Ghana imeamua kutumia Mtandao wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kumtafuta na kumrudisha nyumbani aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Ken Ofori-Atta.
Ofori-Atta (66), ana makosa ya kukwepa sheria wakati wa uchunguzi wa kesi kadhaaa za ufisadi zinazomuhusu.
Kesi hizo ni pamoja na utakatishaji fedha ulioisababishia Serikali hasara kubwa.
Baadhi ya nchi ambazo anasadikiwa kuwepo ni pamoja na Marekani na Uingereza.
#KitengeUpdates.