Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
30 Nov -0001
38 views
VYOTE NDANI GONGA94
Ligi Kuu imeendelea kupiga hatua kubwa katika maendeleo kiasi cha kushika nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS)
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Ligi Kuu imeendelea kupiga hatua kubwa katika maendeleo kiasi cha kushika nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).
.
Hili ni jambo la kujivunia, lakini uwepo wa watu wanaoitwa makomandoo ambao wamekuwa na jukumu la ulinzi kwa timu husika ni tatizo kubwa ambalo halifai.
.
Tukio la juzi kwamba makomandoo wa timu moja wanadaiwa kuhusika katika kuvuruga na kuathiri kanuni za ligi lina paswa kuwa ishara kwamba, hawa watu hawafai na hawastahili kukumbatiwa na timu hizi mbili.
.
Kitendo cha kikundi cha watu kuzuia timu isiingie uwanjani kufanya mazoezi kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuathiri mchezo na kujenga picha mbaya kwa mashabiki, wadau na hata wafuatiliaji wa ligi yetu kinaonyesha wazi ni namna gani tunaiweka rehani hadhi tuliyopewa ya kutambulika kwa ligi hii kimataifa
.
Vitendo kama hivyo vinapaswa kulaaniwa vikali na mamlaka husika zichukue hatua madhubuti ili kudhibiti hali hiyo. Si hilo tu, bali makomandoo wa klabu hizo wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kudhibiti na hata kuzima uhuru wa vyombo vya habari, jambo ambalo linakwenda kinyume na misingi ya uwazi na maendeleo ya soka. Kwa mfano, wamekuwa wakizuia waandishi kufanya mahojiano na viongozi wa timu na hata wachezaji.
.
Hivi Simba na Yanga kwa viwango zilipofikia zinastahili kweli kuwa na watu wa namna hii katika ulimwengu wa soka ambao umetawaliwa na mafanikio na burudani uwanjani. Zaidi ya hayo, makomandoo wengi hujihusika na vitendo vya vurugu na uonevu, hasa katika mechi kubwa kama Kariakoo Dabi. Matukio kama kuzuia wapinzani kutumia miundombinu ya umma kwa ajili ya maandalizi ya mechi ni dalili kwamba timu hizi kubwa bado zinakumbatia ukal? flani katika suala la ulinzi.
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA & Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF
wametoa kibali rasmi cha kuthibitisha kuwa uwanja Wa Hoima City uliopo Uganda, unakidhi viwango vya kimataifa vya kuand...
Tangazo - CEO usinivue mi nimchumba wa mtu mwanzo wa simulizi Hadi Mwisho wa simulizi
CEO usinivue mi nimchumba wa mtu mwanzo wa simulizi Hadi Mwisho wa simulizi
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA
Ligi Kuu imeendelea kupiga hatua kubwa katika maendeleo kiasi cha kushika nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS)
Ligi Kuu imeendelea kupiga hatua kubwa katika maendeleo kiasi cha kushika nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).
.
Hili ni jambo la kujivunia, lakini uwepo wa watu wanaoitwa makomandoo ambao wamekuwa na jukumu la ulinzi kwa timu husika ni tatizo kubwa ambalo halifai.
.
Tukio la juzi kwamba makomandoo wa timu moja wanadaiwa kuhusika katika kuvuruga na kuathiri kanuni za ligi lina paswa kuwa ishara kwamba, hawa watu hawafai na hawastahili kukumbatiwa na timu hizi mbili.
.
Kitendo cha kikundi cha watu kuzuia timu isiingie uwanjani kufanya mazoezi kwa mujibu...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/ligi-kuu-imeendelea-kupiga-hatua-kubwa-katika-maendeleo-kiasi-cha-kushika-nafasi-ya-nne-kwa-ubora-ba
Maoni