_* *AFANDE NILEGEZEE KAMBA ππ«π«* Chapter 7 Siku hiyo ilikuwa ngumu sana, yani hata sijui nilikuwa nafanya nini. Nilisimama tu pale kwa dakika tano nikiwaza "Sasa hii black coffee
Nilihangaika kidogo lakini nikajipa ujasiri, Nikasema ngoja niende nimwulize mwenyewe. Nikapiga hatua kurudi hadi store nilipomwacha, sikumkuta. Kumbe hakutaka hata kusubiri alienda zake kazini akiwa amekasirika. Kama bahati iyo ndo ikawa pona pona yangu
Baada ya hapo nikaanza kusafisha nyumba. Ile nyumba ilikuwa kubwa balaa, nikafanya usafi kama masaa matatu hivi. Na si kwamba kwa sababu ilikuwa kubwa tu, ila ni kwakua mimi nilikuwa sijaizoea kufanya usafi. Ndio maana ikanichukua muda mrefu
Nilikuwa nafanya kidogo, napumzika, kisha naendelea. Baada ya kumaliza ndani, nikaenda laundry room (chumba cha kufua nguo). Huko Nikakuta mashine ya kufua, sabuni, na kapu la nguo chafu
Kuitumia mashine haikuwa ngumu kwa sababu kulikuwa na maelekezo pale. Nikaweka nguo, nikapima sabuni, nikafungua maji, halafu mashine ikaanza kufua.
Wakati mashine inaendelea kulua nikatoka nje kwenda kufagia Uwanja uliokuwa mchafu sana. Nikiwa nafagia fagia kama sitaki mlinzi akaja akaniambia, "Mambo?"
Nikajibu "Poa"
"We ndo house girl mpya?"
"Ndiyo"
"Vizuri Maana nataka nikuambie kitu kuhusu boss wangu. Huyu boss hakal na house girl kwa
muda mrefu. Ni mtu wa hasira sana. Ukivunja kanuni zake, anakufukuza fasta. Kwa hiyo jitahidi ufuate kila kitu anachosema na usimbishie. Mimi ndio maana nimekaa muda mrefu hapa kwa sababu namtii
Nikamuuliza "Umekaa muda gani hapa?" "Kama miaka minne
"Basi Asante kwa ushauri, nitafuata sheria zake, alafu Wewe huwa unakula wapi?"
"Mimi nakula nyumbani. Naishi blocks mbili tu kutoka hapa, Dada yangu huwa ananiletea chakula"
Nikagundua kumbe ndio maana hapakua na haja ya mimi kupika, maana hata mlinzi hakua anakula pale. Nikatabasamu kidogo kisha. nikaendelea kufagia, nilipomaliza nikaingia zangu ndani.
Apo Nilikuwa na njaa mbaya, chakula pekee. nilichokuwa nacho ni mihogo na maji. Nikala. huku machozi yakinitoka, nikikumbuka home.
Nyumbani nilikuwa nakula vitu vizuri sijui kuku, sausage, samaki, mayai, juice, hata ice cream. Lakini huku, duh! Hakuna zaidi ya mihogo.
Nikakumbuka simu yangu, nikaitoa na kuanza
kuangalia picha zangu za zamani.
"Nikimaliza huu mwezi wa mateso, nitarudi home niombe msamaha. Hata kama ni kuolewa, bora nikaolewe kuliko kuteseka Ivii" nilijipa moyo
Baada ya hapo nikaenda kuoga, nikabadilisha nguo, nguo nyingine nikatandika chini kama godoro, huyco nikalala,
Nililala kuanzia mchana hadi jioni. Elton aliporudi alikua ana haraka kama kuna mahali alitaka kwenda. Cha kwanza aliniita mpaka. chumbani kwake..
"Nenda niletee shati langu"
"Shati gani?"
"Lile liko laundry, nataka kulivaa leo usiku. Chap!
Nikasema, "Ooh sawa
Nikatoka mbio mpaka laundry room, sasa hapo ndo nikakumbuka kumbe sikutoa nguo kwenye mashine tangu asubuhi.
Na mbaya zaidi, nilichanganya nguo nyeupe na za rangi! Ambazo nguo za rangi zilichuja kwenye zile nguo nyeupe na kuacha madoa ikiwemo shati lake alilotaka kuvaa. My God.
Mwili ukaanza kunitetemeka, Nikasema sasa huyu jamaa ataninyonga nikiwa najiona.
Nikabaki nimesimama pale kijasho kikitoka. Sasa Elton alipoona nimechelewa kupeleka shati lake akaja mwenyewe. Akanikuta nimesimama tu kama mshumaa
"We ni tapeli? Shati langu liko wapi?
Nikajibu "A-a... bado halijaksuka
"Halijakauka? Unamaanisha nini?"
Akaangalia kwenye mashine, akaona sijatoa nguo. Akafungua mashine, akaanza kutoa nguo moja baada ya nyingine mpaka akaliona shati lake lilivyo pendeza
Alipoliona uso wake ulibadilika. Akaniangalia nusu ya kunimeza akasema "Hii ni nini sasa? Ulishindwaje kutenganisha nguo za rangi na nyeupe? We uko sawa kichwani?"
"Pole, sikujua kama nguo zinatakiwa kutenganishwa.
"Una akili kweli wewe? Umetoka dunia gani usijue kitu simple kiasi hiki?...... Bahati yako nimechelewa kwenye kikao changu. Nikirudi, utanilipa hii hasara. Na sitani"
Akaenda chumbani, akachukua shati lingine akavaa kisha akaondoka zake. Mimi nilibaki nikiwa na wasiwasi, Nilimwomba Mungu asije akanitesa vibaya, maana nilikuwa nimechoka.
kwakwell
Elton Alirudi saa tano usiku, Akaja moja kwa moja store nilipokua nimelala Akaniamsha "Amka!"
Nilitii nikaamka kisha akanitoa nje. Huko akachukua ndoo ya maji baridiiii akanimwagia yote mwilini. Kisha akasema, roll....roll.....chap..chapi "Aya
Mweeeh! Nikaanza kujiviringisha chini kwenye. vumbi kama nipo jeshini. Kila niki roll anaenda kuchota ndoo nyingine ya maji ananimwagial
Niliroll kama mara kumi na tano mpaka alipotosheka Akaniambia "hakuna kubadilisha nguo, lala ivyo ivyo hadi asubuhi. Na Ukichelewa kuamka kesho, adhabu nyingine inakusubiri" kisha Akaingia zake ndani.
Hamuwezi amini nililala nikiwa mbichi nimejaa matope mpaka kwenye pua. Nililia sana lakini haikusaidia kitu. Kweli Elton alijua kunikomesha.
Basi asubui saa kumi na moja kamili nikamka, nikaoga kwanza nikabadili na nguo ndipo nianze majukumu. Nashukuru Mungu niliseti alamu lasivyo ningepitiliza kuamka tena.
Nilifanya usafi tena na Safari hil sikupoteza muda, nilisafisha sehemu chafu tu, ambazo zinaonekana kiurahisi. Na kwakua hapakua na nguo chafu, Tatizo kubwa lililobaki kwenye black
coffee.
Basi sikujua inatengenezwa ajel Na pia kuwasha jiko nacho ni kipengele kingine. Ghafla Nikamkumbuka mlinzi getini. Nikaona nimfuate
nimuashe.
Alilalamika "Unataka nini asubuhi hivi?" "Naomba unisaidie kuwasha jiko"
"Nini??? Jiko??? Ina maana huwezi??"
"Ndio siwezi...please nisaidie kabla Boss hajaamka
Nikamuuliza tena "Unajua kutengeneza black coffee?"
"Sawa" Alifungua mlango akatoka nje ya chumba chake akiwa amejaa usingizi
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi