*CHAGUO SAHIHI*
SEHEMU YA....6
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia.....
Manga alimshika mkono boss wake huyo Taratibu walielekea katika boda boda ile wakapanda wote mishikaki kurudi nyumbani.....
SONGA NAYO........
Majira ya usiku Nyumbani alifika mwanasheria wa Mr Jarden.
Kufika alisema kuwa anahitaji kuzungumza na Joan lakini cha ajabu Joan hakuwepo nyumbani wakati ule.
Jarden Ndipo akamuambia,
"Karibu na kama kuna chochote niambie tu mimi nipo kijana mkubwa".
"Hapana wewe sio kijana wake Hilo lipo wazi mtoto wake wa pekee ni Joan".
Unapewa mwezi mmoja tu kurudisha kila kitu ambacho unakitumia cha hayati Rich Jarden".
"Hapana shida sio mali bali ni baba yangu yule ni baba yangu".
"Ukweli ulitoka na hakuna siri tena majibu ya DNA Hata hospital bado yapo na wakati wanapima Mr rich Jarden alinishirikisha mimi mwanasheria wake kuwa kuna vipimo vinapimwa ila kabla hajanipa matokeo Ndipo alizidiwa, nami nikafuatilia matokeo nikajua.
Nilikuja hapa kumueleza Joan kuwa yeye ndie mrithi kwa kila kitu.
Hata nyumba ile unayokaa ulipewa na Mr rich Jarden kwaiyo unatakiwa kuirudisha.
"Kwanini lakini? Nyumba ile alinizawadia katika harusi yangu na mkewangu Yasinta sio urithi ile bali alinipa kama zawadi".
"Basi ni Joan ndie ataamua hilo akuachie au urudishe.
Na hata katika kampuni ni Joan ndie ataamua Ubaki kama muajiriwa au akufukuze".
Jarden aliishiwa nguvu mambo yamebadilika gafla tu kwa upande wake ni maumivu juu ya maumivu.
Wakati hayo yanazungumzwa manga alikuwa karibu na sehemu hiyo kwa maana alisikia kila kitu mwanzo mpaka mwisho.
Alijikuta machozi yanamtoka akizingatia kuwa lile linalomkuta Jarden ndilo limejirudia hata kwa mtoto wake nafsa aliishiwa hata nguvu.
Sasa wakati huo Joan alikuwa hotelini na Kijana Tizo wakipeana mautamuπ.
Walilala mpaka asubuhi Ndipo walirudi nyumbani.
Kuna ndugu Baba mdogo alikuwepo nyumbani pale bado hajaondoka huyu ni mdogo wake na Rich Jarden.
Alipomuona Joan anashuka kwenye gari na Tizo akawafuata,
"Nyie mwanasheria jana alikuwa hapa alitaka kuonana na wewe Joan mlikuwa wapi?".
"Mwanasheria nitampigia simu anipe muongozo alitaka kusema nini na kuhusu tulipokuwa sidhani kama inakuhusu ila nadhani kinachokuhusu wewe zaidi ni kuomba nauli uondoke kwa sababu kama kaka yako umeshamstiri" .
Alijibu Joan kisha akaingia ndani na kumuacha baba mdogo huyo mdomo wazi. Kiranga kiruuuuπ€£π€£
Joan aliingia mpaka Ndani alipo mama yao,
"Mhhh wewe ndie chanzo mpaka baba yangu kapoteza maisha utaendelea kujiliza unipe hasira au unanyamaza?"
"Niache tafadhali Joan sipo sawa mwanangu naomba niache tu".
"Mhhh kaka Jarden yupo wapi?"
"Ameenda mahakamani kuhusu kesi ya yule bwana msame"
"Ohhh sawa wacha amfunge tu namsubiri".
"Joan naamini hakuna chochote kitakachobadilika si ndio?"
"Mhhh unanipangia cha kufanya? Mimi ndie mrithi wa Baba yangu naamua nini nafanya na nini naacha.
Kaka Jarden kwa niaba ya kale katoto kadogo watakuja kuishi hapa ile nyumba kule nataka kuiuza haraka sana.
Account ya kampuni mwanasheria ameshalock zote na password sasa ninazo mimi hakuna pesa zitatoka bila idhini yangu".
Kweli huko mahakamani Kesi ilienda haraka na bwana msame alikubwa na hatia ya kumteka mtoto na kushirikia mauaji ya Rich Jarden walimbambikia na hilo.
ivyo alihukumiwa kwenda jela miaka 30.
Huku Nancy alihukumiwa jela miaka 10.
******
Jioni Jarden alirudi nyumbani kwake anapoishi siku zote Ndipo alikuta walinzi ambao walimzuia kuingia ndani.
Alishangaa,
"Kuna nini kwani mbona ivi?"
"Hauruhusiwi kuingia bila ruhusa ya boss lady Joan".
"Mhh hapa ni kwangu lakini"
"Hayo ndio maagizo tuliyopewa".
Jarden alimpigia simu Joan na Ndipo binti akampa maagizo hayo kuwa labda akachukue nguo tu lakini hakuna kingine nyumba sio yake tena.
Alimueleza kila kitu hadi kuhusu pesa za account zote zimelock.
Jarden alirudi kwenye gari na kwenda hadi nyumbani kwao kule akaonane na Joan uso kwa uso.
"Unawezaje kufanya ivyo Joan bila kuniambia? Account ya kampuni kuna pesa zangu nyingi sana niliweka huko kwa ajili ya kuendesha kampuni.
Kuna wakati kampuni iliyumba na sikutaka kumpa baba mawazo nikaweka pesa zangu humo nia nizalishe kwanza Nilikuwa na uchungu na kampuni yetu sikutaka iyumbe wewe unailock kwanini?.
Basi sawa nipatie pesa zangu zilizopo humo milioni 350 net".
"Ongea utakavyo Jarden ila nimemaliza kama mtoto wa pekee wa Rich Jarden.
Natamani hata hilo jina la familia yetu usitumie basi tu ndo baba alikupa ila hufai.
Q
Utaishi hapa kwa muda hadi mtoto huyo akue na huyo Manga aendelee kuwa kijakazi hapa mimi nitakuwa boss wake.
Kuhusu kampuni utaendelea kufanya kazi kama mfanyakazi wa kawaida usijihusishe na chochote nitakuwa na kulipa mshahara.
Yote ni hisani kwa kuwa tumechangia mama laa sivyo ungeondoka na nguo zako tu.
Mkurugenzi mpya atakuwa ni Tizo atleast baba ni mjomba wake sio wewe mtoto wa kambo tu".
Wakati yote yanaendelea mama Jarden alikuwa akilia sana Furaha aliyoitengeneza kwa miaka mingi kwa kuficha ukweli hatimae ukweli umejulikana na kuleta sasa mpasuko mkubwa.
Jarden aliny'ong'onyea ni kama kamwagiwa maji ya baridi..
Alitoka nnje huku machozi yakimtoka.
Bahati mbaya na hali ya hewa ulikuwa ni ya mvua mvua basi ndio ilikazana kunyesha lakini Jarden wala hakuisikia kwa uchungu na maumivu aliyokuwa nayo.
Baada ya kama dakika 10 alifika Manga akiwa na mwamvuli na kumfunika Jarden.
"Haisaidii iki inachokifanya hakitasaidia zaidi ya kujiletea matatizo tena.
Kweli unahitaji utulivu kwa kipindi hiki lakini sio kwa namna hii ni hatari.
Kwa sasa unatakiwa kuwa jasiri kwa ajili ya nafsa boss..
inuka tena pambana.
Watakunyima na kukupokonya kila kitu ila kuna vitu vikubwa ambavyo hawana uwezo wa kukupokonya na ndiyo vya muhimu kwako .
Afya njema ni kumuomba Mungu na pili elimu yako iliyo kichwani ivyo vitu ndivyo vya muhimu kwako kuliko nyumba wala magari.
Ukimaliza afya njema na elimu uliyo nayo Mungu atakupa vingine kama ivi.
Usishindane kubali kuanguka ili upate nafasi ya kuinuka tena".
Jarden aliinua uso wake na kumtazama manga binti aliejaliwa mali kauli nzuri kabisa.
Alimuona huyo ndie mtu pekee aliekuwa upande wake mpaka wakati huo.
Basi manga alinyoosha mkono kumpa ishara Jarden amshikie na ainuke na taratibu wakarudi ndani.
Lakini wakati yote hayo yanaendelea Tizo alikuwa juu gorofani akiwaangalia huku anaumia kwelikweli.
Kutoka katika uvungu wa moyo wake anampenda sana sana Manga ila Joan kamkubali sababu ya mali tu.
Sasa kuona manga anamjali Jarden mpaka kamfuata katika mvua ile kubwa aliumia kwelikweli.
"Nadhani natakiwa kufanya namna Joan amfukuze kabisa Jarden hapa nibakie na manga nimtumie kwa upendo na Joan nimtumie kwa mali".
Alijisemea Tizo ambaye sasa alihisi yupo juu ya Jarden yeye ndo kidume.
Manga alimpeleka Jarden mpaka chumba ambacho atakuwa anakitumia.
"Badili nguo nilizileta..niliposikia leo asubuhi dada Joan anasema tutakaa hapa nikafuata nguo zetu Kwaiyo nimekuwekea chumba hiki".
"Asante sana manga asante sana kwa kunipa bega lako niegemee walau nipate kulia kwa utulivu"
"Usijali boss muda wowote saa yoyote usilie peke yako njoo uegemee katika bega langu ndipo ulie" .
Basi manga ile anarudi akaendelee na kazi zake mala akakutana na Tizo uso kwa uso.
"Kaka Tizo".
"Usiku uje chumbani kwangu kile kule kona ni lazima sio ombi kwa faida yako".
Kisha Tizo aliondoka zake.
Manga alibaki tu anamtazama walishamzoea si mala ya kwanza kumtamani ila sasa ni kama kawa serious......
Full 1000.
Whatsapp no 0716730000.
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 7
*CHAGUO SAHIHI*
SEHEMU YA....7
Na
Mamuh mohd
(0716730000)
Tulipoishia........
Kisha Tizo aliondoka zake.
Manga alibaki tu anamtazama walishamzoea si mala ya kwanza kumtamani ila sasa ni kama kawa serious....
SONGA NAYO.......
Usiku ule Tizo akiwa chumbani kwake kwa hamu akimsubiri manga Ndipo kweli akasikia mlango ukigonga.
Alijua ni manga huyo atakuwa kajileta mwenyewe basi akaenda kufungua kwa Furaha kabisa.
Sasa ile kufungua mlango akashangaa kumuona ni Joan.
"Mhhh naanzaje kulala bila wewe Tizo tutalala chumba kimoja".
"Joan hii sio sawa unadhani watatufikiliaje?"
"Kwani kuna mtu unamuogopa mpaka hapa tulipofikia? Hatupaswi kumuogopa mtu yoyote".
Kisha Joan alifunga mlango na kujitupia kitandani
Tizo alitaka kuwa mkali lakini akakumbika kwamba hatakiwi kumkwaza Joan kwa vyovyote vile kwa kuwa ana pesa.
Hofu yake kubwa ilikuwa ni kama manga atafika chumbani hapo nae.
Lakini haikuwa ivyo mpaka asubuhi manga hakwenda chumbani kwa Tizo.
Basi siku iliyofuata walitoka pamoja Joan akiwa na Tizo hadi kwenye gari.
Walielekea katika ofisi ambayo Jarden ndo alikuwa alitambulika kama meneger.
Joan aliwaita wafanyakazi wote na kuwatambulisha kuwa kuanzia wakati huo kiongozi mkuu ni yeye pamoja na Tizo.
Aliwataka wafanyakazi wale wamuone Jarden kama mfanyakazi mwenzao tu yaani wa kawaida.
Jarden alijisikia vibaya sana, alikuwa alivaa nguo za kawaida tofauti na wafanyakazi wengine ambao walikuwa wakivaa sare.
ilibidi sasa na yeye awe anavaa sare kama wafanyakazi wa kawaida.
Alikwenda katika ofisi yake ambayo aliizoea siku zote Akiwa kama meneger lakini sasa alitakiwa kutoka lile lilimuumiza sana.
Mala aliingia Tizo katika ofisi ile na kumkuta Jarden kajiinamia.
"Vipi brooo!!! Usiniambie bado haujakubali matokeo kuwa umeporomoka.
Yote hayo ni makosa ya mama yako mzazi kwaiyi kamlaumu yeye sio kukosa raha hapa.
Nataka kazi zitendeke kwa ufanisi mzuri.
Usisahau nakupa siku mbili ushone sare ya kazini wewe sio staff tena wa kuvaa nguo utakazo".
Jarden alikosa cha kusema alitoka ofisini pale huku machozi yakimtoka.
******
Basi hayo ndio yalikuwa maisha mapya ya Jarden.
Alipitia maneno ya kashfa kutoka kwa wafanyakazi wenzake, wengine walikuwa wakimcheka.
Kuna wengine walimzishia kuwa alimtoa mkewe kafara lakini imebuma kaumbuka.
Yote yale ni maneno ambayo alikuwa akiyapitia Jarden.
Hali ile ilisababisha Jarden kumchukia mama yake ,akawa haongei nae, wanaishi nyumba moja lakini hataki kabisa kuzungumza nae.
Upande wa kazini Tizo alikuwa hajui kazi, vitu vingi alikuwa bado havijui ivyo akawa anatumia Jarden kimabavu amfundishe.
Baada ya Tizo kupata uzoefu ndio alizidi kupata mapembe.
Alianza kuwa hamlipi mshahara Jarden akidai kwamba anaishi kwao anakula kwa mjomba wake ivyo kulipwa sio lazima.
Walifanyia Jarden manyanyaso ya kila aina.
ilifika mahali Jarden aliishiwa pesa kutokana na kulipa ada ya mtoto shule mahitaji kama nguo n.k ivyo aliishiwa pesa.
Hakuna ambaye alimuelewa Zaidi ya manga pekee.
ilifika mahali manga ndie akawa akampatia hadi nauli kutokana na akiba ya mshahara wake Ndipo Jarden anakwenda kazini.
Hali ya kutolipwa mshahara Jarden ilipozidi Ndipo jarden aliamua kuacha kazi katika ofisi ile na kwenda kuomba sehemu zingine.
Kutokana na uzoefu wake hakuchelewa alipata kazi kwa haraka.
Akiwa na manga ndipo alipokea simu ya kuchaguliwa kuanza kazi katika ofisi nyingine.
Jaden alifurahi sana.
"Nashukuru sana manga wacha nikaanza upya kama ambavyo unaniambiaga siku zote".
"Hivi ndiyo inatakiwa elimu yako inakupa kazi mahali popote ivyo haukuwa na haja ya kuteseka.
Uliyopita yanatosha.
Lakini kama hutojali kama unavyokwenda kuanza kazi Sehemu nyingine naomba uwe mwanzo mpya hata kwako na mama yako.
Yaishe ni mzazi alikuchagulia kilichokuwa bora kwako naamini hakuna mzazi anatamani kumpa maumivu mtoto wake tafadhali yaishe".
"Nakuelewa manga Kiukweli sasaivi wewe ndie mtu wa karibu sana kwangu kwa Furaha niliyokuwanayo ya kupata kazi mahali pengine.
Nakwenda kuzungumza na mama na kila kitu kinakuwa sawa".
Manga alifurahi kusikia ivyo basi na ikawa kweli ivyo.
Kitendo cha Jarden kupatana na mama yake hadi mama Jarden alipata nguvu walau alianza hata kufanya shuhuli ndogo ndogo.
"Joan binti yangu amebadilika sana na huyu Tizo ndie kambadilisha yani sielewi amekuwaje.
Siku hizi"
Aliongea mama Jarden huku bibie manga akiwa anamsikiliza tu.
Mwezi mmoja kupita ndipo Jaden alimfuata mama yake na kumuambia.
"Mama nimepata mkopo kazini kwa kuwa ni mfanyakazi mpya watakuwa wakinikataa kidogo kidogo.
"Hongera mwanangu kwa kuaminika ofisini mpaka kupata mkopo hongera sana".
"Asante mama lakini nahitaji kujipanga upya.
Nakwenda kupanga niwe huru niachane na masimango ya kila siku".
"Nakuelewa mwanangu.
Laiti ungekuwa umeshajiandaa mapema ningeomba twende wote lakini jipange kwanza"
"Usijali mama ila kuna kitu naomba kukuambia ili unisaidie"
"Mhhh sawa niambie mwanangu".
"Ni manga mama.... kiukweli nampenda sana manga nimetokea kumpenda sana manga nahitaji kuondoka nae tafadhali mwambie mama akikubali nipo tayari hata kumuoa".
"Ahhh habari njema sana hizi mwanangu umejuaje? Kutoka moyoni mwangu nampenda sana manga hujui tu, laiti usingeniambia basi mimi ndie ningekwambia".
"Mama Zungumza mad tafadhali mimi sina ujasiri nashindwa".
"Hilo niachie mimi usiku nitazungumza nae".
Walifurahi wenyewe Jarden na mama yake ..
Full 1000.
Whatsapp no 0716730000
Tukutane Sehemu ya 8.