IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA*
SONGA NAYO.....
Kimya kifupi kilipita hii ni baada ya mimi kusikia kuwa Zuri ni mke wa mtu nilikuwa naumia sana sio siri jamani ila sema nilijikaza mbele ya mama asigundue
"Unamaanisha kwamba Zuri kaolewa au..??"
Nilirudia kumuuliza mama kwa mara ya pili ili nijihakikishie, mama alinitazama kwa muda kisha akazungumza
"Ndio ni mke wa mtu yule, na ni mama wa mtoto mmoja.."
Eeeh ila wanawake acheni kabisa wanawake saluti zenu walahi, maana unakuta msichana ameng'aa harafu mzuri balaa ukimtazama unajua tu huyu bado hajaolewa
Ila sasa kumbe wameolewa na tena ni mama watoto, jamani jamani mie sikuwa najua kama Zuri ana mtoto lakini pia kaolewa hii ni kwamba zuri ni mzuri mno
Na pia Zuri ako na mwili soft yani ngozi yake inag'aa muda ote na anaonekana bado mdogo mno, sasa ndio maana sikuweza kulijua hilo sasa hapa mama kaniambia na kijana wenu ndio moyo wangu upo pale
So saivi sina hamu kabisa, yani nahisi joto na baridi vikinisumbua kwa wakati mmoja, nikabaki namtazama mama yangu jamani ili walau anionee huruma mtoto wake amshauri Zuri aachane na mumewe na kuja kwangu
Eeh mie nae nimezidi, basi bwana taratibu nikataka kuondoka zangu mama akanizuia kwa kunishika mkono
'Frank nafahamu kwamba unampenda Zuri, ila kijana wangu nikwambie tu zuri ni mke wa mtu na mumewe sio mtu mzuri kabisa, hapo unavyomuona Zuri usomuone anacheka yule
Ila anamaumivu makubwa mno kwa sababu familia ya mumewe wanamnyanyasa sana, huwezi amini Frank hata mshahara wake wote wanachukua wao
So mimi kama mzazi ambaye ninajua uchungu na maumivu ya mwana nikaamua kumchukua Zuri ili aishi hapa kama dada wa kazi lakini pia namfanya kama binti yangu ila kwa muda huu anaishi hapa kama familia tu maana kule ukweni kakwe alikuwa anateseka sana.."
Mama alikuwa anazungumza lakini hata sikuwa namuelewa kabisa, so nikaondoka zangu na kuelekea chumbani kwangu, kichwa kilikuwa kizito hata kuona mbele aikuwa naona kabisa
Siki hiyo ikapita na siku nyingine ikashika nafasi, siku hii bwana niliamka nikiwa na kachuli flan hivi kwa Zuri kisa tu nimesikia kuwa ameolewa lakini pia anamtoto
Wivu sio mzuri kabisa, maana baada ya mimi kufika sebleni nikamkuta Zuri akiwa amekaa anacheki movie yake pendwa, maana ilikuwa tayari saa tano, kutokana na mimi kutokuwa sawa nilichelewa kuamka
"Zima hiyo TV, harafu kuna nguo zangu kule chumbani kwangu nahitaji uzifue.."
Nilimwambia kwa ukali lakini pia na wivu juu, Zuri akabaki ananitazama tu kama sinema ya fimu ya yesu, huku akitaka kulia kabisa
"Unanitazama nini?? Kafue nguo bwana.."
'Sio zamu yangu, ni zamu ya Anita.."
"Hayo mimi sijui, ila ninachotaka nguo zangu ziwe safi basi.."
Nilizungumza kisha nikaa kwenye sofa, Zuri akanyanyuka akiwa mnyonge nikamuita tena akageuka na kunitazama
"Kwahiyo unaondoka, umeniona nimekula au..??"
"Lakin..."
"Nataka chai mimi..."
Eeh mie nae nimezidi bwana khaa hata kama ni wivu ila sio kwa style hii walah
Basi zuri wala hakunijibu nikaona anaondoka tu
nikabaki na hasira kwa sababu nilifikiria. ataninyenyekea ila wapi baada ya muda kidogo akawa ameleta chai na kuniwekea juu ya meza na muda huo huo Ethan na kaka Idress wakawa wamefika pale
Zuri alikuwa ni mtu mtaratibu mno lakini pia mpole ambaye hapendi kuongea sana, basi baada ya Ethan na Idress kufika pale wakawa wamekaa na kubaki wakituangalia tu mtu mbili
sie
"Zuri mbona leo huna raha..??"
Ethan akaanza sasa maswali yake yale, nikamkata jicho ila wapi huyu kijana sijui kichwani mwake anafunza kweli au vipi
"Aah niko sawa tu.."
Alijibu zuri huku akitaka kuondoka lakini nikamzuia
'Mbona chai haina sukari...??"
Nilimuuliza kwa ukali, mpaka Ethan na Idress wakabaki wananishangaa maana sio kawaida yangu kuongea na Zuri namna ile......
Itaendelea..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni