Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....2

19th Jul, 2025 Views 17

*CHAGUO SAHIHI*

SEHEMU YA....2
Na
Mamuh mohd
(0716730000)

Tulipoishia.....

"Hapana isiwe kweli, naamini Joan anatania tu, dada Yasinta lisikupate hili usiniache na siri kubwa isiwe kweli".

Alijisemea manga huku akihisi kubleed muda huo huo...

SONGA NAYO......

Baada ya masaa matatu kupita pia baba yake Na Jaden alifika Mkoani Kilimanjaro kwa usafiri wa ndege hadi Sehemu husika.

Alikuta hali halisi kijana wake hali ni mbaya hadi kapelekwa ICU na mkwewe hayupo tena.

ilibidi kwa siku ile wasikilizie hali ya Jaden lakini mpaka usiku unaingia hakufika ICU Wodi ndipo akaomba wahamishwe daresalam.

Jarden alihamisha kupitia gari ya wagonjwa usiku ule huku Baba Jaden na Kijana Tizo pamoja na miili ile walirudi kwa kutumia ndege asubuhi siku iliyofuata.

Walifika na kupelekwa na timu ambayo baba Jaden aliwasiliana nayo iwapokee.

Huku nyumbani kwa Mr Jaden ndipo taarifa sasa ilibidi ienee na watu kukusanyika kwa taratibu zingine kuendelea.

Baba Jaden kama msemaji mkubwa wa familia aliagiza watu wale wastiriwe tu maana hakuna ndugu aliyejitokeza wa yule kijana japo walitangaza kila mahali.

Kweli Taratibu zilikamilika na kuwastiri Yasinta na hamisi.

Wakati huo Jaden bado alikuwa wodi ya ICU katika hospital kubwa presha ikiwa inamsumbua.

Sio tu kumpoteza mkewe bali nampoteza katika mazingira ya kuumiza sana ndicho kikubwa kilimtesa Jaden.

Huku manga nae nyumba akiiona chungu kutwa akawa ni mtu wa kulia tu huku tumbo linamuuma.

*****

Baada ya wiki moja kupita ndipo Jaden alipata afuheni hata anarudishwa katika wodi ya kawaida.
Mtu pekee ambaye alikuwa faraja kwake hata alimuona hali inakuwa nzuri ni mtoto wake yule mdogo princess nafsa.

Mtoto yule alipelekwa hospital walau akawa tiba kwa baba yake.

Jaden hakutaka mtoto wake atoke karibu yake hata kwa sekunde moja, alikuwa ndie mtu wake wa kumliwaza.

Hali ile ilimfanya hata manga nae kuwa maeneno karibu na hospital kwani ndie mlezi mkubwa wa mtoto yule.

Basi mwezi mmoja baadae Jarden aliruhusiwa na kutoka hospital kuendelea na shughuli zake za kawaida.

Afya yake ilidhohofika kwa kiasi kikubwa sana.
Wafanyakazi wake warembo hawakuacha kujigonga kwake wakiamini jimbo sasa lipo wazi huwenda wakaonekana.

Kila mahali si kazini ,si kwenye gari hata nyumbani, jarden alikuwa akikaa anatazama picha ya mkewe huku machozi yakimtoka.

"Kwanini umeniachia maumivu makali kiasi hiki Yasinta, afadhali nisingejua hili kwanini Yasinta.
Ulikuwa unanisaliti kwanini Yasinta kwanini? Kipi ulikosa kwangu ahhhh".

Ni maneno ambayo jarden alikuwa alijiambia na kuishia kulia tu.

Familia ya Jaden mama na ndugu zake walihamia kuishi nyumbani kwa jarden nia wawe karibu na kijana wao huyo.

Pia mama Jaden alifanya hivyo ili pia awe karibu na mjukuu wake yule mdogo.

Sasa shuhuli ilikuwepo kwa kijana ambaye ni Tizo huyu ni binamu yake na jarden lakini alitokea kumpenda sana Manga.

Kila wakati akiwa jikoni alikuwa akimfuata,

"Hatima sasa imetufanya tunaishi nyumba moja bado hauamini jinsi gani Akipenda manga?".

"Tizo sina la ziada la kukuambia zaidi ya kwamba haiwezekani...mmekuja hapa kumliwaza ndugu yenu basi iwe ivyo mimi kwanza sipo sawa kabisa yani bado sielewi niache tu".

"Mhhh unajikuta keki sana manga eti? Wewe ni binti wa kazi tu fursa kama hizi zinakuja unajitia kubezi utazeeka unaosha viombo kwa watu ivi ivi".

Kashfa ambazo alizipokea manga kutoka kwa kijana huyo wa kuitwa Tizo.

Sasa wakati Tizo anarudi chumbani kwake mala akakutana na Joan mdogo na jarden akiwa anatokea chumbani kwa Tizo.

"Wewe ulikuwa unataka nini chumbani kwangu?"

"Hakutaka wewe binamu yangu Tizo nifanye nini ujue nakupenda why?"

"Unajichosha na kupoteza mda Joan sijawahi kufikilia hili sisi ni ndugu.
Angalia tupo ugenini hapa unaleta mapenzi wewe mzima kweli? Wifi yako amekutoka husikitiki unawaza ujinga".

"Mhhh uhuni wake ndio ulimponza kutaka wanaume wengi sasa mimi inanihusu nini? Tizo tuongee ya kwetu buana".

"Ebu toka nipishe".

Tizo aliingia chumbani kwake nae binti Joan akaingia na kufunga mlango hatujui nini kiliendelea hapo.

Manga alipomaliza kuandaa chakula alitenga mezani kwa maana kila mmoja muda ambao atahitaji kula basi ruhsa.

Mala alisikia akiitwa na Mama jarden,
"Manga binti yangu nawaza tuongeze msichana mwingine wa kazi ili awe anajisaidia na wewe uwe beneti na mtoto nahisi unachoka".

"Mama kama mtongeza msaidizi sawa lakini nipo sawa wala hakuna kazi hata.
Nguo nafua kwa mashine viombo, usafi na kupika wala sio kazi nikilinganisha na kulima kwetu".

"Sawa nashukuru hata ivyo tuna ugeni, ni shangazi yake na Yasinta anakuja kukaa hapa kwa muda kwa ajili ya mjukuu wake hakuweza kuja wakati wa matatizo nasikia alikuwa hospital alipata mshtuko pia.
Huyu ndie aliemlea Yasinta kwaiyo ni mzazi wake tutakuwa nae hapa".

"Sawa mama nadhani natakiwa kwenda kuandaa chumba kwa ajili yake".

"Sawa mwanangu natamani Joan angekusaidia lakini mwanangu huyu hataki kabisa kufanya kazi dukani kwake penyewe haendi anamuachia mtu auze yeye kutwa instagram na page yake ya udaku ".

"Hapana tatizo mama...karibu chakula".

Basi manga aliondoka na mwanamama huyo alibaki akimtazama alivutiwa nae kiasi fulani kwa upole na uchapa kazi aliokuwa nao binti huyo.

Kweli majira ya usiku Jarden alirudi nyumbani akiwa na wageni hao walikuwa wawili shangazi wa Yasinta kwa maana mkwe wake na pia alikuwepo binamu wa Yasinta mtoto wa shangazi yake alieitwa dorice.

Walipokelewa vizuri japo shangazi huyo aliyeitwa bi Mwamvua alifika na kuangua kilio kizito.

"Ant yangu ant uwiiiii ant Yasinta wangu nitamuomba nani sukari mimi nimeumbuka uwiiiiii uwiiii".

Alilia mwanamama huyo jambo ambalo liliibua simanzi upya kwa familia hiyo.

Baadae hali ilitulia na Watu kupata kuzungumza na kutambulishana.

Sasa baada ya yote muda wa kupumzika mwanamama huyo bi Mwamvua alikuwa na binti yake huyo aliyekuja nae dorice chumbani.

"Kama tulivyokubaliana Yasinta alikuwa sehemu nzuri tusikubali itupite jitingozeshe mwanangu uolewe wewe.
Kabla hata Yasinta hajaolewa unajua jinsi gani tulipambana huyu mwanaume awe wako lakini ikashindikana sasa bahati kubwa hii tena imejirudia".

"Mama safari hii ama zake ama zangu jarden hatoki mikononi Mwangu wacha kwanza tuisome hali ilivyo ".

"Sawa jitahidi mwanangu ohooo akiolewa mwanamke mwingine wa familia nyingine kwisha habari yetu".

Basi hapo ndipo tunapata kujua kumbe mbali na ndugu hao kufika katika nyumba hiyo kama Kuhani, lakini nao wana jambo lao buana 🀣🀣.

Muda mwingi wa ziada Jarden aliutumia kwenda Sehemu mbalimbali na mtoto wake pamoja na manga kama dada wa kazi kwa ajili ya mtoto.

Huko jarden alifurahi na mwanae walau ni inakuwa nafuu kwa upande wake.

*********

Mwezi mmoja ulipita Ndipo sasa bibie Dorice na mama yake walibakia hapo nyumbani huku mama jarden na Tizo pamoja na Joan walirudi nyumbani kwao.

Dorice ndipo akamuambia mama yake,
"Mama kuna kitu nimekiona ili niwe karibu na jarden huyu msichana wa kazi manga aondoke.

Huoni wanatoka mala wanakwenda kutembea ufukweni akiwa hayupo hiyo nafasi itakuwa ya kwangu mimi tupange namna aondoke".

"Wala haina kujipanga tunamuambia tu aende maana hata mimi nimeona hili ngoja nikamwambia Sasaivi".

Mwanamama bi Mwamvua akamfuata Manga akiwa jikoni anaosha viombo.

"Manga kuna kitu nataka kukwambia kwamba urudi tu nyumbani kwenu.
Boss aliekuajiri hayupo tena na mtoto sisi tupo mimi bibi yake na mama yake mdogo ivyo ungerudi kwenu walau nawe ukaanzishe familia yako umri unaenda".

"Hapana shangazi mimi nimeridhika kufanya kazi hapa isitoshe nimemzoea sana Nafsa tafadhali naomba niendelee kufanya kazi au kuna kitu nimewakwaza?"
"Hapana sio kwa ubaya nitakupa laki moja ya mtaji hata ukauze nyanya kwenu ".

Manga alipiga magoti,
"Nakuomba shangazi niendelee kubaki hapa nakuomba shangazi".

Bi Mwamvua kuona ivyo saa ngapi asiwe mkali sasa,

"Vipi wewe? Mkataa kwao mtumwa inang'ang'ania hapa nini? Au kutoka na jarden pamoja na mtoto unajikuta wewe ndio mkewake? Unasubiri nini sasa hapa.
Kama familia tumeona uondoke unakatalia nini sasa? Huna kwenu? Nenda kapanga kila kitu chako uondoke Sasaivi".

Manga alilia lakini bi Mwamvua aliungana na binti yake wakimtaka aondoke kwa nguvu.

Manga alifika hadi chumbani kwake akiwa analia akampigia simu Boss wake huyo jarden,

"Boss nakuomba niendelee kufanya kazi hapa naomba nisiondoke boss nakuomba... shangazi ananifukuza nakuomba nitetee boss nimemzoea nafsa atakuwa mpweke sana".

Jarden kusikia vile alimtaka Manga asiondoke nyumbani muda sio mrefu.

Basi manga akaamua kukaa tu ndani huku akilia sana.

Walimgongea mlango lakini binti hakufungua mlango.

Mr jarden akiwa anatoka usiku ofisini kwake katika eneo la mapokezi ndipo akashtuliwa na secretary wake.

"Boss nilikuwa nakutafuta kuna binti huyu amekuja kwa ajili ya usahili ulisema mda huu ndipo kutakuwa na usahili ".

Jarden alimtazama binti huyo ambaye alikuja kwa usahili na kumwambia,
"Samahani sana ila utafanyiwa usahili na msaidizi yupo katika kidogo ".

Kisha aliondoka nae msichana yule aliridhia kubwa hakuna kwake kilichobadilika.

Sasa Mr Jarden kufika nyumbani Ndipo alimanga alifungua mlango na kutoka.

"Mnamfukuza huyu manga nyie kama kina nani? Hapa? Kwanza nawashangaa kwanini mpo hapa mnapata ujasiri gani kwa kile alichokifanya ndugu yenu na bado mpo kama hakuna kilichotokea.
Nilijikaza tu kuwaambia haya ila naomba msifuatilie familia yangu muacheni huyu ni mlezi wa mwanangu kisha nyie mmeshatupa pole asante mnaweza kuondoka".

Aliongea Mr Jaden hata bi Mwamvua na binti yake pozi liliwashuka.
Jarden anawamalizia hasira wao kwa kile alichokifanya Yasinta.

Jarden alielekea zake chumbani kwake ndipo manga akamfuata,

"Boss asante sana kwa kunitetea umerudi kwa ajili ya kunitetea hakika nashukuru sana".

"Ni kwa ajili ya utendaji kazi wako tu na sio kingine manga kwaiyo unaweza kwenda kuendelea na kazi zako".

Manga alijibu kwa kutikisa kichwa na basi akarudi kuendelea na majukumu yake....

Full 1000.
Whatsapp no 0716730000.

Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 3.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....2  >>> https://gonga94.com/semajambo/chaguo-sahihi-sehemu-ya-2
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest