NAKUPENDA BILA MIPAKA 131 - 140 SEASON THREE
Nikawa natoa ile bahasha. Vile natoa, namuona Boss Yule anakuja. Ni wazi alisikia kengele au aliniona kwa juu. Nikasema kwa ndani “niondoke?”
Ataona Kama namkimbia, Nikajikaza pale kusubiri. Basi kweli alifika, akaita jina langu akisema “Nazwi, ni nini hii?”
Nilimtazama na kusema “Samahani Boss, nimeona siwezi kuendelea kufanya kazi hapa. Nimeandika barua ya kuacha kazi. Nitakuwa nasubiri majibu ili nifuate vitu vyangu.”
Alinitazama, akashika kiuno hivi halafu akaniuliza “Hivi unataka nichanganyikiwe ndiyo ufurahie.”
Eenh nikashangaa, Boss mbele ya Mlinzi, boda yupo hapa yeye anaongea hivi. Wallah nimejua mchanganya. Nikasema kwa upole “Boss Naomba niende Boda ananisubiri.”
Akanitazama, akachukua ile barua akachanachana mbele yetu. Halafu akamuuliza Boda “Unadai bei gani kaka?”
Baraka akajibu, akatoa elfu kumi na kumpatia, Mimi nashangaa, nasema “boss unajua hii barua nimeandika usiku, watu wamelala Mimi naandika barua halafu wewe unachana hata hujasoma kweli.”
Mimi nipo hapo nalalamika, nainama niokote vipande vyangu vya karatasi.Alinishika mkono akaanza kunivuta ndani. Sasa Mimi nipo hapo nalalamika “Boss Mimi naumwa, unaniumiza unajua, kwanini unafanya hivyo eenh.”
Kwani hata ananisikiliza, hanisikilizi hata kidogo aliendelea kunitembeza kuelekea ndani. Tumefika ndani namuona dada Maria Hana mbavu.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:132
Ni Kama imekuwa vituko, Boss haelewi Mimi sielewi. Sasa namwambia dada Maria “dada Maria Mwambie Boss wako Mimi nataka kuondoka. Boss Niachie Niachie.”
Nikawa sasa sitaki, nasema “unaniumiza, niwache unaniumiza Mimi naumwa.”
Jamani, hata sijui alikuwa ana nini, nikabebwa shwaaaa, sijui hata alinibebaje, Mimi moyoni naona raha huku najifanya nimekaza.
Bass huyu huyu Mr Serious kanibeba, huyu nilikuwa naogopa hata kumsogelea jamani, sasa anavyonukia jamani. Kumbe bora nimeleta utata bila utata ningebebwa Mimi. Nastahili pongezi, nastahili makofi matatu ya Hongera.
Ni raha kubebwa, ni raha kubebwa. Jitazame ndugu yangu, ukiwa unasumbuasumbua Muanko wako anaweza kukubeba, eneh anaweza kukunyakua au utabebwa kwenye maombi. Mwenzako nimebebwa. Alinipeleka mpaka ofisini. Akanikalisha halafu akawa ananitazama.
Nikainamisha kichwa changu chini, alivuta pumzi na kusema “Nazwi una tatizo gani, Nimeomba msamaha.”
Nilimtazama na kusema “Najua Umeomba msamaha na nimekusamehe. Lakini ni wazi sihitajiki hapa , nitafanya vipi kazi na unaniambia naweza kumuua mama. Mama ambaye Mimi siku zote nimempenda.”
Akanitazama na kusema “Mungu wangu!!, Mungu wangu!!. Nani kasema hakuhitaji, eenh Nani kasema hivyo, nakuhitaji sana Nazwi. Wewe ndiyo mtu muhimu namtaka humu ndani, Hakuna kitu nahitaji zaidi yako unanielewa.”
Eenh jamani, nahitajika mimi, mimi nahitajika hapa ndani.Huyu si ndiyo aliniuliza mimi Who I am, ndiyo namuonesha sasa mimi ni Nazwi Tena darasa kutoka kwa mama yake.
Nilimtazama na kusema “Mr Gallen, mimi nilikuwepo hapa kwasababu ya mama peke yake. Na sasa naona siwezi kufanya kazi Tena mahali hapa.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:133
Unazungumza hivyo kwasababu mama yako ananihitaji na sio wewe, sasa unafikiri tutaishi vipi humu ndani. Sitakuwa huru. Nitaogopa kufanya chochote kwa mama. Mimi naona mtafutie tu nesi mwingine.”
Alinitazama, sasa si mimi nilikuwa nimekaa, yeye amesimama. Huwezi kuamini Ila ndiyo nakuambia alinishika mikono na alichuchumaa mbele yangu kwa huruma na ile sauti yake kusema “upo sahihi, ni kwaajili ya mama yangu, lakini ni kwaajili yangu pia. Naomba, naomba usiache kazi, najua una hasira, najua unachukia kuniona najua niliongea maneno mabaya.
Natamani nirudishe muda nyuma nisiwe nimezungumza Yale maneno. Kwenye maisha yangu yote, sijawahi kujisikia vibaya Kama ambavyo nimejisikia kwako Baada ya hili, nimeumia sana, nimejilaumu nimejuta nakuomba usituache.
Mama yangu anakuhitaji, anakupenda sana, nakuhitaji pia hapa. Tangu ufike hapa nimekuwa na furaha sana na mama yangu, tafadhali.”
Hivi unajua kadri amechuchumaa ndiyo anapiga magoti kabisa. Hivi unajua ni mkubwa kwangu huyu. Mbona Tena magoti Kama anataka kunipa laana mtoto wa watu.
Amepiga magoti, natamani kupiga kelele, natamani watu wa humu ndani wanavyo muogopa wamuone. Raha jamani, hivi mimi ni wa kupigiwa magoti kweli?, huyo niliyemzalia Labda anipige mokofi sio kunipigia goti mimi eti ananibembeleza.
Nilimtazama na kusema “Boss usifanye hivi, nakuomba unavyofanya hivi unakuwa kama unanionea. Ndiyo maana nilindika ile barua usiku usiku hata hujajali umeichana yote. Tafadhali naomba muda juu ya hili. Nitafikiria hili na nitaweka mambo sawa Ila kwasasa naomba niondoke bado sijisikii vizuri.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:134
Aliinuka na kusema “naomba nisamehe, naomba nisamehe sana. Ila kiti unachotaka kufanya sikubali. Naomba nikupeleke nyumbani tafadhali na uniahidi unataka siku ngapi za kufikiria.”
Ukimuona sasa macho yake, amechoka maskini, ni kama halali. Jamaa anampenda mama yake, sasa na mimi naona hapahapa ndiyo nitamnyoosha maana sina namna.
Aliniambia kwa upole “unataka muda gani wa kunipa majibu Nazwi.”
Nilimtazama na kusema “wiki mbili.”
Alicheka akisema “unafanya utani si ndiyo Nazwi.”
Nilimtazama na kusema moyoni “angejua nafurahia kumrusha roho huyu mbona atakoma.”
Nikamjibu “basi wiki.”
Alinitazama na kusema “naomba chukua siku 2 tu, nakuomba siku mbili halafu Njoo kwa mama. Mama yangu atakufa akiwa anakuhitaji utajisikiaje ukisikia hivyo na ulikuwa na nafasi ya kuwa karibu na yeye.”
Hapa hata kufanya masihara Nilishindwa, alikuwa sahihi sana. Nilimtazama na kusema “usiseme hivyo sasa, basi nitafikiria tutaona.”
Alinitazama Akatabasamu na kusema kwa sauti ndogo “safari hii nimekamatika.”
Nikamuuliza kwa upole “Naweza kwenda sasa Mr Gallen.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:135
Aliniambia kwa upole “nakuomba sana, nisubiri tutoke wote.”
Nilimtazama tu, offer Kama hii ya kutoka na Mr Gallen naanzaje kukataa.
Basi nilianza kutoka, nilipofika mlangoni alinishika mkono na kusema “nakuomba, siku mbili tafadhali, hata moja Kama inawezekana.”
Sikujibu, badala yake nikafungua mlango, nafungua mlango nakutana na uso wa dokta umekasirika, macho yameiva balaa. Halafu mimi Nikatabasamu na kusalimia “Shikamoo Dokta, Kumbe ulikuwepo hapa?”
Alinitazama tu. Nilitabasamu Tena na kusema “mimi natoka, tutawasiliana.”
Alinitazama, halafu alitabasamu, tabasamu la chuki na hasira. Kimeumana.
Sasa yeye aliyemwambia asimame mlangoni kusikiliza ni Nani, na mimi ningejua yupo mlangoni ningefanya kusudi akome. Ila sio mbaya, eenh sio mbaya. Kamsikia mwenyewe mwanaume anayemtamani vile ananibembeleza.
Nilielekea jikoni, yeye huku aliingia kwa Mr Gallen. Dada Maria kuniona alisema “Wewe nesi, umefanya nini?, humu ndani hapakaliki ni nesi ni nesi. Leo ndiyo Mmenichekesha sana Kama watoto bado.
Sasa Subiri nikupe umbea. Shoga yako dokta alikuwa anasema watafute nesi mwingine. Kaka akasema haiwezekani mama anamuhitaji Nazwi na Nazwi ndiyo nesi wa mama kesi imeisha. Yeye akawa anasema “Nazwi hayupo makini si umeona?”
Kaka alimwambia “ni mama alitaka, na ile ingenikuta hata mimi. Badala unishauri nitafanyaje kuhusu mimi kumfokea vile bila kujali yote aliyoyafanya wewe unaleta mambo yako. Hivi unaona mama yangu, Ana Hali mbaya kule hospitali na midomo yake ni nesi wake unanielewa.”
Dokta alibaki kimya, aliondoka na kaka aliniita akaniuliza “unafikiri Nazwi atarudi Tena kazini?”
Nilimjibu sijui, niliona kabisa anajisikia maumivu. Namjua kaka yangu, sijawahi kumuona hivi hata Mara moja.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:136
Nazwi tofauti na mama hapa naona kuna kitu.”
Nilimtazama na kuuliza “Unaona nini?”
Akashusha pumzi na kusema “Naona kaka anakupenda sana.”
Nilimtazama na kusema “unachanganyikiwa, ni mkubwa Yule, achana na ukubwa mimi siendani naye hata kidogo.”
Akacheka akisema “umechanganyikiwa?, mkubwa amekuzaa yeye.
Mdogo wangu, Kama hisia zangu zipo sahihi, usichezee bahati, kaka yangu atakuoa. Kama nipo tofauti basi.”Halafu aliendelea kucheka akisema “Ila Leo, aanh Leo nimecheka.”
Nikacheka na kusema “eenh vipi Hali ya mama?”
Alinitazama na kusema “nikuombe kitu?”
Nilimtazama na Kisha alisema “najua kilichotokea umeumia sana. Lakini mimi ni shahidi. Nilielezea kilichotokea na bado hakuwa na haki ya kukutamkia Yale yote. Kaka anajutia sana. Lakini sahau mdogo wangu.
Mkumbuke mama, furaha yake, tabasamu lake na namna alikuwa anakufurahia. Nenda kamuone, sijui kivipi Ila anatamani kukuona. Kila nikienda lazima aulizie.”
Kabla sijajibu nilisikia skokonko nikajua tu kumekucha, alitoka dokta kanuna huyo. Dada Maria sasa eti Dokta “Upo sawa?”
Alinikata Hilo jicho, mimi sasa natamani kucheka vipi. Nilimtazama dada Maria na mwisho tuliangua kicheko halafu
nikasema “Shhhhhhh!!!, atasikia.”
Dada Maria kujizuia hawezi, Mara nilisikia harufu nzuri. Boss anatoka, nakuambia kavalia kaptura fulani hivi, fupifupi fulani, viraba fulani simple eenh, miwani fulani hivi. Halafu alisema “tunaweza kuondoka sasa.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:137
Nilimuaga dada Maria, alinitazama akisema “nitakupigia nesi.”
Nilitabasamu tu, sasa vile natoka, Boss aliniacha nitoke kwanza yeye alifuata. Dah, kuongozana naye tu ni raha.
Zoezi lenyewe lililonileta limegonga mwamba Baada ya barua kuchanwa ndiyo kwanza naenda zangu kupanda gari. Alinifungulia mlango wa gari na kisha alianza kuondoa gari. Tulifika mpaka barabarani Hakuna mtu anamsemesha mwenzake.
Tulifika mbali kiasi simu yake iliita, kuangalia alikuwa dokta Kabale. Nilimtazama, yeye alitazama tu simu halafu alisonya. Mimi Tena uvumilivu ulinishinda nikasema “Dokta Kabale anapiga pokea.”
Alinitazama tu hakusema kitu, simu iliita tena, nilimtazama tu. Na yeye alinitazama halafu alisema “Mungu nisaidie.”
Nikameza mate hapo nawashwa kuuliza maana naona nanyongwa koo langu.Nikajikaza na kuuliza “Dokta Kabale ni mwanamke wako?”
Alikohoa na akinitazama “Koh!!, koh!!, koh!!”
Nilijikuta nasema “samahani.”
Alitabasamu na kuniuliza “kwanini swali hili?”
Nilishusha pumzi na kusema “hanipendi, alinipa onyo nikae mbali na wewe, akiniona karibu na wewe ana kasirika.”
Akacheka akisema “Wewe zingatia nafasi yako. Achana naye, muache nitajua cha kufanya.”
Nilimtazama tu Kisha nilisema “samahani kwa swali nilitaka kujua tu.”
Alitabasamu na kusema “bila samahani. Niambie unajisikiaje, bado unaumia sana, unajisikia vibaya au unahitaji chochote?”
Nilitabasamu tu, na nilimwambia “nashukuru.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:138
Safari iliendelea, tukiwa tu kimya hapo mimi natamani Kama aniongeleshe tena Ila ndiyo haiwezekani. Amekaa zake tu kimya.
Nilifika mpaka nyumbani, nilimwambia “nashukuru sana, nimefika.”
Alinitazama na kusema “naomba sana fikiria juu ya nilichokuomba. Nisamehe.”
Nilitabasamu na kusema “ni sawa, nitafikiria.”
Akaniambia “nakwenda hospitali, mama yako atakuulizia niseme nini?”
Nilitabasamu na kusema “nimemkumbuka sana. Nimemkumbuka.”
Alitabasamu na kuniambia “nitakupigia Naomba upokee, nitatuma ujumbe Naomba nijibu. Nakuomba.”
Boss mbona ananishangaza mwenzenu, nazidi kuchanganyikiwa. Naona Kama navurugika kabisa nasahau hata Kama nilienda kuacha kazi.
Nilimtazama na kusema “Sawa.”
Nilishuka zangu, huku moyoni nasema “anacheza na akili yangu huyu hanijui vizuri, ni kichaa. Usiku nimeacha usingizi wangu nimeandika barua yeye kachana hivi anachanganyikiwa.”
Nikacheka mwenyewe Baada ya kukumbuka alipiga magoti, mimi huyu nimepigiwa magoti nyie ni maajabu halafu kuna raha fulani hivi inakuja naona Kama dunia yangu mimi hapa peke yangu.
Sikukuta mtu nje Ilinibidi niingie ndani, Nimeingia ndani nakuta mama analia, nakuta rafiki yangu analia. Nikawa nashangaa kuna nini tena. Nikauliza “Dorice, mama, mna shida gani mbona mnanishangaza?”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:139
Mama alivuta pumzi na kusema “nilikuwa najua rafiki yangu ana mambo mengi nikajivuta mbali naye. Lakini amenielezea Dorice kwa maumivu sana, I Nilijisikia vibaya sana, nikaona tusiishie hapo. Nilimwita ndugu yangu hapa tuzungumze.
Lakini mwanangu, ameishia kufoka, kumtukana Dorice akiongea maneno hata siamini. Nilipo jaribu kuzungumza naye hakunielewa kabisa ndiyo Kama nilizidisha.”
Dorice akawa analia akisema “nimechoka sana mimi Nazwi, nimechoka. Naumia sana roho inaniuma sana sijui hata nifanye nini.”
Nilimkumbatia rafiki yangu, nilimsihi sana asilie.Alikuwa analia sana, mimi namuelewa ni mama yake. Lazima aumie. Aliniambia kwa upole “Naomba nilale kidogo.”
Nikamlaza kitandani, mimi pia nilikuwa nimechoka nikaamua zangu tu kulala. Tuliamka jioni sana, kuamka nakuta missed calls za Mr Gallen Kama zote. Nikashangaa “kuna nini tena?”
Dorice akanitazama na kuuliza “kuna tatizo?”
Nilimtazama na kusema “shoo Leo haupo sawa Ila mambo ni mengi.”
Alinitazama na kusema “wewe una kichaa, ndiyo sipo sawa ndiyo uninyime habari.”
Nilicheka na kuanza sasa kuelezea kuanzia nafika getini. Basi nasimulia mwenyewe Dee anasema “eenh, Nipe, eenh ikawaje.”
Nilipofika kwa Kupiga magoti, Dee ana shangaa yupo weee usiniambie, mimi nikaendelea, kufika kwa Dokta sasa cheko, tulicheka tukisema “Leo analala roho juu juu safi sana, safiii wewe nikuambie kitu. Tajiri amekuelewa, nakuambiaje Dokta chali na sisi tunaibuka kidedea.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:140
Nilisema kwa upole “natamani iwe hivyo lakini najua haiwezekani nafurahia tu haya mambo mimi.”
Dorice alisema “lakini rafiki yangu mama yake hajakukosea ukipata muda tafadhali nenda kamuone, nakuomba sana, nakuomba.”
Nilivuta pumzi na kusema “Upo sahihi, hayupo sawa. Hata mimi nimemkumbuka sana.”
Nilitabasamu na kusema “ni mcheshi sana unajua, nimemkumbuka. Nitafanya hivyo.”
Basi Dorice alijawa na furaha na mimi nikampotezea tu Mr Gallen.
Nakumbuka Sana, tumekula, tumekaa hapo nje na kaka Baraka. Anatufundisha kusoma Biblia. Anatuelekeza, basi tunamtania anacheka huku mama akisema “muacheni mwanangu, nitawachapa.”
Sasa sisi tunacheka, kuna jambo mimi niliona Dorice na kaka wanavyo tazamana. Nikalimeza tu. Tukaingia chumbani tulipomaliza nikamtania Dorice nikisema “Dorice jamani, nimewaona na kaka Kwema?”
Akatabasamu akisema “ushaanza.”
Nilicheka nikisema “kaka yangu ndiyo kwanza ameokoka unataka kumuharibia uvulana wake.”
Tukacheka sana kwa sauti hata mama alisema “ushapona sasa, saa 6 hii kelele zote hizo nyie watoto lakini.”
Tulitazamana na kujizuia kucheka. Mara ujumbe ukaingia kwa simu yangu “Nipo nje kwenu.”
Nilimtazama Dorice nikisema “huyu amevurugwa eti yupo nje saa 6 hii.”
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni