JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 8
Mwandishi:lissa mwalla
Babaaa! Niliita kwa mstuko, baba akasema tayla wee taaaay... Kabla hajamaliza niligeuka nyuma na kuanza kuondoka, kumbe DA frida alikua anatembea na babangu siku zote hizi? Baba kampangia anaishi nae pia dar? Umekuaje DA frida kamfanyia hivi mamangu? Nilijihoji bila kupata majibu, nilikaza mwendo nikaskia anitwa nyuma, alikua ni babangu anaita akasema tayla simama wee tee mwanangu simama nikuambie. Niligeuka niliona baba yupo na kitenge ananifuata tuu na singlend nikaona nitazidi mfedhehesha zaidia nikasimama. Akanifikia akasema mwanangu nakuomba turudi tukazungumze. Nikimtizama kwa hasira nikasema baba mm sina cha kuzungumza na ww, akasema usiseme hivo nataka tukazungumze kuhusu ulichoona, nikasema baba wewe ni baba yangu hipaswi kuniambia mm kitu ila unapaswa kumwambia mama. Baba akasema unanidharau si ndio? Pamoja na yote mm ni babako usisahau hilo pumbavu wewe. Twende hukooo haraka. Niligeuza na kuanza kurudi. Tuliingia pale kwa DA frida tukakuta DA frida amekaa kibarazani akiwa na mawazo mengi sana. Baba akasema ingia ndani, frida alinyanyuka akawa anaingia na mm nikawa namfata nyuma. Tuliingia seblen palikua pazur tu kuna sofa nzuri sana na tv kubwa ukutani pia kuna picha kubwa ya baba ingine ya frida baba na mtoto wao, nilimuonea huruma mama. Nilikaa baba nae akakaa akasema tee najua umestuka lkn sikupanga ujue kwa styl hii,siwez kuelezea mengi sana ila jua tu frida ni mwanamke wangu na huyu mtoto ni mdogo wako, sasa sitaki umwambie mamako ila mm mwenyew ndio nitamwambia wakati ukifika sawa??mm nilishindwa kujibu, mama yangu alimpenda frida sana, alimpa mpaka vyombo vya kuanzia maisha hakujua baba ndie anaanza nae maisha ,baba akasema unaniskia niaksema kwa nn lkn? Kwa nn mmemfanyia hivi mama yangu? Baba akasema sina sababu ya kukuekezea ww ilikuaje ni sababu za ndani kabisa mm na mamako ndio tunapaswa kujua na Si watoto. Nikasema sawa nimekuelewa. Akasema sitak kuskia hili popote had mm nitakaposema na kama mm babako basi utHmaheshim maamuz yangu vinginevo utapata laana. Na pia nataka umuheshim frida sana ni mamako mdogo huyu. Nilintizama frida nae alinitizama sikuamin, siwez msamahe kwa hili. Baba akasema mama tim leta juic hapa, DA frida aliamka akaenda let's, ilibidi ninywe kisha nikaaga. Baba alinipa pesa sh lak 1 naona alikua ananiziba nisiseme. Niliondoka zangu na kwenda kina Bella, nilikua sina raha wala aman, nikimuonea huruma sana mama yangu. Bella alijua sina raha akasema kulikon mbona hivo?,niaksema bela ivi ukijua babako anamsalit mamako utafanya nn? Akasema heee nitatumia hio kama fimbo mbon nitamchuna mshua hadi akome? Nikacheka niakasema akili zako ww unazijua mwenyew,akasema ndio mana unaweza mwambia mamako akafa presha bure sasa kilichobaki ni kumchuna mshua tu ili nufiche sir.nilifikiria kwel kumwambia mama ni hatar vip akipata presha kwel?mmh hapana.bella akishajiandaa tukatoka zetu na kwenda zetu coco.tulifiks tukanunua vinywaji vyetu tukaenda kuzunguka pemben ya ufukwe huku tukiongea ongea.tukifika sehem tulioona nzur bella akasema tuoge dia ,nikasema mm nabrid leo sigusi hayo maji.akasema poleeee ngoja mie nikaogelee.akatoa nguo akabakia na chupi tu na sidilia tu.nikamshkia simu na nguo pale nilopokaa.alienda akaogelea wee mm hapo niko mbali sana kimawazo kiasi kwamba alikuja mtu Kakaa jirani yngu lkn sikumskia hadu alivonishika bega ndipo nikastuka nikamtizama alikua n mkaka tu mtefu maji ya kunde.akasema unawaza nn mrembo?,nimekuita sana hujaitika.nikasema amna bana,akasema mmh haya bana mamboo lkn?,nikasema powa tu za ww? Akasema poa,mbn huogelei?nikasema siko poa leo.akasema okay.umekuja na nani?nikasema na rafiki angu.akasema ahaaa okay.basi alikaa pale kwa muda akinipa stor mwishon akaomba namba ya simu.nilisita kumpa lkn aliomba sana nikampa tu.tuliliendelea na stor hadi bela alivotoka kwenye majindio akaniaga sasa na kusema anaondoka.bella aliona akauliza akasema nani yule mkaka?nikasema hata jina simjui alikaa tu hapa.akasema ahaa nikajua umepata bwana.nikacheka nikasema bwana wapii niache mm. Muda ulikua umeenda kidogo Bella akavaa akasema twende tukale nataka leo nikuspoil dia wangu nikununulie misosi na bia kama unataka kunywa kunywa nina pesa. Pia nataka tutoke usiku na sie mana kama kusoma tunasoma siku moja moja tukishi kawa wasichana wenzetu wa chuo sio mbaya na sie tupate cha kusimulia wajukuu. Nikacheka akasema Ndio twende club bana, nikasema powa. Akasema haya tukale kwanza kisha twende geto kwako tukaoge tubadilike tutoke. Nikasema sawa. Tulienda pale pale tukaagiza chips zetu mishkaki na firigisi na maini tukaanza kula. Tulimaliza vyombo vikatolewa lkn muhudumu akawa haji kudai pesa, bella akasema huyu vipi yn katoa vyombo anataka hata kuchukua pesa tumbeambeleze? Hanijui nitaondoka mm. Nikasema. Mmh Bella watu wengi bana usifanye hivo mwite tu. Akasema sawa akamuita yule dada halafu akamwambia umeshiba pesa nn mbona hufati? Mhudumu Akasema Ishalipiwa yenu ndio mana. Bella akasema nani kalipia? Akaonesha meza fln walikaa wakaka wawilina mdada mmoja. Nilivoangalia alikua ni yule mkaka alinifata ufukweni. Bela akasema Mwambie tunashukuru. Tukinyanyuka na kuanza kuondoka. Tuliita bajaji tukapanda mara msg ikaingia ktk Simu yangu imeandikwa "mrembo unaondoka hata kuniaga jmn? Sio poa hivo"nilijua ni yule mkaka lkn sababu sikujua jina lake nikajibu "sorry nani mwenzangu?" "Akasema mm Elvis nimekutana na ww ufukweni nikaomba namba"
Nikasema "sorry kwa kuondoka bila kukuaga pia asante kwa msosi"akasema "usijali kwa hio mnaelekea wapi? Ningewasogeza"nikasema "usijali tumeshaondoka"akasema "powa basi "sikumjibu hio. Tulifika kwangu tulioga tukajiremba tukavaa nguo za kawaida tu surual na top tukatoka sasa. Tulienda club tukajiachia mnoo, tulivochoka tukarud nyumbn. Elvis aliendelea kunichatisha kila siku akiomba tuonane, nilijua mwishi wa hii n kunitongoza na mm. Nilikua sina mshipa wa kupenda hata yy sikumpenda sana. Siku moja nilikua chuoni nimemaliza vipindi nimekaa zangu namsubir bella alikua anamalizia pindi mara nikaskia tee mbona unanifanyia hivo? Nilistuka kuchrk ni Elvis ,mmh kanionaje hapa? Nikasema we umenionaje hapa na umefata nn? Akasema nilikuja kwa jamaa yangu ni mhasibu haba ndio nikakuona umekaa hapa. Nikasema ahaa
Akasema umeamin kwamba milima Haikutani ila binadam hukutana? Nikasema nimeamin, akasema wiki ya tatu hii hutaki tuonane kwa nn?nikasema masomo yamebibana, akasema ooh unasoma nn dokta au? Nikasema ndio, akasema utapendeza sana ukiwa dokta nikasema asante. Basi tuliongea kisha akaaga huku akiomba tuonane. Niliitikia lkn wiki mbili zilipita. Weekend ikifika kama kawa club tukaenda na bella katika kucheza nilishangaa nakumbatiwa na mtu, nikistuka kumchek n Elvis, niliona aibu nikajichekesha. Elvis akasema leo sikuachi mpaka tuongee. Nikasema sawa. Nikawa nae sasa huku akitambulisha rafiki ake. Walikua watatu yy na rafiki zake. Tulijiunga nao na kuendelea kunywa na kucheza. Tulicheza had usku mwingi tulichoka tukamwambia elvis akasema tuondoke atupeleke. Tulitoka nje ya club tukitembea kuelekea kwenye gari simu yangu ikikua inatetema nijaingiza mkono mfukoni nitoe huku siangalii mbeke mara niligongana na mtu nijaangusha pochi. Alienigonga aliinama kuokota kisha akanyanyua uso wake kunitizana ๐ณ๐ณ๐ณ๐ณ๐ณ๐ณ๐ณ๐ซsikuamini macho yangu niliekutana nae ...........
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni