JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 11
Mwandishi:lissa mwalla
Sikumsukuma wala,na sikujiskia ile vibaya wala,nikasema tu jmn Keanu si uniachie watu watatuona,akaniangalia akasema okay kweli watu watatuona,akasema nakutakia usikumwema,nikacheka aniaksema sawa asante nawe pia.akasemaingia ndani mm ndio nitaondoka,nikasema sawa,nilingia ndani yeye akiwa amesimama palepale,nilivoingia nikachungulia haraka dirishani,mana ukiwa dirishan unaweza kuona mtu wa mlangoni.nilimuona anageuka aondoke huku anatabasam.mmh huyu anatabasam nn sasa?mara msg ikaingia kwenye simu yangu,imetoka kwake amesema βleo imekua siku nzuri sana ,nimeenjoy sana kampan yako na pia nimeondoka nikiwa salama nashkuru sanaβnikacheka nikajibu βsiku nzur kweli hata mm nimeenjoy sna,ila kwa nn umesema umeondoka ukiwa salama?β akatuma viimoj vya kucheka kisha akajibu βnilivokukumbatia nikajua kabisa leo nitaishia mochwari mana ungenisukuma ningeangukia ngazi huko baaassss kwisha habari yangu?nilicheka sanaaaa nikajibu βhakuna bana ilikua amani tu,siku hizi mm sio wa kiivo" akasema "mmh kweli eeeh?umekuaje siku hizi?"nikacheka nikajibu "watu wanabarikiwa kwa sasa nipo kwenye point naskia aman na maisha yangu sana na natamani sana kuishi" akajibu "naweza kupigia?" Nikasema nipigie haina shida,alipiga simu nikapokea muda huo nilikua peke angu tu,keanu akasema tayla nimefurahi sana kuskia hivo kuhusu ww,naamin sasa nitakua rafiki ako wa karibu kama utaruhusu.nikasema naweza ruhusu.akasema asante sana,unaweza nipa ratiba yao ya kesho'?nikasema kesho nitaenda kanisani kisha mida ya mchana nitakua huru,akasema kanisa gani unasali?nikasema roma,akasema mm niko anglican nutafutahi sikumuishiriki nasi kwenye ibada,nikasema siku utafika tu,akasema naomba jioni unisindikize mahali nikatizame mpira kama hutojali,nikasema sawa haina shida.akasema asante snaa.basi tulipiga piga stor tulaagana mm nikapanda kitandani nikalala zangu.kulikucha bella kama kawaida yake yy alifika mbeya akapata na mwanaume wa mbeya hivo alienda kulala kwake mida ya kwenda kanisani akarudi tulajiandaa pamoja tukaenda kusali wala sikumuambia kitu.baada ya kusali tulirudi tukapika mana dokta alietuachia nyumba alikua amehamishwa japo hakuahamisha vitu alipelekwa mkoa mwingine hivo tulikua wenyewe kwa wakati huo.baada ya kula nikaangalia kuda ilikua saa tisa na nilishakubaliana na keanu kuwa saa 10 anifate hivo niliingia bafunintena nikaoga,nikavaa suruali yangu ya jeans na top yangu flan nzur snaa fupifupi,nikajipulizia marashi ili ninukie bella akasema ww mbn kama unajuandaa kuna mahali unaenda? Nikasema ndio kuna mahali naenda ,akasema wapi?nikasema keanu ameomba tukaangalie mpira wote.bella akasema keanu n nani?nikamwambia ndio stewart hilo keanu ndio jina lake halisi,akasema mmh hadi meanza kupelelekana mpirani mambo so mabaya.mm nikacheka tu,akasema kweli kabisa m naona Maendeleo sasa kama ndo hivo?ujitahidi sana dia na wa upate bwana khaaaa,tena keanu anafaa sana kwa matumizi ya binadam.nikacheka nikasema niache basi ushaanza mambo yako,bella alinitania mpaka simu yangu ikaita alikua keanu akisema anakaribia kufika,mm kwa mdomo wa bella nikamwambia ukifika nistue nitatoka,bella akaicheka sana.nilivaa viraba vyangu simple na kinainai changu begani nikatoka nje nikapanda gari hao tukaanza kuelekea zetu sasa mpirani.tulienda kwenye bar moja maarufu mbeya huko tukakutana na rafiki zake kibao tukaka nao pamoja.niliambiwa niagize kinywaji nikaagiza windhoek ikaletwa nusu katoni mezani nishindwe mie,yy aliagiza heinken tukaendelea kunywa mdogo mdogo.keanu alinijali sana,kila muda japo mpira unaendelea alihakikisha ananitizamanna kuniuliza kama niko powa,mie namjibu nikopoa,mara aseme agiza chakula dia,mm nilikua bado nimeshiba nikasema badae nitaagiza usijali.basi waliangalia mpira huku na mm nipo
Sikuboeka mana kila muda ananijali tu.baada ya mpira kuisha tuliendelea kunywa na rafiki zake hadi mida yaa saa nne usiku nikaomba kuondoka mana nilishachoka sasa na bia ilikua imenikolea.keanu akakubali na kunipeleka nyumbn.tulifika akaniaga kwa kunikumbatia kisha akaondoka baada ya mm kuingia ndani.nilimbebea bela bia nilizobakisha hivo nilivoingia tu akazidaka na kuanza kunywa huku akisema nisimulie kila kitu usiache kitu.nikasema hakuna hata kipya,nikamsimulia vya mpira na kunywa basi,akasema anakuvutia kasi huyo we suburi tu.keanu alipiga simu kunijuza amefika salama kisha akanitakia usiku mwema.tulilala kulipokucha tukajiandaa kwenda hospital kazini sasa mafunzoni, kulikua busy sana kuasi sikuweza kabisa shika simu,mida ya saa nne ndio nilipata muda sasa,nikaenda kunawa mara nikaskia mtu ananiulizia nikasema mm hapa nilimtizama alikua kashia kimfuko kizuri na maua rose mengi mekundu yaliofungwa pamoja nilistuka siuwah haya mambo mie.akasema nina zawadi zako hapa.mmh zawadi?toka wapi?aKasema utamjua tu,hizi hapa pokea,nilipokea zile zawadi yy aaaga zae.yale maua yalikua na kikad,nilifungua kimeandikwa " maua mazuri kwa msichana mzuri,tayla wewe n mzuri kwangu mfanowa ua rose.i lov u. Its keanu"uwiii nilijiskia furaha et nikayanusa πmmmh yananukiaaaa nikafungua kifuko kilikua na kikontena cha vyumba vyumba kina vipande vya keki,sambusa,sosej na kipande cha kuku kikubwa cha kukaanga na juice ya box na kiglas cha take away.nilifurahiaaaa nikashika simu nakutana na missed call zake na msg za salam na kaz njema.nikapigia kushukuru.hio ilikua tabia ya keanu kuleta maua kila siku japo moja hata na msos asubuh na mchana jion tunakua wote.nilikua naskia raha sanaaa na hakua na haraka.baada ya wiki tatu akaniambia kuwa ananipenda sana anaomba niwe wake,sikukataa wala nilikubali japo moyoni hauwepo ila malezi na huduma zake zilinifanya nikubali.tulianza upenzi mm na yy kwa kasi sana.tulidumu mpaka nikamaliza intern madokta na manes walituaga kwa sherehe na keanu alikua anamaliza pia ili arudi dar sasa jeshin mana alikua kikos cha dar.kabla hatujaondoka alinitambulisha kwa dokta peru kuwa mm ni mpenzi wake na Mungu akipenda ndie nitakua mama wa watoto wake.dokta peru alifurahi sana.tuliondoka wote na gari yake hadi morogoro tukiwa mm na yy na bella tukalala moro mjini kesho yake bella akaenda kwao dodoma mm na keanu tukaenda kwetu lkn hakufika alinishusha jirani tu na nyumbn.yy akaenda dar.tuliendelea na mawasiliano maZuri huku akinipa ahadi mbalimbali za kunioa mm mwezi ukapita sikuona siku zangu.nilienda kupima nikakuta imo.nikaona acha nimwambie.nilimpigia akapokea akanisalimia vizur kisha akasema mambo vipi lkn?nikasema sio shwali ,akasema nn bby unaumwa?au huna pesa mama nikutumie?alizoea kunipa sana pesa.nikasema hapana mm nimetoka kupima hapa nina mimba,akasema unasemaje?nikasema nimetoka kupima hapa nina mimba akasema unasema kweli au unanitania?nikasema ni kweli kipimo ninacho hapa.mara akakata simu π³nikapiga haipatkani π₯Ί.........
πππππππππππππππππππππππππππππππππ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni