MR ARROGANT SEHEMU YA KUMI NA TATU*
Usiku ule Leon alirudi nyumbani akiwa hana amani kabisa. Alipoingia sebuleni aliweka lile ua juu ya meza, macho yake yaliendelea kuliangalia kana kwamba lilikuwa na nguvu ya ajabu ya kuvuta mawazo yake. Alijaribu kulipuuza, lakini kila mara alipojaribu kuliangalia alihisi kuona taswira ya Jasmine ikicheka, ikitabasamu na hata namna alivyolala usingizi ndani ya gari ilijirudia kichwani mwake.
“Kwa nini huyu msichana ananifanya nipoteze mwelekeo? Huyu ni secretary wangu tu… nothing else!” Leon aliongea kwa hasira huku akinyanyua grass cha maji ya kunywa akanywa kidogo Lakini hata alipokunywa, moyo wake haukupoa.
Kesho yake kazini, Jasmine aliingia ofisini akiwa amevalia suti ya rangi ya blue iliyokaa vizuri mno, nywele zake zikining’inia mabegani. Alionekana mrembo kupita kawaida. Kila mtu ofisini alimkodolea macho na kumsifia . aliingia moja kwa moja ofisini kwa Leon akiwa na tabasamu lake la kibabe.
“Habari za asubuhi njema Boss,” alisema kwa sauti ya taratibu, huku akimwekea faili mezani.
Leon alinyanyua macho yake na kumtazama kwa sekunde chache Kisha akajifanya mkali.
“Jasmine, fanya kazi zako. Sitaki drama zozote leo.
Jasmine alicheka kwa kebehi kidogo.
“Boss, drama unazozungumza wewe ndizo zinazoishi moyoni mwako. Mimi nimekuja kufanya kazi tu.
Maneno yale yalimchanganya Leon zaidi. Hakuwa na namna ya kumjibu. Alibaki akimtazama tu huku akijaribu kuficha tabasamu lisitokee usoni mwake.
Siku iliendelea, lakini Leon kila mara alijikuta akimwangalia Jasmine bila yeye kujua. Aliona jinsi alivyo na ujasiri, jinsi alivyo na akili kazini, na hata utulivu wake kwenye kufanya kazi Kila kitu kilianza kumvutia zaidi, japokuwa alikuwa anapinga moyoni.
Wakati wa mchana, Jasmine alifika mezani kwake akiwa amebeba chakula cha mchana.
“Boss, niliona hukutoka kupata lunch. Nilipita nikakuchukulia hii nadhani itakutana.
Leon alijiangalia kile chakula alafu akamuangalia Jasmine usoni
"Usijali, siyo sumu.
Leon aliendekea kumuangalia kwa macho makali, lakini ndani yake kulikuwa na joto fulani.
“Huwezi kuniwekea heshima kidogo Jasmine? Mimi ni Boss wako. Safari hii Leon waliongea kwa sauti ya taratibu na upole.
“Na mimi ni secretary wako, Boss,” Jasmine akamjibu bila woga, “na secretary bora humjali Boss wake hata mbali na kazi tu.
Leon alibaki kimya, akashusha pumzi. Lakini alipoangalia chakula kile, alihisi tofauti kama vile kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kulikuwa na mtu anayemjali kwa dhati.
" Asante acha hapo nenda kaendelee na kazi.
" Sawa.
Jasmine aliondoka . Alipofungua mlango tu Leon alianza kula kile chakula .
Moyo wa Leon ukawa katika vita kubwa: upande mmoja ukimwambia amuepuke Jasmine kabisa, lakini upande mwingine ukimwambia Jasmine ndiye dawa ya upweke wake.
Siku hiyo leon akijisemea liwalo na liwe hawezi iuishuhurisha akili yake kwasababu ya moyo.
Alimpigia simu Jasmine akamwambia.
" Jioni kabla hajaondoka nataka tuonane .
" sawa boss. Na kuna kitu kingine unahitaji boss wangu?
" Mmmh hapana.
" Sawa.
Leon alikata simu akakuna kichwa chake .
" Daaaah yani sijawahi kuijua rangi yake halisi kuna muda dishi kinayumba, kuna muda anakuwa mstaarabu. Mmmh kweli mchumba kisima huingia mwenyewe leo Leon ninedumukia kwenye kisima nilichochimba mwenyewe.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni