"Karibuni niwasaidie nini?"
Gabriella aliwauliza Raymond na Nadya
"Unahitajika kituo Cha polisi kwaajili ya kuchukua maelezo yako "
" Maelezo yangu kuhusu nini?"
Aliuliza Gabriella
" Maswali mengi ya nini binti kwanini usiongozane na sisi utaenda kujua huko huko kituoni "
alisema Raymond
" Lakini anatakiwa kujua kabla ya kuongozana na nyie anahitajika huko kwasababu gani " alisema Gladness
" Hatuna muda wa kumuelezea anahitajika haraka sana kituoni " Nadya alimshika mkono Gabriella ,Gladness alitaka kuwร fuata Raymond akamzuia
"hutakiwi kuongozana nae unaweza kuja baadae kituoni "
alisema Raymond
" Gladness usijali nitakuwa sawa unaweza kuja baadae "
Gabriella aliongozana na Raymond pamoja na Nadya Walimpelekea kituoni , Raymond alienda kwenye ofisi ya mkuu wa kituo
" Mr George mpigie maverick umwambie aje haraka sana Gabriella amekamatwa kwa kosa kubwa sana afanye haraka afike kituoni " Raymond alimwambia mkuu wa kituo Mr George
" Michezo yenu ni ya hatari vipi kama captain maverick atakasirika ?" Aliuliza Mr George
" Acha uoga Mr George Nina uhakika maverick atafurahi sana akimuona Gabriella mana anatamani sana kumuona na kuongea nae "
" Sawa basi nitampigia Sasa hivi "
Mr George alimpigia maverick na muda huo alisema yupo njiani anaelekea kituoni Ndani ya nusu saa maverick alifika kituo Cha police alienda ofisi ya Mr George
" Mr George kimetokea nini mbona sielewi Gabriella anakosa gani lililopelekea kukamatwa ?"
Aliuliza maverick
" Tulia kwanza captain maverick hii kesi sio kubwa sana tunaweza kumuachia ila Gabriella aliomba kuongea na wewe kabla ya kuruhusiwa kuondoka " alidanganya Mr George
" Yuko wapi ?"
Aliuliza maverick
" Ingia chumba hicho hapo "
maverick aliingia alimkuta Gabriella amekaa kwenye kiti
" Gabriella uko sawa ?" Maverick alienda kushika mikono ya Gabriella
Offer offer offer
Soma yote kwa sh 600
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments