Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 07

14th Sep, 2025 Views 49



Kwakweli sikuona Kama Ana umuhimu kwa wakati huo nilichofanya ni kumalizana na mapishi yangu na kwenda Kuwalisha watoto wangu.

KWa Mara ya kwanza watoto wangu wakapata chakula wakiwa chumbani kwao lakini pia walikula bila baba Yao, Yaani niliamua kuishi maisha yangu tu, na nilikuwa tayali kuondoka pale kwa mume wangu Leo kesho Ila watoto wangu tu ndio waliniweka pale.


Nikiwa nimetulia zangu chumbani kwangu, naperuzi tu mtandani gafla mlango wangu ulifunguliwa kwa nguvu sana na hamad ndio aliingia, Ila mapenzi yakiisha Walahi hakuna kitu unaweza kuogopa.

Hamad aliingia chumbani kwangu akiwa amevimba kama mbogo lakini Wala sikushtuka Wala kuogopa zaidi Nikamuangalia na kuendelea kuchezea simu yangu.

“Ina maana unioni au ??”

Hamad aliniuliza.

Pia sikujibu kitu niliendelea na mambo yangu.

“Shamsa nakuona hizi siku tangu umetoka hospital Sijui wapi wapi umekuwa na kiburi sana, Yaani umekuwa mtu wa tofauti sana,sasa sikia hizo dharau zako fanya lakini Kaa ukijua Kuwa Mimi ni mume wako Sawa “

Hapo nilinyanyuka na kujibu.

“İlo siwezi Kusahau na siwezi kusahau Kuwa wewe ni muuaji wa Mtoto wangu “

Hapo hamad alishtuka sana na kuniangalia kwa macho ya wasiwasi sana.

“Shamsa “

“Shamsa jina langu Sawa, hamad toka chumbani kwangu nataka kulala “


“Yaani unalalaje ikiwa umu Ndani sote hatujala?”

“Labda wewe na Hadija lakini Mimi na watoto wangu tumeshiba na watoto wangu wameshalala”

“Unamaanisha nini kusema mmeshakula ? Umenunua chakula kutoka nje au ?”

Nilimuangalia hamad kisha Nikatabasamu na kujibu.

“Mimi sio mtu wa kununua chakula Aswa likija suala la watoto wangu, Mimi Kama mama nimeingia jikoni na kupika”

“Kwahiyo umepika na Mimi ujanihesabia Wala Khadija si ndio ??”

“Hamad kwani huyu Khadija ni Pambo au ? Kwa haraka haraka Khadija ni mke wako wa halali kabisa na anastahili kukuhudumia na kubeba majukumu yake Kama mke, nilishika nafasi yangu na sasa ni nafasi yake “

Hamad hakuamini kabisa Kama ni Mimi ndio namjibu hivyo kwa hasira ya hali ya juu akatoka nje na kubamiza mlango kama anaugomvi nao vile.

Aaah kuna Namna niliona Kuwa natakiwa Kuwa imara kama hivi na sio kulia lia hovyo hovyo.

******

Siku ziliendelea kwenda uku nikiwa imara kuliko kawaida, nilihakikisha Kuwa siwi mnyonge Yaani ni mwendo wa kukaza tu.

Nikiwa Nyumbani siku ya jumatatu, niliweza kupokea simu kutoka kwa Neha na akaomba tuonane,
Kwakuwa uoga ulishaniisha kabisa nikatoka zangu na kwenda kuonana na Neha.

“Kuna kazi uko nimekutafutia shoga Angu Sijui Kama uko tayali kufanya”

Nilimuangalia Neha kisha Nikatabasamu na kumuuliza.

“Yaani nikatae kazi ? Weeeeh Neha acha utani shoga Angu, Yaani nataka kazi Leo kesho, nataka kumiliki Pesa zangu Mwenyewe na niwatoe watoto wangu pale”

“Nakuelewa ndio maana najaribu kukusaidia, hii sio kazi Kubwa lakini kwa kuanza nayo na ukiwa na akili Basi utafanikiwa kufanya chochote kitu”


“Ni kazi gani nawe nambie Yaani hapa natamani kuanza ata sasa “

“😂🙌 Ila wewe ni kazi ya gym, Nina shemeji yangu Ana gym kubwa sana na Anafanya na watu wa kubwa mno uwa analipa watu vizuri sana sasa nimekuombea uwe msimamizi wa pale kwenye usafi na mambo mengine “

Walahi nilijikuta nikicheka sana Yaani sio kucheka maana daaaah.

“Unacheka nini sasa ??”

Neha aliniuliza.

“Neha unataka nikaharibu kazi za watu au ? Yaani na huu mwili nawezaje kwenda kwenye gym ya watu ? Nitaleta mfano gani kwa watu ambao wamekuja kwaajili ya kutengeneza Miili yao”

“Shamsa huyo mwanaume wako ameshaharibu ubongo wako kwakweli, unajua siku ya kwanza pale hospital mume wangu ndio alianza kukuona na akaniambia huyu msichana ana body nzuri sana, imagine mume wangu ameshindwa ata kujua Kama wewe ni mama wa watoto wawili, Shamsa una shape nzuri sana Rafiki yangu ni vile tu mume wako anatumia nguvu zote kukufanya ujisikie vibaya “

Aaaah unacheza na kusifiwa nini, nilijikuta nikianza kutabasam kwa aibu aibu uku nikiangalia chini.

“So nitakufuta kesho Saa 4 asubuhi then nakupeleka sehemu husika dear ili ukaonane na boss wako maana Mimi nikishamaliza kila kitu “

“Asante sana Neha Mungu akubariki sana “

Tuliendelea kupiga story zingine pale kisha huyo nikarudi Nyumbani kwangu.

Ikiwa ni Majila ya saa 2 usiku nacheza na watoto zangu, muda huo huo hamad akaja na sauti yake ya kibabe akazungumza.

“Nina mazungumzo na wewe Shamsa “

Niligeuka na kumuangalia kwa muda, kisha nikawageukia wanangu na kuwaambia.

“Endeleeni nakuja sasa hivi”

Kisha nikanyanyuka na kutoka nje na moja kwa moja nikaenda kwenye chumba cha wageni ambacho kilibadilika na Kuwa chumba changu.

“Nafikili ni muda muafaka wa Mimi na wewe kupeana taraka “

Alizungumza hamad baada ya kuingia chumbani na kufunga mlango.

Nilimuangalia kWa muda kisha nikajibu.

“Ni moja kati ya Naombi yangu kila siku, lakini swali langu ni vipi kuhusu watoto wangu ??”

“Watoto wako ??”

Hamad aliniuliza Kana kwamba hakuwa amenielewa.

“Yaaah watoto wangu, hamad hawa watoto bado ni wadogo sana hivyo bado ni watoto wa mama Yao ambaye ni Mimi “

“Watoto wangu watabaki hapa, awawezi kwenda kuishi kwenye ufukara wenu uko”

“Mimi pia sitapokea taraka mpaka pale utakaporuhusu Mimi kuondoka na watoto wangu, Unafikili naweza nikaamini usalama wao mbele ya huyu mwanamke wako au wewe ? “

“Unafikili naweza nikawazuru watoto wangu ??”
Hamad aliniuliza uku akiniangalia kwa kunikazia macho.

“Vyote vinawezekana, lakini pia Mimi Kama mama nataka kuangalia makuzi ya watoto wangu”

“Shamsa haya mapembe uliyoota kuna siku Utakuwa kujutia trust me “

Alizungumza hamad kisha akaondoka zake.

KWa haraka nikarudi chumbani kwa watoto wangu lakini nikakuta wakiwa wameshalala hivyo niliweka vitu vyao vizuri kisha huyo nikarudi zangu chumbani kwangu.

******

Asubuhi na mapema nikaamka zangu na kufanya usafi wa kila kona kisha nikaanza kifungua kinywa cha watoto wangu tu na Mimi, Yaani umu Ndani majukumu yangu ni watoto wangu tu hao wengine ni watu wazima wajiongeze tu.

“Leo sitaenda kazini “

Alizungumza hamad kwenye meza ya chakula ambapo Mimi nilikuwa nikipata kifungua kinywa na watoto wangu.

“Mama ujaweka chai ya baba”

Mtoto wangu mkubwa aliniuliza.

“Baba yupo kwenye mfungo kwa sasa “

Yaani Nilijibu Mwenyewe halafu nikajikuta nikicheka 😂 Yaani Sijui Kwanini nilishindwa kujizuia kucheka.

Hamad alibaki akiniangalia kwa hasira sana lakini pia alishindwa kunifanya chochote kile.

Baada ya muda school bus ya watoto wangu ilifika na watoto wangu wakaondoka.

“Mbona uniulizi Kwanini siendi kazini ??”

Hamad aliniuliza na Mimi nikamuuliza.

“Kwanini nikuulize?”

“Kwa sababu mimi ni mume wako “

“Point of correction sio mume wangu mume wa wote “

“Vyote Sawa lakini Mimi ni mume wako na lazima ujue hatua zangu zote “

“Hamad unajisikia lakini ? Kama Mimi ni mke wako na nastahili kujua hatua zako Mbona hukunishirikisha wakati unamuoa Khadija ? Mbona ukuwai kunishirikisha kwenye chochote kile ? Hamad umefungua biashara kila kona uko lakini naishia kuzijua kupitia mitandao ya kijamii tu, ushawai kufikilia kuhusu Mimi ata siku moja ? Hamad kila mtu afanye yake “

Muda huo huo akaingia mama mkwe akiwa na Wifi yangu, Yaani mama mzazi wa hamad lakini pia na dada wa hamad.

“Muone Mdomo wake juu juu Kama kasuku “

Alizungumza mama hamad ni wazi Kuwa amesikia baadhi ya Maneno yangu.

“Shikamoo mama “

Nilimsalimia.

“Ningepata Mtoto Kama wewe ningemtupa uko uko hospital”

Alijibu mama mkwe wangu, nikaona hizi dharau zimezidi sasa, Nikamuangalia kisha nikataka kuondoka haraka akanirudisha nyuma kwa kunivuta mkono wangu.

“Ukinishika Tena huu mkono ndio Utajua maana halisi ya Kuwa mke wa kwanza kwa huyu Kijana wako kichaa Tena kwa ndoa ya mkeka “

Nikajitoa kwenye mkono wake na kutaka kuondoka, weeeh Wifi yangu si ndio akajichanganya na kunivuta eeeeeh 😂🙌 Leo ameyakanyaga nikamtuliza na kibao kizito sana cha shavu na vile ni mfupi 😂🙌.

My zangu hii vita bado mbichi..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 07  >>> https://gonga94.com/semajambo/mume-wangu-alivyoniolea-mke-wa-pili-sehemu-ya-07

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest