MREMBO YATIMA. NA KIJANA TAJIRI *SEHEMU YA 40* Nilirudi Tanzania nikiwa na huzuni nyingi lakini ndo hivo maisha lazima yaendeleee 😒😒😒...
Nilituliza akili zangu nikarudi chuoni kipindi hiko ndo nilikuwa mwaka wa tatu chuoni katika stage ya Degree..
Nilikuwa naendelea na masomo yangu huku naendelea na Driving course...kwenye kudrive hata sikuchelewa kujua😂
Ndani ya week mbili niliweza kuondosha gari😂😂😂viuoga kutetemeka kwenye usukani ndo vitu mwalimu alibaki kushughulikia🤗🤗
Na kunifundisha kuhusu alama za barabarani...that time maisha yalikuwa mazuri kiasi coz Romy alikuwa anasimamia kila kitu..
Na alikuwa ananilipa Girl friend allowance🥰🥰🥰..basi bwana maisha yalizidi kusonga mwezi ukapita and guess wat sikuingia period..
Nilichanganyikiwa 🙌🙌 kabla ya kwenda kupima nikamshirikisha Romy nikamwambia mi huku sizioni siku zangu..
Aliniambia nipime then nimpe majibu😴😴😴nilikwenda hospital nikafanya kipimo cha mimba majibu yakatoka nina mimba🤨🤨..
Nilimpigia simu Romy nikampa majibu😞😞akayapokea kwa mikono yote miwili😴😴aliniambia nisiwe na mashaka ye yuko tayari kuwa baba na atatutake care mimi na mtoto..
Duh wala sikuwahi kutarajia kama nitazaa bila ndoa lakini ndo ishatokea hakuna namna🙏🙏na jambo zuri zaidi mhusika alilipokea swala hili vizuri sikuwa na hofu saana..
Niliendelea na masomo huku tumboni nikiwa na ujauzito 🥰🥰🙈 Romy aliendelea kutujali alikuwa anafanya mawasiliano namimi mara kwa mara na alihakikisha sipati shida yoyote..
Mwezi uliofuatia nilitaarifiwa gari tuliloagiza tayari limeshawasili tuliambiwa siku arobaini ila lilichukua siku karibia 90..
Nilimtaarifu Romy akaniwekea pesa nikamalizie malipo nichukue gari🥹❤️... nilifanya hivo baada ya kulipia nililetewa gari mpaka nyumbani..
Lilifanyiwa service zote kuhakikisha liko sawa🥰🥰nilifurahi sana❤️❤️nilimshukuru sana Romy🥹 aliniahidi siku siyo nyingi atakuja kuniona..
Kweli baada ya miezi kadhaa Romy alirudi Tanzania alikuta ujauzito umeshakuwa mkubwa miezi saba na kipindi hicho nilikuwa likizo tulikuwa tumefunga chuoni..
Romy aliniambia inabidi tuondoke wote kwenda UK alidai anataka mtoto wake akazaliwe huko na siyo Africa 🙂🙂🙂alisema mtoto akizaliwa huku itakuwa ngumu kupata uraia wa kwao..
Ilibidi tuanze kuhangaikia visa🙌🙌🙌haikuwa rahisi but mwisho wa siku nilifanikiwa kupata visa ya UK...wakati huo mdogo wangu alikuwa ameshamaliza mitihani yake ya form four anasubilia matokeo..
Haikuwa rahisi kwangu kuondoka Tanzania na kumuacha mdogo wangu peke yake😭😭😭...nililia niliumia mno lakini ndo hivo ilikuwa ni lazima kumpeleka mtoto aende akazaliwe nchini kwa baba yake...
Nilianza maisha mapya UK nikiwa na tumbo la miezi minane... nilikuwa mpweke sana nilikuwa nikimfikilia mdogo wangu ndo kabisaaa nakuwa mtu wa kulia kila siku..
Romy aliniahidi atamleta poppy UK tuishi pamoja... niliteseka mwishowe nikazoea🙏🙏.. tulilea ujauzito mpaka ukafika miezi tisa..
Nilifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume❤️❤️🥰 baada ya kujifungua nilikaa miezi sita tukafunga ndoa na Romy ❤️❤️..now he is my husband and I am his wife ❤️❤️..tunapendana sana..
Baada ya ndoa tulirudi Tanzania kushugulikia mpango wa kumhamisha poppy Tanzania...
Wakati niko Tanzania siku moja nilienda katika ofisi moja hivi kugongewa mhuri kwenye barua za kupeleka huko uhamiaji😂😂😂
Nimefika huko nikakutana na Hemed bwana alishtuka Bella ni wewe🥺🥺 nikamwambia ndiyo ni mimi..za siku nyingi nikamwambia ni njema kabisa..
Umepotea sana napiga sana namba yako hupatikani hahahaa namba yenyewe nilibadili kitambo..Hemed alianza kuleta pigo zake za mara ooh nahitaji tuongee Bella unajua bado wazazi wangu wananitaka nikuoe wewe..
Namimi najua wewe ndo mwanamke wangu nisamehe kwa kila kitu cha nyuma tuanze upya🥺 hahahagaaaaaa
Nilicheka sana😂😂😂nikamuuliza kwani bado hamjafunga ndoa na yule mwanamke wako,.?? Akaniambia wameshaachana wanalea tu mtoto😂😂
Nilimpa pole nikamuonyesha Pete😝😝nikamwambia mimi nishachukuliwa Boy😝😝Hemed alichanganyikiwa akaanza kuniambia nimuache mwanaume wangu anioe yeye nyoo hiyo ni ndoto baba😂
Nilimwambia amka unaotaaaaaa wewe saivi siyo type yangu 💔💔 you are not my type😝😝..nilimuacha hapo nikaendelea na kilichonipeleka pale..
Mdogo wangu poppy alifanikiwa kupata visa ya masomo nchini UK 🙏🫂 tulifurahi sana🥰🥰
Angalau nilijisikia amani kwenda kuishi na ndugu yangu pamoja UK.. hata yeye alifurahi sana❤️❤️ ...
Tuliuza baadhi ya vitu tulivokuwa navyo Tanzania ikiwemo gari aloninunuliaga Romy niliuza nikaja kununua ingine hapa ulaya..
Tuliuza na ile nyumba tuliyoachiwa na wazazi wetu tukanunua kiwanja sehemu ingine ambapo tumepanga kujenga nyumba kubwa nzuri ambayo tutakuwa tunafikia tukija Tanzania...
Hiyo ndo historia ya maisha yangu... kwa sasa ninaishi hapa UK na mme wangu Romy...bado tuna mtoto mmoja nasubilia afike miaka mitatu nirudi shuleni..
Nimepanga kusoma course fupi hapa UK ili iwe rahisi kupata ajira hapa...mdogo wangu poppy yeye kwa sasa anasoma katika chuo kimoja hapa UK..
Asanteni sana kwa wote mlioifuatilia hii story nina imani kuna chochote mtajifunza❤️❤️❤️...
*mwisho*
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi





Maoni