*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....3 Na
SEHEMU YA....3
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia......
Manga alijibu kwa kutikisa kichwa na basi akarudi kuendeleza na majukumu yake.....
SONGA NAYO......
Bi.mwamvua na binti yake mambo yaliwageukia ilibidi sasa wakapange nguo zao waondoke.
Hawakutegemea kama Jarden angewatolea uvivu wa namna ile.
"Mama tungemuomba msamaha tukabaki kuendelea kukaa hapa mama".
"Mwanangu tumefeli wewe huoni kwa jinsi alivyoongea anaonekana kabisa anatuchukia, hatuwezi tena kukaa hapa mwanangu elewa hilo".
Basi walijiandaa na siku iliyofuata asubuhi na mapema waliondoka zao.
********
Baada ya siku mbili kupita mrembo wa kuitwa Nancy alianza kazi katika ofisi ya Mr jarden baada ya kufuzu katika Usahili wake.
Alikuwa ni mchapa kazi mzuri kiasi cha kuwa karibu sana na Mr jarden hadi wakazoeana.
Mala ambapo Nancy alimuona jarden hayupo sawa basi alipenda kumuomba watoke out kwa ajili ya kurefresh wote pamoja.
Nancy alifahamu alionekana kama mtu ambaye anafahamu yote yanayomuhusu mr jarden na ndio maana alikuwa akitumia nafasi hiyo kumliwaza.
Basi walijikuta wameingia katika mahusiano ya kimapenzi.
Waliodumu kwa takriban miezi Sita ndipo jarden akaamua kutangaza ndoa.
Mr jarden alikwenda mpaka nyumbani kwa wazazi wake na kuwaambia suala lile.
Baba yake jarden alimuu ninga mkono kijana wake kwani alichokuwa anataka ni kuona mwanae ana furaha tu.
Lakini mama jarden kwake alilipokea lile kwa utofauti,
"Mwanangu unauhakika imechagua chagua sahihi kwako? Kumbuka ni mapema bado tokea yatokee yale matatizo kuwa makini.
Una mtoto tazama anahitaji kupata malezi mazuri je huyo mwanamke unamuona ni sahihi? Bado una waamini wanawake wa mjini".
"Mama yeye ndie chanzo mpaka walau nimefikia katika hali hii, nafurahi,naenjoy ni kwa sababu yake kwaiyo namuamini sana"
"Sawa kama ni ivyo basi na iwe heri mlete nyumbani tumuone".
"Hilo ndilo la msingi mama nadhani kesho nitamleta".
Walikubaliana na kweli siku iliyofuata jarden alikwenda kumtambulisha Nancy kwa wazazi wake ivyo ndoa ikapangwa.
Nancy alikuwa akiishi na baba yake tu na maisha yao yalikuwa ya kawaida ivyo Nancy kupata kazi ndo kama walionekana kuwa na ahueni ya maisha.
Ndoa ilifungwa na maisha yakaendelea.
Awali Nancy alionesha kuwa anampenda mtoto nafsa ambaye sasa ni mwanae wa kambo.
Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda alianza kumchukia mtoto yule.
Hakuwa akimpa nafasi kabisa ya kukaa nae pamoja wala kujua chochote kinachomuhusu mtoto yule.
Manga alilishtukia lakini halikumsumbua kwa kuwa yeye yupo na anamjali mtoto yule basi kwake ilitosha kufanya majukumu yake.
Kitendo cha Jarden kuonesha kumpenda mtoto wake kiasi hata maeneo ambayo alikuwa wakienda kutembea basi mwanae pia alikuwepo.
Lile lilizidi kumkera Nancy aliona ni kama anakosa uhuru wa kuwa na mumewe.
Alitamani familia ikamilike kwa watoto ambao yeye akawazaa na Jarden na sio yule ambaye tayari alikuwepo.
Nancy aliona njia ni kumuwekea sumu mtoto yule akiamini Kama ni matatizo yatamuangukia Manga wote wataondoka kisha yeye atabaki na furaha katika mjengo ule.
Roho mbaya ilimjaa mrembo huyo sio kawaida.
Sasa kulikuwa na ukawaida kwamba mtoto akitoka shule anakunywa ajuice tu na manga alikuwa akimuandalia na kuiweka mezani.
Alichokifanya Nancy siku ile ni kuwahi kurudi nyumbani alafu kisha akaweka sumu katika juice ile akimlenga Nafsa akipewa tu lolote limkute.
Lakini wakati anatoka Upande wa mlango wa nyuma alikuwa anaingia Manga akashangaa tu kukuta juice kama imetingishwa na Nancy akiondoka haraka haraka.
Alijiuliza kwa haraka haraka kuwa madam huyo alikuwa akitumia kinywaji kile au vipi?.
Hakuwaza kibaya ivyo Aliendelea na shuhuli zake.
Sasa kama kawaida mda wa mtoto kurudi nyumbani ulipofika Manga alimuandaa kwa kumbadilisha nguo na kisha Akamuandalia juice anywe kisha akacheze kama kawaida.
Alimuacha mtoto akiendelea kunywa juice huku akicheza game katika Tablet alionunuliwa na baba yake.
Manga akiwa jikoni anaosha viombo si ndio mala mtoto yule akamfuata akiwa anakohoa huku anatapika.
"Nafsa unajisikiaje? Kuna nini? Niambie nini mamaaa".
Alimbeba ndipo mtoto yule akaanza kutapika mapovu.
Manga alishtuka akahisi basi amekula kitu sio kizuri.
Kuna maziwa katika fridge yalikuwepo Ndipo akamimina na kumnywesha mtoto yule.
Kisha bado hakuridhika alitoka na mtoto yule huku amechanganyikiwa machozi yanatoka kumuwahisha hospital.
Alijihisi yeye ni kama mama kwa mtoto yule,alijihisi ni kama Yasinta kamuachia mtoto yule amlee yeye ivyo nae alimpokea mtoto yule kama wa kwake.
Bahati alibahatika kufika hospital na mtoto yule alipokelewa emergency kwa ajili ya uchunguzi kuanza.
Bahati sumu ile haikusambaa kuleta shida kwa mtoto ivyo kuna drip aliwekewa nafsa huku manga akiwa anamshikia mkono drip ipite vizuri.
Wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni mama yake Jarden akafika haraka hospital na kumkuta Manga akiwa na mtoto yule wodini.
"Manga nini kinaendelea siku zote asinywe sumu akanywe leo kweli?".
"Mama sio kwa ubaya lakini namuwazia vibaya dada Nancy nahisi ameweka nilimkuta maeneo ya pale dinning baada ya chakula cha mchana.
Sikujua alikuwa anafanya nini sikutaka kumuwazia vibaya ila kwa hili ni yeye mama.
Nimekosa ujasiri wa kumpigia simu kaka Jarden naogopa nitamuambia nini asinifikilie vibaya".
"Sawa nakuelewa nakuamini na isitoshe nakupenda sana manga.
Wewe sasa sio mfanyakazi bali ni kama ndugu kwetu.
Wacha tuone jarden nampigia simu aje na nitakueleza kila kitu alafu pengine niachie mimi kuna kitu nitafanya mbaya hatojificha".
Mwanamama huyu aliyekaa hekima ya hali ya juu Ndipo alimpigia simu Kijana wake jarden kumuambia yaliyotokea na kumtaka afike hospital pale.
Jarden alipofika alielezwa kilichotokea lakini hakuamini kwa haraka.
"Mama huwenda hiyo sumu hata shuleni huko mkewangu wala manga hakuna anaeweza kufanya ivyo ".
"Sawa Mwanangu tuishi humo lakini nataka uchagua moja kati ya haya mawili".
"Jambo gani mama?"
"Mtoto aje kuishi nyumbani kwangu au ufunge Cctv camera nyumbani kwako naamini kama kuna kitu kibaya utakijua lakini iwe siri yako asijue mtu mwingine yoyote zaidi yako ".
"Sawa mama nitafanya ivyo na nitaomba waniunganishie niwe natazama popote nilipo siwezi kukaa mbali na mwanangu nadhani unalijua hilo mama".
Basi walikubaliana hapo na kufikia usiku walirudi nyumbani jarden akiwa na Mwanae pamoja na manga.
Nancy alishangaa kuwaona wacha aanze kumfokea manga.
"Nipo chumbani ukashindwa kuniambia kilichotokea kwanini? Unaitaka kazi au huitaki.... mmewangu alivyofanya unaona ni sawa kweli?".
Mr jarden alimtaka Manga aingie ndani na mtoto kisha akabaki na mkewe.
"Usijali mkewangu huwenda alichanganyikiwa kwa hali ile ya mtoto hadi akashindwa kukuambia.
Mimi mwenyewe hakunipigia simu yani kaomba simu kampigia mama moja kwa moja hadi namba ya mama kaikumbuka kuliko ya kwangu".
"Mhhh lakini anatakiwa kujua kuwa mimi ndie mama Wa huyu mtoto sasaivi".
"Usijali mtazoeana tu".
Basi usiku ule ulipita kwa namna hiyo.
Baada ya siku kadhaa kupita hali ya nafsa ilikuwa sawa ndipo Jarden akaamua kufanya wazo kama la mama yake alivyomshauri.
Alimuaguza Manga kwenda super market na mkewe alimuacha ofisini kisha yeye akarudi nyumbani na mafundi kufunga Cctv camera.
Hakutaka mtu mwingine yoyote ajue kama njia ya kumlinda mtoto wake kutokana na kile kilichotokea.
Kila dakika macho yake yalikuwa ni kutazama tu hata akiwa ofisini na Sehemu zingine.
Wiki ilipita pasina kubaini kitu chochote.
Basi siku hiyo Bibie Nancy Alikwenda nyumbani kwa baba yake.
"Baba njia ile niliyojaribu nimeshindwa kiukweli sijui njia gani nyingine nitumie".
"Mhhhh mwanangu wewe lazima uwe malkia wa pale utimize nilichokutuma katika ile familia".
"Baba mimi nataka kufanya kazi uliyonipa kisha niishi na jarden waumize wengine wote sio Jarden ".
"Haya njia ya pili tutume watu wamteke shuleni yule mtoto hapo vipi".
Nancy kuambiwa vile akaona sawa akatikisa kichwa.
Hapo ndipo tunapata kujua kumbe Nancy anaendeshwa na baba yake kufanya hayo anayofanya hatujui ni kwa sababu gani tutajua hapo baadae....
Full 1000.
Whatsa no 0716730000.
Tukutane Sehemu ya ....4
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni