Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI❣️ SEHEMU YA 01

10th Sep, 2025 Views 33


Asubuhi na mapema mimi na mdogo wangu Poppy tulikuwa tunapalangana jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya wateja..

Tunamiliki kimgahawa kidogo tulichozungushia mabati mabovu hicho ndo kinatumatia kula na ada..

Wazazi weshafariki waliniacha nikiwa chuo mwaka wa kwanza na mdogo wangu poppy alikuwa ndo yuko form two..

Kwetu tumezaliwa wawili tu mimi Bella pamoja na poppy mdogo wangu..

Wazazi baada ya kufariki kitu pekee walichotuachia ni kijumba kidogo tulichokuwa tunaishi..

Hatukuwa na uwezo mkubwa kimaisha tulikuwa tunaishi kawaida na wazazi wetu walikuwa wafanya vibarua vya hapa na pale hivo ndo vilikuwa vinatulisha na kutusomesha..

Mimi na poppy tulishauriana kila likizo tuwe tunajishugulisha kuuza chakula ili tuweze kupata pesa ya ada..

Siku moja asubuhi wakati tunaendelea na shughuli zetu mgahawani hapo tulipata ugeni wa wateja wengi kidogo..

Walikuja vijana 12 ni mafundi ujenzi waliagiza chakula kisha wakatuambia Boss anakuja kulipa muda si mrefu❤️❤️..

Hatukuwa na kipingamizi maana sehemu walikokuwa wanajenga ni karibu na pale kazini kwetu..

Walikunywa chai hiyo asubuhi na mchana wakala cha mchana ilipofika jioni mimi na poppy tulikwenda kuchukua pesa..

Tulifika pale tukawakuta mafundi ndo wanabadili nguo kwa ajili ya kuondoka..

Walituambia Boss yuko njiani tumsubilie kidogo..tuliketi pale pembeni baada ya muda ikaja gari fulani hivi kali sana🤗🤗🤗...

Wale mafundi walisogea kumpokea aliyekuwemo kwenye gari alikuwa mkaka mdogo dogo tu umri kama miaka 30 mpaka 33..

Waliongea naye pale akawagawia pesa baada ya hapo akasogea tulipo tukasalimiana baada ya hapo akatuuliza tunadai sh ngapi..

Nilimtajia kiasi cha pesa tunazodai akachomoa waleti akatoa pesa nyingi zaidi ya ile tunayoidai baada ya kuzihesabu zile pesa nilishangaa😳😳

Nilitoa tunayoidai ingine nikamrudishia...yule kaka aliniambia it's okay itawasaidia hiyo..

Mdogo wangu aliipokonya ile pesa akasema asante kaka...mimi niliichukua nikamrudishia kisha nikamwamuru dogo tuondoke😒😒

Baada ya kuondoka pale mdogo wangu alianza kunigombeza...

Alidai shule zinafunguliwa na hatujapata ada ya kutosha sijui hata ni kwanini umeikataa ile pesa Dada..???🥹

Hebu kaa kimya poppy hivi unafikili kuna cha bure??.. koma kupalamia pesa za watu zitakuja kukutokea puani mdogo wangu.....😒

Sasa Dada ada tunalipa na nini??? Usijali poppy mi nitajua cha kufanya...

Lakini dada kwanini umeiacha ile pesa??? Huenda yule kaka ametupatia kwa sababu sisi ni yatima😞

Poppy tafadhali acha ujinga😳😳😳hivi mtu anakusaidia bila kukujua??.hebu acha tamaa ada tutaipata tu..

Wakati tunaendelea kubishana na poppy ghafla tukasikia mtu anatuita kwa mbali kugeuka tukamuona moja ya wale mafundi akiwa anatukimbilia..

Tulisimama kumsubilia... alitufuata akatuambia Boss amesema kama itawezekana tumsaidie namba yetu ili siku watakazokuwa wanakuja kujenga awe anatuambia tupeleke chakula🙄🙄

Niliona hiyo ni fursa siku watakazokuwa wanajenga mafundi tutakuwa tunaamka saa 10 za usiku..

Tunawaandalia kiamsha kinywa asubuhi kabla sijaenda chuoni nitakuwa nawapelekeaa nipate na pesa ya nauli za kwendea chuoni🥰🥰🥰...

Nilimpatia namba akaondoka....mimi na poppy tulirudi pale mgawahani kwetu tukaosha osha vyombo tukapaweka sawa then tuliondoka kwenda nyumbani..

Siku tunazokuwa mgahawani huwa tunaondoka huko tumekula cha usiku tukifika nyumbani ni kuoga na kukisomea tu..

Siku hiyo baada ya kufika home nilioga nikamaliza nikaanza kujisomea... simu yangu ilianza kuita huo usiku namba ngeni nikapokea..

Sauti kama naijua🤔🤔ni kama ya yule Boss aloomba namba ili awe anaoda chakula hahahaaa..

Itaendeleaaa
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI❣️ SEHEMU YA 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/mrembo-yatima-na-kijana-tajiri-sehemu-ya-01

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest