*NDOA YA MCHONGO BIBI NA MAMKWE🙌* *1-5* * Facebook
*SEHEMU YA KWANZA*
Huyu aliyegundua cabbage ni mboga, jamani jamani, nikimkamata uko kiama patachimbika 🤨, nikiwa nawaza kwa sauti, na hasiraa, bibi yangu akanipa za uso uku ananisogelea, "hio mboga imekukuza mtoto wa marehemu usinitibue saivi, inashida gani? Kila tukipika cabbage lazima uzinene ubaya, ndio maana ukizipika wewe haziwi nzuri, mwanamke ukiwa jikoni unatakiwa kuwa na furaha, furahia unachokipika kitatoka vizuri na radha ya kipekee, sio kunung'unika hutopata chakula kizuri potea jikoni kwangu kwanza kaniletee kafungie kuku, jamani uyu Bibi yangu ni anakelele🙌, alinitoa jikoni na kofi juu, Bibi nitaenda kukushtaki uku sio Bongo ujue 😭, nilimsema huku nakimbia nje nisijerushiwa mwiko 🤣, naitwa Angle, binti Ibrahim, ila huyo Ibrahim mwenyewe sasa, hajui ata binti yake nafananaje, anachojua yeye ni kutuma ada, mengine hajui, toka kaniona nikiwa darasa la nne mpaka nimemaliza form 6 najianda kuingia chuo hajui nafananaje, mama angu kafariki nikiwa form 1, ajabu hakuja ata kumzika, na tulishindwa hata kumsafirisha Mama angu😭, tumemzika huku Dernmak, alikuwa akifanya kazi za ndani huku, ikabidi bibi aje kushika nafasi ya mama, Tunashukuru Mungu walikubali mpaka kumhifadhi mama angu kwenye maeneo yao😭, baba angu pesa anayo ila hakutaka ata kuchangia chochote, na mpaka saiv tunaishi Dernmak na masomo yangu nimemalizia uku apa nasubili tu kuingia chuo..
Nilitoka nikafungia kuku tuko kwa wazungu ila bibi yangu maisha ya kuku za kwenye frizer yamemshinda kachukua kibali japo ni kazi sana huku ila tulipata, nikiwa nafungia kuku nikapata wazo, bibi huwa mara nyingi halali apa, japo tuko nyumba moja na boss wetu ila sisi nyumba yetu iko pembezoni hatushei nyumba, hivyo yeye anaenda kulala nyumba kubwa kwa sababu kuna mzee anamlea mle na siku izi usiku ndio anasumbua zaid, basi bwana mimi na cabbage ni maadui, paka na panya, bibi alivyoivisha akapakua, bibi yaani tunakula kama mbuzi😭, nilianza kulia, " wewe wewe tena usinipande kichwani soma ule unavyotaka sio kwangu, moyoni nikawaza kwangu ama kwa watu huyu mzee vp 😏...
Nilikula nikawa nahisi chakula kinanikaba tu, nikazila nikaenda chumbani, bibi yangu ata hakuja kunibembeleza akamaliza kula nakusepa kazini kwake, alivyotoka tu mimi huyo kuna kuku nilimficha sikumuingiza kwenye banda lake, nilifika nikakaba shingo yake ila mpaka namchukua alitoa sauti, nikajua leo bibi atanishika mimi, bahati nzuri hakusikia, nikatoka zangu huyo, nikafanya kila kitu, nikampika nikala, wakati naenda kufukia manyoya ya kuku, si nikakutana na mpaka mweusi, nikataka kupiga kelele, nikakumbuka ninakesii ya kuku wa bibi, mimi jamani😭, nikajikaza nikapiga ya kichwa yule paka, bahati ilikuwa kwangu nina shabaha, alikuwa kama kachanganyikiwa anataka kukimbia nikawahi kumponda miguu ashindwe kukimbia, nilihakikisha kabisa nimemmaliza dah ila wachawi wakijijini kwetu jamani, sasa ndo wanifate adi huku jamani 😏🙌...
Nililudi zangu kulala uku mboga iliyobaki nimeificha, asubuhi kukakucha, nikaenda kumsaidia bibi kazi za kule, tukiwa tumemaliza ndo tunaandaa chakula, madam boss akapiga kelele analalamika uku analia kabisa kwa uchungu, uku amembeba yule paka nilomuua usiku, nikizani, katumwa na watu, wa kijijini kwetu , nilimwangalia yule mama wa watu anavyoomboleza kwa maumivu makali, nikasema moyoni Angle umekwisha, nikawaza eneo nililomtupia ni nje ya geti sasa wamempataje, nilikuwa natetemeka japo eneo nililomuulia hakuna camera ila hawa wazungu hawatabiriki huenda waliweka kwa siri jamani, mama wa watu anavyolia kwa uchungu, sijui itakuwaje jamani, wa wazungu wasivyonadogo apo tayari msiba na watu wataalikwa, nilibaki nakesi zangu moyoni nisijue zinalipuka saa ngap na hatma yangu ni ipi 😭...
*SEHEMU YA PILI*
Apo ninaogopa heka heka zilivyopungua mimi nae huyo nikarudi kwenye kajumba ketu na Bibi ili wasinishtukie naweza kuwekwa gerezani kama utani, nilirudi nikalala kabisa nakuja kuamka nikaanza kupika nilijua tu bibi yangu atakuwa bado na kazi, nilitamani kwenda kumsaidia ila kila nikikumbuka nina msala ukijulikana mimi jela bila kizuizi, naishiwa pawa kabisaaa, nikajizuia sikwenda kumsaidia Bibi na huwa sio kawaida yangu, saa 7 usiku bibi yangu ndo kamaliza kazi akaja kachoka kweli 😭😭...
Cha kwanza akenda kuoga katoka akanikamata nikajua tayari kumekuchaa, "ulizani sitajua ee? Yaani kwa hizo akili zako mbili ulifikiri mimi mjinga sitojua ulichokifanya ee? Ivo wewe mtoto unajitambua kweli? Ulichokifanya wakijua tutafanyaje🤨, alinifinya jamani apo sitakiwi kutoa sauti, nikitoa wakanisikia nitajulikana, nikawa najizuia nisitoe sauti nalia kimya kimya tu, ila aliniumiza jamani 😭😭...
Apo hajajua kama ata kuku wake tu nimeshampeleka tumboni, asubuhi akawahi kuamka akaanzia kwenye kuku zake saa ngap asimkose kuku wake pendwa, hee alirudi mbio ndani nilisikia tu kishindo usingizi wote ukakata, pale pale nikapigwa kofi, sijatulia teke, hasira alizokuwa nazo Bibi yangu mmmh 🤐, alichukua kamba ya mazoezi akatumia kunichapa nayo, nilishindwa kujizuia, nikatoa sauti kuomba msaada, make nina miaka sijapigwa, huwa ni kunitukana na kunifinya kidogo tu, ila hii ya leo 😭😭, nilihisi ananiua...
Pamoja na kulia sikupata msaada nikaona apa dawa nikukimbia, nilichomoka, " wee rudi hapa ukiondoka ujue ntakupa laana utakutana nayo huko huko kwenye simu yako" bibi alinambia wakati nakimbia, nikamjibu Bibi simu siiwashi tena naiacha siondoki nalaana naondoka na baraka, Bibi nisamehe tu 😭, ukweli mimi kabeji inanishida Bibi yangu nakupenda nisamehe, nitapambana nikipata kazi tu nitakununulia kuku wengi, niliongea nikiwa nishafika getini uku bibi yuko nyuma ananifukizia, nilimuomba mlinzi anisaidia Bibi anahasira atanivunja mikono leo, mlinzi alinielewa nilichomoka, nikaenda kwa rafiki yangu apo mwili umejaa mijeredi...
Nilifika kwanza akanishangaa, nakunishauli ety nimfungulie kesi bibi yangu, ila wazungu wao huwa hawajari hii ata sio shida yao, Fiona huyu ni Bibi yangu ndo kila kitu kwangu, kufanya hivi kwa tamaduni za Africa ni sawa, ananifundisha nimekosea, tamaduni zenu na zetu tunatofautiana, siwezi kumshtaki Bibi yangu, uyo ndo Baba, Mama, Kaka yani ndo furaha yangu, natamani namimi ningekuwa na wadogo zangu ama kaka zangu au dada, lakini sina huyu mmoja nilienae peke yake tu, nampenda sana yaani sana, ata yeye ananipenda basi tu nimemkosea najua hawezi ata kula kama hatoniona siku nzima atachanganyikiwa, namjua Bibi yangu nakunipiga kote lakini huwa analia nikiwa nalia, nilimfafanulia kwa upana japo hakuelewa sana ilibidi tu akubaliane na maamuzi yangu, basi nilishinda siku nzima kwa Fiona, jioni mida ya saa kumi jioni tukapata ugeni, alikuwa ni Madam boss na Bibi na kwa kumtazama tu unajua kabisa uko nyumbani kimeshanuka yaani hakuna usalama kabisa...
EP 3
Nilianza kutetemeka, hawakukaa zaidi ya madam Boss kusema tu, “ Angle tufate”, aliongea huku wakiaga kuondoka, nilitamani kukimbia ila nikikumbuka, Bibi yangu nitamuumiza na kumuachia matatizo nikawa mpole tu, niliwafata tukapanda gari kimya kimya mpaka nyumbani, tuliingia moja kwa moja mpaka chumba cha kikao ile nyumba ilikuwa kubwa, kulikuwa na chumba cha kikao, cha mazoezi, cha ibada, adi ukumbi jumba lilikuwa kubwa mno, tuliingia mimi, bibi, na madam Boss…
Tulikaa apo macho chini, aliwasha PC yake ikinionesha nilivyopita na paka naenda kumtupa kumbe camera ya nje nilikomfukia ilininasa nilivyokuwa namuua kulikuwa na giza sikuonekana ila kuna eneo la mwanga nilipita nikaumbuka mie, nilipiga magoti nikanza kuomba msamaha, Boss naomba unisamehe sana, ukweli sikujua kama ni paka wako, nilijua ni mchawi katumwa, kweli tena nisingefanya hivyo kama ningejua ni wako, naomba unisamehe, niliomba msahama uku nalia kwa kumaanisha kabisa, “unajua thamami ya Gift wangu? Paka wake alikuwa anaitwa Gift, aliongea kwa uchungu mama wa watu adi analia, nikajua kabisa apa akuna msamaha, cha kufanya nimtie Bibi yangu kwenye hili janga langu tu…
Boss sikujua, kama msahama hauwezekani nisawa niko tayari kwa adhabu ila nakuomba sana 😭, bibi yangu asiingizwe kwenye hili, nakuomba Boss nilindie tu bibi yangu, sina ndugu mwingine zaidi yake 😭 naomba plz🙏..
“Kwa hilo ulilolifanya, angekuwa mtu baki, ungeshakuwa gerezani ama ningekuzika pamoja na Gift, na hakuna ambae angenizuia wala kufanya chochote, ila kwa namna nilivyoishi na mama ako, heshima alioitengeneza kwenye hii familia, na hata bibi yako, nakupa nafasi ya kuchagua, no. moja uende jela, no. mbili nadhani unamkumbuka kijana wangu Gold, anashida ya kiafya hivyo hawezi kumfanya chochote mwanamke, natafuta matibabu, lakini nataka uolewe nae siku za hivi karibuni, uhakikishe unafuta uvumi unasemwa na watu kuwa mwanangu sio mwanaume, nimeshapata mtu wakumtibu akishatumia dawa hakikisha inaniletea wajukuu ndio deni langu na wewe litaisha”, nilichoka yani mimi niolewe na uyo kauzu kwanza mimi na wazungu sina interest nao kabisa, mtu mwenyewe ata kumkumbuka simkumbuki, mara ya mwisho nilimuona, lakini hakuwa anapokea ata salamu yangu 😭, sasa huko kuolewa jamani, kabla ata sijamaliza kuwaza Boss akasema, “ nawapa nusu saa mfanye maamuzi niko sebleni nasubiri majibu”, alitoka akatuacha sasa familia tunatapatapa, “Angle mjukuu wangu, najua hili ni zito kwako, sitaki kukupa lawama sasa hivi, ila naomba kwa sasa hivi kubali kuolewa, kwanza hawezi kukugusa, wakati wanahangaika kumtibu, mimi nitatafuta njia ya kukutoa tutakuwa sawa, kuliko uende jela” bibi yangu aliongea kwa uchungu uku machozi yanamtoka, sikuwa na ujanja tena, bibi yangu ni mtu ninaemsikiliza sana, akisema moja ni nadra mimi kusema mbili, nilikubali, tulipeleka majibu, Madam Boss alifurahi mno, kabla ata hatujatoka mwamba Gold akaingia apo ana miaka kama 5 ivi ajakanyaga nyumbani apo natetemeka ni mkari, aliingia akawasalimia mama ake na bibi yangu mimi akaishia kunitizama jicho kari tu, nilimsalimia lakini kabla ata sijamaliza salam yangu akatoka…
Chapter 4
Nilichoka nikaona kabisa uyu mtu kuishi nae ni kimbembe, madam Boss alitabasamu akanambia "usijal hapendi kuitwa kaka, na wewe kila siku unapenda kumuita kaka" nilibaki hee sasa si aseme, mimi nimuite nani akati ni mkubwa kwangu, nikaamua kunyamaza tu ila uku kichwani bado naongea mwenyewe, tulitoka nikaambiwa nikalale badae kutakuwa na heka heka, sikutaka ata kujua hizo heka heka zinahush nini, make bado kichwani nina ajenda zangu kibao...
Nilienda adi home, nikaingia kulala, upande wa Madam aliamua kwenda kuongea na kijana wake, aligonga mtoto akamfungulia, "mama karibu" Gold alimkaribisha mama ake, "kijana wangu, nimekuita ili tuongee kwa kina nadhani wakati unaondoka unakumbuka nilikuahidi nini si ndio? "Mama sitaki umlazimishe tafadhali, naheshimu hisia zake na mawazo yake alishasema hapendi kudate na mzungu" mama ake akamkatisha pale pale, "Gold alisema kudate sio kuolewa, labda nikutoe tu wasi wasi kama huniamini nimuite mwenyewe aseme, nimemuuliza zaidi ya mara nne, kama kweli anahitaji kuolewa na wewe, kutoka moyoni kasema ndio" Gold alimtizama mama ake kwa umakini kuhakikisha kama ni kweli nimekubali mwenyewe...
Hakumuamini akatoka na kuja kumuomba bibi niitwe anamaongezi na mimi, muda huo niko zangu kitandani nawaza mpaka kichwa kinauma, bibi alivyotaka kuja Gold akamzuia nakusema apewe no tu anipigie, alipewa akapiga, nilijua ni Fiona nikachukua na kupokea bila hata kutizama vizuri mpigaji, napokea nashangaa sauti ya kiume, niliisearch kichwani nikajua ni ya nani, hakutaka kujieleza akatoa tu amri nitoke nje ananisubiri...
Mmh uyu kiumbe vipi, mbona mwendo wa ki Africa akati wazungu wako romantic uyu wangu vipi tena, ata ivyo kuna tatizo la kiufundi huenda ndio maana, nilitoka nikamkuta yuko na gari akanifungulia bila kusema chochote, samahani bro nikajizuia, make nishaambiwa hio bro haipendi, G naomba nimuage bibi, "anajua na ndie aliyenipa no zako nilichoka nikapanda tu apo sijui napelekwa wapi, kuuliza naogopa, alinipeleka nyumba nyingine kabisa ilikuwa mbali kidogo na nyumbani, naijua ni nyumba yake ila haina watu ina mlinzi na mke wake ndo anaeisafisha, tuliingia wakatukaribisha vizuri, mimi huwa nina vibe langu tu kama mtu hatishi naongea, niliwachangamkia, na wao walinipa full saport, kabla ata hatujamaliza kuongea nikashikwa mkono, bila kusemeshwa chochote nikavutwa ndani...
Sikuogopa make najua zana haina makari, aliniingiza chumbani na kunambia anamaongezi na mimi, sikuogopa kukaa nae room moja peke yetu tena mlango ukiwa umefungwa haikunishtua najua kabisa hakuna kitu apo kati, Gold aliniuliza "Angle unauhakika uko tayari kuolewa na mimi kutoka moyoni? Bila kufikiria nikajibu ndio akauliza tena nikakubali saa ngap asidake mdomo ghafla tu...
Itaendelea....
Chapter 5
Nilishtuka ila nikajipa moyo hakuna madhara, wazungu na hii kitu kwao huwa ni kama salamu tu, nikampa ushrikiano ila sasa nikajiona kabisa napoteza akili zangu, nilianza kujitoa lakini niko hoi naona aibu ata kumtizama, nikama alinielewa, alinivuta karibu yake akanikumbatia ata yeye alikuwa anapumua kwa shida sana, nikajiuliza kwani kitu ikiwa hainyooki hisia huwa zinaamka kweli maajabu, kumbe anaweza kuhisi ila kufanya ndo hawezi duh, niliimezea ndani kwa ndani, sijakaa sawa akanibeba mpaka kitandani, niliinua macho kumtizama alitabasamu, hili tabasamu huwa ni adimu sana kwa huyu mwamba nilifurahi kuliona make akitabasamu aisee ni bonge moja la mwanaume ni mzuri kama angekuwa mzima asingethubutu kunioa mimi, yaani kuna yule mtu ukimuona tu unajiongeza kabisa hii dio hadhi yangu, moja wapo ni huyu sasa, anakisura cha kike japo wa kiume, mikono milaini hio ngozi sasa, dah sina la kusema mtoto wa Ibrahim mie...
Nilijikuta tu namwambia kwa aibu ukitabasamu unavutia balaa, alizidi kutabasamu uku akinitizama, ujasili ukashwaaaa, nikashusha vijicho vyangu chini haraka sana aliendelea kunitizama uku hali yake ikazidi kubadilika, alifumba macho kwa hisia akaniambia "Angle napenda sana rangi yako, natamani ningekuwa na rangi kama yako, nakupenda sana Angle"...
Aliongea kwa shida kama mtu alieshikwa pabaya, yani upwiru umemkaba vibaya mno, nilifunika macho yangu pia nisimtizame make namtamani tu, apo nishaanza kumvutia picha akipona, nilikumbuka kanambia ananipenda, na kwa hali yake nisipomjibu vizuri atahisi namtenga, nikajibu tu kwa ajili ya kumtia moyo ajione wa thamani, G niliita kwa sauti ya mbali kiaina mtoto wa mama mkwe avurugwe vizuri nakupenda, aliniomba nirudie hajasikia nilifunika macho yangu kwa mikono yangu miwili kisha nikarudia kuongea nakupenda...
Gold alifurahi, alinikumbatia kwa nguvu, kilichofata ni mdomo wangu, alihakikisha siwezi ata kujisongeza nimelegea kama mlenda, nilimuomba aniache nateseka, akauliza kama niko tayari kwa shoo, hee shoo tena nilishtuka kivipi kabla sijamaliza kushtuka vizuri mwamba akatoa nguo yake ya juu kaniachia kifua chake nivurugwe vizuri, alivyoona ninavyomshangaa akaniuliza tena, uku akisema yeye yuko tayari ni mimi tu, ivi wenzangu mnaelewa anachosena uyu kijana...
Itaendelea...
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni