Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI 💔💔 SEHEMU : 16

23rd Aug, 2025 Views 54



" Simama hapo wewe boya "
maverick alienda kumzuia Tristan asipande kwenye gari lake
" Unataka nini ? Pisha nipite "

" Hasira zako haziwezi kusaidia kitu Tristan ukweli utabaki pale pale ulimuacha Gabriella kipindi alipokuwa anakuhitaji sana na ulikuwa na mwanamke mwingine unajua ni Kiasi gani ulimuumiza ?,Sasa nakwambia hivi Kaa mbali na Gabriella sitaki kumuona anahuzuni tena kwasababu yako " alisema maverick

" Nini ? Unakisikia unachokiongea maverick,wewe ndo unatakiwa kukaa mbali na Gabriella kwasababu ni mke wa ndugu yako "

" Umesahau kwamba ulipoteza hiyo haki ya kuwa mume kwake? ,sitaki kuongea sana Tristan nakuonya tena hii ni mara ya mwisho Kaa mbali na Gabriella la sivyo nitasahau kama wewe ni ndugu yangu, "
maverick alipanda kwenye gari akaondoka

Kwa upande wa Gabriella Hakwenda nyumbani kwao alienda nyumbani kwa Veronica

" Gabby ulisema utakuwa kwenye sherehe mbona upo hapa ?"

" Maverick amerudi lakini nachanganyikiwa nahisi kuchanganyikiwa kabisa Vero "
Gabriella alikaa chini

" Kwanini uchanganyikiwe badala ya kufurahia baba wa mtoto wako amerudi, au humpendi tena ? "
Veronica alimuuliza Gabriella

" Nampenda bado nampenda sana Rick yeye ni mwanaume wa tofauti sana hakuniwekea wafanyakazi kama alivyofanya Tristan ila upendo wake ulikuwa wa kipekee na alifanya juu chini nijue vitu muhimu ambavyo mwanamke anatakiwa kujua kuhusu nyumba na Hata kupika , lakini kilichotokea Leo sielewi kama ni masikio yangu yananidanganya au laa nimemsikia maverick akimuita Mr Edward uncle "

" What ? Embu nielezee vizuri "
Gabriella alimuelezea Veronica jinsi alivyokutana na maverick kwenye sherehe

"Lakini Hilo sio tatizo sio kama umemcheat Tristan mlikuwa mmeshaachana "

" Tatizo watu wataniangaliaje mimi si wataniona mdangaji hao ni kama watoto wa baba mmoja vero "

" Acha ushamba shoga yangu historia yako na Tristan imeshafutwa na Sasa ni wakati wako wa kuandika historia yako mpya ya mapenzi na mwanaume unayempenda nae ni maverick bila shaka... na ni baba wa mtoto wako pia "

" Hapana siwezi Vero hiyo ni ngumi sana najiona kama mjinga sijui kwanini nilimpenda maverick haraka kiasi hiki Sasa naishia kuumia tena "

" Ukiumia utakuwa umechagua mwenyewe iwe hivyo, kama maverick anakupenda hakuna haja ya kuwa na wasiwasi watu wanaenda hata kinyume na familia zao kwasababu ya upendo tu"

" Usinishauri ujinga Vero haya ni maisha halisi sio kama kwenye michezo ya kuigiza , siwezi kuitupa familia yangu najua watakasilika sana kusikia natoka kimapenzi na kaka wa Tristan "

" Apo unaharibu Sasa sio kaka ukisema hivyo inakuwa ni kama wamezaliwa tumbo moja na wakati kila mmoja ana wazazi wake "

" Hata hivyo pia siwezi , hata ikitokea wazazi wamekubali ila mimi sitoweza kuolewa na maverick "
Gabriella hakutaka kuelewa alishikilia msimamo wake ule ule hataka kuonana na Tristan Wala maverick alitaka kuishi maisha yake

Maverick alijitahidi kumpigia Gabriella na kumtumia message lakini hakujibiwa

Siku moja Gabriella alikuwa supermarket mdogo wake Gladness Gabriella aliishikwa mkono kugeuka alikuwa ni maverick

" Maverick niachie " Gabriella alitaka kujitoa kwa maverick

" Nataka kuongea na wewe nipe dakika moja tu "
kabla Gabriella hajajibu chochote alishtukia ameshikwa mkono wake mwingine kugeuka alikutana na Tristan Gladness alibaki kushangaa hakujua kama ule ulikuwa ni mchezo wa kuigiza au maisha halisi alishuhudia dada yake akigombaniwa na wanaume wawili tena wote wakiwa watanashati

"Achia mkono wa mke wangu maverick sitojali kama sisi ni ndugu nitakuumiza "
alisema Tristan

" Kwanza Gabriella sio mke wako futa hiyo kauli na hayo maneno nilitakiwa mimi nikwambie wewe , achia mkono wa Gabriella kabla sijazifanya kitu mbaya hizo Taya zako "

" Usinitishe maverick mimi sio muoga kama unavyofikilia "
Maverick alicheka kwa dharau alimsogelea Tristan alitaka kumpiga ngumi Gabriella akamzuia

" Sitaki mpigane kwasababu Yangu kati yenu hakuna hata mmoja nitakaye mchagua msipoteze muda wenu kwangu na kama mnataka kupigana piganeni kwa yenu " Gabriella alimshika mkono Gladness wakaondoka waliwaacha maverick na Tristan wanatunishiana vifua

" Nakupa onyo Tristan sitaki kuona unamsogelea Gabriella ..narudia hili ni onyo la mwisho " maverick aliondoka Alienda nyumbani kwa dada yake Nicole

" Umeshaongea na Gabriella?"
Nicole alimuuliza maverick

" Hapana sikupata muda wa kuongea nae hataki kunisikiliza hata mara moja "

maverick alienda kukaa kwenye kochi

" Sasa itakuwaje?" Aliuliza Nicole

" Nasubiri atakapokuwa tayari kunisikiliza basi nitamuelezea kila kitu bila kumficha "

" Okay ,lini unaenda nyumbani kuwasali wazazi mama amekumiss sana " alisema Nicole

" Nitaenda weekend hii hata mimi nimemiss sana mama yangu " Weekend kama alivyosema maverick alienda nyumbani kwao

" Mama... "
maverick alienda kumkumbatia mama yake

" Sitaki niachie ,Yani kuja kumtembelea mama yako mpaka uombwe mtoto mbaya wewe "
alisema bi Vanessa

" Sio hivyo mama Kuna mambo yaliingiliana ndomana sikuweza kufika hapa nisamehe hili halitojirudia tena " maverick alimkumbatia tena mama yake

" Sawa nimekusamehe na Leo nitakupikia chakula kitamu sana " alisema bi Vanessa

" Wow na mimi nitakuwa hapa kusaidia vitu vidogo vidogo " maverick na mama yake walipika huku wanapiga story

" Nicole aliniambia umepata mchumba"

" Ndiyo mama nampenda sana huyu mwanamke ila tumekwaluzana kidogo na hataki kuongea na mimi "

" Fanya juu chini uongee nae na muyamalize mimi nasubiri ndoa tu sitaki ucheleweshe nataka wajukuu " aliongea bi Vanessa huku anatabasamu

" Usijali mama nitamaliza tofauti zetu na soon atakuwa mke wangu ".....

Offer offer offer
Soma yote kwa sh 800

Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI 💔💔 SEHEMU : 16  >>> https://gonga94.com/semajambo/captain-maverick-na-mission-ya-mapenzi-sehemu-16

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest