Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
27 Sep 2025
27 views
VYOTE NDANI GONGA94
Yanga SC na Singida Black Stars Waibuka Kidedea, Watinga Raundi ya Pili Michuano ya Afrika ⚽
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Wikiendi hii imekuwa ya furaha kwa wapenzi wa mpira baada ya vilabu viwili kutoka Tanzania kuonyesha ubabe wao kwenye michuano ya Afrika.
👉 Singida Black Stars wametinga raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mkondo wa kwanza, walihitimisha kazi kwa kuichapa Rayon 2-1 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mabao ya Stars yalifungwa na Diomande (43’) na Anthony Trabi (57’), huku Tambwe Gloire (37’) akiwafutia machozi wageni.
🔜 Singida sasa wanasubiri mshindi kati ya Al Akhdar (Libya) na Flambeau du Centre (Burundi) ambapo Warundi wanaongoza kwa 2-1 kabla ya marudiano kesho Septemba 28.
👉 Wakati huo huo, Yanga SC nao wametinga raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa kishindo, baada ya ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Williete SC ya Angola. Wanajangwani walishinda 3-0 ugenini kisha wakamaliza kazi nyumbani Benjamin Mkapa kwa ushindi wa 2-0 kupitia mabao ya Pacome (70’) na Andabwile (86’).
🔜 Safari ijayo Yanga itakutana na Silver Strikers ya Mali waliovuka kwa faida ya bao la ugenini baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Elgeco Plus kisha kutoka 0-0 nyumbani.
🔥 Tanzania bado tupo kwenye ramani ya soka la Afrika! Je, unaamini Yanga na Singida Black Stars watafika mbali msimu huu? 🟢⚫🟡
_* *AFANDE NILEGEZEE KAMBA 😊😫😫* Chapter 7 Siku hiyo ilikuwa ngumu sana, yani hata sijui nilikuwa nafanya nini. Nilisimama tu pale kwa dakika tano nikiwaza "Sasa hii black coffee
Inatengenezwaje? Na hili jiko linawashwaje? Nitamuambiaje huyu jamaa kichaa kuwa siwezi kutengeneza black coffee?" Nili...
Yanga SC na Singida Black Stars Waibuka Kidedea, Watinga Raundi ya Pili Michuano ya Afrika ⚽
Wikiendi hii imekuwa ya furaha kwa wapenzi wa mpira baada ya vilabu viwili kutoka Tanzania kuonyesha ubabe wao kwenye michuano ya Afrika.
👉 Singida Black Stars wametinga raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mkondo wa kwanza, walihitimisha kazi kwa kuichapa Rayon 2-1 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mabao ya Stars yalifungwa na Diomande (43’) na Anthony Trabi (57’), huku Tambwe Gloire (37’) akiwafutia machozi wageni.
🔜 Singida sasa wanasubiri mshindi kati ya Al Akhdar (Libya) na Flambeau du Centre...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/yanga-sc-na-singida-black-stars-waibuka-kidedea-watinga-raundi-ya-pili-michuano-ya-afrika
Maoni