Enock Kisha akaelekea ndani akaanze majukumu yake
"Waoo! Binti yangu huyo... Bora umekuja shogaangu maana nilikumisije" aliongea aunt Nina na kufanya Isabela atake kucheka ๐
"๐Aunt bwana, Kwa hiyo ulinimis"
"Aah! Naachaje kukumis na wewe ndio kampani yangu"
"๐ Haya Sasa ndio nimekuja kampani Yako" akasema huku nikiweka pochi kabatini Kisha akafungua kwenye kabati la nguo anapohifadhi uniform ya kazi mara akashtuliwa na sauti ya aunt Nina
"Tena nimekumbuka Isabela, hebu badili hizo nguo uende ukamsikilize Nickson maana amekuulizia sana"
Alisisitiza aunt Nina ila Isabela hakutaka kuuliza sana maana anamjua Nickson ni mtu wa utani, alichofanya ni kubadili nguo Kisha akatoka Moja kwa Moja kwenda chumbani kwa Nickson ambapo alikuta mlango umefungwa hivyo akaanza kubisha hodi ghafla akashtukia sauti ya Nickson ikitokea nyuma yake
"Naona head girl ndio anaingia saa hizi" akatania Nickson na kufanya Isabela ashindwe kujizuia na kujikuta akionesha tabasamu
"Umefurahi mwenyewe... Mbona hukunitaarifu kama upo njiani, nimeboeka sana aisee"
"Umeboeka na Nini Nickson, kwani Antony si yupo๐".
"Nani Antony!?... Aah! Yule ameshasafiri kaenda kwenye mambo yake... Ila hata hivyo Antony ni Antony na wewe ni wewe, vitu viwili tofauti... Sikia Mimi nimefurahi nimekuona tena Isabela nahisi Sasa hata nikila chakula kitashuka"
"๐ Eti chakula kitashuka, Nickson bwana Mimi naona huna jipya... Ngoja niende hivi Kuna kazi naenda kuifanya"
Isabela alijibu haraka haraka akiondoka hapo mlangoni kwa Nickson na kuelekea Moja kwa Moja kilipo chumba Cha Antony kwa ajili ya kubadili mashuka ila kitendo cha kuambiwa Antony amesafiri kilimsukuma aanze na ukaguzi, hakujua anataka agundue Nini ila aliamua tu kukagua chumba hicho, hivyo akaingia na kuanza upekuzi, kwa Bahati nzuri vyumba vya kulala vilikaa tofauti tofauti mtu akiwa chumbani kwake hawezi kujua kinachoendelea chumba kingine Hadi aende akasikilize kwa karibu hivyo uwanja ukawa wake akaanza kuangalia uzuri wa chumba hicho akikikagua kwa macho hatimaye macho Kisha akasogea kwenye droo vile anafungua tu anakutana na laptop
"mmh! Kwani Antony kasahau hii๐.... Kwani si Kuna mambo yake muhimu humu.... Ila sidhani kama kaiacha itakuwa labda kasahau" alijiongelesha huku akiitoa kwenye droo na kwenda kukaa nayo kitandani
"mkaka mzuri ila msahaurifu nahisi hata mpenzi wake akimuagiza zawadi Huwa anasahau huyu.... Mmh! Tena nimekumbuka humu siwezi kukosa picha za demu wake Tena ngoja nimuone kama ana mwanamke mzuri au anaturingia tu hapa"
Hapo hapo akapata wazo la kuiwasha kwa Bahati nzuri haikuwa na password hivyo ilimrahisishia kazi akaanza kupekua mafaili akitafuta sehemu zilipohifadhiwa picha japo amuone huyo mrembo anayetoka na Antony , bwana bwana katika kupita pita si akakutana na faili la picha ๐คฃ
"Yes! Afadhali hizi hapa nimeziona"
Alijisemesha huku akifungua Hilo faili na kuanza kupitia picha Moja Moja ila sasa akajikuta akikutana na picha za Antony tu na za familia yake, mara nyingine kapiga na marafiki zake , nyingine amepiga na wasichana tofauti tofauti yani kwa kifupi zote zilionekana ni za kishkaji tu ๐คฃ
"Sasa kamficha wapi huyo mwanamke wake anayemringia ๐ .... Kama yeye mwanaume kweli si angemuweka wazi tumuone kama mzuri kweli ๐ "
Hata mwenyewe Isabela hakujua hasira zimetoka wapi ila alijikuta akichukia na kuamua kuzima hiyo laptop akaona airudishe kwenye droo alipoikuta aendelee na kazi yake iliyomleta, basi akaweka laptop kwenye droo na kulifunga vizuri Kisha akageuka kutaka kuanza usafi ghafla anakutana na picha kubwa ya Antony imetundikwa ukutani, kwa kweli alishindwa kukwepesha macho kuiangalia akajikuta ameganda kwa muda akiitazama hiyo picha ghafla akajikuta akitabasamu, ila Hilo tabasamu lilitoweka baada ya dakika chache tu kutokana na kukumbuka jinsi alivyodharauliwa na huyo kijana mkubwa wa familia hiyo
"Mimi Sina ndugu yoyote zaidi ya Nickson" "Nick huyu Isabela amekuja kufanya nini humu ndani"
"Eti nimekuja kufanya Nini... Msyuu! Kaka mzuri kazi ujeuli tu na kujiona๐"
...
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni