*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO* *1-5* *
*SEHEMU YA KWANZA*
Naitwa Nelly ni mtoto wa kwanza kwa baba yangu wazazi wangu hawakuwahi kuishi pamoja hivyo niliishi na mzazi mmoja tu ambaye ni mama .
Niliishi na mama yangu hadi nilivyofika kidato cha kwanza mama akaanza kuugua hatimaye MUNGU alimpenda zaidi mimi nikakosa mtu wa kukaa nae ndugu wa mama wengi wao maisha yao yalikuwa chini sana ikabidi nikaishi na baba yangu muda huo alikuwa tayari ana familia nyingine. Walibahatika kupata watoto wawili wa kiume mapacha na mwingine binti mkubwa alimkuta kwa mkewe tulipishana miaka mitatu yeye alikuwa mkubwa kwangu nilimkuta yupo kidato cha tatu alikuwa anaitwa Victoria.
Wenzangu walikuwa wanasoma shule za kulipia yaani shule za magari ya njano Victoria yeye boarding ila mimi nikapelekwa shule ya kata ,
Mwanzoni tuliishi vizuri kimbembe kilianza nilivyofika kidato cha nne kazi zilikuwa haziishi nyumbani na hivi nilikuwa nasoma shule ya kutwa ndio kabisa nilikuwa sipati muda wa kujisomea vizuri. Mungu alisaidia hivyo hivyo nikamaliza masomo yangu nikwa nasubiria matokeo ila kipindi nipo nyumbani🏡 cha moto nilikiona kwa kweli .
Hapo binti yake yupo chuo watoto wake wanarudi jioni sana hapo walikuwa wanasoma darasa la saba kwahiyo nilibaki peke yangu nyumbani 🏡 muda mwingi.
Nelly wewe Nelly hebu amka unalala hadi sasa hivi una raha gani kwa mfano ufanye uamke hapo nje kuna mikazi kibao sauti ya mama ilisikika ikiniamsha na hapo jana yake nilikuwa nimechelewa kulala kisa kazi hizohizo.
Niliinuka taratibu mama jamani usiku wote huu niliongea nikaangalia saa ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri nikatoka nje kufanya usafi nilimaliza kazi zote hadi mida ya saa tatu za asubuhi nilikuwa tayari nishamaliza kila kitu.Mama alitoka nje akanikuta nimekaa ukiwa kwangu lazima kazi ufanye hakuna cha bure kama unataka kudeka uende ukadeke kwenu.
Mama unanifanyia hivi ni kwa sababu unajua sina pa kwenda niliongea kwa upole.
😄wewe huyo huna pa kwenda si uende ukakae kwa ndugu zako mama yako kwani hakuwa na ndugu, lazima uishi hapa na sisi yaani naomba matokeo yatoke hata kesho uondoke huko shule na kwa hizo akili zako sijui kama utafaulu mtoto unanikosesha amani kweli wewe na ndoa yangu .
Nilibaki nimenyamaza kimya namsikiliza tu maana ningemjibu angeona najibizana nae kuishi na mama wa kambo ni kazi sana basi tu japo mimi alinikuta tayari nimeshazaliwa sijui chuki zinatokea wapi.
Itaendelea……
*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO💋🙌02*
💋
Niliingia chumbani nikajifungia mlango nikaanza kulia 😭 nirifikiria mengi huenda mama yangu angekuwepo yasingetokea haya mateso ila ndio hivyo ndugu wa mama nao maisha yao hayakuwa mazuri sana ningeenda kuishi hata kwao .
Siku matokeo yametoka nilikuwa sijui mama ndio aliniambia kuwa matokeo yametoka nimtajie namba yangu ya mtihani ili tujue . Nilimtajia namba yangu nilikuta nimepata division four nilijikuta nakata tamaa 😔 kabisa lakini cha ajabu mama alikuwa ananicheka 😂 yaani wewe nilijua tu huna akili bora hata baba yako hajakupeleka shule ya kulipia mbona angepata hasara tu ufanye uolewe ale hata mahari usije ukazalia nyumbani 🏡 ukazidi kututia aibu.mitoto kama hii huwa inawazaga urithi tu wazazi wafe wapate mali Mama aliongea kama kameza cd mimi kama kawaida yangu nilibaki nimenyamaza kimya . Siku hiyo sikuwa hata na hamu ya kula kabisa nilienda🚶 kujilalia zangu chumbani .
Kuna ule msemo unaosema ukimpiga chura teke umemuongezea hatua sasa ndicho kilichonikuta mimi mwenyewe alijua ananikomoa kumbe ananifundisha maisha ni nini 🤔 .
Mida ya jioni mama alikuja kuniita chumbani kwangu kuwa anataka aniagize hapo kwa jirani ambaye ni rafiki yake na mama niende nikamchukulie mzigo . Sikujua ni mzigo gani niliamka nikaenda hadi hapo aliponiagiza hapakuwa mbali na nyumbani 🏡 kwetu ni nyumba ya tatu kutoka nyumbani kwetu. Nilifika nikagonga geti likaja kufunguliwa na mlinzi, karibu unamuulizia nani binti mlinzi aliniuliza? huku akinitazama usoni kwa umakini.
Karibu unamuulizia nani binti ? Mlinzi aliniuliza namuulizia mama Denis mama kaniiagiza kwake nije nichukue mzigo
Sawa karibu ndani bosi katoka kidogo ila atarudi muda sio mrefu utamsubiria kidogo hapo nje kwenye kibaraza. Sawa nilimjibu yule mlinzi nikaenda kukaa kibarazani nikawa namsubiria huyo shoga yake mama.
Kichwani nililkuwa na mawazo mengi sana kuhusu hatma ya maisha yangu yatakuwaje baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari matokeo ndio yamekuja mabaya.
Nikiwa katikati ya mawazo nje gari 🚗 ilipiga honi mlinzi alifungua geti likaingia ndani nilijua ni mama Denis lakini hakuwa yeye alishuka mkaka🧍 walisalimiana na mlinzi akawa anakuja ndani akanikuta kibarazani nimekaa .
Nilimsalimia aliitikia akaingia ndani baada ya dakika kadhaa alitoka nje akanikuta bado nimekaa.
Mbona umekaa nje muda mrefu ? Namsubiria mama Denis nimeagizwa kwake nilimjibu huku nimetazama chini .
Ingia ndani mama hayupo ila atakuja muda sio mrefu karibu ndani.
itaendelea
*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO💋🙌03*
Asante nilisimama nikaingia ndani , Dada mpatie maji mgeni anamsubiria mama mimi naondoka akija utamwambia nilikuja sina nafasi nitamsalimia siku nyingine.
Sawa kaka Denis dada wa kazi alimjibu hapo ndipo nikagundua huyu ndie Denis mwenyewe.Aliondoka nilikaa kama nusu saa ndipo mama Denis alikuja .
Shikamoo nilimsalimia , marahaba umekuja muda Nelly nilikuwa na kikao kazini mwanangu mama yako kakuagiza uje uchukue mzigo?
Ndio ,Mama Denis alienda chumbani kwake akaniletea bahasha . Hiyo mpelekee mama yako nilichukua nikampelekea mama , alikuwa amekaa sebuleni akaenda chumbani baada ya dakika kadhaa akatoka tena sebuleni huku ile bahasha akiwa ameifungua akakaa kwenye sofa akampigia mama denis .
Simu📱 iliita baada ya sekunde kadhaa ilipokelewa. Alooh shoga mbona hela haijatimia hii ? Nimetoa hela yote mbona kwani ipo kiasi gani ? mama Denis aliuliza . Nimekuta milioni na laki tatu tu laki mbili hakuna mama alijibu mimi nikawa namsikiliza tu mama alikata simu📱kisha akanigeukia umepeleka wapi hela nyingine wewe mtoto ?.
Hela gani mama hiyo bahasha nilivyopewa ndivyo nilivyoleta.
Umeiba hela Nelly hizi hela sio zangu ni za baba yako kwahiyo sasa mtajuana wenyewe ngoja ninyamaze kimya mimi, lakini mama mimi sijaiba hela yoyote ile.
Shhs 🤫kimya usiniambie chochote kile utakuja kumwambia baba yako maana nikiongea mimi nitaonekana nakuonea kulea mtoto wa mtu kazi sana . Mama aliondoka sebuleni akaenda chumbani kwake nilibakia sebuleni nisijue cha kufanya . Niliamua niende zangu kulala tu usiku baba alikuwa ametoka safari aliyoenda nilienda kumpokea ila sikuwa na furaha😔 kabisa . Wewe vipi tena hauna furaha una shida gani🤔 ? baba aliniuliza lakini kabla sijajibu kitu mama alikuwa tayari ameshakuja akadakia mwambie makosa uliyofanya baba yako ajue yaani mwanao siku hizi kawa mwizi na hela sijui anapeleka wapi? pia matokeo yametoka amefeli wastani kapata mbaya .
Nelly anayoongea mama yako ni kweli🤔 baba aliniuliza nilikuwa na machungu sana moyoni mwangu nilishindwa kujibu baba alinitandika kofi 👋 moja nilihisi nyota nyota . Mimi sijaiba nilipewa hela nimeleta kama zilivyo . Kwahiyo unataka kusema mama Denis ni muongo huyu inabidi nimkague itakuwa tu kaiba kweli. Mama aliongea huku akielekea chumbani kwangu baada ya dakika kadhaa kweli alitoka na hela nilikuwa nimehifadhi kwenye mfuko wa sketi yangu ya shule.
*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO💋🙌04*
Hizo hela zilikuwa zangu mimi mwenyewe nilikuwa nazitunza kipindi nasoma ili nije ninunue simu nahisi mama aliziona akaamua anifanyie mchezo ijulikane nimeiba hela mimi .........
Baba mimi sijachukua hizo hela , hizo hela ni za kwangu nilikuwa natunza . Unatunza hela unazitoa wapi kama sio kutuibia sisi ,mama alidakia.
Kwanza umefeli , pili unaiba hela nimekuchukua kukulea kama msaada tu kwa sababu mama yako amefariki ila sina shida na watoto tena mtoto mpumbavu kama wewe msaada wangu ulipofikia unatosha kusanya kila kilicho chako kesho nakupeleka kwa mama yako mkubwa ukaishi huko ndicho ulichokuwa unakitaka. Baba aliongea hakutaka hata kunisikiliza aliingia ndani nilibaki nimesimama sina cha kufanya.
Si ukakusanye virago vyako au hujaelewa mama aliongea huku akicheka 😂 akaingia ndani na yeye. Niliingia ndani nikaenda kupanga nguo zangu taratibu, mara mama alikuja kusimama nyuma yangu tena ngoja nije nikuangalie usije kuiba nguo za binti yangu bure maana mwizi ni mwizi tu .
Sikujibu kitu nikawa naendelea na kazi ya kupanga nguo hadi nilivyomaliza nilitoa begi nje ndipo mama na yeye akatoka nje nilikaa sebuleni nikawa namsubiria baba , Moyoni nilikuwa na machungu 🥲 sana ila niliona bora niondoke tu manyanyaso niliyachoka. Baba alitoka chumbani vipi ushakusanya vitu vyako tayari? Baba aliniuliza nikamjibu ndio nimeshakusanya haya twende kwa mama yako mkubwa labda mtawezana kwa hizo tabia zako.
Kwa kuwa baba alikuwa ana usafiri wake tulifika mapema nyumbani 🏡 kwa mamkubwa , alipaki gari 🚙 tulishuka bahati nzuri mamkubwa alikuwa amekaa njee alishangaa kuniona nipo na mizigo. Enhee 😳 kulikoni tena na mizigo ghafla tena bila taarifa 🤔 mamkubwa aliuliza. Nimemleta mwanao ili tusaidiane kulea siku hizi amekuwa na tabia za hovyo mimi sikai sana naomba niende .
Baba aliaga kisha akaondoka zake nikabaki na mamkubwa pale nje.
Nelly unaona maisha yalivyo magumu unapata nafasi ya kulelewa bado unaleta ujinga kwanini ? Mamkubwa aliniuliza , mamkubwa unanifahamu mimi vizuri sina hizo tabia mama mwenyewe ndio ana matatizo ananisingizia mimi vitu ambavyo sijawahi kufanya .
Sasa kama hujafanya kwanini umekubali kosa nimpigie simu 📱baba yako sasa hivi hapa nimwambie kama umesingiziwa, Hata ukimwambia haisaidii hana kauli kwa mke wake kwanza mimi mwenyewe nishaingiwa na kinyongo siwezi kurudi tena pale.
Mhh🤔 haya ila mimi maisha yangu ya hapa ni magumu sana nifanye vibiashara ndio nile na kusomesha mwanangu utaweza kuishi na mimi kweli? Kwanini nisiweze wakati wewe ndio mama yangu nitakaa na wewe hivyohivyo bora ugali dagaa kwenye amani kuliko wali nyama vitani.
*SEHEMU YA TANO*
Haya karibu Ingia mizigo yako ndani huko kisha uje usonge ugali tule nimeshanunua fungu la dagaa mchele tutalumagia tu.
Niliinuka nikaingiza mabegi yangu ndani kisha nikatoka nje nikaenda jikoni kusonga ugali, Huyu ni mama yangu mkubwa anaishi kibaha loliondo ndipo alipojenga nyumba 🏡 yake ya vyumba viwili na sebule sehemu nyingine alikuwa hajamalizia . Akitoka yeye ndie anafuatia mama yangu kisha mdogo wao wa mwisho wa kiume nae alishaoa mama yangu mkubwa alijaliwa mtoto mmoja tena alichelewa kuzaa kweli ndio kwanza yupo shule ya msingi darasa la sita. Niliivisha chakula🍴nikaandaa ili tule bahati nzuri na mwanae alikuwa asharudi shule tukala pamoja.
Kesho yake asubuhi 🌄 na mapema mamkubwa aliamka ili aende kwenye biashara yake na mimi niliamka , Na wewe kuamka mapema asubuhi 🌄 yote hii kulikoni mamkubwa aliniuliza, Nataka nikusindikize kwenye biashara yako nikusaidie kuuza nilimjibu. Haya kwa kuwa umetaka mwenyewe mimi nauza karanga na korosho pale stendi ya magari mbezi na huo usista duu wako sijui kama utaweza 🤔.
Mamkubwa usidharau mtu unaweza kukuta mie nikauza hadi ukashangaa kila mtu na nyota yake. mhh🤔 ngoja tuone mtu mwenye nyota yake leo. Mtoto wake alienda shule na sisi tukaenda mbezi kuuza korosho na karanga ana meza magari yakipita naenda kuuza nilijitahidi kuuza hadi mamkubwa alinisifia .Giza lilipoingia tukarudi nyumbani kweli uliniambia una nyota leo nimeuza sana kuliko siku zote shika elfu mbili hii utanunua chochote . Mamkubwa hata usijali hiyo hela tutanunua hata mboga nashukuru 🙏 sana niliirudisha ile hela tulipika zetu ugali na matembele tukajilalia zetu .
Kesho niliamka asubuhi 🌄 nikafanya usafi tukaenda zetu kwenye biashara kama kawaida yangu nikawa nikiona magari au daladala naenda kuuza, Mamkubwa akawa anauza kweli ulipita mwezi nikawa nimeshazoea kuuza . Siku hiyo kuna gari 🚙 lilipita karibu na sisi likasimama inaonekana mwenyewe alikuwa anataka akanunue vitu mimi tena nikaona mteja si ndio huyu nikaenda kupeleka korosho na karanga. Karibu korosho kaka niliongea tulivyotazamana na yule kaka wote tukabaki tunashangaana nikajisemea nisitoke kwenye reli hapa nikajikausha , Kaka korosho tamu hizi grade one kutoka mtwara kuna mbichi na zilizokaangwa unataka zipi🤔. Dada samahani nakufananisha kama nimekuona mahali hivi 🤔 yule kaka aliniuliza , utakuwa umenifananisha . Sawa naomba korosho za elfu kumi. 😳 nilibaki nimeduwaa za elfu kumi tena . Mbona unashangaa niletee hizo korosho nilienda kuchukua alibaki ananiangalia hadi nilivyokuwa narudi akanipatia hela, nikaondoka nikarudi kukaa maana sikuwa na ujasiri hadi alivyoondoka yule kaka na gari 🚙 lake.
Mbona kama umepoa ghafla ? mamkubwa aliniuliza , Hapana mama nipo sawa tu nilimjibu kisha nikachukua korosho nikaenda kuuza giza 🌃 lilipoanza tulirudi nyumbani 🏡 usiku 🌃 kucha nikawa namuwaza 🤔 yule kaka.
Kesho yake mamkubwa akaniomba niende mwenyewe yeye hajisikii vizuri sikuwa na hiyana nikaenda kuuza mwenyewe nikiwa nimekaa sina hili wala lile nikasikia mtu ananiita jina langu Nelly niligeuka nikaitikia nilimkuta ni Denis yule kaka ambaye nilikutana naye jana .
MWISHO WA KIONJO
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni