NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO
:66
Mimi nilitoka nikiwa na furaha sana, Niliondoka hapa ni Kama nimezaliwa upya. Moyo wangu ulikuwa umechangamka mno. Ingawa nilifika kwa kujivuta sana lakini siku imeisha na tabasamu pana kwenye uso wangu.
Unajua sasa nilikuwa naona Kama dada Dee mpaka kumfikia umbea ninachelewa nikaona tu asinitanie bora nimpigie. Nimpigie nimwambie Dokta Kabale Leo limemshuka kanuna balaa. Basi nilimpigia dada Dorice. Dada Dorice alipokea, nilimwambia kwa furaha “dada Upo wapi?”
Akaniuliza “eenh binti hiyo furaha ni nini, ndiyo natoka kazini.”
Nikacheka na kusema “nakuambia kitu kuhusu muanko ndugu yangu.”
Akacheka na kusema “mimi tena na Muanko eenh mmeongea Leo si ndiyo?”
Nilicheka na kusema “unajua Leo nilitakiwa nisije kazini si unakumbuka ujumbe wa jana?”
Dada Dee akasema “eenh nilishasahau tena, imekuaje umeenda kazini leo?”
Nikacheka, basi nikaanza msimulia. Dorice akasema “maskini, huyu dokta wako atakuwa ana matatizo au ni mnene Kama mimi.”
Nikacheka na kusema “sasa Dee unene unahusikaje?”
Alicheka akasema “sisi muda mwingi tunawaza diet pekee si unaona anavyohangaika.”
Nikacheka nikisema “Ila dada Dee, Muache ana hangaika tu basi ungemuona ungecheka na huyo Muanko sasa alivyo hataki utani na mama yake Acha kabisa leo kimeumana.”
Dorice Nakumbuka aliniambia “sijui sana kuhusu ulimwengu wa roho na Mungu lakini nimewahi kusikia kitu nataka na wewe ujue.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:67
Nilishusha pumzi na kusema “kitu gani tena ushaanza hivyo.”
Aliniambia kwa upole “sikia mdogo wangu, huyo dokta sio mpumbavu Kama unavyohisi.
Acha kujiona wa kawaida, Acha kujiona huna zaidi yake. Mtu hawezi kuanzisha vita na wewe bila chanzo. Mwenzako tayari amekuona tokea ndani.
Pengine kiroho wewe ni mzuri zaidi yake kimuonekano, pengine kiroho wewe ni mshindani wake, kiroho wewe una kila kitu kushinda yeye na hujui hilo.
Usijichukulie poa kabisa, Mwambie Mungu aoneshe kile kilichopo ndani yako, simama kutetea, simama kupigania usiache upumbazwe.
Ndiyo ile mtu anakuja kwako anakuambia Naomba laki nitakurudishia. Wewe unacheka na kushangaa mtu huyu amenionaje mimi, natoa wapi laki?.
Kumbe ulimwengu wa roho wewe unaonekana una pesa, una zaidi ya hiyo pesa watu wanakuona hivyo. Usijishushe Mwambie Mungu hizo pesa wanazoona Naomba zinifuate kupitia hiki nafanya.
Unanielewa Nazwi?, Dokta anakuona tofauti na unavyojiona sasa muoneshe tu kwamba unajua hicho anachokiona na upo Kama anavyotaka. Muheshimu lakini acha kumuhofia yeye sio muajiri wako.Usikute mwenzako kashaona huko kiroho wewe ndiyo Mrs muanko basi kila anachofanya anataka kuzuia.”
Nilishusha pumzi na kusema “inawezekanaje sasa, dada Huyo muanko mwenyewe hajawahi hata kuonesha kuvutiwa na mimi.”
Alicheka na kusema “wewe unataka tu leoleo hakuoneshe. Tulia binti, tulia wewe endelea na kazi mengine achana nayo. Hata hivyo sio lazima akupende yeye utapata hata mwingine. Kwani Ina maana wewe una hisia na Muanko?”
Haraka haraka Nikajibu “akuuu, akuuu ujana wale ale na Nani na ukubwa wake aje kunichosha mimi.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:68
Tukacheka huku Dorice akisema “hilooo huna lolote kila ukimzungumzia unatabasamu, sura yako inabadilika.”
Nilitabasamu na kusema “nilisahau, mama yangu ameninunulia Biblia.”
Dorice sasa anavyoitikia “weee usiniambie, mbona Kama.”
Nilicheka nikisema “mbona kamaaaa!!”
Basi ilikuwa ni furaha kubwa sana, niliongea muda mrefu sana na dada Dorice hata sijui barabarani nilifika vipi mpaka nikapanda gari ni kucheka tu.
Lakini Baada ya kufika mahali nilishuka na Baada ya hapo niliingia sokoni. Eenh binti mama amenipa maneno huko inabidi sasa nikae kisichana, nijipambe hata sina utajiri Ila nihakikishe nakuwa smart sana. Nikanunua baadhi ya vitu vidogo vidogo vya hapa na pale na Kisha kuanza safari ya nyumbani.
Taratibu nilianza kurudi nyumbani, tofauti na siku zingine. Leo nimechoka lakini Nina furaha sana. Nina furaha kuliko kawaida. Nilifika nyumbani, siku hii hata binti yangu hakuwa amelala. Alinipokea kwa furaha akiita “mama!!, mama!!, maaaamaaa!!”
Nilikuwa nasikia raha sana huku sauti ya Yule mama nilisikia kwenye ngoma za masikio yangu “kuna vitu unapata kwasababu ya mtoto wako, mengine yanakuepuka kwasababu yake, mtoto ni zawadi yako, furahia.”
Nilijikuta nambeba kwa furaha nikisema “Priya wangu huyo, eenh mtoto wangu mzuri unajisikiaje.”
Mwenyewe sasa anasema “mama nataka pipi.”
Nilitabasamu, najua anapenda pipi hivyo nikampatia.
Mama alinitazama na kusema “eenh mwenzetu leo una furaha sana.”
Nilitabasamu na kusema “hamna mama jamani kawaida tu eenh niambie mbona Kama Umependeza na mjukuu wako kulikoni?”
Mama yangu alitabasamu na kusema “ni kweli, tulipeleka maandazi si nilikwambia eenh, tumerudi hapa sio muda.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:69
Nilishusha pumzi na kusema “kuna chakula kweli?”
Mama akanitazama na kusema “nilivyochoka leo binti yangu Mungu ndiyo anajua. Nimenunua dagaa hapo na nyanya za kachumbari. Maji ya ugali nishatenga kuna na Yale maharage ya jana. Wewe nenda kabadili uje ukate kachumbari Kisha tuendelee na mambo mengine.”
Nilishusha tu pumzi nitafanya nini, nimechoka na mama yangu amechoka tena pengine zaidi maana ana Baki na mtoto mimi nikienda kutafuta huko.
Niliingia ndani, nikavua nguo na kuchukua tu kanga na kishati changu hapo. Ule mfuko wa Biblia nikaweka kitandani. Nikatoka nje na kuanza kusaidiana na mama kazi za hapa na pale.
Tulimaliza, tukaandaa vile tumemaliza na kaka yangu alifika. Nilimtazama alinitazama akitabasamu. Halafu alisema “mama nimerudi na mboga hapa.”
Mama alinitazama na Kisha alipokea, ilikuwa ni nyama. Mama alinitazama na Kisha akamtazama mwanaye na kusema “Mungu akubariki sana baba. Asante sana. Ulipotoa leo kwaajili ya nyumbani aongeze Mara elfu. Nimefurahi sana mwanangu.”
Nilitabasamu, niliona tabasamu la kaka yangu na Kisha alinishika kichwani akisema “dada yangu huyo, eenh vipi hesababu yangu ipo nikae?”
Mama alisema “kaa mwanangu.”
Nilikuwa namtazama siamini Kama ni kaka yangu maana akili zake Mungu wangu, ni Mungu tu anajua. Basi nakuambia alikuwa amekaa hapo na anaongea ongea na Priya wao huelewana sana.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:70
Akanawa mikono na Kisha tulianza kula pamoja. Kiukweli tulifurahia maisha yetu sana, tulikuwa tunakula huku tunacheka, tulipomaliza akambeba anko wake akisema “tunaenda dukani Mara moja.”
Mama alisema “mwanangu usiku sasa usichelewe na mtoto.”
Kaka Baraka alisema “usijali mama.”
Mama alinitazama, alitokwa na machozi ya furaha na alinitazama tena Kisha ule mfuko akisema “ameleta nyama tena ni kilo hii.Mwanangu Nazwi, Mungu yupo.
Maskini kijana wangu mzuri anataka kuharibika tu. Eenh Mungu wangu usiniache, endelea kumbadilisha, endelea kumfanya wako, endelea kumtengeneza Mungu wangu.”
Nilitabasamu na kusema “mama, usiseme hivyo. Miaka yote hiyo Mungu ameshakusikia na niamini mimi, Mungu atafanya zaidi.”
Mama alisema “hujui tu mwanangu. Nimefurahi sana. ‘Leo hii mwanangu amegusa moyo wangu. Embu inuka tengeneza hii mboga.”
Nilitabasamu.
Mama alikuwa na furaha sana. Tazama moyo wa mama ulivyo, mama ni mtu ambaye yaani kitu kidogo tu kizuri ana furahia na anakupa baraka zote. Najua unasema una kidogo, kazi yako sio kubwa.
Kwenye hiko kidogo unaweza kufanya kitu, nunua hata unga, nunua hata nyama, nunua hata viungo vya jikoni rudi navyo nyumbani uone namna mama atakavyo furahia.
Kuwa na uhusiano mzuri wa mama na mtoto peke yake haitoshi.Unataka Nani ampe zawadi tena usikute baba hayupo tena au yupo lakini na yeye kwasasa anakutazama wewe. Upendo kwa vitendo ndiyo kitu kizuri sana.Hivyo siku hii ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye anga la nyumba yetu. Mbingu imetuchekea, tuna furaha.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:71
Basi walirudi, nikamchukua mtoto na kumuogesha, na mimi pia nilifanya hivyo maana natakiwa nipumzike kesho niwahi zangu kazini. Mwanangu alilala, mimi nikaweka alarm na mambo mengine sawa. Kisha nilipanda kitandani na kuchukua ile Biblia.
Kusema kweli sio Kama sijui kuna Biblia najua sana Ila mimi Kama mimi sijawahi kumiliki Biblia, sijawahi hata kufunua Biblia Kwahiyo kwa Mara ya kwanza kwangu hapa naona Kama mimi huyu hapa halafu Mungu huyu hapa.
Nilifumba macho na kuvuta picha ni Kama nazungumza na Mungu nikisema “Asante Mungu nimekutana na wewe.”
Nilishusha tena pumzi na kusema “sijui hata nianze wapi, nifanye nini maana sielewi.”
Nikafunua mwanzo kabisa wa Biblia, na nilikutana na mwanzo. Nilianza kusoma sasa mimi nasoma Kama nasoma simulizi vile, ile mwanzo 1 mimi nilisoma haraka haraka naona hata sielewi nikawa nafunuafunua nikisema “hata sielewi sasa ni nini hiki mbona nitachanganyikiwa.”
Nikiwa najiongelesha nilisikia hodi, nikajua huyo lazima ni kaka. Nikajiweka sawa na kuruhusu aingie, alikuwa ni kaka yangu kweli. Baada ya kufika Nilitabasamu, alitabasamu nami nikamwambia “kaa kaka yangu.”
Alikaa, Nilitabasamu na kusema “kaka leo umefanya kitu kikubwa sana.”
Alinitazama na kusema “dada nimetafakari sana maneno yako, nimetafakari hata nikakosa raha. Na wakati ule sasa nimetoka kuna mzee huwa anapita pale kijiweni anaongea Kama wewe tu.
Nikaona ni Mungu ananipa ujumbe tu. Niliamua nikatafute kazi dada. Sijapata kazi ya maana lakini hivyohivyo, nipo hapa kusema Asante dada na nimeanza kubadilika uniombee tu.”
Nilimtazama na kusema “kaka niambie hutanii.”
Akatabasamu akisema “utaona kesho natoa hizi nywele huku kichwani.Nikipata tu pesa ya kununua suruali mbili tatu nachoma hizi nguo za ajabu ajabu. Nataka kuwa baba wa familia sasa.”
Nilijikuta namkumbatia kwa furaha nikisema “Asante Mungu, Asante Mungu.”
Alitabasamu na kusema “hii ni Biblia?”
Nilitabasamu Kisha alisema “Naomba nikasome.”
Nilishangaa na kusema “kaka Baraka, na Biblia wapi na wapi.”
Alitabasamu na kusema “dada Acha maneno Naomba nikasome.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:72
Nilitabasamu tu na kusema “mimi hii nimepewa zawadi lakini naona sielewi. Kaka Naomba usome na urudishe Kama ilivyo sitaki tugombane.”
Alinitazama na kusema “nakuahidi, lakini Naomba ukipata nyingine niletee.”
Hivi unajua nashangaa, nilikuwa nashangaa hata nashindwa jizuia. Kaka yangu alitoka. Niliona siwezi kulala bila kumpa mama hizi habari njema.
Nikaenda kwa mama na kumuelezea, mama alilia, alifurahi akisema “Asante Mungu kwaajili ya vijana wangu. Wakumbuke Mungu wakumbuke.”
Basi ilikuwa ni furaha sana. Nilifurahi na mama yangu na mwisho nikarudi kulala.
Asubuhi na mapema niliamka, nilisaidiana na mama kuweka mambo sawa halafu nikajiandaa. Muda wa kutoka nikachukua tena maandazi hata mama akaniuliza “ulisema unakula hapo vipi imekuaje?”
Nilimtazama na kusema “mgonjwa wangu anayapenda sana mama.”
Mama alitabasamu tu na Kisha Nilicheka na kuanza kuondoka.
Siku hii nilipofika kituo cha huko nnapoenda nilikutana na Baraka Boda. Unajua tena walivyo hawa bodaboda basi alinichangamkia sana. Nikawa natabasamu akawa ananiuliza “vipi nikupeleke.”
Mimi nasema “natembea tu usijali.”
Yeye anasema “acha zako nitoe hata buku nikupeleke.”
Mimi nacheka tu, alikuwa sahihi lakini kamuda kalikuwa kameniacha kiasi fulani. Hivyo nilikubali, alinipeleka lakini siku hii hakuwa na mazungumzo sana hata nilikuwa nawaza au ana shida.
Lakini sikuwa na uwezo wa kumuuliza niliamua tu kupotezea. Alinishusha nikampa hela yake mimi nikaingia ndani.
Nilipofika sikuona mtu pale ndani, nikaingia zangu tu kwa chumba changu. Nilipokuwa nabadili nguo. Dada Maria alikuja, tulisalimiana na Kisha aliniambia “nguo zako zinakupendeza sana. Uzuri wewe ni msafi.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:73
Nilitabasamu, halafu nikasema “Asante umenianulia nilisahau kabisa jana.”
Alitabasamu na kusema “nilitaka ninyooshe nikaona siwezi.”
Nikacheka nikisema “usijali nimeshapasi mwenyewe niambie.”
Alinitazama na kusema “Boss anakuita ofisini kwake.”
Nilimtazama na kusema kwa kuuliza “dokta amefika?”
Alinitazama na kujibu “hapana, bado.”
Nilishusha pumzi na kusema “sawa, Asante dada Maria.”
Alitabasamu tu na kutoka zake. Nilibaki mwenyewe najiuliza naenda kuambiwa nini tena, dokta sijui atakuwa amenisilibia nini Tena kwa boss.Basi nikajiweka sawa, na baada ya hapo sasa nilitoka.
Sikufanya kitu chochote zaidi ya kuelekea ofisini kwa Mr Gallen. Nilipofika nilibisha hodi na nikasikia akinijibu “Ingia tafadhali:”
Niliingia, Tena kwa upole na heshima. Unajua tajiri mwenyewe alivyo kauzu. Nilisimama nikasalimia kwa heshima “shikamoo Mr Gallen.”
Bila hata kunitazama alijibu “marahaba, keti tafadhali.”
Kwa upole nilifuata kitu kilipo nikaketi. Baada ya kukaa, aliinua kichwa chake, sasa nirudie Tena kusema kwani, mwanaume huyu ana mvuto mimi akinitazama si ndiyo naishiwa nguvu kabisa. Nilikuwa natabasamu tu Kama kawaida yangu.
Alinitazama na aliniuliza swali ambalo sikutegemea “mtoto anaendeleaje?”
Nilimtazama, mimi sijawahi kuzungumza naye kuhusu mtoto, itakuwa mama huyu. Sikutaka mambo mengi Ilinibidi tu niseme “anaendelea vizuri namshukuru Mungu.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:74
Alinitazama akaniuliza Tena swali la kunishtua “vipi na leo umeleta Tena maandazi.”
Nilitabasamu na kujibu “nimeleta mama anayapenda.”
Alitabasamu na kuinama akawa ana bonyeza kitu kwa pc yake na kusema “sio mama tu hata mimi nimependa.”
Nilijikuta natamani kucheka kwa furaha Ila ndiyo najizuia sasa. Vile Yule mtu unatamani kuongea naye halafu ndiyo unaongea naye Tena vitu vya kuchekesha.
Nilitabasamu na kusema “basi nitaongeza idadi.”
Akacheka na kusema “nilitaka kujua mtoto anaendeleaje. Nimefurahi kusikia yupo sawa. Siku nyingine sema ili usimuache ukaja kazini. Hii sio adhabu.”
Nilikuwa nashangaa, huku ndani yangu najiuliza boss kacheka au nimesikia vibaya mimi jamani, pengine naota.
Nikamtazama, akaniuliza Tena “umesema umeleta siyo?”
Nilitabasamu na kusema “inaonekana unazungumza mengi kuhusu mimi.”
Alinitazama, akatabasamu akaniambia “mama yangu anakupenda sana, nafurahi kuona mnaelewana. Anapenda kukuzungumzia vizuri. Naona anatamani hata uwe unalala hapa.”
Nikacheka kidogo, akasema “unaweza kwenda sasa.”
Niliinuka na kusema “Asante sana.”
Vile ndiyo nataka kutoka akaniita jina langu vizuri, si nilisema vile anaongea vizuri, na sauti yake nzuri eenh, basi hapo nikaitwa “Nazwi!!!”
Nilisimama, akaniambia “Siku ya kwanza nilisema marashi yako si mazuri, sikusema usitumie tena.”
niliinamisha kichwa, akavuta mfuko na kunipatia akisema “tumia hii sasa, ikiisha usiogope niambie nitanunua tena.”
Haraka nilipokea, nikachungulia. zilikuwa ni boksi mbili za pafyumu, nilitabasamu nikisema “nashukuru sana Boss. Ubarikiwe sana. lakini sikatwi mshahara wangu siyo?”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:75
Alicheka kidogo na kusema “hii ni asante kwa kumtunza mama yangu vizuri.”
Sasa vile anaongea, mimi hoi, sikutaka hata kusubiri. Tajiri kanipa zawadi mimi ni nani nikatae, natamani hata ungeniona. Unajua vile mtu namuona wa muhimu sana kwangu, kaniongelesha, kacheka na mimi na bado kanipa pafyumu.
unafikiri jambo dogo hili. Nilipata furaha ya ajabu sana, nimetoka pale ninafuraha kutoka ndani ya moyo wangu.
Vile natoka tu, nikakutana na dokta, furaha yangu yote ikakata. Maana nilikuwa na furaha yeye aliponiona tu furaha yake ilikata na alianza kunitazama kwa jicho la chuki na hasira niliona hilo. Lakini safari hii nilijikaza, nikakumbuka maneno ya rafiki yangu Dorice, nisimuhofie, niwe Imara na nimuoneshe kuwa nafahamu kuwa ananihofia.
Nilimsalimia Kama kawaida yangu, hakuitikia. Unajua ni mzuri, ni mzuri sana. Sasa sijui ana wasiwasi gani. Alinitazama kuanzia juu, akanishusha. Akavua miwani yake, akaivaa tena halafu akashusha pumzi mimi hapo nasema moyoni “Dokta wee, mwisho ufe presha bure mimi mwenzako nipo sina hata cha kukufanya maskini ya Mungu.”
Nikamuuliza “vipi Dokta, upo sawa?, kuna tatizo?”
Nilimuuliza tu makusudi, aliniambia kwa sauti yenye ukali fulani hivi “nifuate.”
Nilitabasamu tu wakati ameanza kutoka. Mimi hata sikujali, nilipita kwa chumba changu nikaweka mfuko wangu na Kisha nilimfuata.
Alienda kwa bustani ya hii nyumba, ni bustani nzuri sana. Alisimama, akanitazama na aliniuliza “ulikuwa unazungumza nini na Mr Gallen?”
Nilimtazama Nikatabasamu na kumuuliza “natakiwa kuomba ruhusa pia?” Alinitazama, Kisha aliniambia kwa dharau “sikiliza Nazwi.Upo hapa kufanya kazi ya kumuuguza mama. Na mimi ni kiongozi wako. Unatakiwa kuwa na heshima na Mipaka.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:76
Kitu kimoja nakuomba, kaa mbali na Mr Gallen, kaa naye mbali na hutakiwi kuzoeana naye kwa namna yeyote ile hivyo kwa Mara nyingine nakuuliza, mlikuwa mnaongea nini?”
Nilitamani kucheka vile anachanganyikiwa, nilikuwa na uwezo wa kumwambia tu kuhusu mama yake. Lakini siku hii nilitaka kumkera pia. Nikatabasamu na kumuuliza “Dokta samahani kwanini Jana haukufika?”
Alinitazama na kusema “hayakuhusu Nazwi, jibu kile nilichokuuliza.”
Nilitabasamu, na kusema “Natamani nijibu Kama ulivyo jibu. Lakini wewe ni Boss wangu nakuheshimu sana ni vile tu wewe hauheshimu wengine. Dokta samahani, mimi sio ninaye paswa kukaa mbali na Mr Gallen.
Nenda kwa Mr Gallen, Mwambie Akae mbali na mimi kwasababu mimi nipo hapa kwaajili ya kazi tu. Halafu Dokta nikuulize kwanini unanihofia?, niambie.”
Dokta alichukia, mimi nikawa natabasamu, alikuwa anataka kuinua mkono wake. Nikaona hapa anaweza anipige kibao nikashindwa mjibu hapo naogopa Ila nikajipa moyo na kusema huku natabasamu “Dokta usijaribu, nipo hapa kwaajili ya kazi, naomba nikamuhudumie mama sasa.”
Nilianza kuondoka nikitabasamu huko nyuma sasa, ndugu amevimba anataka kupasuka, ukimuona sasa, ukiona alivyosimama, Mungu wangu Dokta atapasuka kwa hasira.
Lakini kwani najali sasa, natembea natabasamu nimemnyoosha kidogo atakuwa ananiogopa. Nafika Tu mlango wa kuingia ndani, Mr Gallen huyu hapa, alikuwa na uso wa kukasirika, nikawa tu mimi nataka kupita, akanishika mkono na kunisimamisha. Nilimtazama Kama hakuna shida, alinitazama na kuniuliza “
😋😋🙌🙌
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni