MZUNGU TULIA MOYO HAUNA RANGI part 2 to 3
SEHEMU YA 2
Hata mi sikujali kwanza niikuwa natamani nimmeze huyo mdada... Na vile tunalingana mwili sasa.
Aliyetustopisha alishuka taratibu kisha sasa yule mdada akawa anamfuata huku akilia kwa sauti ya chini... " Nini shida?" aliuliza kijana huyo ambaye, alikuwa na rangi kama ya huyo binti, pia alionekana kuwa serious sana kuliko kawaida๐.
"Nimemuuliza tu wewe ni nani, akataka kuninyang'anya kikombe cha chai huku akisema ananjaa ndio ikammwagikia... Sasa nashangaa anaanza kunitukana eti mimi nilimwagia makusudi," kibinti hiko kilisema huku kikiendelea kulia kifuani mwa kijana huyo ambaye, hakushughulika na kumbembeleza hata.
"Nani kaja na huyu binti?" aliuliza na kufanya wafanyakazi wote waogope... Sada alijitokeza mbele ya kijana huyo, kisha akapiga magoti.
"Samahani boss, huyu ndio yule mfanya kazi ulitaka wa kupika maandazi๐ข," Sada aliongea akiwa pale chini tena kwa uoga.
"Ooh! Njooni nae ofisini!" aliamuru kijana huyo kisha akaondoka, yule binti nae akamfuata kwa nyuma.
"Love, hivi hasira zako huwezi kujizuia au? Ona sasa tumeitwa hatujui tunaenda kuambiwa nini sasa๐คฆ!" alisema Sada akiwa kama kachanganyikiwa.
"Da Sada bana ๐! Mi nilishindwa kujizuia na siunajua kama hili dera langu ni jipya!" nilimfanya da Sada atabasamu kidogo, kisha tukaingia ofisini kwa kijana yule.
"Ndio boss, tumeitikia wito," alisema Sada kwa unyenyekevu.
"Good! So, anaumri gani? Na anahisi kutumikia kazii hii muda gani?" aliuliza huyo boss... Hapo nilitaka kujibu ila alinikata jicho na kusema kuwa hajaniuliza mimi nikae kimya.
"A.... ana miaka 21 tu, na kazi hii anaweza kutumikia muda wowote," Sada alisema...
"Okey! Mpe sare zake, na aliweke jina lake kwenye sare hizo; na baada ya kazi aje ku saini mkataba mpya," alisema kijana huyo.
Aliitikia Sada kisha tukatoka nje... " Hein๐ณ, hivo ulikuwa umebana pumzi!" nilimuuliza Sada kwa mshangao.
"Unajua Love, hii kazi walahi utanifanya nifukuzwe... Liam ni mkaka mmoja serious, na kuongea ni mara kidogo sana, sasa kwanza naona ajabu kuona katuacha... Njoo kwanza uvae sare zako," Sada alinipeleka kwenye chumba cha kubadili mavazi.
"๐ณ Da Sada, mbona ni fupi sasa! Kwa kweli mi siwezi kuvaa," niligoma kwasababu: kwanza ni sketi ya kubana nyeusi fupi, shati jeupe la mikono mirefu tena tunachomekea, na tie nyeusi.
"Nilijua tu! Ebu vaa halafu, ukienda ku saini mkataba utamwambia boss swala lako sawa?" niliitikia tu kwa kichwa... Ila kiukweli nilikuwa mwoga sana.
Nilichukuwa mtandio wangu wa dera nikajifunga kama kanga... Wafanyakazi wote walinishangaa.
"Loveness, mbona unavaa hivo? Unaficha nini na hauna hata nyama udugu wangu๐," alisema binti mmoja hapo... Nilisoma kwenye uniform yake nikaona anaitwa Zai.
"Ndio na mimi nashangaa hata nikiyaacha wazi hakuna atakae yataka... Kwasababu hata wenye nyama zao bado wapo hawajaambulia chochote," niliongea hivo kisha nikaondoka zangu.
Baada ya kazi, Sada alinisubiri nje mi nikaingia ofisini kwa boss... Lahaulaaaa! Siamini nacho๐๐... Basi nikarudishia mlango.
Lakini alikuwa ashaniona boss wangu... " Come in!" aliniamuru...
"Hivi wewe hauwezi kubisha hodi au?" kiliniuliza kidada hicho baada ya mimi kukutana kikiwa kinamlamba bosi mashavuni na hata mdomoni.
"Sasa humu si ofisini au? Na sio sehemu ya starehe, vyumba vipo! Mgeingia huko," nilisema hivo...
"Wewe! You are in my office! Sitaki kelele๐ ," alisema boss akiwa anapiga ngumi mezani kwake.
"Babby ni....( Sonia nikukute kwenye gari!)" aliamuru hivo baada ya kumkatisha yule binti maneno yake.
Nikasogea sasa kutazama mkataba, pia akanipa dakika 30 nisome kwanza... Tobaaaa ๐ณ! Nilichoka baada ya kuona sharti la mwisho.
To be continued ......๐ฅ
SEHEMU YA 3
"Boss๐ณ! Kazi tuliokubaliana si hii," nilisema nikiwa namshangao... Lakini boss wala hakujibu chochote.
Baada kimya kirefu alisimama na kunifuata... " Kama umemaliza ku saini unaweza kwenda na kama bado unaweza kwenda pia," alisema boss.
Jamani, hivi huyu mnamuelewa kweli au ndio ile wanasema kuendeshwa kwa vitisho... Hanijui sasa kenge huyu...
"Boss, hii sio sawa!" nilisaini nikiwa kama sijapenda kabisa.
"Usinipangie kwenye kazi yangu! Ulishafanya makosa, ukarudi tena ukavaa vitambara vyako, pia ukamtukana mke wangu, halafu unanipangia! Unaitaka adhabu siet?" boss alikuwa akifoka sana... Hapo sasa mwenzenu nishayafunga macho yangu kwa uoga.
Nikachukuwa na ku saini... Mkataba unasema hivi: Asubuhi napika maandazi ya hoteli, halafu hadi mida ya jioni nitamfanyia massage bibi yake yupo hapo hapo hotelini chumba namba 108; mshahara ni 500k kwa mwezi... Jamani khaaaa, kwanza mshahara ulinishawishi nikakubali.
"Ila boss, nitakuwa na sharti moja nami pia... (Sharti gani?)" niache nivae madera yangu mi sipendi nguo fupi," nilisema hivo.
Boss wangu alicheka sana kisha akaniambia niondoke bila kunipa jibu... Niliondoka nikafika nje nakuta dada Sada kanuna yaani kama alikuwa na hasira ya kufilisika kwa biashara.
"Haya muda wote huu unafanya nini huko ndani?" aliuliza Sada akiwa na hasira.
"Sasa da Sada, si ulinileta huku kufanya kazi sasa shukuru nimetoka salama humo ndani," nilisema nikiwa nasimamisha bajaji...
"Eeeh weee, ebu niambie kulitokea nini huko?" aliuliza Sada kwa hofu kidogo... Mi nilimuhadithia kila kitu lakini alionekana kununa balaa.
โSasa unakasirishwa nini we nawe! Badala ushukuru eti unanuna!" nilimshangaa sana Sada...
"Hiko ki Sonia kinakera! Nisikilize Love: pale inabidi umtege boss; kwani we hutaki maisha mazuri au?" Sada aliniuliza hivo...
"Da Sada ๐ณ, sasa kama nataka maisha mazuri ndio nimtege mkaka wa watu eeh! Hapana bana nitafanya kazi kama kawaida mengine siyataki... Na hata hivo hajanivutia," nilisema kisha tukashuka baada ya kuwasili home.
Basi hatukula maana tunatoka huko tushakula... Tulioga tukawa tunapiga story kibarazani na Kasie pia alikuja.
"Wifi, vipi mbona mpo nje?" aliuliza Kasie...
"Ndio, tunapata upepo wa saa tatu usiku," Sada alimjibu haraka sana...
"Khaa kwani nakusalimia wewe hata!" Kasie alisema...
"Eeh we Kasie, ebu kuwa na adabu bana! Si mkubwa kwako au?" nilimsema Kasie akaondoka.
Lakini baada ya muda, Fredy alikuja na kumvuta pembeni Sada, mkononi akiwa na mfuko mdogo tu...
To be continued.......๐ฅ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni