Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’‡๐’๐’–๐’“ ๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 141

25th Aug, 2025 Views 59



Amekomeshwa sasa chezea shemu wangu. Stewart anakupenda sana. Sikia mdogo wangu. Simamia mahusiano yako usiogope chochote yapiganie.โ€

Nikavuta pumzi na kusema โ€œndiyo dada, tujiweke naye mbali sio mtu mzuri.โ€

Dada alisikitika sana, na mara simu yake ikaita. Nilishtuka maana pia ilikuwa mpya. Akaongea alipomaliza nikamuuliza ndiyo naye akanielezea kuhusu furaha yake na Mr Fabian.

Aliniambia pia watoto wanampenda na Mungu akipenda amekubali kuolewa na huyo baba. Mimi nani niache kumbariki dada yangu na kitu kizuri kama hicho.

Nilifurahi sana dada pia ana furaha sasa, hana kizazi ila kapata watoto watatu kwa mara moja na atakuwa mama. Alifurahi hakika.

Ulikuwa wakati wa furaha sana. Nakumbuka Martha alipiga simu yangu. Nilishangaa sana. Nikamuonesha dada. Dada alisema โ€œpokea tumsikie.โ€
Nami nikafanya hivyo, Martha alisema โ€œnipo mbele ya nyumba yenu. Nina maongezi na wewe.โ€
Dada alisema โ€œhuendi peke yako. Twende wote.โ€
Nikamtazama tu, na kisha tukatoka. Alipotuona alishtuka. Dada alimsogelea na kusema โ€œumenitia aibu sana. Najua nina dada kumbe huna akili. Kwanini umfanyie hivyo mdogo wangu ambaye na wewe ulisema unampenda.โ€
Nakumbuka Martha alisema โ€œnaomba kuongea na Ndeana wewe tutaongea siku nyingine.โ€
Dada alitaka kujibu, nikamwambia dada kwa upole โ€œdada nisubiri pale. Usijali.โ€
Dada alitii na kusogea pembeni.

Nakumbuka Martha aliniambia โ€œNdeana, kaa mbali na Stewart. Ni mwanaume wangu, ninampenda sana. Wakati wewe unaenda sikujua kama itakuwa hivi, nilijua ni kama anavyowafanyia wengine. Sijui umemfanya nini kakuganda ila nataka utambue ni wangu. Hakuna mwanamke atakuwa naye, nipo tayari kwa lolote ila sio kuwa mbali na Stewart. Yule ni mwanaume wangu tu.โ€

Nikajikuta nacheka nikisema โ€œkwahiyo ulitaka kuharibu maisha yangu. Sasa kama ni mwanaume wako upo hapa kufanya nini. Kila mtu atumie nafasi yake vizuri. Wewe ni wako haya tamba naye na mimi ni wangu nitatamba naye.

Mwanaume mwenyewe yule utakulaje peke yako dada. Hata hivyo mlipokuwa mnafanya mapenzi sikuwepo, na sasa ni muda wangu. Kama unampenda sana. Kamwambie akae mbali na mimi.
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 142

Ila kwa ushauri kwako wifi yangu kipenzi. Ni bora wakati kama huu mimi nipo nyumbani, wewe kafurahi naye, maana akija kwangu hatorudi kwako. Likaka kama lile nakuachia vipi ufaidi peke yako eti wizouh.โ€

Alinitazama kwa hasira midomo ikitetemeka na nikamwambia โ€œnikupe pesa yako ya mafuta maana umetoka mbali, karibu ndani basi upate hata maji.โ€
Aliniambia โ€œsasa cheka utalia Ndeana, utalia sana.โ€
Nikacheka na simu yangu ikaita. Nikamuonesha anayepiga hapo nimesave โ€œMy sweet person. โ€œ
Nikapokea na kusema โ€œHello chautamu wangu.โ€
Akacheka akisema โ€œtotoo, niko tayari. Hapa nilivyo na hamu na wewe nikikukamata.โ€
Nikacheka nikisema โ€œhata mimi nipo tayari my love, lakini dada yako kipenzi Martha yupo hapa ananisumbua sana.โ€
Alibadilisha sauti na kusema โ€œhivi huyo malaya ananitafuta nini lakini, kwanini anakusumbua, nakuja hapo sasa hivi mke wangu, nakuja please usinune nakuomba sana.โ€
Nikadeka nikisema โ€œnaanzaje kununa dady wakati tunamtoko wetu leo. Nakusubiri.โ€
Aliniambia โ€œI love you my Sweet person, Nakupenda.โ€
Nami nikajibu โ€œNakupenda my sweet person, ninakusubiri kwa hamu.โ€
Stewart akashuka pumzi na kusema tena โ€œNakupenda.โ€
Kisha nikakata simu.

Martha alichanganyikiwa huku akisema โ€œmalaya mimi, malaya, mimi malaya kweli Stewart. Utaona, utaona Ndeana. โ€œ
Alikuwa anajikuna nywele zake na kuingia kwa gari. Mimi na dada tulitazama na kuanza kucheka huku dada akisema โ€œsaafi sana, umekua mdogo wangu safi.โ€
Nikacheka na kushikana mikono na dada yangu kuingia ndani huku dada yangu akiuliza โ€œalikuwa anasemaje?โ€

Nilimsimulia basi tulicheka sana huku dada akisema โ€œdada mnafiki yule, marafiki wengine wanafiki sana na nafutilia mbali namba yake simtaki tena. Mtu mzima hana akili kabisa. Roho ya kwanini mbaya sana.โ€

Ingawa uso wa dada yangu hauna ile nuru kama zamani unajua tena anayopitia ila najitahidi sana kumfanya afurahi na nashukuru Mr Fabian kaweka mambo sawa walau dada hata maumivu ya kusalitiwa yanapungua na hata ya kukosa mtoto walau ana watoto wa Mr fabian wanamchangamsha hivyohivyo maisha yanasonga
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 143

Baada ya kufika ndani nilionelea ni vyema nikaoge kwa maana My baby kaniambia anakuja na hivyo nimemvuruga na Martha basi najua atafika sio muda. Nilibadili nguo zangu na kutoka kwenda bafuni. Basi nikiwa bafuni yeye alifika nyumbani na alipokelewa na dada yangu. Mimi nilipofika sebuleni tu, tukagongana macho tukishangaana. Kisha nikasalimia, aliniitikia kwa kusubirisha sana. Ilinibidi nipite niwaache kwanza pale mimi nikavae haraka haraka.

Nimefika tu chumbani, nimekutana na meseji yake. Ameniandikia โ€œUnafanya nini sasa totoo, unataka niumbuke mbele ya dada huku unaniamsha na hiyo kanga yako. Ndeana hivi unajua wewe ni mzuri sana. Wewe ni mzuri aiseee!!, nimechanganyikiwa. Nakupenda sana, Nakupenda kama nikukamate huko chumbani kwako ila ndiyo siwezi sasa.โ€

Nikacheka na kusema โ€œNjoo, unamtania baba Vee wewe. Atakupiga ufe. Nakupenda baby wangu mzuri mzuri, navaa haraka tuondoke.โ€
Basi alikaa kimya nadhani alikuwa anaongea na dada yangu.

Mimi nikajindaa vizuri, nikapendeza. Nikabeba na ile pochi yangu mpya.Hakika nilipendeza sana. Hata mimi mwenyewe nilijua nimependeza sana.

Basi taratibu mtoto mzuri nikatoka. Waliponiona, Big Boss akasimama. Taratibu alinifuata tena karibu yangu na kusema โ€œumependeza sana. Umependeza.โ€
Dada pia alisema โ€œSanaa mdogo wangu, umependeza mno.โ€
Nilitabasamu nikisema โ€œinatosha basi mnanifanya najisikia vibaya sana.โ€

My boss akatabasamu, kisha akanikumbatia akisema โ€œNakupenda sana Ndeana, nakupenda sana. Nisamehe kwa yote yanayotokea. Sijui niseme nini kwasasa, Sijui nimfanye nini Martha. Kwasababu sitaki mtu yeyote akusumbue. Ila yote kwa yote nisamehe mimi.โ€

Dada yangu aliinuka na kusema โ€œShem, acheni kumpa shetani. Mnakaa mnamzungumzia mtu ambaye lengo lake ni kuwaharibia furaha yenu. Msimpe shetani nafasi. Ni kitu kibaya sana kwenye mahusiano kuongelea mambo ambayo yamepita na yanawaumiza. Zaidi nawatakia mapumziko mema. Shemeji yangu Happy birthaday.โ€

Stewart wangu alitabasamu tu na kisha alisema โ€œnashukuru sana shemeji yangu. Nafurahi sana kusikia maneno haya kutoka kwako. Asante sana.โ€
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 144

Yaani Nilikuwa nasikia raha sana, nilikuwa nasikia raha mno, nilisahau kabisa kama tuna dereva mule ndani. Hivi jamani, huwa mnapenda kukiss kama mimi na mnapata raha kama nnayopata mimi au mnakiss ili mradi tu.

Nilikuwa na utalivu nafurahia busu kama sipo duniani vile. Hakika nilifurahia sana. Barabara yote sisi tunaambiana kwa kunongโ€™ona โ€œI love you baby!!โ€
โ€œ I love you baby!!โ€
โ€œNakupenda.!!โ€
โ€œNakupenda.!!โ€
Huku vimidomo kama tunakula ndimu tu โ€œmwaaaah!!, mwaaaahh!!, mwaaah!!โ€
Mimi moyoni najisema โ€œmwanaume huyu sitosheki, sitosheki hata kidogo asiache kunibusu. Anikiss tu na hata sijui wapi tunaenda.

Nimekuja kushtuka gari imefika uwanja wa ndege. Ndiyo Dereva anasema โ€œTumefika.โ€
Nikamtazama Baby wangu. Hapo dereva alishuka tukabaki wawili.

Basi Boss wangu aliniambia โ€œnatamani nikukamatie nisikuachie. Yaani siwezi hata kutembea baby, una nini lakini, kwanini wewe mtamu hivi baby?, niambie unapakaga nini totoo, maana utakuja kuniua ujue.โ€

Nikatabasamu nikisema โ€œunachopakaga ndiyo na mimi napaka.โ€
Akacheka akisema โ€œIna maana na mimi ni mtamu kumbe.โ€
Nikacheka nikisema โ€œmapenzi matamu nikiwa na wewe.โ€

Akaniuliza akitabasamu โ€œwanaosemaga mapenzi mabaya kwani huwa wanafanya nini baby wangu. Mapenzi yamepatwa na sisi yaani tumeyapata.โ€

Nikacheka nikisema โ€œsasa baby, tunaenda wapi mbona sikuelewi.โ€
Akatabasamu na kusema โ€œumewahi kwenda Zanzibar baby?โ€
Nikatikisha kichwa changu kukataa tena huku natoa macho yangu.

Alitabasamu na kusema โ€œbasi ndiyo tunaenda hivyo, hotel kubwa sana ukaone wenzetu wanavyofanya. Nakuamini najua utatoka na kitu. Si ndiyo mpenzi?โ€
Nikamuuliza kwa kushangaa โ€œYaani mimi napanda ndege?โ€

Akatabasamu akisema โ€œacha kunichekesha ndiyo uongee na vitendo baby.โ€
Nikacheka nikisema โ€œSijawahi kupanda ndege hata siku moja. Naogopa sana unajua hili. Naogopa mwenzako.โ€
Akasema โ€œusijali, upo na mimi, upo na mimi kipenzi changu. Nataka ufurahi kama hutokuja kufurahi tena.โ€
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 145

Nikatabasamu ila ndiyo naogopa. Huo uwanja wa ndege wenyewe sijawahi fika. Basi nikapata ma muda wa kumpigia baba yangu na hatimaye tuliingia ndani sasa huku Stewart akisema โ€œyaani na ushamba wako nakuchukua video mpaka uchanganyikiwe.โ€

Mimi nikawa tu mnyonge tu maana naogopa mno nilikosa raha. Nikamuuliza tu โ€œsasa kwanini mimi sina nguo?โ€
Akasema โ€œwewe achana na mimi, twende nikakucheke.โ€

Nikacheka tu nikisema โ€œwewe haya tu.โ€
Basi akafanya utaratibu wote muhimu, kisha sasa tukaelekea kwenye ndege sasa. Tulipigana picha wenyewe. Kisha alinishika kwa kunikumbatia sisi hao tukaingia ndani ya ndege.

Sitaki hata kuelezea palivyo na raha yake. Ni pazuri sana. Mimi nikakalishwa sehemu yangu maana sijui hata wapi natakiwa kukaa. Akakaaa pembeni yangu, akanifunga mkanda. Basi muda wa ndege kuondoka ulipofika.

Mkiniona nilivyomshikiria, mngecheka. Nilimkumbatia kwa nguvu hata ilipokuwa sawa kabisa ndiyo nikafumbua macho yangu. Stewart sasa mkimuona anavyonicheka, anacheka hana mbavu, mimi nami nikaanza kucheka. Tulicheka ila mwisho wa siku yakaisha, atafanyaje sasa na mwanamke ndiyo mimi mtoto wa uswahilini.

Basi mwenzenu nilitamani safari isiishe ila sasa ni safari fupi sana. Tulifika mji mzuri sana. Pale pia tulichukuliwa na usafiri maalumu wa ile Hotel. Basi kufika kwenye ile Hotel. Ni nzuri sana, nilimtazama na kutabasamu nikisema โ€œbaby ni pazuri sana, ni pazuri sana hapa. Kwanini umenileta sehemu nzuri hivi.โ€

Akatabasamu akisema โ€œumefurahia?โ€
Nikasema โ€œbaby Hotel ni nzuri sana unajua, nzuri mno.โ€
Akatabasamu tena akisema โ€œI told you, tuingie ndani sasa.โ€

Nikawa nachekacheka tu. Basi sasa tukaingia ndani yaani pazuri. Mimi natabasamu tu. Tulipokelewa mpaka kupelekwa kwenye chumba chetu maalumu. Nyie!!!, nyie!!, jamani mnaonaga zile video mtandao wamepamba maua kuanzia mlangoni mpaka kitandani halafu taa fulani hivi. Ndiyo!!, hizo hizo najua umewahi kuona. Sasa mimi, mimi Ndeana baby wangu aliandalia chumba cha hivyo.
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 146

Nilijikuta naanza kulia, naanza kulia kwa furaha. Wale wahudumu walimuimbia tena Happy birthaday, nilijikuta namkumbatia nalia kwa furaha kwa vyote ambavyo amewahi kunifanyia.

Nililia huku na yeye tena akilia kwa uchungu akiniambia โ€œNdeana wangu Nakupenda. Asante kwa kubadilisha maisha yangu.โ€

Nilisema kwa hisia nikimtazama huku machozi yananitoka machozi ya furaha โ€œNakupenda Stewart. Nakupenda baby.โ€
Akanibusu tena kwa hisia akisema โ€œYou Know what totoo(unajua nini totoo?โ€

Nikasema kwa kulia huku nadeka โ€œsijui baby, sijui kwanini unanipenda hivi, kwanini?โ€

Akatabasamu huku akiwa na hali ya kulia akisema โ€œNdeana, I am not getting enough of you(sitosheki na wewe) Sikuchoki kabisa. Wewe ni mwanamke mzuri sana. Sijawahi kukutana na mtu mzuri kama wewe kwenye maisha yangu. Najua kuna mapungufu na mazuri. Nivumilie sana, usinichoke.โ€

Nikasema kwa kulia โ€œi will baby, mimi pia niambie utanivumilia?โ€
Alitabasamu akisema huku ameshikilia kiuno changu โ€œNdeana, nataka nikuambie kitu. Promise me utakubali?โ€
Nikajibu haraka โ€œunataka kuniambia kitu gani baby, Please tell me!!โ€

Akanitazama akisema โ€œNiambie utabaki na mimi hata baada ya kukuambia?โ€

Nikamtazama nikasema kwa upendo na kusema โ€œhakuna kitu cha kunitenga mimi na wewe, hakuna Stewart tell me.โ€

Akashusha pumzi yake ndefu sana, Akafumba macho yake na kusema kwa hisia sana huku machozi yakitaka kumtoka (Ndeana, nisamehe sana... Ndeana mimi.. โ€œ
Mimi nikamtazama nikisema โ€œTell me, tell me Stewart!!โ€
Akanibusu kwa hisia sana na kusema ......๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃnyie sijui hata nachekacheka nini๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹
NAAAAAAAAAM
Offer inaanza rasmi leo
Malizia SEASON FOUR na FIVE zote kwa offer ya sh 1000
Kumbuka mwisho wa story ni season five.
Na hapa facebook tutaishia season FOUR tu five itapatikana WhatsApp pekee
Kwa hiyo mdau, njoo umalizie leo vipande vyote vya season four na five kwa offer ya sh 1000
๐‘ต๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’๐’Š๐’‘๐’ ๐‘ฝ๐’๐’…๐’‚๐’„๐’๐’Ž ๐‘ด ๐’‘๐’†๐’”๐’‚ 0743433005 ๐’‹๐’Š๐’๐’‚ ๐‘จ๐‘ฎ๐‘ถ๐‘บ๐‘ป๐‘ฐ๐‘ต๐‘ถ
๐‘ผ๐’Œ๐’Š๐’๐’Š๐’‘๐’‚ ๐’๐’Š๐’„๐’‰๐’†๐’Œ๐’Š ๐‘พ๐’‰๐’‚๐’•๐’”๐‘จ๐’‘๐’‘ ๐’Œ๐’–๐’‘๐’Š๐’•๐’Š๐’‚ ๐’๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ +255743433005 ๐’๐’Š๐’Œ๐’–๐’‰๐’–๐’…๐’–๐’Ž๐’Š๐’†

KUMBUSHO, Hapa Facebook story hii itaishia season four pekee, season five italipiwa
LET'S GOOOO.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’‡๐’๐’–๐’“ ๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 141  >>> https://gonga94.com/semajambo/season-four-jamani-boss-mi-naona-aibu-141

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest