๐๐๐ฃ๐ฆ๐ (๐๐ผ๐๐๐ฒ ๐ ๐ฎ๐ถ๐ฑ ๐ช๐ฎ ๐ธ๐ถ๐๐ผ๐บ๐ฎ๐น๐ถ) _________________________________________ SEHEMU YA 1 ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ โHapsa, hapsa, we hapsa weweโ Ni sauti nzito ya kiume na yenye hasira Kali sana ikiitilia Jina la hapsa ambaye alikuwa jikoni akipika na alikaa kimya kana kwa
โKwahiyo ninavyokuita unisikii au ??โ
Aliuliza mwanaume huyo baada ya kumkuta hapsa jikoni akisafisha vyombo.
Hapsa Anageuka na kumuangalia KWa muda na kumjibu.
โYaani unaniita Kama umepatwa na kichaa ndio nini Yaani, unapaza sauti kiasi hiko utazani Mimi ni KIZIWI vileโ
Mkaka huyo anamshika hapsa vizuri sana na kumshushia mabao matatu mfululizo.
โNafikilia Leo ndio utajua maana ya kumuheshimu mtu si ndio ! Hapsa mimi ni mkubwa sana kwako na haujafikia hiyo level ya kunijibu Kama hivyo Sawa ? Ninapokuita lazima uitike haijalishi nimekuita kWa sauti gani Sijui unanielewa.
โVice niachie unaniumizaโ
Alilalama hapsa uku akilia na machozi yakimtililika kama maji.
Vice akamsukuma hapsa kWa nguvu sana na kuondoka nje kwa hasira.
๐๐ ngoja kwanza nicheke huyo ni Mimi sasa ๐ Yaani huyo aliyechezea mabao hapo juu ni Mimi hapa HAPSA BINTI WA MANSUL.
Anyway Jina langu halisi ndio ilo hapsa, ni Binti wa kisomali pure kabisa, mrembo kuliko maelezo ya urembo wenyewe, nimebarikiwa kishape Fulani hivi cha uchokozi, mrefu Kiasi.
Najua hapo mnajiuliza inawezekanaje Binti mrembo kama mimi Tena wa kisomali kuja kufanya kazi za Ndani, eeeh umenisikia vizuri mimi ni mfanyakazi wa Ndani.
Iko hivi, Mimi nimezaliwa na kukulia uku buza Ndani Ndani kabisa, kule kwa mparange hivyo mimi ni mswahili pure, Yaani mswahili mpaka mswahili Tena.
Katika makuzi yangu sijawai kumjua baba yangu, Ila mama yangu aliniambia Kuwa baba yangu ni msomali ndio maana na Mimi ni msomali.
Mimi Bwana kwenye elimu nimeishia kidato cha pili tu, na sababu ya kuishia kidato cha pili ni baada ya kupata ujauzito, Tena nimezaa na baba Mwenyewe Nyumba wetu, Sijui Kama mnanielewa iko hivi, Mimi maisha yangu Nimekuwa na mama yangu tu na tumekuwa tukiishia kwenye Nyumba za watu za kupanga na ndio nikiwa kidato cha pili nikazaa na baba kwenye Nyumba wetu.
Mpaka Leo Mimi na mama yangu tunaishi kwenye Nyumba hiyo hiyo pasi na kulipa kodi ๐๐ Yaani ni mtelemko tu, sasa hivi Binti yangu summy Ana miaka mitano na anasoma darasa la kwanza na kila kitu ni juu ya baba yake.
Najua mtajiuliza Kwanini nisiolewe na huyo baba, aaah kuolewa na huyu baba ni kazi nzito sana kwanza yeye ni mume wa mtu na ana ndoa ya kikristo na mke wake yuko hapo hapo, lakini ajui nini kinaendelea.
Kwa sasa Nipo nafanya kazi za Ndani kwenye Nyumba Fulani hivi ya kishua sana uku MASAKI familia Fulani hivi iko na Pesa sana na imebarikiwa watoto wanne wa kiume na wote wanakaa umo umo Ndani.
Mtoto wa kwanza wa familia hii ndio huyu VICE Mpole mpaka Ana kela, wa pili ni Temy huyu dakika Mbili mbele Yaani ukimchokoza tu anakunyoosha, watatu ni Femi, huyu sasa Naompa salute huyu ni mtu wa mademu tu, kila siku ana babe Mpya ๐๐, wa nne ni LOGAN huyu ndio yupo yupo tu umu Ndani huyu muda wote anasikiaga njaa na ndio last born wa familia.
Hii familia inapendana sana na wanaushirikiano sana.
Eeeh nilitaka kusahau, mimi Bwana Nina tatizo moja, fliji langu uwa aligandishi, Yaani Mimi ni mmbea kuliko huo umbea wenyewe ๐ siwezagi kinyamaza ata kwenye mambo ambayo hayanihusu ๐ nakupa taadhali hakikisha sipati Siri zako.
TUENDELEE.
Ni Majila ya jioni, mama na baba wa familia hiyo ndio wamerudi Nyumbani, kwa haraka nikatoka chumbani na kwenda Kuwapokea kwenye gari Yao.
โShikamoo mama, shikamoo Babaโ
โMarahaba ? Za hapa?โ
Alijibu baba.
โSalamaโ
Huyu baba Bwana ni mtu Fulani yuko simple sana Yaani mpaka raha, baada ya salamu huyo akaingia Ndani.
โMamaโ
Nilimuita boss wangu wa kike.
โEeeh hapsa umeanza haya kuna nini Leo Tena ??โ
Alijibu mama huyo maana ananijua kabisa sijawai kukosa cha kusema.
โLeo vice amenipiga mchanaโ
Kabla mama ajajibu kitu, gafla tu vice akajibu.
โNa nataka kukupiga Tena mbele ya kila mtuโ
Nikaโฆโฆ
HUU NI MWANZO TU JE UNAIONAJE ?
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni