Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
18 Mar 2026
3 views
VYOTE NDANI GONGA94
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco,
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Kufuatia uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco, mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané, ameonyesha kusikitishwa na uamuzi huo na kueleza kuwa unaua soka la Afrika ambapo amedai rushwa imetawala kwenye uamuzi huo.
Uamuzi wa kuipa Morocco ubingwa na ushindi wa mabao 3-0 unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON ambavyo vinaihukumu Senegal kwa kutoka nje ya uwanja wakati wa mchezo wa fainali bila ruhusa ya mwamuzi.
Kupitia taarifa yake ya leo Jumatano Machi 18, 2026 aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii Mané ameeleza kuwa uamuzi huo unakatisha tamaa na kuua hamasa ya soka huku akionya kuwa vitendo hivyo vinadhoofisha uadilifu wa mchezo huo na kuharibu uhusiano kati ya soka na mashabiki wake barani Afrika.
"Kilichotokea kimezidi. Hii siyo soka tunalolipigania, siyo Afrika tunayoamini. Rushwa imekuwa kubwa mno kwenye mchezo wetu, na inaua hamasa ya mamilioni ya mashabiki. Wachezaji wanajitoa kwa kila hali uwanjani, lakini maamuzi ya nje ndiyo yanaamua mechi na mataji," amesema
"Nimesikitishwa si kwa Senegal pekee, bali kwa soka la Afrika kwa ujumla. Tunastahili bora zaidi. Mashabiki wanastahili haki, uwazi na heshima" ameongeza nyota huyo wa klabu ya Al Nassr FC ya Saudi Arabia.
#KitengeSports
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA & Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF
wametoa kibali rasmi cha kuthibitisha kuwa uwanja Wa Hoima City uliopo Uganda, unakidhi viwango vya kimataifa vya kuand...
Bila ya msimamo ule leo watu wangeshasahau kama Afcon ilichezwa Morocco, bila ya huyu Mwanaume muda huu Morocco wangekuwa wanashangilia Kombe la dhulma.
Bila ya jamaa kutoa vijana wake leo Mutsepe angekiri kuwa Senegal walionewa lakini isingesaidia kitu tayari Morocco Bin...
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco,
Kufuatia uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco, mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané, ameonyesha kusikitishwa na uamuzi huo na kueleza kuwa unaua soka la Afrika ambapo amedai rushwa imetawala kwenye uamuzi huo.
Uamuzi wa kuipa Morocco ubingwa na ushindi wa mabao 3-0 unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON ambavyo vinaihukumu Senegal kwa kutoka nje ya uwanja wakati wa mchezo wa fainali bila ruhusa ya mwamuzi.
Kupitia taarifa yake ya leo Jumatano...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/shirikisho-la-soka-afrika-caf-wa-kuwavua-senegal-ubingwa-wa-afcon-2025-na-kuwapa-morocco
Maoni