Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐿𝑜𝑣𝑒𝑆𝑡𝑜𝑟𝑦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 𝐁𝐎𝐑𝐍 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐎𝐔𝐒𝐄 𝐆𝐈𝐑𝐋 (𝙎𝙝𝙖𝙣𝙜𝙖 𝙆𝙞𝙪𝙣𝙤𝙣𝙞) 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊 SEHEMU YA 07

27th Aug, 2025 Views 102


Kiukweli kwa hali halisi ya maisha ni kwamba watu ambao maisha yao ni duni wanaogopaga sana kutoka na watu ambao wana maisha mazuri, hii ni kwa sababu ya kushindwa kulinganisha hadhi, hivyo basi Nasma alivyokuwa anawaza kuhusu kija Raymond aliona kama vile anapoteza muda wake.

Ray alimaliza kupiga mswaki akaenda chumbani na kuchukua taulo halafu akazama bafuni akioga “Mh yaani Rose atahisi nimesusa jamani wakati ninampenda sana” aliwaza akiwa bafuni anajipaka sabuni taratibu. Maana tangu jana usiku alikuwa hajamtakia hali mpenzi wake wa jijini Dar aitwaye Rose.

Ray alioga haraka haraka na kuweza kurudi chumbani, muda huo bado mama yake alikuwa amelala, ila mzee alikuwa akichunga mbuzi wake mitaa ya jirani kidogo kutoka pale nyumbani.

Ray alitoka nje akiwa ananukia, hasa, halafu akasimama mlangoni na kumuangalia binti aliyekuwa anamalizia kufagia uwanja “Heeeh kaka” Nasma alianza mazoea

“Nini” aliuliza Ray

“Unaoga kila saa?” alimuuliza

“Kawaida, nimezoea, kule Dar kulivyo na joto lazima mtu uoge mara 3 mpaka 4 kwa siku”

“Mungu wangu ni nyingi sana” alisema Nasma

“Vipi wewe umeoga kweli tangu jana, maana nguo zilikuwa hizo hizo” Ray aliuliza

“Hamna, nimeoga, sema tu, nguo mimi ninazo mbili tu, hii ya kufanyia kazi, ila nikishaoga navaa hiyo nyingine nzuri nzuri”

“Mungu wangu, nguo mbili? Unalipwaga mshahara?” alimuuliza

“Nalipwa, ila hivyo nyumbani kuna maisha magumu, mimi ndo mtoto ninayetegemewa na wazazi mshahara wangu huwa unatumwa kwao wote”

“pole sana” alisema Ray binti akatikisa kichwa na kuinama kuendelea kufagia uwanja wake “Utaratibu wa chai vipi?” aliuliza Ray

“ngoja namalizia usafi halafu nitatengeneza” alisema binti

“vitafunwa je?” aliuliza

“Kuna kiporo cha makande”

“Hahahaaa…..kwa huu mjengo nilijua maisha yamebadilika lakini kumbe wapi, embu niacheni kidogo bwana mimi ngoja nikalete vitafunwa nje huko.” Alisema Ray na kurudi ndani akachukua pochi pamoja na simu yake akatoka nayo mpaka njiani.

Alitembea tembea, kutafuta sehemu yakununulia chapati au vitafunwa vingine vitramu vitramu, akaona kama vile pale kijijini hakuna, ndipo akaanza kuelekea katika duka moja kununua mkate. Kabla hajafika akasikia sauti

“We, Raymond” ilitokea sauti nyuma yake, akatazama, ni Elinami pamoja na Doto walikuwa na mizigo ya majani wanapeleka nyumbani.

“Naaam” aliitika na kusimama kuwasubiri mpaka wakafika pale

“Heh, ni wewe unanukia barabara nzima jamani?” Elinami alianza kumpamba lakini Ray alimtazama kwa aibu kidogo

“kawaida mbona?” alisema Ray na kumgeukia Doto aliyekuwa pembeni mwa Elinami

“Shikamoo” alisema Doto huku akimkagua kuanzia juu mpaka chini

“Marahaba wewe ni yupi tena?” aliuliza

“Doto” alisema binti

“Doto yupi….wale niliwaacha vidonchi juzi juzi wa kwa mama Saumu?” aliuliza

“ndio”

“Duuuh mnakuwa sana” alisema na kumgeukia Elinami “Vipi natafuta sehemu wanayouza chapati chapati ntapata kweli humu kijijini?” aliuliza

“Dah, ni mbali, karibia na sokoni mule….ina maana umeshasahau mitaa hii miaka michache tu mh” alimuuliza binti

“Hamna, maisha yamebadilika, mimi kipindi natoka huku kulikuwa hamna maendeleo hivi, nyumba kama hizi hapa, zote hazikuwepo” alisema akizungusha mikono angani kuonyesha nyumba zilizokuwa zimejaa maeneo yale

“Ndo hivyo lakini, wewe nyoosha na hii barabara, utapaona kumechangamka kidogo kuna kabango kameandika Rukia Food” alisema Elinami

“Ok powa asante” Ray alisema, ndipo Elinami akamkonyeza kwa style fulani kwamba watawasiliana kwenye simu, halafu jamaa aliondoka zake akiwa anatabasamu.

Alimtext Rose, Good morning babe” alitum text kwa furaha lakini kwa bahati mbaya Rose hakujibu kabisa ile message akajua labda yuko bize na kazi yeye akaendelea na mishe zake

Kweli alifikia maeneo fulani akaona bango dogo limeandikwa Rukia Food, akatazama, akamuona mama mmoja mweusi mweusi akisukuma chapati

“Shikamoo” alisilimia ikabidi yule mama atabasamu bila kuitikia salamu yake “Vipi mbona unatabasamu” aliuliza

“Hahaaa…..hivi Ray, wewe ni wa kunipa shikamoo mimi?” mama yule alimfahamu

“mh…..mbona sijaelewa hapo kumbe najulikana”

“Embu kwenda bwana,….yani mkishatoka mjini ndo zenu, mnasalimia hadi wadogo zenu, au kisa tumezeeshwa na maisha sisi?” aliuliza

“Mmmmh hapana, sister sorry sijakujua fulani hivi”

“Humkumbuki dada mkuu wako ee?” aliuliza huku akimkazia macho, ndipo Ray akakumbuka na kucheka

“Hahahaaaaaa……Sawa bana, jina la Rukia likanichanganya kumbe Mwanaidi…ok sorry sana nimezeeka mpaka kumbukumbu zimeenda mbali

“Achana na mimi” alisema huyo dada kwa jeuri, halafu akainuka “Embu nipe zawadi yangu kutoka huko mjini, au ndo umemletea mama yako peke yake” alisema mwanamke yule

“Hamna cha zawadi wala nini, sikia, nifungie chapati 3 mara 4, nikale raha mimi” alisema Ray

“Mh yaani chapati kumi na mbili?” aliuliza mwanaidi

“Yaaap” Ray alisema na kutoa noti ya 5000 kwenye pochi akamkabidhi, na yule dada alifanya hivyo “Shilingi ngapi inakuwa” aliuliza

“3600” alisema huyo dada maana chapati moja ilikuwa sh 300 tu

“Ok iliyobaki kunywa soda”

“Hayo ndo maneno, lakini kabla ya yote uoee” alisema mama huyo

Wote walibaki wakicheka huku akizidi kumuwekea chapati kwenye gazet. Akiwa anasubiri chapati pale ziwekwe vizuri, Doto alitokea akikimbia na kusimama pale, akamtazama Ray na kumuongelesha kwa sauti ndogo “Unisubiri” alisema hivyo ili muuzaji asielewe kinachoendelea

Hata hivyo mwanamke huyo alimaliza akamuwekea vizuri na kumkabidhi Ray, wakaagana Ray aliondoka kwa mwendo wa taratibu huku akimsubiri Doto taratibu alikuwa anataka asikie kwamba ataambiwa nini

“Doto leo umekujua huku?”aliuliza

“Ndio,naomba unipe chapati mbili haraka ninawahi” alisema Doto

“sasa mbona kuna moja tu imebaki hizo zingine ni za kusubiri” alisema mwanaidi

“Basi nipe hiyo hiyo, inatosha” aliongea kama vile ni mtu anawahi sana, kumbe alichokuwa anawahi ni kwenda kuongea na Ray.

𝐿𝑜𝑣𝑒𝑆𝑡𝑜𝑟𝑦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 𝐁𝐎𝐑𝐍 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐎𝐔𝐒𝐄 𝐆𝐈𝐑𝐋
(𝙎𝙝𝙖𝙣𝙜𝙖 𝙆𝙞𝙪𝙣𝙤𝙣𝙞)
𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
SEHEMU YA 08

Alipatiwa chapati moja na kuondoka akikimbia akamuwahi Ray, huku akicheka na kuhema sana

“We kaka, shikamoo” alimuamkia

“Kila saa??” Ray aliuliza

“Hamna jamani…si lazima nikuamkie kila saa kukuheshimu au hupendi?” aliuliza

“Ok marahaba, shule vipi?” Ray alijifanya kukaza asijeonekana mrahisi

“Shule nzuri, naona umeamua kuja kututembelea huku kijijini” alisema

“Hahaa….nimekimbia maisha magumu Dar wewe” alisema Ray
“Mmmh muongo, maisha magumu upendeze hivi?” aliuliza dotto

Ray alicheka kisha akamuambia “By the way sitakaa sana, nitaondoka siku sio nyingi”

“Unawahi nini? Au ndo wifi? Eeh naona, ila sawa kweli hawezi kuwa wifi” alisema mtoto huyo aliyekuwa na uchangamfu uliozidi kipimo

“Kwanini asiwe wifi?” Ray aliuliza

“Hahaa.. wanaume wa Dar hizo mambo mh, kwani mnakuwaga nazo?” alimuuliza ikabidi Ray asimame na kumshangaa kidogo

“Hiv wewe ni Doto au nakufananisha, mbona unaongea sana?” alimuuliza “Mtoto wa juzi una maneno mengi hivi, kwanza wewe una miaka mingapi?” aliuliza

“kumi na saba”

“Kumi na saba ndo uongee hivyo?” embu acha mambo yako, nambie kwanza mambo mazuri mazuri

“Mazuri ni yapi kaka? Embu kwanza, kwani hayo niliyoongea sio mazuri? Mbona jamani watu wanayang’ang’ania wanasema ni matramu”

“Shit………. Doto….kimbia uende nyumbani” alisema Ray”

“Haya sawa, basi nipe namba yako kaka”

“Elinami anayo kamuombe” alisema Ray

“Poa bye”
Binti alianza kukimbia mpaka akaenda nyumbani kwa Elinami huku akiwa ameificha chapati ili Elinami asishtuke kwamba alimfukuzia Raymond kule kibandani.

“Eliii” alimuita mwenzake

“Nini dogo?” alimwambia kwa kejeli

“Una message unisaidie nimtumie mtu?” aliuliza binti

Elinami alitoka na simu mkononi kisha akampatia binti mkononi “zipo chache” alisema na kuingia ndani kwake alikuwa anafanya fanya usafi kidogo

Kumbe ili ilikuwa ni gia ya binti kuiba namba ya Ray alitaka anagalao aibe namba ya Ray kwenye simu ya Elinami, hata hivyo bahati kama bahati ni kwamba Elinami alikuwa amesevu namba ya Ray hivyo hivyo kwa jina la Ray hivyo basi haikumpa taabu kuipata na kuiiba akaweka kwenye kisimu chake kidogo lakini kalikuwa ka-smartphone ka Samsung ambako ni version ya zamani halafu akamuita Elinami

“Shogaaa” alimuita “Mi naenda kufua simu yako niweke hapa?” alimuambia

“Nyooo, uweke simu yangu hapo? Je wakiiba” alisema mtoto wa kike huku akitoka ndani na kuipokea simu yake

“Asante ee” alisema Doto halafu akakimbia kuelekea nyumbani alipofika nyumbani hivi alikunywa kwanza chai na ile chapati yake

*
Upande wa Ray yeye muda huo alikuwa yuko mezani anakunywa chai na mama yake baba bado alikuwa anachungua mbuzi na kondoo wake, Ray alikula chapati mbili halafu akawa hoi na kuachana nazo halafu akatoka nje ya nyumba akamkuta Nasma akiwa ameketi kwenye ndoo akabaki anamshangaa

“Hivi wewe mbona hauna raha muda wote?” alimuuliza

“Samahani kaka, ndo hivi nilivyo mimi nina raha sana”

“Haya kale chapati huko ndani halafu leo kwani una kazi ngumu sana?” alimuuliza

“hapana ninafua nguo za baba na mama, halafu nitapika” alimuambia

“Ok basi, wewe nenda kanywe chai pale kuna chapati, ukishamaliza oga vizuri nikuone na nguo nyingine hiyo ni chafu sana” aliongea akimnyooshea kidole maana alijua uchafu tu ndo kilichokuwa kinamponza mpaka wazazi wakawa wanamdharau

“Sawa kaka….nilikuwa na mpango huo pia” alijitetea baada ya kuhisi amedharaulika.

“Sio kwamba nimesema hauogagi lakini nimekuambia uvae nyingine, wewe mbona mzuri ukiwa kila saa msafi basi utavutia saaanaa…hujioni ulivyo mweupe?” alimuuliza, Nasma alitabasamu kwa furaha kwani mwanamke anapenda kusifiwa sana

Alitazama chini kichwa mwake wakiwa anawaza kwamba mh kanipenda au? Lakini ni kwamba jamaa alikuwa anamsaidia tu kimawazo, sio mapenzi.

Hata hivyo baada ya maneno hayo, Ray aliondoka akaenda mpaka pale baba yake alipokuwa anachunga mbuzi “Mzee umeamkaje?” alimsalimia

“salama umeamkaje wewe?” alimuuliza

“sijambo, emb niachie mbuzi hapa ukanywe chai kidogo” alisema Ray na kusogea kwenye jiwe akaketi

“Huh, kuna chai na nini viporo mimi sili bwana” alisema

“Hahaha, mzee unaringa… kule nimeleta chapati za kutosha” alisema kijana huyo

“Hapo sawa” mzee alisema akitabasamu na kuanza kuondoka kuelekea nyumbani.

Sasa alipomuacha Ray pale na mbuzi Ray alipata muda wa kupiga selfie za kutosha, halafu aliwatumia marafiki zake aliokuwa akifanya nao kazi huko jijini Dar.

Lakini pia alimtumia Rose na kuweka captions “Ukwen kuko hivi utakuja kweli wewe mtoto mayai?” alisema na kumtumia, akaona imefika na kusomwa tayari, lakini haikujibiwa ikabidi ampigie simu aelewe labda ni ubize ama

“hallow Rose” aliongea baada ya binti kupokea simu

“Usiniite tafadhali niache na maisha yangu” Rose aliongea kwa hasira na kukata simu

Hilo suala lilimpa taabu sana Ray maana alimpenda yule mwanamke japo alikuwa akimsaliti mara kwa mara. Alimpigia simu tena na binti hakupokea simu kabisa ikabidi jamaa abaki akicheka maana hakuelewa kosa lake liko wapi “ni hasira kisa sijamtafuta asubuhi atakuwa powa tu” alijisemea Ray na kuchukua jiwe akamrushia kondoo aliyetaka kuondoka eneo lile.

Baada ya kumrushia jiwe, alisikia ujumbe umetumwa akaufungua ni namba mpya
“Hello, uko pouwa?”

“Niko powa, nani?” alimuuliza

“Mi Doto, ingia WhatsApp kuna kitu nimekutumia” alisema Doto

“Ok” Ray alijibu na kuingia WhatsApp moja kwa moja, alipongia hivi aliona ametumiwa ujumbe na Doto, akaingia kwenye msururu, alichokiona kutoka kwa Doto wala hakuamini…………..JE KAONA NINI?
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐿𝑜𝑣𝑒𝑆𝑡𝑜𝑟𝑦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 𝐁𝐎𝐑𝐍 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐎𝐔𝐒𝐄 𝐆𝐈𝐑𝐋 (𝙎𝙝𝙖𝙣𝙜𝙖 𝙆𝙞𝙪𝙣𝙤𝙣𝙞) 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊 SEHEMU YA 07  >>> https://gonga94.com/semajambo/lovestory-last-born-na-bikira-ya-house-girl-shanga-kiunoni-burudan-simulizi-sehemu-ya-07



#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war

#love #instagood #photooftheday #fashion #beautiful #happy #tbt #followme #picoftheday #art #nature #travel #fitness #motivation #life #fun #instagram #friends #smile #food


 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork