MFALME KIPOFU 25 -- 26
Whatsapp.............0748697173
ilipoishia sehemu iliyopita.......
Maneno ya Lindiwe yalimfanya Princess Nailet kutabasamu nakutulia kuwaacha waongonzane watu watatu tu Malikia,Prince Yao na Amma mwenyewe kwenda kutafuta iyo dawa......
ENDELEA NAYO..........
Malikia andwaa aliongoza msafara wa watu watatu na wapitia sehemu ya ulipokuwa mlango wa siri wakielekea polini.
Walifika polini na kazi ya kwanza Amma ilikuwa ni kwenda kwenye mti wa ajabu.
Amma kwake yeye ile ilikuwa ni kazi nyepesi mana mti wa ajabu alikuwa anaufahamu vizuri mno, sifa kuu ya mti huo ni mti anaotibu magonjwa mengi ndio mana hupenda kuuita mti wa ajabu,
Walielekea katika mti huo na kwakuwa Amma ni binti aliyekulia maisha ya kila aina alipanda na kuchuma majani mawili makubwa na kurudi kwenye farasi kwa ajili ya kuendelea na safari.
ila Malikia Andwaa alishangaa baada ya kumuona Amma anapanda tena kwenye Farasi badala ya kumtibu Prince Yao,
"Wewe binti dawa siumechuma iyo mbona unapanda kwenye farasi???",malikia aliuliza
"Unataka mwanao apone au hutaki???"
Malikia alikuwa mpole baada ya jibu la Amma na kuamua kunyamaza kwa kufata maelekezo yake, walielekea katika mto unaoitwa ADEYU mto utokeao katika falme ya YUNDI na kupita ADELI na walifanyikiwa kufika kwenye mto husika.
Amma alishuka kwenye farasi akiwa na majani yake mawili alielekea katika mto na kuchukua maji kupitia kiganja cha mkono wake na kuyadondosha yale maji kwenye kila jani alipomaliza alimfata Prince Yao aliyekuwa haelewi kilichokuwa kikiendelea.
Jani moja alimgusisha kwenye jicho la upande wa kulia na jana jingine nalo alifanya hivyohivyo kwenye jicho la upande wa kushoto.
Tangu kuzaliwa kwake leo hii macho yake yanapata nafasi ya kuona mwaga wa jua ukoje,
na kumshuhudia mama yake mzazi pia nakuiona sura nzuri ya mwanadada Amma.
"Na mimi naona!!!,mama mwanao naona!!!!, Prince Yao aliongea.
Prince aliongea kwa furaha huku machozi yakimtoka hakuamini kama ipo siku atakuja kuona kwenye maisha yake.
Binti nashukuru sana kwa kumtibu mtoto wangu sijui nikupatia zawadi gani???, malikia furaha ilimzidi mpaka akasahau kama waliwekeana ahadi na binti Amma.
"Hii ilikuwa ni ndoto iliyokuwa ikinisumbua tangu nilipokuwa mdogo nilizaliwa ili nije nimtibu Prince wa falme hii ya ADELI".
Amma aliongea na kuwasimulia kila kitu Prince Yao pamoja na Malikia Andwaa jinsi ndoto ile ilivyokuwa ikimsumbua tangu alipokuwa mdogo mpaka kukua kwake.
Safari ilianza ya kurudi katika jumba la kifalme na upande wa Prince safari kwake ilikuwa ni fupi kutokana na kushangaa kile alichokuwa akikiona njiani.
****************
"Jamani huu sasa ni ujinga kwanini tunahangaika ivi huku tunaweza kwenda kwa mfalme wa hili taifa na akatusaidia kumpata Princess",moja ya asikari wa YUNDI alitoa wazo kwa wenzake.
"Hapo umefikilia jambo la maana twendeni kwa mfalme"
Makubaliano yanafanyika juu ya asikari hawa kutoka katika ufalme wa YUNDI na waliamua kwenda kwa Mfalme wa ADELI ili waeleze shida yao.
********************
Nzegi anafanyikiwa kufika nje katika jengo la kifalme na kwakuwa ni mtu aliyefanya kazi kwa mda mrefu katika jengo hilo anapata mbinu ya kuingia ndani katika jengo la kifalme na alipitia sehemu ambayo ni ngumu kwake kuonekana.
"Kuingia nimeingia kumpata huyu binti ndio tatizo kubwa,ngoja nielekee huku"
Nzegi alielekea upande ambao mfalme amelazwa, alikuta walinzi mlangoni ila yeye alizunguka upande wa nyuma nakupitia dirishana.
Wakati yote hayo yanaendelea Prince Yao,Malikia Andwaa na Amma wanaingia katika jumba la kifalme huku Prince Yao akiwa na hamu ya kuwaona Lindiwe na Princess Nailet.
Nzegi anafika chumbani na kumkuta mfalme akiwa amelala akiwa hajitambui,alichomoa upanga wake kwa ajili ya kumkata Mfalme ila alipotaka kumkata na upanga mfalme alikohoa kwa mara kwanza,
"Khokhokhokhokhokho!!!!"
Hali iliyopeleka walinzi wasukume mlango na kumkuta Nzegi akijiandaa kumshambulia mfalme walimuwahi na kuanza kupigana nae,
Sauti za mapanga zilizokuwa zikisikika pale, sauti zile Princess Nailet alizisikia na kumfanya asogea eneo la chumba hicho cha mfalme.
Princess Nailet alikuta tayali Nzegi ameshaua walinzi wengi kasolo mmoja tu hali iliyomfanya Princess Nailet kupiga kelele kwa sauti ya juu iliyowafikia Prince Yao na Malikia Andwaa mana walikuwa tayali wameshafika katika jumba hilo la kifalme na ata watu wengine kwenye jumba lile la kifalme walisikia sauti ile ya Princess Nailet.
Nzegi alikasilika baada ya Princess kupiga kelele alirusha upanga wake ulioenda kumchoma moja kwa moja Princess Nailet kwenye tumbo lake,
Nae alisahau kama alikuwa yupo kwenye mapigano, alishangaa jamvia linazama tumboni kwake na kutokezea upande wa mgongoni palepale Nzegi aliaguka chini na kupoteza maisha.
Prince Yao akiwa na malikia pamoja na Amma wanafika katika chumba cha mfalme na kukuta kitu ambacho hawakutegemea.......ITAENDELEA.
Nini hatima ya Princess Nailet amekufa baada ya kuchomwa upanga na Nzegi au bado yupo hai???tukutane sehemu inayofata.
KESHO TUNAMALIZIA SIMULIZI YETU HII PENDWA NDUGU ZANGU na ndio mwanzo wa simulizi nyingine inayoitwa FARASI MWEUPE jumatatu itakuwa hewani karibuni sana.
[12/12/2025, 6:40 AM] zooper simulizi2: Story.....................MFALME KIPOFU
Mtunzi...................Zooper
Sehemi..ya............ 26
Whatsapp.............0748697173
Ilipoishia sehemu iliyopita........
Prince Yao akiwa na malikia pamoja na Amma wanafika katika chumba cha mfalme na kukuta kitu ambacho hawakutegemea...............
ENDELEA NAYO.....
Hawakutegemea kumuona Princess Nailet akiwa katika hali mbaya,
Prince Yao hakuamini macho yake mwanamke ambae alipanga kuja kumwona kwa mara ya kwanza alafu leo hii anabahatika kumwona kwa mara ya kwanza tena akiwa kwenye hali mbaya.
Princess Nailet alinyoosha mkono kumuita Prince Yao ambae nae alisogea huku macho yake yakitoka machozi na kushindwa kuyazuia.
"Hatimae umeona sasa Prince,nimefurahi leo kuona mboni za macho yetu zimekutana kwa mara ya kwanza Prince Yao",Princess Nailet aliongea kwa tabu.
"Naomba usiongee tafadhali hali yako sio nzuri na daktari yupo hapa atakutibu na utapona tu Princess".
"Prince eeeeee umeshachelewa Prince"
"Unaongea nini Nailet naomba unyamaze ili utibiwe", Prince Yao aliongea kwa uchungu.
"Princee eee naomba uende ukaniombe msamaha kwa baba yangu najua nimemkosea sana, mwambie nilikuwa binti mjinga sana na msumbufu kwake, na neno la mwisho kwake mwanambie Mfalme Tengu kwamba mwanae nampenda sana".
Princess Nailet aliongea maneno yaliyomgusa karibu kila mtu aliyekuwa pale ata Malikia Andwaa nae alijikuta machozi yakimtoka.
Princesa Nailet bado aliendelea kuongea,
"Ombi langu la mwisho kwako Prince naomba siku ukioa basi uchague mwanamke mwenye sifa za Amma, awe binti mpole na mtaratibu kama Amma huyo ndiye atakayekufaa"
"Unaongea nini Nailet?,tulia utibiwe Amma njoo umtibu huyu wewe si dakitari mbona unaangalia tu".
Prince Yao alimwita Amma lakini hakuwa na chochote cha kwenda kufanya zaidi ya kuangalia tu mana ilijizihilisha ni ngumu Princess Nailet kupona.
"Nataka kulala,naitaji kulala prince naomba usinipigie kelele kwa kulia nitashindwa kulala Princee....."
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya mwisho kutoka kwa Princess Nailet akifia mikononi mwa Prince Yao,
Si Lindiwe wala Prince Yao ambao walilia sana kutoka na kifo cha Princess Nailet ilikuwa ni huzuni katika jumba hilo la kifalme.
***************
Walinzi waliotumwa kuja kumchukua Princess Nailet ili wamrudishe kwa mfalme Tengu nao walifika katika jumba la ufalme wa ADELI kwa ajili ya kutoa tarifa juu ya ujio wao pale ADELI kutoka katika ufalme wa YUNDI.
Majonzi yakiwa bado yanaendelea Malikia andwaa analetewa tarifa kuwa kuna ugeni unaomhitaji.
Asikari walitoa salamu kwa heshima mbele ya malikia na kuelezea kilicho waleta pale ADELI na hawakusema kingine zaidi ya kumtafuta Princess Nailet,
"Mmesema mliyekuja kumtafuta anaitwa Princess nani???",Malikia Andwaa aliuliza.
"Anaitwa Princess Nailet",moja ya mlinzi wa YUNDI aliongea.
Masikio ya Malikia ni kama haya kusikia vizuri aliwauliza na wakalitaja lile jina kwa mara nyingine tena.
Malikia aliondoka na mlinzi mmoja kutoka YUNDI ili ajihakikishie kama ni yeye kweli aliyefariki pale mda mchache uliopita au la,
Mlinzi aliingia na kumkuta Prince Yao analia na alisogea na kumwona Princess Nailet ametulia kumaanisha kuwa hayupo duniani tena na hapo ndipo alipopata uhakika kuwa ni yeye Princess Nailet na amefariki,
Alitoka na kwenda kuwaeleza wenzake ambao nao walisikitika sana kwa tarifa zile.
"Princess ameshariki tunafanyeje sasa ndugu zangu"
"Ni kumsafirisha tu hakuna kingine cha zaidi", mmoja ya walinzi alijibu.
Taratibu zilifanyika za kuusafilisha mwili wa Princess Nailet na Prince Yao alijumuika katika msafari ule wa kuelekea katika falme ya YUNDI.
*************
General Tengeli akiwa na rafiki wa Zengi ambae ni marehemu pamoja na Cheki mwenyewe walisikitika juu ya kifo cha Nzegi kilichompata katika jumba la kifalme,
Cheki aliona mambo hayaendi vizuri kama walivyopanga aliamua kufanya maamuzi aliyoona ni sahihi kwa upande wake,
"General mimi naona ni mda sahihi wa mimi kurudi katika ufalme wetu sihitaji tena hii nafasi uliyonipa",Cheki aliongea na kunyenyuka ili ainze safari,
"Unauhakika hutojutia maamuzi yako??",General alimuuliza.
"Ndio General",
"Aya kawasalimie"
Askari alishangaa kuona amelukiwa na damu, kuangalia ni kichwa cha Cheki kilicho kuwa kimetenganishwa na mwili.
"Watu kama hawa ata wakienda huko bado wataendelea kuwa wasaliti kwa wenzao,leo nimaombelezo juu ya kifo cha Nzegi na sio kuagana hapa".,General aliongea.
Cheki aliuliwa kikatili na General ukawa ndiyo mwisho wa Cheki.
Nguvu ya General ilipungua kwa kiasi kikubwa baada ya kumpoteza Nzegi,sasa amebakiwa na mtu mumoja tu.
***************
Prince Yao na wenzake wanafanyikiwa kuufikisha mwili wa Princess Nailet katika ufalme wa YUNDI,
Mfalme Tengu anashangaa kuona ujio ule usio kuwa wa kawaida wakiongozana na Prince Yao tena nyuso za asikari wake zikitawaliwa na uzuni.
"Nini kimetokea mbona Princess Nailet simuoni???"
Kila mtu alikuwa kmya walishindwa waanzeje kumweleza mfalme Tengu ili awa elewe.
Nawauliza, Princess Nailet yupo wapi mbon..?
alipokuwa anaongea alitazama Pembeni haku amini kuona mwili wa binti yake...........ITAENDELEA
Mfalme tengu atachukua maamuzi gani baada ya mwili wa Princess Nailet kuletwa katika ufalme wake?? Tukutane sehemu inayofata kwa ajili ya mkasa huu wa kusisimua zaidi.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni