Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....8 Na 9

30th Jul, 2025 Views 16

*CHAGUO SAHIHI*

SEHEMU YA....8
Na
Mamuh Mohd
0716730000

Tulipoishia....

"Hilo niachie mimi usiku nitazungumza nae".

Walifurahi wenyewe Jarden na mama yake....

SONGA NAYO......

Basi majira ya Usiku kweli mama Jarden alimuita manga chumbani kwake.

"Mama kwema kweli? Kiukweli nimeshtuka sana"

"Kuwa na amani binti yangu.
Nataka leo wewe na mjukuu wangu wote mlale chumbani kwangu".
Manga hakuwa na hiyana ivyo alikwenda chumbani kwa mama Jarden akiwa na mtoto yule nafsa.

Walianza kuzungumza mambo mbalimbali, mama Jarden ndipo akaanza kwa kumuuliza,

"Manga mwanangu bi hautamani labda siku upate mume uolewe na ukaanzishe familia yako".

"Mama hiyo ni ndoto ya kila mwanamke lakini kama ujuavyo mama yangu ni kubahatisha kumpata mume mwema mama.
Historia ya mama yangu huwa nikiikumbuka naamini ndoa sio jambo la kukurupukia.
Mpaka leo ana ulemavu wa maisha shauri ya kupata mwanaume ambaye kutwa alikuwa akimpiga sana".

"Ohhh ni kweli mwanangu lakini ikitokea umepata mwanaume sahihi naamini utakubali".

"Hakika mama".

"Basi mwanangu kuna hodi ya posa kwa ajili yako".
"Mama imewezekanaje? Hao wageni wamekuja lini? Mbona sijawaona".

"Mhhh wala hatoki mbali ni jarden amekuposa kwangu.
Katangaza nia kwamba anataka kukuoa.
Amepata Kaela kazini anatamani kuanzisha upya familia, kama ujuavyo wanaume kupata wanawake wa kuwalea vizuri huwafanya hata kuwa sawa kifikra.
Amekupenda wewe mwanangu.
Naomba mkubalie mkaanze maisha yenu polepole mtapata tu".

Manga hadi machozi yamemtoka,
"Mama kiukweli siwezi kusema Hapana lakini siamini kabisa".

"Huo ndio ukweli na inakubidi uamini mwanangu".

Manga bila hata kupapasa macho alikubali maana nae pia kuna vichembe vya upendo alikuwa navyo kwa jarden.

"Manga mwanangu ,wewe unamfahamu Jarden kwa muda mrefu kidogo.
Maumivu aliyopitia unayajua.
Kila kovu la kidonda chake basi wewe manga unajua chanzo chake.
Tafadhali nakuomba ukamsahaulishe yote haya.
Manga mwanangu wewe una upendo sina wasiwasi kuhusu nafisa alibaki hapa na mimi bibi yake ni sawa na hata akitaka akae kwako pia ni sawa sababu sina shaka na wewe katika malezi".

Manga alibaki akimsikiliza mwanamama huyo huku machozi yakimtoka.

Basi buana Taarifa zilifikia Jarden kuwa manga amekubali ivyo haraka taratibu zianze.

Manga alimalizana na wazazi wake kwa njia ya simu tu kijijini huko.
Mahari iliyotoka walitumiwa na wazazi wakatoa baraka zao.

Walikubaliana baada ya ndoa sasa Ndipo manga atampeleka mumewe kijijini kwao.

Habari zile ziliwafikia Joan pamoja na Tizo.

Tizo alishangaa na hata Joan pia.

"Kweli kaka jamani hadhi yake imeshuka.
Sasa amefikia kudate mpaka kutaka kumuoa beki 3 jamani jamani jamaniiii".

Aliongea kwa dharau sana Joan mpaka manga alisikia kashfa zile.

Huku Tizo ndo uzalendo ulimshinda hadi akamfuata manga jikoni.

"Wewe huna lolote kumbe Mjinga tu.
Kabisa unanikataa mimi mtu na pesa zangu inamtaka jarden aliekuwa boss wako.
Mwenyewe unahisi kwamba jarden atakuwa tajiri kama kipindi cha nyuma uishi nyumba nzuri.
Hahahahha sahau utakwenda kutesema mpaka utanikumbuka mimi mjinga wewe".

"Mapenzi sio pesa Tizo bali mapenzi ni hisia.
Sijali maisha gani tunakwenda kuishi kikubwa kwetu ni kupendana tu".

Tizo alimcheka sana Manga yaaani mpaka ilikuwa kero manga akaamua kumuacha na kuendelea na shughuli zake.

Siku ya ndoa ilifika Ambapo walialikwa viongozi wa dini na watu wawili watatu kushuhudia ndoa.

Joan na Tizo waliona ndoa ikiendelea wao walitoka zao wakiwa wanaelekea beach huko kuponda raha.

Mama Jarden aliwaona sasa akawafuta haraka,

"Joan karibu ndoa inafungwa sasaiv mnaenda wapi?".

"Ni wao mama na sisi wacha tukapange ya kwetu kwani kuna ubaya? Kukubali tu ndoa ifanyike nyumbani kwangu ni mchango tosha.
Huyo mwanao bado tu anahangaika na ndoa wakati hizo ndoa zake huwa zinamletea shida.

Hili ndoa yake ya mwisho ndio kabisaaaaa hadi mambo makubwa yameibuka na sasa anaoa wafanyakazi wa Ndani mhh haya".

Aliongea kwa dharau joan kisha akaondoka zake pamoja na Tizo.

Mama Jaden hakuongeza neno aliwatazama tu wawili hao hadi wakaondoka.

Jarden alifunga ndoa kwa mala nyingine tena na bibie manga pale.
Kisha kuna chai na maandazi ambayo yaliandaliwa watu wakapatiwa na ndoa ikawa imeisha.

Siku ileile waliondoka nyumbani pale kwa kuwa Jarden alikuwa ameshapanga Sehemu ya wao kukaa.

Manga alitamani kuondoka na mtoto yule nafsa lakini mama Jaden aliwazuia kwanza.

Aliwataka wakakae Fungate kwanza kisha watamfuata mtoto wao.

Kweli walifika Fungate wenyewe Wote wakiwa na furaha kwamba wanafungua ukurasa mpya.

Kufikia usiku Kiasi saa 4 ndipo Jarden alipigiwa simu na mama yake.

Alipewa taarifa ambazo zilimshtua sana.

Alipomaliza kuzungumza na simu Jarden akamuambia mkewe.

"Natakiwa kufika Hospital Joan na Tizo wamepata ajali.
inasemekana walilewa sana kwaiyo wakati wanarudi nyumbani wamepata ajali".

"Mmewangu nimeogopa sana tafadhali twende wote huko hospitali nina wasiwasi ".

"Sawa jiandae twende ".

Wote usiku ule waliwahi hospital.

Huko walimkuta mama Jaden akiwa analia tu.

"Mama jikaze usilie sasa mama".

"Ahhhh balaa gani hili? Wangenisikiliza wakabaki kushangilia harusi yenu haya yasingewakuta jamani.
Joan hali yake ndio sio nzuri kabisa mwanangu jamani".

Mama Jaden alikuwa analia tu, jarden sasa kama kijana wa kiume ikabidi kwanza akatafuta madaktari ajue hali ya wagonjwa wanaendelea.

Upande wa Tizo Alipata majereha madogo lakini Joan alivunjika mguu.
ilibidi matibabu juu yake yaanze ambayo yalichukua muda mrefu.

Kalibia miezi 6 ilipita ndipo Joan alipata kutengamaa kwa kuwekewa mguu bandia lakini bado alikuwa hawezi kutembea vizuri

Wakati huo Tizo alikuwa akiendesha kampuni Ovyo ovyo kwa huo muda wa miezi 6 kampuni ilikuwa ikidaiwa kutoka bank mbalimbali.

Tizo alikuwa hawezi kuzalisha kiasi kikubwa cha pesa mpaka wakati mwingine analazimika kukopa pesa bank za kuwaza kuendesha kampuni.

Hii pia ilichangiwa na tabia mbaya ya uhuni aliyokuwa nayo..

Joan aliyafahamu yote hayo aliishia kulia tu.

Alimuita kaka yake jarden nyumbani kwake kumuomba msamaha na kumtaka arudi katika kampuni yao.

