MFALME KIPOFU MtunziZooper ...................Sehemi..ya............16 & 17
Ilipoishia sehemu iliyopita......
Asikari",Mfalme Tengu aliita kwa hasira
"Nendeni mkawarudishe haraka"
"Mfalme tayali wameshavuka mpaka"
"Nimesema nendeni mkawarudishe"
Waliondoka na kumuacha Mfalme akiendelea .....
SEHEMU YA 16
ENDELEA NAYO......
Waliondoka na kumuacha mfalme akiendelea kuongea na binti yake huyo ,
"Chondechonde binti yangu ata kama akija naomba usiolewe na yule kipofu sitaki kuona ufalme wangu unaongonzwa na kipofu itakuwa vyepesi sana ufalme huu kuanguka".
"Lakini mimi nampenda sana Yao???, nataka awe mume wangu"
"Binti yangu sio kila unayempenda lazima uwe nae mda mwingine hatima huamua, ata mimi pia nilimpenda mwanamke mwingine lakini hatima ikaja kunikutanisha na marehemu mama yako"
Manane ya mfalme yalimfanya aelewe Princess Nailet.
"Sasa naomba tuweke makubaliano ata kama wakirudi lazima utii makubaliano yetu"
"Sawa baba nimakubali kiwekeana makubaliano"
"Sitaki kuona unakuwa karibu na Yao na nita kutafutia mtu mwingine wa kukuoa".
Princess Nailet hakuwa na jinsi kwakuwa alitaka Prince Yao na Lindiwe waweze kurudi aliamua kukubali tu.
"Sawa baba nimekubali,sitaki kuona mtu asiye na hatia anafukuzwa kwa ajili yangu nataka kumuona Yao akirudi hapa pamoja na mama yake.
******************
Prince Yao na Lindiwe wanakaribia kuingia katika ufalme wa ADELI,
"Yao huku ni kama nyumbani kwenu tunakoenda naamini utapapenda zaidi"
"Natamani ningekuwa na uwezo wa kuona nione kinacho endelea,Yao aliongea kwa huzuni".
"Ipo siku utaona".
"Ni miaka mingi sasa imepita, huwa unanipa tumaini la kuja kuona ila sioni izo dalili mama za kuona".
"Mungu anasababu zake Yao naamini ipo siku utaona tu".
Lindiwe aliendelea kumtia moyo japo ata yeye alijua ni ngumu kwa Yao kuweza kuona.
Lindiwe aliwaza ni sehemu gani ya kwenda atakapofika kwenye ufalme huo wa ADELI, baada ya kuondoka kwa mda Mrefu na sasa anarejea akiwa n Prince Yao.
**********
Majira ya usiku General pamoja na Nzegi wakijiandaa kwa ajili ya kwenda kutekeleza mipango yao katika nyumba ya waziri mkuu,
Waliondoka na kuelekea kwenye nyumba ya waziri mkuu.
Waziri mkuu ni mtu anayependa kulewa sana hawezi kulala bira kunywa pombe na siku iyo kama kawaida yake alikuwa amekaa peke yake akiburudika na kinywaji.
"Naona unafurahia maisha tu"
"General......ume..in..gia...je.humu"
"Leo naona umepatwa na tatizo la kigugumizi emu nimininie na mimi ninywe ni mda mrefu hatujanywa pamoja"
Waziri mkuu alikiona kifo kipo mbele yake pombe zote zilikata.
"Walin........,kabra ata hajamaliza kutamka neno walinzi upanga wa General ulipita kwenye kolomeo lake huo ndio ukawa mwisho wa waziri mkuu"
General alitoka na kumkuta Nzegi amesimama nje akiangalia usalama ili wasipate changamoto yoyote,
"Kazi tayali imeisha anayefata ni mfalme sasa ivi"
"Heeeeeh!! Mfalme!!!!!".
"Ndio mfalme mbona umeshangaa??"
"Kuna ulinzi wa kutosha sasa ivi katika jumba la kifalme ni njia gani tutatumia kuingia katika kasili hilo la kifalme"
"Ndio mana nilimwambia yule asikari amlete Prince feki".
General ni mtu hatari sana na anakila mbinu ya kufanya kitu pale anapozamilia.
****************
Mfalme Tengu na binti yake maelewano yalirudi na sasa Princess aliamini Yao atakuwa ameshapatikana na watafika mda wowote katika ufalme wao,
Wakiwa wameketi wanapata chakula cha usiku walinzi walioenda kuwatafuta Prince Yao na Lindiwe walifika na kuleta tarifa,
"Mfalme hatujafanyikiwa kuwaona tumeangalia kila sehemu"
"Nyie wajinga kweli mumeshindwa kufatilia njia inayoenda katika ufalme wa ADELI"
"Tusamehe Mfalme hatukujua"
"Pumbavu kabisa emu tokeni hapa"
"Baba kwahiyo watakuwa wameenda ADELI?????"
"Ndiko walikotokea nazani watakuwa wameelekea huko".
Binti mfalme alinyenyuka akutaka kuendelea tena kupata chakula alielekea chumbani kwake na alichokuwa anawaza kwenye kichwa chake ilikuwa ni siri yake mwenyewe.
*******************
Lindiwe na Prince Yao wanafanyikiwa kufika ADELI na walipitia njia iliyokaribu na msitu mkubwa wa ADELI unaotumiwa na General pamoja na Nzegi kama sehemu ya makazi yao ya muda.
Prince Yao kwa mbali alisikia sauti ya watu wakiongea,
"Mama nasikia sauti za watu kwani unawaona hao watu????:
Lindiwe alitege sikio vizuri na kweli alisikia sauti emu njoo huku alimvuta Prince Yao pembeni na kujificha sehemu ambayo ni ngumu kuonekana.
Namu sura ya General haikutoka
machoni mwake alimuona
General akiwa......ITAENDELEA.
Princess Nailet atafanya mamuzi gani??baada ya kuletewa tarifa za kukosekana kwa Yao na Lindiwe,na Mfalme Kojo atapokeaje tarifa za kifo cha Waziri mkuu?? sehemu inayofata inamajibu zaidi.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni