*CHAGUO SAHIHI*
SEHEMU YA....4
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia.......
"Baba mimi nataka kufanya kazi uliyonipa kisha niishie na jarden waumize wengine wote sio Jarden".
"Haya njia ya pili tutume watu wamteke shuleni yule mtoto hapo vipi".
Nancy kuambiwa vile akaona sawa akatikisa kichwa.
Hapo ndipo tunapata kujua kumbe Nancy anaendeshwa na baba yake kufanya hayo anayoyafanya .....
SONGA NAYO.......
Wiki moja ulipita ndipo siku hiyo muda ulipita ambao mtoto nafsa huwa anarudi nyumbani lakini haikuwa ivyo.
Siku hiyo Manga alisubiri pasina kuona mtoto akifika.
Punde alirudi Nancy mapema ndipo manga kumuona akamuwahi.
"Habari za kazini dada?"
"Nzuri vipi?"
"Samahani nilikuwa nataka kuwapigia simu hapa mtoto hajarudi mpaka sasaivi labda muwasiliane na walimu wao kama wamechelewa kutolewa leo".
"Ok sawa nashuhulikia".
Alijibu Nancy bila hata kuonesha mshtuko sana kisha akaondoka zake kuelekea chumbani.
Manga alibaki akisikilizia kama dakika 5 akaona Nancy hatoki chumbani kumueleza kama labda kashafanya mawasiliano kabaini chochote.
Wasiwasi alionao manga akajikuta anashindwa kusuburi ndipo akaelekea chumbani kwa Boss wake huyo ili amuulize yeye walau apate nafuu.
Basi kabla hajagonga mlango akamsikia Nancy akiwa anazungumza na simu.
"Sawa baba mmeshamteka huyo mtoto kinachofuata nini? Kuweni makini sana sana.
nimempigia simu Jarden amechanganyikiwa akienda polisi lazima watachunguza sana kuweni makini....haya kila kitu nitakuwa nawaambia".
Manga alishtuka haraka akaondoka hapo hadi chumbani kwake.
Alipata kuujua ukweli wa Nancy akaona hata asinyamaze liwalo na liwe.
Alishika simu na kumpigia Mr jarden lakini simu kwa wakati ile ikawa haipokelewi.
Akaamua kumpigia Mama jarden na kumueleza ukweli ule wote aliousikia.
Kwa wakati ule mama jarden alikuwa katika gari akielekea katika kituo cha redio ili akatangaze kupotea huko kwa mjukuu wake.
Baada ya jarden kuwapigia simu wazazi wake basi kila mmoja alipanga lake ivyo mama jarden yeye aliwaza kwenda redioni.
Sasa alipopewa habari zile na manga ikabidi ampigie simu kijana Tizo ambae alijua atakuwa pamoja na jarden kwa Wakati huo.
"Haloo shangazi"
"Mpo wapi na kaka yako umebaini chochote kuhusu mtoto?"
"Hapana broo amechanganyikiwa tu hapa yaaani analia kama mtoto mdogo".
"Mpe simu muambie nataka kuzungumza nae kitu muhimu".
Tizo alifanya ivyo kama alivyoambiwa Ndipo jarden akapata kuzungumza na simu ile,
"Haloo mama"
"Jarden nisikilize kuna kitu manga ameniambia sasa kama ni kweli tutajua angalia kupitia vile tulipoongea ".
Basi Jarden ikabidi awe mpole kwanza akarudi katika katika gari lake nia kutazama.
Aliunganisha kiasi cha kuweza kuangalia Cctv camera ya nyumbani kwake akiwa kwenye gari au ofisini.
Alifuatilia hatua kwa hatua ndipo akaona wakati ambao Nancy alirudi nyumbani na kupewa habari zile na manga.
Pia alimuona Nancy alipoingia Chumbani na kufanya mawasiliano yote.
Alisikia kila kilichozungumzwa hapo sasa ndo ilikuwa balaa.
Bila kusema kitu Jarden alishuka kwenye gari huku Tizo akiwa amepigwa na mshangao.
"Nini kimetokea kaka umeingia kwenye gari yako mala umeshuka usemi kitu kuna nini?"
"Mhhh subiri Tizo kila kitu kipo sawa turudi kwa polisi".
ilibidi waende tena kwa polisi jarden akawapa maelekezo kuwa waende nyumbani kwake wakamkamate Nancy.
Aliwaeleza ukweli ule wote ikabidi waanze safari sasa kuelekea nyumbani kwa Jarden.
Baada ya muda kidogo walifika na bila kupoteza muda Nancy alishikwa kama mtuhumiwa.
"Kuna nini mmewangu mbona mmekuja mnanikamata mimi?"
"Utakwenda kuyajua haya na mengine kituoni Nancy".
Nancy alipata wasiwasi sana lakini alijikaza na kupanda kwenye gari kuelekea polisi.
Jarden alimtazama manga ambae alijawa na wasiwasi kisha akaondoka pasina kusema chochote.
Punde alifika mama Jarden nyumbani hapo kwa Jarden na kumkuta Manga.
"Asante sana umekuwa masada mkubwa sana katika familia hii mwanangu atasema wapi mtoto alipo na ameolewa hapa ana nia gani".
"Mama vipi kama atakana na kunisingizia mimi naogopa sana".
"Hawezi upo ushahidi na umeshapatikana Hawezi kukataa kwaiyo kuwa na amani".
Manga alibaki ameduwaa hajui huo ushahidi ni upi na umetokea wapi.
Basi Nancy kufika polisi ndipo aliambiwa kila kitu, Jarden hakubakisha jambo alimueleza ukweli wote kwamba alifunga Cctv camera.
Nancy hakujua aseme nini kwani aliumbuka.
"Nisemehe Jarden naomba nisamehe tafadhali ".
Mbele ya polisi pale alipokea makofi kutoka kwa Jarden,
"Cha kwanza namtaka mwanangu kabla ya kila kitu kuendelea unajua yule ndie mboni yangu aliyobakia? Yule ndie sababu ya mimi kuwa ivi unavyoniona nina Furaha ni kwa sababu yake nampenda sana sana tena sana ".
Nancy alilia sana akaamua kusema ukweli kuwa alitumwa na bwana ambae anajulikana kama ndie baba yake mzazi Nancy lakini kumbe haikuwa ivyo.
Alieleza ukweli kuwa huyo sie baba yake mzazi ila walipanga tu iwe ivyo akiwa hajui sababu nini.
Walimtaka Nancy awapeleke nyumbani kwa baba yake huyo ambaye jina halisi aliitwa bwana msame.
Kufika huko walimkuta bwana msame ndipo kuona Nancy amefika akiwa analia pamoja na mapolisi alielewa kuwa wamekamatwa.
"Nancy umefanya nini Nancy umeamua kunizalilisha si ndio?"
"Nisamehe baba nimekamatwa".
Bwana msame Palepale aliwekwa chini ya ulinzi na kushurutishwa aseme wapi mtoto alipo.
Nancy alikagua vyumba vyote pale na kutoka akiwa na Mtoto yule nafsa.
Jarden alimchukua mwanae anamkumbatia.
Huku bwana msame na Nancy wote waliwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi kufunguliwa.
Kufika kituo cha polisi bwana msame alibanwa sana aseme kwanini alimtuma Nancy kufanya kitendo hicho aligoma kabisa kusema.
Alipewa adhabu kali mpaka alikiri kusema ukweli.
Alimuambia Jarden,
"Kama unataka kuujua ukweli kwanini nimefanya ivi basi njoo na wazazi wako utajua kila kitu".
"Wazazi wangu? Wewe unawajua wazazi wangu? Umewajuaje?"
"Majibu hayo yote ukitaka kuyajua fanya kama Nanyokwambia njoo na wazazi wako hapa".
Jarden alikosa cha kusema alijawa na shauku ya kujua kwanini bwana msame kamuambia aende na wazazi wake.
Muda ulikuwa umekwenda usiku ovyo alirudi nyumbani na mtoto wake pamoja na kijana yule Tizo.
Kufika alimkuta mama yake bado yupo nyumbani pale akamuelezea kila kitu.
Walikubaliana kuwa siku
inayofuata wataenda wote sasa huko polisi wakajue ukweli.
Basi kweli siku iliyofuata wote walielekea polisi.
Hadi Manga pia alikwenda kwa ajili ya kuwa karibu na mtoto kwani mtoto huyo alitakiwa kuwepo kwa kuwa kesi ilimuhusu.
Basi kufika familia walikaa katika chumba cha askari mkuu wa kituo na punde watuhumiwa Nancy na bwana msame walifika wakiwa wamefungwa pingu.
Mama Jarden kumuona Bwana msame alimshangaa sio kawaida.
Bwana msame ndipo akawaambia,
"Asanteni sana kwa hili lakini Jarden ulitaka kujua ukweli sasa muambie mama yako akuambie ukweli mbele ya baba yako hapa akikataa nitakuambia mimi".
Mama Jarden aliinuka huku jasho zinamtoka.
"Wewe mzeee haufai hata kusikilizwa unataka kuongea nini?kwamba Unatufahamu sisi au?"
"Mhhh naweza kuwa siwafahamu wote ila hakufahamu wewe na kijana wangu huyo jarden.
Muambie ukweli kuwa mimi ndiye baba yake mzazi huyo mumewako ulimbambikia tu sababu ana pesa mimi ukaniacha sema ukweli".
Wote walishtuka sio kawaida Manga haraka aliibuka na kutoka eneo la nnje kwanza maana aliona mambo mazito.
Mama Jarden alikataa kata kata huku akilia na kumkana huyo mzee msame.
"Kama mimi nadanganya basi tufanyieni vipimo mimi ndie baba mzazi wa Jarden na nimefanya hivi kwa sababu zangu binafsi ili niwe karibu na damu yangu basiiii ".
Jarden alipata hasira akamkwida bwana msame.
"Siku zote ulikuwa wapi mjinga wewe hadi umejileta leo una njaa sio? Mama yangu hawezi kufanya ujinga kama huo hata siku moja ".
"Usiukimbie ukweli jarden tupime DNA itaamua majibu".
"Na iwe kweli laaa sivyo nitakunyonga kwa mikono yangu".
Aliongea kwa hasira na uchungu sana Jarden.....
Full 1000.
Whatsapp no 0716730000
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 5.