"itakuwa ngumu Joan mdogo wangu kazini kwangu nimeaminika tayari nimetengemeza cv nzuri siwezi kuacha.
Naelewa ugumu niliokuwa napitia mpaka pesa zangu nyingi niliweka katika kampuni ilihitajika akili ya ziada sio rahisi tu".

"Kaka maji yameshamwagika tazama hali yangu nisaidie.....chukua hati ya nyumba yako ile ni ya kwako alikuzawadia baba ni Tizo ndie alinishawishi nikaichukua kwako.
Sina budi niuze hii nyumba na kampuni pia nilipe madeni ya watu".

Jaden alibaki kimya maana hakuwa na msaada katika hilo.

Basi Tizo baada ya kuona madeni yamemuelemea aliamua kuondoka na kwenda south Africa kujificha huku mzigo wote akumuachia Joan.

Joan alilazimika kuuza nyumba yao ile ya familia, magari, mashamba walau alipata nusu ya pesa ya kulipa.

Nusu iliyobaki ilibidi kampuni waiweke rehani na kupewa muda wa mwaka mmoja waigomboe lakini mwaka mmoja ukipita pasina kuigomboa basi watakuwa wamepoteza.

Joan sasa na mama yake Pamoja na jarden na familia yote walirudi katika nyumba ile ya Jaden baada Joan kumrudishia Jaden nyumba yake.

Manga alifurahi kuona mumewe Jaden sasa kila kitu chake kinaanza kurudi.
Heshima yake, nyumba yake aliamini na kila kitu chake kitarudi.

Kwa wakati huo manga alikuwa tayari ni mjamzito lakini hakuna kilichobadilika kwake.
Alimlea nafsa kama mwanae hakumfanya ajihisi amepungukiwa na chochote.

Muda ulikwenda Manga alijifungua salama nae pia mtoto wa kike.
Walifurahi na kumpokea kama familia na mtoto huyo aliitwa Nayla.

Watoto sasa walikuwa ni wawili katika familia nafsa mwenyewe miaka 10 kwa wakati huo na mtoto mdogo huyo alieitwa Nayla.

Haikuishia hapo tu baada ya miaka 5 tena kupita Manga alipata mtoto Mwingine tena wa kiume huyu alikuwa kipenzi zaidi kwa baba yake wa kuitwa Kahan.

Kwa wakati huo Nafsa alikuwa mdada yupo secondary kidato cha Pili.
Alikuwa akisoma shule ya boarding mkoa wa jirani tu...

Baada ya miaka miwili kupita ulifika wakati wa Nafsa kuhitimu elimu yake ya O level (kidato cha nne).

Wanafamilia walijiandaa kwa ajili ya kwenda shuleni kwao huko.

Joan alimfuata wifi yake manga na kumwambia,

"Tukienda wote atabaki mama mkwe wako tu hapa unaonaje usibaki nikaenda mimi na kaka".

"ingekuwa ivyo lakini jarden ana kikao kazini wiki hii hawezi kusafiri kwayo itabidi tuende sote".

"Alafu mama je atabaki peke yake na dada wa kazi?".

"Nafsa hatofurahi kama hatoniona mimi si unamjua anty yako alivyo kisirani".

"Mhhh unamuendekeza sana ndio shida mhhh haya ".

Manga alimuona wifi yake kama hajafurahishwa na lile basi katika kutaka kumfurahisha akakubali.

"Sawa basi nitabaki namuandalia ya hapa nyumbani itabidi niandae na hapa".

"Hilo ndo ulibakiza wifi yangu wewe mama wa nyumbani baki mimi nitakwenda na kurudi nae".

Manga aliona sawa basi akakubali.

Sasa Joan moyoni mwake alikuwa akijisemea,

"Kaka yangu maisha sasa yanamuendea vizuri unakazi ya kumjazia watoto tu kisa ana hela.
Mtoto wa familia hii ni nafsa hao wengine siwapendi hata kidogo.
ili litimie hili lazima nafsa awe upande wangu".

Ndicho alikuwa anakutaka Joan hakuacha roho mbaya yake.

ikiwa ni miaka 6 imepita tokea manga afunge ndoa na Jarden wakiishi kwa amani na furaha sasa balaa jipya linakwenda kuibuka..

Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 9

*CHAGUO SAHIHI*

SEHEMU YA....9
Na
Mamuh mohd
(0716730000)

Tulipoishia.......

ikiwa ni miaka 6 imepita tokea manga afunge ndoa na jarden wakiishi kwa amani na furaha sasa balaa jipya linakwenda kuibuka....

SONGA NAYO......

Basi siku iliwadia Joan alisafiri kwenda katika mahafali ya binti nafsa.

Kufika alionana na mtoto huyo ambapo nafsa alishangaa kumuona shangazi yake huyo amekuja akiwa peke yake.

"Anty mama na baba wapo wapi? Mbona upo peke yako? Au hawajajua?"

"Mhhh ndio mwanangu baba yako ana kazi za kiofisi lakini unajua jinsi anavyokupenda na Zaidi atakuandalia zawadi.
Shida ni huyo mama yako".

"Mama? Amepatwa na nini?"

"Ahhhh sikiliza tumalize shuhuli then tutaenda kulala hotelini nitakuambia kila kitu sawa".

"Lakini mama yupo salama si ndio? Usiniambie kuna shida yoyote because I can't handle it please ....you know how much nampenda mama".

"Ok nipo natangulia ukumbini nenda kaungane na marafiki zako part inaanza soon okay?".

Nafsa alikubali tu lakini moyoni mwake alianza kupata wasiwasi sana.

Alikosa raha akajikuta anakuwaza mama yake kwamba kwanini hajafika katika mahafali yake.

Hata wakati part inaendelea ambapo nafsa alichaguliwa kuonesha baadhi ya show mbele ya wageni wote.
Nafsa alishiriki lakini alionekana wazi alikosa Furaha kabisa.
Alihisi huwenda shangazi yake anamficha tu lakini mama yake pengine amepata shida.

Basi shuhuli ilimalizika na nafsa hakutaka hata kukata keki.

"Nafsa sasa kwanini umebadilika ivyo? Kuna shinda gani jamani?"

"Shida ni mama....nataka uniambie mama yangu kwanini hajafika, ikiwezekana Mpigie simu niongee nae ndipo nitakuwa na amani".

"Mhhh mwanangu natamani ungemfahamu vizuri upande wake wa pili hata usingekosa raha kiasi icho.
ivi unatambua kuwa yule sio mama yako mzazi? Yule ni mama mzazi wa Nayla na Kahan kwa sasa anawapenda sana watoto wake kuliko wewe.
Anawapambania watoto wake na sio wewe.
hiyo yote ni kwa sababu baba yako anakupenda sana wewe ndicho kimemuuma sasaivi naona kabisa ana chuki kwako.
Kuwa makini sana Nafsa mwanangu wewe mchunguze polepole utaona tu.
Natafuta sababu chungu nzima ndio maana hajaja kwenye graduation yako".

Nafsa kuambiwa vile basi alijawa sumu kweli, mtoto alikuwa ni kisirani yule mwenye hasira za karibu.

Basi siku iliyofuata ndio walirudi jijini Daresalam.
Nyumbani manga aliandaa mazingira ya part kwa ajili ya binti yao huyo.
Alisimamia kila kitu kuanzia mapambo na chakula n.k.

Alirudi Mr jarden anafurahia maandalizi yale.

"Lakini Mkewangu nilitarajia wewe ndiye ungeenda si unamjua Binti yako atasusa".

"Naamini atafurahia nilivyomuandalia wifi alinisihi nibaki namuangalia mama".

"Sawa naelekea uwanja wa ndege kuwapokea".

"Sawa nadhani mkifika kila kitu kitakuwa sawa".

Basi Jarden alijiandaa na kuelekea uwanja wa ndege.
Lakini kabla alipitia Katika duka la kuuza maua, alinunua ua zuri kwa ajili ya kumpatia binti yake pindi akikutana nae.

Alijua binti yake huwa anapenda sana chocolate,basi ndani ya ua lile akamuwekea chocolate zile classic kabisa.

Safari hadi uwanja wa ndege.

Kweli walifika nafsa akiwa na shangazi yake Joan.

"Congratulation my princess".

Aliongea Mr jaden na kumpatia ua nafsa.

Nafsa alilipokea ua lile na kulikanyaga chini.

"Kwa ajili gani wakati hamnipendi? Serious ,you were at work an what about mom she didn't attend at my graduation, I celebrate my graduation without you and momy ,and finally you are here at airport to give me flowers for what !!!?"

"Please don't do that my daughter....kuhusu mama yako tutalizungumza sawa?"

Nafsa akatangulia kwenye gari na kubaki Joan na kaka yake,

"Mhhh kaka inabidi uwe mkali kwa mkeo maana nilimuambia aje yeye lakini kakataa kadai ohhh anabakia na mama ivyo yani.
Kaka ulikosea sana kumuoa mfanyakazi wa ndani yani sasaivi anajikuta yeye ndie mama mjengo anaamua nini cha kufanya".

Jarden hakujibu kitu wakarudi wote kwenye gari na kurudi nyumbani.

Sasa wakati huo Manga ameshawakaribisha wageni, majirani zao na watoto wao ambao ni marafiki wa Nafsa kwa ajili ya kumpokea nafsa.

Baada ya nusu saa walifika nyumbani ndipo watu wote wakainuka wakampokee mlengwa wao.

Manga alikuwa mstari wa mbele kwenda kumlaki nafsa lakini cha ajabu binti alimsukuma mbele za watu.

"Nafsa mwanangu upo sawa mamaaa?"

"Acha unafiki wako na sitaki hiki mlichokiandaa hapa sitashiriki".

Nafsa alipitiliza kuingia ndani hadi bibi yake mama Jarden akishangaa.

Manga ikabidi amfuate lakini mumewe Jaden akamtaka kwanza waende chumbani.

"Kama mama umeshindindwa kumpa Furaha binti yangu? Umeshindwa kuwa mama bora kwake eti? Kwa kuwa na wewe una watoto wako.

Sikiliza hata uzae watoto mia kamwe hatokuja kupatikana mtoto nitakaempenda kuliko nafsa.
Binti yangu wa kwanza aliekuwa faraja yangu wakati napitia magumu.

Siku yake ya furaha leo umeifanya kuwa na huzuni sijapenda".

Manga alikosa hata cha kufanya yaaani alibaki ameduwaa mithili ya mtu aliyemwagiwa maji ya baridi bila kutegemea.

Lakini akikumbuka kwamba nnje kuna wageni waalikwa watabaki na mshangao.

Licha ya nafsa kumsukuma mbele za watu alimfuata binti huyo chumbani kwake na kumpigia magoti hadi machozi yanamtoka.

"Nisamehe mwanangu sitamani kukunyima raha binti yangu.
Nakuomba mwanangu nisamehe na uvae nguo yako nzuri niliyokuandalia ukaenjoy part na wenzako.
Marafiki zako kina Asha,Nancy, Michael wote wapo kwa ajili yako tafadhali mwanangu".

Nafsa kusikia vile akashangaa,

"Heeeee!!! Hadi Michael yupo? Ok ok naona nakuja".

Binti alikubali si kwa ajili ya kumsamehe mama yake bali ni kusikia kuna mtu anaitwa michal, nadhani ni kwa kuwa tayari ana miaka 16 Ameshakuwa mwali ivyo ana vihisia fulani fulani ivi.

Manga alijilazimisha tu lakini aliumia sana.
Akikumbuka jinsi alivyomlea nafsa tokea akiwa mdogo leo yeye ni wa kumzalilisha mbele za watu.

Maneno ya mumewe aliyomuambia, yalijirudia na kumuumiza sana kiasi macho yalishindwa kujikaza na kutiririsha machozi.

Mala alifika mama Jarden na kumshika mgongoni,

"Usilie mwanangu wewe ni shujaa umevumulia mengi sana.
Ni hatua za ukuaji watoto wanakuwa wajeuri ivi kwaiyo kuwa jasiri mwanangu simama kama mama".

"Ni kweli mama haya twende katika party nafsa anajiandaa anakuja".

"Haya mwanangu".

Manga alifunika kombe mwanaharamu apite basi akatoka nnje kuendelea na shuhuli....

Full 1000.
Whatsapp no 0716730000.

Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 10.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....8 Na 9  >>> https://gonga94.com/semajambo/chaguo-sahihi-sehemu-ya-8-na-9
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest