FATE TO LOVE YOU π 10 MTUNZI UHURU MEDIA Stephen na mama yake walitoka pale kituoni wakasimama nje na kuanza kujadiliana . " Stephen
" Bado siamini , Angelo ni wakili mkubwa sana hapa na kwa uwezo wa lina haiwezekani kabisa.
" Basi kutakuwa na mtu nyuma ya hili.
"Atakuwa ni nani?
" Sijui.
Walijadili mwishowe waliondoka bila kuwa na jibu.
Stephen alienda kupanda kwenye gari yake akaendelea lakini akili yake ilikuwa ukiwaza Lina ana uhusiano gani na Angelo .
" Angelo amejzana vipi na lina mpaka akamtoa ndani?
Inawezekana Lina akawa na uhusiano wa kimapenzi na Angelo? Hisia za wivu zilianza kumtafuna Stephen alichukua simu yake na kupiga namba za Lina.
Wakati huo Lina, shangazi yake na Jerry walikuwa wamekaa wakimalizia kupata kifungua kinywa.
" Stephen anapiga.
Lina alimwambia shangazi yake.
" Achana nae, isipokee hiyo simu. Lina alimfuata agizo la shangazi yake .
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa waliondoka wakamsindikiza shangazi yake Lina stendi kwaajili ya kuanza safari ya kurudi kijijini.
" Lina naomba uwe makini kwenye huu mji.
" Hili ndilo ninalozingatia shangazi.
" Kaa mbali na Stephen anaweza akakusababishua matatizo mengine.
" Sawa .
Waliachana pale kisha bi Eliza akapanda kwenye basi , lina na Jerry walirudi nyumbani.
Usiku baada ya kupata chakula lina na Jerry walikaa kwaajili ya kuongea mipango ya kazi.
" Lina unaweza kufanya kazi gani?
" Naweza kufanya kazi yoyote.
" Unaweka kazi yoyote kwahiyo hata nikisema kati ya kuitunza moyo wangu pia unaweza?
Lina alimtolea macho , wote waliangaliana usoni kwa muda . Badae Kina aliangalia pembeni na kusema.
" Naweza kufanya kazi ya kupika na shuhuri zote za nyumbani.
" Basi sawa, umeajiriwa.
" Asante.
Lina alishukuru lakini hakuwa anajua atalipwa mshahara kiasi gani.
Usiku Lina alikuwa chumbani kwake akitafakari na kupanga kuhusu maisha yake na jinsi atakavyoweza kubalance mshahara wake.
" Mipango mingi sana na sijui nalipwa kiasi gani, acha nilale kesho kuwahi kuamka nianze kazi mapema.
Usiku ule alilala usingizi mzuri wa amani. Alikuja kushtuka kutoka usingizini muda wa saa tatu asubuhi tena baada ya kusikia mlango wake wa chumbani una gongwa , alikurupuka kutoka kitandani huku akiwa amevaa night dress yake akaenda kufungua mlango. alipo fungua mlango akakutana na Jerry akiwa kwenye tabasamu bana na nyuma kulikuwa na muhudumu aliekuwa kabeba trei iliyokuwa na vitafunwa , chupa ya chai pamoja na kikombe. Lina aliona aibu ndio kwanza siku ya kwanza lakini amechelewa kuamka , boss kwamba mapema na wamemtetea chai.
" Habari za asubuhi Lina!
" Salama boss...
Yule mfanyakazi aliingiza chai ndani kisha akaondoka na kuwaacha .
" Samahani ... Nimechekewa kuamka sijui kwanini imetokea hivi . Aliongea lina kwa uwoga.
" Usijali Lina kila kitu hapa kwangu kipo sawa. Unatakiwa ukisikia upo nyumbani.
Lina bado alikuwa akiangalia chini kwa aibu.
" Furahia kifungua kinywa chako.
Lina aliitikia kwa kichwa kisha Jerry akatoka pale chumbani.
" Uuuuh! aibu gani ya mwaka huu yani siku ya kwanza kazini. Nimechekewa kuamka na matokeo yake mimi ndio nahudumiwa kama malkia, hii sio sawa.
Lina alienda bafuni kuoga alipotoka akanywa chai haraka kisha akatoka na viombo. Kabla hata hajafika jikoni alitokea mfanyakazi kumpokea.
" Hapana nitaenda kusafisha.
" Hapana miss Lina hii sio kazi yako. Yule mfanyakazi alichukua na kwenda navyo jikoni.
Lina alizunguka kote kutafuta kazi ya kufanya lakini kila kitu kilikuwa sawa.
Alienda kukaa nje maeneo ya bustani akawa anafurahia harufu nzuri ya mauwa na upepo mwanana.
Siku zilienda lakini lina hakuwa na kazi ya kufanya pale kwenye jumba la Jerry bali yeye ndio alikuwa akihudumiwa.
Lina alianza kujihusi vibaya maana hakuna mfanyakazi aliemruglhusu kushika hata kijiko kwaajili ya kusuuza.
" Siku moja alikuwa jikoni akamkuta mfanyakazi mmoja .
" Leo zamu ya kupika ni yangu, tunapokea chakula gani?
" Hapana wewe hutakiwi kushika kazi yoyote hapa ndani nenda kapumzike miss Lina.
" Hivi mnajua mimi ni mfanyakazi kama nyie lakini hamtaki kuniona nimefanya kazi hapa ndani kwani nia yenu ni nini hasa?
Wale wahudumu waliokuwepo pale hawakujibu.
" Mna choyo , hamtaki nifanye kazi hapa?
" Hapana miss Lina.
" Sikilizeni hata mimi nategemea na familia natakiwa kufanya kazi nipate pesa sasa mnavxonifanyia hivi unafikiri nitapata wapi pesa. Lina aliongea kwa unyonge .
" Miss Lina ,sisi hatuna maana hiyo ila ukweli ni kwamba boss hataki uguse kazi yoyote ile hapa ndani bali unatakiwa kuhudumiwa tu.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi