Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI❤SEHEMU : 17

25th Aug, 2025 Views 43



"Nicole aliniambia umepata mchumba"

" Ndiyo mama nampenda sana huyu mwanamke ila tumekwaluzana kidogo na hataki kuongea na mimi "

" Fanya juu chini uongee nae na muyamalize mimi nasubiri ndoa tu sitaki ucheleweshe nataka wajukuu " aliongea bi Vanessa huku anatabasamu

" Usijali mama nitamaliza tofauti zetu na soon atakuwa mke wangu "

" Nimuone basi huyo mka mwana wangu haya kwenye picha "
alisema bi Vanessa Maverick alitoa simu yake akamuonyesha mama yake picha ya Gabriella

" Huyu si ni Gabriella mtoto wa Mr Alphonse ?"
Aliuliza bi Vanessa

" Ndiyo mama ni yeye najua utakasilika lakini ameshaachana na Tristan "

" Wala sijakasilika mwanangu Leo nimeamini mtu huenda alikopangiwa na mungu hata iweje "

" Unamaanisha nini mama ?"

" Mmmh unakumbuka miaka miwili iliyopita nilikutafutia mchumba lakini ilibidi uchumba uvunjwe kwasababu ulienda congo "

" Nakumbuka mama "

" Basi huyo binti alikuwa ni Gabriella "
alisema bi Vanessa

" Mmmh mama apo unanidanganya Gabriella huyu huyu au mwingine? "maverick alianza kucheka

" Siwezi kukudanganya maverick na baada ya uchumba kuvunjwa tulikuja kupewa kadi za mualiko kuwa Gabriella anaolewa na Tristan " alisema bi Vanessa Maverick hakuamini anachokisikia kabisa

siku hiyo maverick alishinda nyumbani kwao walikula pamoja kama familia na jioni aliondoka aliamua kwenda nyumbani kwa kina Gabriella Alimpigia Gabriella

"Shida yako ?"
Aliuliza Gabriella baada tu ya kupokea simu

" Naomba tuonane nataka kuongea na wewe"

" Sina muda huo " Gabriella alitaka kukata simu

" Nipo nje ya nyumba yenu kama hautatoka basi nitaingia ndani mimi mwenyewe " Gabriella alisimama alisogea dirishani alifungua dirisha kweli alimuona maverick akiwa amesimama nje ya geti

" Usijalibu kufanya ujinga wa aina yoyote maverick,baba yangu ana bastola atakuuwa nakwambia "
Gabriella alijaribu kumtishia maverick

" Siogopi bastola Wala hio risasi yenyewe ninachoogopa ni kukupoteza wewe Gabriella , maisha yangu yatakuwa hayana maana yoyote bila wewe ,wewe ndo tulizo la moyo wangu "
maverick aliongea kwa huzuni huku anamuangalia Gabriella aliyekuwa dirisha la chumbani kwake ghorofa ya pili

" Nakuja usifanye ujinga wa aina yoyote " Gabriella aliamua kwenda kuonana na maverick

." Niambie unataka nini ?"

" Nimekuja kuomba msamaha kwa kilichotokea na kueleza hisia zangu kwako " maverick alitoa maua kwenye gari akampa Gabriella

" ulijua mimi ni mke wa Tristan ndugu yako ....ndugu yako maverick lakini bado uliamua kunitumia au ulitaka tu kujua ndugu yako alikuwa anakula vitu vya aina gani ? Umeshajua Sasa umefurahi ? "
Aliongea Gabriella kwa kufoka

" Mimi sio mwanaume wa namna hiyo Gabriella nakupenda kweli na mwanzo sikuwa najua kama ex husband wako alikuwa ni Tristan nilijua Hilo kwenye ile sherehe ya rafiki yako lakini sikuweza kujizuia tena kwasababu nilikuwa nimeshakupenda sana "
Gabriella hakumsikiliza maverick aliyaangalia Yale maua aliyopewa na Maverick

"Maua ...unahisi mimi ni mtoto mdogo wa kudanganywa kwa maua ,usirudi tena hapa iwe mwanzo na mwisho "
Gabriella alimtupia Yale maua maverick akaingia ndani

" Mlinzi akija huyu mjinga kwa mara nyingine ita polisi akienda selo naona atajifunza kuheshimu watu na nyumba zoa "

" Sawa madam " Gabriella aliingia ndani

" Hahaha kutamba kote kule kumbe Gabriella Hana time na wewe " Tristan alishuka kwenye gari lake akamsogelea maverick

" Haya ni ya muda tu Gabriella ananipenda mimi na sio wewe Tristan,ulimchukua Gabriella mwanzo kutoka kwangu lakini sitoruhusu hili litokee tena "
maverick alitabasamu akaondoka alimuachia Tristan maswali mengi

" Nilimchukua kutoka kwake anamaanisha nini ?"
Tristan aliamua kuondoka
Maverick aliumizwa sana na maneno ya Gabriella aliamua kwenda baa aliagiza pombe na kuanza kunywa maeneo Yale Yale alikuwepo captain Raymond na Nadya walimuona maverick wakaenda kuungana nae

" Mbona unakunywa kwa pupa sana Gabriella ameshindwa kukuelewa au umekuta ameshaolewa " Raymond alimchokoza maverick

" Muache unaona kabisa hayupo sana na wewe unaanza kuleta utani "

" Gabriella .. Gabriella wangu hataki hata kuniona ..hataki kunisikiliza mimi nitaishije bila yeye Sasa "
maverick aliongea sauti ya kilevi

" Huyo Gabriella ni mzuri kiasi gani mpaka unamlilia hivyo ? Ukute WA kawaida tu kweli mapenzi upofu "
alisema Raymond

" Weeee usiseme hivyo hujawahi kumuona huyo Gabriella ni chombo ukimuona tu hata wewe hutoboi "
alisema Nadya

" Basi tufanye mipango tumsaidie mshkaji naona anateseka " alisema Raymond

" Poa "
Raymond na Nadya walikubaliana kufanya juu chini maverick apate nafasi ya kuongea na Gabriella ️Kesho yake Raymond aliongozana na Nadya mpaka nyumbani kwa kina Gabriella walikalinishwa ndani mage ,walimkuta Gladness anaangalia tamthilia

" Gladness Hawa ni wageni wa Gabriella " alisema mage

" Oh karibuni sana "

" Asante ,ila sio wakaaji sana tunaomba utuitie Gabriella "
alisema Raymond

" Okay nitaenda kumuita Sasa hivi"Gladness alienda chumbani.kwa Gabriella Gladness alirudi akiwa ameongozana na Gabriella

" Karibuni niwasaidie nini?"
Gabriella aliwauliza Raymond na Nadya

"Unahitajika kituo Cha polisi kwaajili ya kuchukua maelezo yako "

" Maelezo yangu kuhusu nini?"
Aliuliza Gabriella

" Maswali mengi ya nini binti kwanini usiongozane na sisi utaenda kujua huko huko kituoni "
alisema Raymond

" Lakini anatakiwa kujua kabla ya kuongozana na nyie anahitajika huko kwasababu gani " alisema Gladness

" Hatuna muda wa kumuelezea anahitajika haraka sana kituoni " Nadya alimshika mkono Gabriella ,Gladness alitaka kuwàfuata Raymond akamzuia

"hutakiwi kuongozana nae unaweza kuja baadae kituoni "
alisema Raymond

" Gladness usijali nitakuwa sawa unaweza kuja baadae "
Gabriella aliongozana na Raymond pamoja na Nadya.....

Offer offer offer
Soma yote kwa sh 800
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI❤SEHEMU : 17  >>> https://gonga94.com/semajambo/captain-maverick-na-mission-ya-mapenzi-sehemu-17

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest