Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....11 Na

19th Jul, 2025 Views 20


Mamuh mohd
(0716730000)

Tulipoishia.....

Alikuwa akiongea hukud analia manga hadi jarden akaamua kuinuka na kumsogeza kitandani....

SONGA NAYO...

Jaden alifanya tendo la ndoa kwa Manga pasina kujali hali yake kihisia.
Yani hakujali kama anamfurahisha aliangalia hamu yake tu.

Alipomaliza akamtaka manga aondoke chumbani.

"Mmewangu kwaiyo ni sumu kabisa mimi kulala chumbani kwako mpaka asubuhi"

"Manga hisia zangu kwako zilishakatika zamani sana,
yani nimeshakuchukulia wewe kama mtumishi.

Ni mapito yale ndio yalipelekea nikakuoa wewe lakini nadhani unajua kwa hadhi ambayo nilikuwa nayo usingeweza kuwa mke wangu, ni vile tu niliyumba ndio maana nikakuoa wewe.

Lakini ukweli ni kwamba wewe ni kijakazi na itabaki kuwa hivyo haupendezi hata kuwa mama mwenyewe nyumba yaani hadi aibu eti anakuja mtu nakutambulisha wewe jamani huyu ndio mke wangu mama mwenye nyumba, yaani nitaonekana mtu wa ajabu sana.

manga vipi kuna maelezo mengine unataka kuyasikia kutoka kwangu kama hamna nenda kalale uwe na usiku mwema okay.........

samahani nilisahau kingine huna mamlaka ya kunifuata kuniambia una hamu na mimi pengine mimi naweza nikakuhitaji wewe kwa hiyo iwe mwanzo na mwisho kuja chumbani kwangu eti kusema una hamu na mimi..... ondoka"

Manga alikosa hata cha kujibu lilimshuka shuuu.

Alitoka na kurudi chumbani na kuanza kulia lakini hakuna kitu ingesaidia.

*******
Basi siku iliyofuata Majira ya jioni Jaden alirudi nyumbani na kumkuta Manga akiwa jikoni na mtoto wake Nayla akimsaidia kumenye Menya vitunguu.

Jarden alimtazama weweeh kisha akamuambia,
"Naona dalili ya watoto wangu nao wanaanza kupewa taaluma za kuwa wafanyakazi wa ndani.
Ndio zitakuwa kazi za ndoto zao".

"Mmewangu Hapana haiko ivyo ananisaidia tu na isitoshe huyu ni mtoto wa kike kufanya shuhuli ndogo kama hizi sio kosa kwake".

"Nyamazaaaaa unataka kusemaje? Kwamba binti yangu asiefanya hizo kazi yeye sio mwanamke? Au unataka kusema wewe ndie unajua sana kulea eti?"

"Samahani sikuwa na maana hiyo mmewangu".

"Ok ni ivi napambana kwa ajili ya watoto wangu kufanya kazi kama hizo wao kwao sio lazima.
Watapata elimu bora watakuwa na kazi zao maisha mazuri wataajiri wafanyakazi kama wewe kwaiyo sitaki iyo kitu ijirudie".

Katoto kale Nayla kusikia vile alielewa akajibu,

"Hapana baba mimi namsaidia mama hata shuleni tunafundishwa kusaidia kazi wazazi".

"Ohhhh okay kwaiyo unatetea mama yako si ndio? Unaniona nayozungumza mimi ni kama mjinga eti? Sawa subiri".

Jarden alikuwa akiondoka huku Manga alimfuata,

"Jarden Hapana huwezi kumjibu ivyo mtoto mbona alichokizungumza sio kibaya tafadhali ni mtoto tu yule".

Jarden hakumjibu kitu zaidi aliingia chumbani kwake na kubamiza mlango.

Manga ilibidi arudi na kumshika mkono binti yake.

"Mama mbona baba anakuchukia mimi ananiuzi".

"Mhhh usijali ni baba yako mzoee baba yenu ni mkali sana lakini usijali...sasa nenda kafanya homework si unakumbuka tulikubaliana unanisaidia kazi basi saa 2 usiku alafu unaenda kufanya homework eeh.
Haya nenda namalizia kupika"

"Sawa mama.....namchukua na mdogo wangu Kahan naenda nae chumbani"

"Hapana Kahan muache chumbani kwa bibi yake huko atakufanyia fujo sawa...".

"Sawa".

Manga alijitahidi kujikaza mbele ya mwanae lakini ukweli alikuwa akiumia sana.

Kwa wakati huo Nafsa na shangazi yake Joan walikwenda mikumi huko kutalii hawakuwa nyumbani.

Nafsa alikuwa ni mtu wa kuomba pesa kwa baba yake kila wakati alitaka pesa tu.

Basi maisha yaliendelea Ambapo nafsa alikwenda kuendelea na masomo yake.

Siku hiyo Jarden alikuwa akitoka asubuhi Ndipo Manga akaniambia,

"Ada ya Nayla shuleni inatakiwa amepewa barua hii".

"Sina pesa wacha aendelee kujifunza mapishi si ana ndoto za kuwa mpishi bora ".

"Mmewangu acha basi ivyo ni...."

"Nyamazaaaa nimesema Sina pesa.
Ada ya shuleni kwa Nafsa ni milioni 8 bado matumizi nimetoka kumtolea juzi tu huyo muache aendelee na upishi".

Manga alihisi huwenda ni utani tu lakini kumbe jarden alikuwa akimaanisha.

Wiki moja ilipita mpaka mwezi hapo hata walimu waliamua kumsimamisha shule Nayla kwani walivumilia ndani ya mwezi wakijua ada italipwa lakini haikulipwa.

Bado jarden wala hakushtuka kumuona Nayla yupo nyumbani.

Mama Jaden aliingilia kati suala lile akamfuata kijana wake huyo,

"Jarden umekuwaje mwanangu mbona unabagua watoto kwanini?"

"Mama najuta kuoa tena na kupata watoto wengine hali ya kuwa tayari yupo kipenzi cha moyo wangu.
Nadhani nilitaka kubaki na kaprincess Kangu mtoto alienizalia mwanamke niliempenda sema basi tu"

"Hapana Hapana watoto ni watoto mwanangu mlipie ada aende shule na huyu mdogo pia kamuanzishe shule".

"Ahhh nahisi natupa tu hela yani ebu niache".

Wakati jarden anajibu hayo Manga alikuwa akisikia ndo aliumia kupita kiasi.
Alijuta kukubali kuolewa na jarden na kuzaa watoto wale.

Huku familia yake wakijua Manga naishi maisha mazuri kutwa wanampigia simu awasaidie lakini hawakujua tabu anayopitia yeye na watoto wake.

Manga aliamua kuchukua maamuzi ya kumuhamisha shule Mwanae na kumpeleka st kayumba (shule ya serikali).

Jarden kuona ivyo aliona ni kama anamzalilisha.
Nyumba ambayo mtoto anatokea, jina anakitumia na shule anayosoma ni aibu.

Alimfuata manga na kumfokea,

"Ulijiona unajimudu sana ungehama hapa nyumbani sio kunitia aibu sasa ondoka".

Kwa dharau Jaden alimpatia laki moja Manga kuwa mshahara wake wa mwaka mzima aliofanya kazi.

"Sawa jarden nashukuru sana Nisamehe mimi mjinga mfanyakazi niliekubali kuolewa na wewe.
Jarden umesahau kuwa maisha mazuri yanaweza kuharibika wakati wowote na ukawa fukara.
Mimi huyu huyu ndie nilikuwa hadi nakupa nauli ya kwenda kazini hadi umefikia hapo ulipo.

Leo umesahau hayo yote na mbaya zaidi hadi watoto wako unawatelekeza eti umezaa na mfanyakazi wa ndani mala eti binti yako kipenzi ni nafsa.
Laiti ungejua Jaden laiti ungejua acha tu wacha ninyajaze naamini chaguo sahihi kwangu ni kunyamaza kuliko athari ambayo itakukuta Jaden usinifanye nije kuzungumza ".

Aliongea hayo manga kisha akaondoka zake lakini Jarden wala halikumshtua neno aliishia kumfyonza tu.

Wakati huo manga alikwenda chumbani na kuanza kupanga nguo aondoke huku amekasirika kwelikweli.

Mama Jaden ndipo akamfuata manga,

"Mwanangu Hapana usiondoke tafadhali nakuomba mzoee tu jarden waache watoto wakae hapa ni kwao.
Maneno uliyoongea nimeyasikia yameniumiza sana tafadhali kuna nini kinaendelea kwani? Najua unajua mengi ya Jarden wakati hajafanikiwa alikuwa akikupenda.
Vipi kuna kitu kibaya unalijua kuhusu yeye au kazini kwake? Tafadhali niambie mwanangu ".

"Hapana mama si kitu ila wacha tuondoke....nitapanga mahali nitakaa".

"Hapana sikuruhusu uondoke ukiwa mfanyakazi sembuse sasa wewe ni mke na pia ni mama wa familia hii.
Hapana baki hata kwa ajili yangu manga mwanangu ".

Mama Jarden hadi alianza kulia ndipo manga nae akajikuta hasira zinaisha akamkumbatia mwanamama huyo.....

Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 12

*CHAGUO SAHIHI*

SEHEMU YA....12
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)

Tulipoishia......
Mama Jarden hadi alianza kulia ndipo manga nae akajikuta hasira zinatisha akamkumbatia mwanamama huyo....

SONGA NAYO.....

Maisha yaliendelea ambapo hakuna kitu kilibadilika kwa Jaden.
Manga alilazimika sasa kuwasomesha watoto wake yeye mwenyewe kwa shule za serikalini.

ilifika mahali hata suala la mapenzi kwa Jaden manga alilitoa kabisa.
Alifika mahali alichoka kuendelea kuvumilia alikata shauri kuendelea na maisha yake.

Manga alifikia hatua hadi ya kifungua genge eneo la nyuma na pale nyumbani baada ya kuona kuna uhitaji wa genge Sehemu ille.

Alilazimika kuwa anafanya shuhuli zake nyumbani na kisha kwenda gengeni kutafuta hela.

mama Jarden alikuwa alimpenda sana manga hadi umri umesogea na akaanza kuumwa maradhi ya utu uzima manga ndie alikuwa akimhudumia kwa kila hatua.

Jarden hakuwahi kuoa tena zaidi aliishia kutembea tu na wanawake tofauti tofauti.


Miaka ilizidi kusonga na Binti Nafsa alikuwa mdada wa maana kabisa.
Alikuwa ni kipenzi cha Mr jarden, kila ambacho Jarden alilifanya kiwe ni cha maendeleo au laa basi ni Nafsa ndie alikuwa mshauri wake.

Binti alijawa na maringo na jeuri ya hali ya juu.

Alikuwa ni binti anaetembea na mwanaume anayemtaka mwenye pesa.
Hilo alifudishwa na shangazi yake Joan.

Joan alimfanya Nafsa azidi kujiona ni mwanamke wa thamani Kiasi kwamba hata wanaume anaotakiwa kuwa nao pia ni wa thamani.

Basi hayo ndio yalikuwa maisha yake na miaka ilisonga na kusonga na kusonga.

*******

ilikuwa ni majira ya Asubuhi katika hospital ya Taifa, kuna wanafunzi ambao walitakiwa kufanya field katika chuo icho sasa kuna majukumu ambayo walitakiwa kupewa kuanza kazi.

Basi mala punde waliitwa katika semina fupi kwa ajili ya kusikiliza.

Maelekezo yalitolewa pale na baada ya kama saa moja wote walitawanyika.

Binti mmoja wa makamo kiasi miaka 21, alikuwa ni mrefu, rangi yake kahawia mrembo kwelikweli.
Alionekana kuwa amefumba macho huku akitembea anazungumza,

"Ohhhh naomba dua, nifaulu katika hii field nihitimu chuo...
Huyu daktari niliepangiwa kuwa sambamba nae asiwe mkali nikafeli mimi.

Mama yangu amenisomesha kwa tabu sana naomba nifaulu".

Basi mala binti akashtuka amepamiana na mtu.

Haaaa....hii ilitokea yeye binti amefumba macho anaomba huku anatembea alafu na yule aliekuja mbele yake nae alikuwa akitumia simu huku anatembea basi hawakuonana.

"Samahani kaka samahani nisamehe... nisamehe tafadhali".

"Ok usijali samahani pia".

Alikuwa ni daktar handsome si haba akaendelea na safari yake alipokuwa anakwenda.

Basi binti yule akafika katika ghorofa aliyotakiwa kwenda alitembea hakupanda lifti mpaka katika chumba cha mlango kilichoandikwa,

"Dr Michael".

Alijaribu kugonga ila hapakuonesha dalili ya kuwepo kwa mtu.

alisimama pale na punde kupitia lifti alifika yule daktari ambaye alipamiana nae njiani.

Daktari yule alisoma kuna faili alilishika,

"Dr Nayla jarden ni wewe?"

"Ndio...ndio ni mimi"

"Ok nilifuata faili hapa nilipigiwa simu kwamba yupo daktari mtarajiwa ambaye nitakuwa nae sikujua kama ndie wewe....nice to meet you....am doctor Michael"

"Asante naitwa Nayla jarden kama ulivyoniita".

Waliingia ndani ya ofisi ile ambapo Dr michael alionekana kuwa mcheshi sana walianza kwa kupiga story ile kujuana.

Katika maongezi yale Ndipo Nayla alimtambua Michael kuwa kwao ni pale Tanzania ila alikwenda nje ya nchi kuongeza elimu.

Nayla alijikuta anavutiwa sana kuona yule ni Daktari mkubwa.
Yeye anamalizia chuo mwaka wa 3 ila huyo anaeongozana nae amesoma miaka 7 jumla.

Mapokezi yalikuwa mazuri kwa nayla ni kama ambavyo alikuwa akiomba.

Majira ya jioni Nafsa alikuwa nyumbani eneo la nje amekaa na shangazi yake wanazungumza.

.
Maongezi yenyewe yalihusu masuala ya wanaume.

Nafsa alikuwa alimsimulia shangazi yake kuwa amekutana na mwanaume mwingine mzungu akiwa kazini
ivyo alie nae wakati huo anamuacha.

Joan alikuwa akimuunga mkono Ndipo mala Manga akatoka hadi nje pale.

"nimesikia inayozungumza ivi wewe Nafsa unataka hatma gani katika mahusiano yako? Kama huyo shangazi yako eti?.

Nawaona na sio mala ya kwanza hii ni wazi shangazi yako anakupotosha na isipoangalia utaishia kama yeye bila ndoa bila familia umri unaenda Nafsa".

"Heeeee!!! Makubwa haya...bibi tafadhali hayo maneno yako kamuambie mwanao si una mtoto wa kike wewe au? Sina utoto huo mie wa kuelekezwa na wewe sitaki niache.
Ndoa yako wewe mwenyewe umekushinda baba amemuacha haya ataniambia nini mimi? Zaidi ya miaka 10 upo hauna mume sasa cha ajabu nini mpaka uniseme mimi?.
Afadhali mie nina pesa baba yangu ana kampuni kubwa nipo princess wake unadhani nitachunda kama wewe unaeosha viombo tokea upo kijana mpaka unazeeka bado nyota hiyo ukawapa hadi watoto wako ovyo".

Nafsa aliyamaliza maneno yote hakuacha hata akiba.

Manga wala hakulia kama ilivyokuwa zamani, ni miaka mingi alishaozoea kejeli kama hizo.

Punde aliingia binti sasa nayla nae ndo akiwa anarudi.

Nafsa kumuona alicheka sana,

"Nakuona bado unapambana ohhhh pole mdogo wangu jamani huna hata gari yani unasoma kishamba sana sio kosa lako ni nyota mbaya ya mama yako......naweza kumlazimisha baba akununulie gari ikiwa utabadilika kuanzia kimavazi Yani kimuonekano.
Sio siri naona hata aibu kukutambulisha eti mdogo wangu kwa ivyo ulivyo.
Na hiyo fani unayosomea ndio unazidi kujichosha huna cha kuambulia".

Nayla alimshika mkono mama yake wakataka kuingia ndani Ndipo Nafsa akasema,

"Haya wenye mama zenu sie wengine tuna baba zetu".

Nayla alimtaka mama yake waingie ndani akamsimulia Furaha aliyo nayo kukutana na Dr michael.

Nayla kufika ndani kweli alimsimulia mama yake kila kitu.

"Mhh afadhali kubwa ujitajidi mwanangu".

Palepale mala simu ya nayla ikaita.

Binti kuangalia ni namba mpya aliyochukua siku hiyo ya Dr Michael.

Basi aliipokea ambapo Michael alikuwa akitaka kumjulia hali nayla kwamba amefika salama .

Baada ya nayla kumaliza kuzungumza Ndipo mama yake akamuambia,

"Mwanangu na iwe kwa ajili ya kazi , isije kuwa mambo mengine kama itahusisha wewe kutoa ngono Hapana usikubali mwanangu".

"Mama kuwa na amani ni mstarabu sana sana hakuna kitu kibaya....wacha nikaoge mama niingie jikoni kazi zilizobakia niachie mimi".

"Haya sawa na mdogo wako Kahan nae nimeongea nae mwanangu anapambana jeshini"

"Tunamuombea mama kila mahali ni utafutaji hakufaulu kuendelea na masomo hata huko jeshini naamini hatujapoteza mama.
Umetupambania sana watoto wako mama hadi hadi kufikia chuo ndio baba akaanza kunipa pesa unajua fika ".

"Haya mwanangu changamka, mimi nipo chumbani kwa bibi yako".

Manga aliinuka na kutoka chumbani huko kwa nayla.

full 1000.
what'sapp no 0716730000.

Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 13.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....11 Na  >>> https://gonga94.com/semajambo/chaguo-sahihi-sehemu-ya-11-na
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest