wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya.
K sal ft ferooz Mwana mkiwa
Hii ngoma ilivuma sana miaka ya 2000, baadaye K sal akatoa ngoma ingine aliofanya na Mandojo & Domokaya inayoitwa starehe na fedha ila haikufanya pouwa baada ya hapo kimya hadi leo
Kali P - Imekaa vibaya
Baada ya hii ngoma sijawahi mskia tena huyu jamaa mpaka leo
Kalapina - Mstari wa mbele
Hili dude la Mwana kikosi cha mizinga ni kali sana, na mpaka leo Kalapina hajawahi tena hit nyingine kama hii, ngoma zote zilizofuata ni average
K basil - Ridhiki
Ni moja ya nyimbo pendwa kwa wakati ule, ila jamaa hakufanikiwa kutengeneza Hit song nyingine mpaka leo
Balozi Dola soul - Kwenye chati
Baada ya hii huyu mkali hakuwahi tengeneza hit nyingine
John mjema - Wachumba 30
Jamaa alitoa hit song moja, mpaka anafariki hakuweza kutoa ngoma ingine kali
Ziggy D -Eno mike
Hii ngoma ilivuma sana kipindi imetoka naweza kukiri ni moja ya ngoma nnazopenda hadi leo, ila Ziggy dee hakufanikiwa kutoa ngoma ingine kali kama hii
Fresh P ft Juma Nature Tina
Jamaa alitamba sana mwaka 2006 kipindi hii ngoma inatoka baada ya hapo mpaka leo hajaweza kurudi tena
Richie longomba -Funguo
Hii ngoma ilikua kali sana ule mdundo sijui nani aliupiga ila ni moja ya ngoma iliyovuma sana
Ocg ft Juma nature Aqwelina
Hawa jamaa walikua watatu wakitumia herufi za mwanzo za majina yao ndo wakaunda hilo kundi walifanikiwa kutoa hit song moja iliyotengenezwa studio za Bongo record na producer alikua Soggy doggy
Rich one ft Juma nature Hatuna kitu
Huyu jamaa naona mziki anafanya kama fani tuu, alitoea hii ngoma yake moja ambayo mpaka leo hajaweza kurudi na ngoma ingine
Dolo ft Juma jature Razia
Dolo naye ni kama rich one tuu amebebwa sana na crew yake ya TMK ila uwezo wa kawaida, ndo maana baada ya radhia hakuweza kurudi tena
Mazense crew ft Juma nature - Riziki
Hawa jamaa nao walipata ngekewa kupata chorus ya juma nature ngoma ikawa kali sana ila tangu kipindi hiko hawajaweza kurudi tena
Adili -ft Mandojo & Domo kaya - Peke yangu
Huyu jamaa hii ngoma ilimtambulisha vizuri sana lakini kwa bahati mbaya hajawahi kufanya ngoma ingine kubwa kama hii
Fagio la chuma - Fagio la chuma
Hii ngoma ilivuma sana miaka ile ya 2000 baada ya hapo jamaa hawakurudi tena
Squeezer ft Juma Nature - Naja
Huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana, ila katika solo project ana hitsong moja tuu hii aliyofanya na Juma nature
Univeral corner - T.shirt & jeans
Hii ngoma ilifanya watu wakaanza kuvaa T.shirt na jeans ilivuma sana ila jamaa hawakuweza kuja na ngoma ingine
Tng squard - Bongo dotcom
Hii pia ilitikisa sana miaka ile inatoka lakini hawa jamaa ni kama walibahatisha tuu
Man ex ft Duly sykes - Nimechezea bahati
Huyu jamaa alifanya hii ngoma kwa beat ile ile ya wimbo wa Bwana misosi nitoke vipi, ngoma yake ikawa kubwa sana ila hakuweza kurudi tena
Picco - Kikongwe
Huyu jamaa hii ngoma ilipendwa sana miaka ya 2002 baada ya hapo jamaa yuko chalii
Stopper ryames - Mtu tatu ndani ya track moja
Jamaa namkubali sana kwa uwezo wake ila hajaweza kutengeneza heat song nyingine kama hii
H mbizo - mpenzi wangu
Huyu jamaa baada ya kutoa hii ngoma akapotea mazima
Pingu na deso ft Mr blue - Jonita
Hawa jamaa walikua ni member wa Tiptop connection chini ya kaka yake Babu tale, the late Abdu bonge, walifanikiwa kutoa heat song moja wakapotea mazima
Dani msimano - siku nzuri
Huyu jamaa alikua ni rafiki wa karibu sana na Mr ebo & wagosi wa kaya, hii ngoma yake ilipendwa sana, ili akashindwa ku maintain akapotea mazima
Pig black - Nini mnataka
Huyu jamaa alipata bahati ya bit kali sana na ngoma yake ilivuma sana baada ya hapo jamaa akapotea
Mack dizo ft Duly sykes Suger mamy
Hii ngoma ilimtambulisha vizuri sana mack dizo ila hakuweza kuendelea kutoa ngoma nyingine kali
Alcom ft mishi - selina
Huyu ustazi ana roho safi sana watu wanaokaa kinondoni B wanaweza kumuelezea vizuri anaishi jirani na Hardman yule aliyetamba na ngoma ya Tamala,
Alcom baada ya selina hajawahi kufanya hit song nyingine
Chelea man - Msela
Huyu jamaa alishawahi kupita pale tiptop connection, alibahatika kutoa hit moja tuu hii ya msela , baada ya hapo alishirikisha ngoma ingine inaitwa heshima ,ngoma ni ya Afande sele ila haikufanya pouwa sana baada ya hapo akapotea mazima
Oten -Nicheki
Hii ngoma ya Oten ilivuma sana miaka ile ya 2000, baada ya hapo alitoa ngoma kadhaa zilifanya pouwa lakini hajawahi kutoa hit song kali kuifunika hii ngoma yake ya kwanza iliyo mtambulisha
JI -kidato kimoja
Ngoma ilitoka 2008 na ilifanya pouwa sana ila mwamba baada ya hapo akapotea mazima
Roho saba - Nakupenda hiphop
Huyu jamaa namkubali sana, nafaham ngoma zake nne
•Nakupenda hiphop
•Waite polisi
•stay
•Focus
Ila zote hizi hazikufikia level ya Nakupenda hiphop, nliskia jamaa ni mwanajeshi na ameacha muziki
Rado- Usiulize
Hii ngoma ilifanywa studio za Baucha kinondoni, ilikua ni dis truck kwa Fid q, ngoma ilisumbua sana, baada ya hapo rado alitoa ngoma zingine lakini mpaka leo hajaweza kutoa ngoma kali tena na ameshapotea
Sajna - Iveta
Hii ngoma ilifanya pouwa sana, akaja na ngoma ingine akimshirikisha Lina, baada ya hapo kapotea mazima
2 berry ft shirko - Wewe tuu
Hawa jamaa walitia hitsong moja baada ya hapo wakagombana kila mmoja akawa anafanya kazi kama solo artist, Berry black aliweza ku maintain kwa kipindi kifupi akaja kupotea , Berry white hakuweza ku maintain kabisa
Offside trick ft AT - Samaki
Hawa jamaa baada ya hii ngoma hawakufanikiwa kutengeneza hit nyingine
Amini - Bado robo saa
Amini licha ya kua THT baada ya robo saa mpaka leo hajatoa hit nyingine
Vumilia - Utanikumbuka
Huyu dada naye alipita THT, na anaonekana alitokea maisha magumu sana, alifanya ngoma kama mbili ila hii ya Utanikumbuka ndo ilimtambulisha kwenye game baada ya hapo, akatoa ngoma ingine inaitwa tatizo ni umaskini haikufanya poa sana, na kuna ngoma alifanya na Ney wa mitego pia haikufanya vizuri, akapotea mazima
Edru g ft barnaba - Scola
Baada ya scola alifanya ngoma zingine lakini hakuna iliyopenya akapotea mazima
Mataluma -Mama mbaya
Huyu jamaa naye alibahatisha ngoma moja na akapotea
Top c ft Ali kiba -Ulofa
Ngoma ilitengenezwa chini ya studio za Bob junior magomeni, ngoma ilipendwa sana hii, ila top c hakuweza kutengeneza hit nyingine safari yake ikaishia hapo
Spince ft Ali kiba - Ayaya
Huyu bwana mdogo naye baada ya ayaya hajaweza kurudi tena
Ally nipishe - My
Baada ya hii alifanya ngoma zingine akishirikiana na wasanii wa THT lakini hakuweza kurudi tena
Chibwa ft juru - Nishai
Chibwa anauwezo mkubwa sana nashindwa kuelewa alipatwa na nini baada ya hii nishai sijamskia tena kwenye solo project mpaka leo
Mo music - basi nenda
Jamaa alitubariki ngoma moja ya mapenzi iliyopendwa sana ila hakuweza ku maintain akapotea mazima
Juru- Mbulula
Huyu bwana mdogo wa arusha alituletea hit song moja akachimba mazima
Coyo - Itakucost
Huyu ngosha alikimbiza sana na hii ngoma, akatoa zingine zikawa average baada ya hapo kapotea
Gigy money-Nampa papa
Gigy naye alibahatisha hii ngoma moja na mpaka leo hana ngoma ingine kali kama hii
Lody music - Kubali
Huyu bwana mdogo hii ngoma aliitendea haki sana, baada ya hapo kajitahidi kurudi lakini wapi
Kontawa ft Nay wa mitego- Champion
Baada ya champion,sijawahi kuskia ngoma ingine kali kutoka kwa huyu bwana mdogo, ngoma zote anazotoa ni average, sahv kinachomfanya aendele ku rotate ni content zake anazofanya instagram ila huku kwenye music simuoni kama ana safari ndefu
Dayoo - Mwaka wa kuforce
Baada ya mwaka wa kuforce dayoo hajaweza kutoa hit nyingine mpaka leo japo anapambania nafasi
Kama kuna wengine nimewasahau ongezea kwenye comment.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni