๐ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐ 8,9,10
O8
Unamaanisha hii simu๐ฑni yangu ๐ค nilimuuliza , Ndio ni yako lete nisevu namba yangu baadae nataka tuongee kuhusu kazi . Sawa nashukuru ๐ sana kaka Denis Mungu akubarikii ulipotoa akuzidishie. Asante Nelly mimi naenda tutaongea baadae, Denis aliondoka nikabaki namtazama hadi alivyoondoa gari ๐ lake.
Kuna watu mna nyota ya kupendwa yaani hadi mnaletewa zawadi nimetamani kama ningekuwa mimi vile sema uzee huu jirani yake anapouza mamkubwa aliongea huku akicheka ๐, ni kaka yangu tu huyu wala hakuna kitu chochote tulikuwa tunakaa mtaa mmoja zamani nyumba ๐ก zetu ni majirani. Jambo jema ila huyu anakupenda tena hasa hawa watu wenye pesa wanatongoza kwa kutumia pesa tu ila ni mkaka mzuri anafaa kwa matumizi. Nikaona huyu mama sasa anaenda mbali ndio mambo gani haya ya kuongea kwa watu nilibaki nimenyamaza kimya mwisho wake azidi kuropoka aseme ana mashine nzuri ๐.
Usiku ulipoingia nilifunga biashara nikarudi nyumbani ๐ก nilimkuta mamkubwa amekaa nje nilimsalimia nikakaa chini, Enhee leo umerudi na jipya gani maana kila ukirudi una mpya mamkubwa aliongea huku anacheka. Kama ulikuwepo mama yangu leo nimeongwa simu ๐ฑ sijui hata ananitakia nini huyu kaka. Anakutaka wewe msikilize anachosema cha muhimu hapo ujikinge na mimba na maradhi tu usimuamini mtu kwa macho mimi nakuambia ukweli sikufichi kitu wewe ni binti yangu sijui unanielewa ๐ค . Nakuelewa mama unachosema , basi ni vizuri tulikuwa tunakusubiria wewe tuje tule tulikula tukaenda kulala ๐. Nikiwa nachezea chezea simu iliingia meseji mambo kusoma jina ni Denis maana alisevu namba yake kabisa nikamjibu poa niambie, Naweza kukupigia simu ๐ฑ usiku huu Nelly๐ค , ndio nipigie nilimjibu kisha nikanyanyuka nikaenda nje ili niongee na simu sikutaka kumsumbua mamkubwa.
Alipiga nikapokea Aloh samahani kwa usumbufu sasa hivi ndio napumzika ndio maana nimekupigia simu sasa hivi , Usijali kaka hamna shida nilmjibu. Usiniite kaka niite Denis tu inatosha Nelly mimi nimetokea kukupenda na nipo tayari kutimiza mahitaji yako yote unayoyataka kuanzia sasa naomba unikubalie ombi langu hata usiponijibu sasa hivi nakupa muda unijibu . Sawa nilijibu , basi nikutakie usiku mwema kesho nangojea jibu langu, asante ๐ na kwako pia nilimjibu kisha nikakata simu ๐ฑ nikarudi ndani kulala ๐.
Usiku ๐ kucha nilikuwa nawaza nimkubalie huyu mtu nikijiangalia nina malengo mengi bila msaada siwezi kuendelea kabisa yaani ngoja tu nimkubalie ili mimi mambo yangu yaninyookee anaonekana ni mtoaji sana .
O9
Basi sikutaka kusubiri hata kesho mimi nikampa jibu muda huo huo kuwa nimekubali ombi lake ila aniheshimu na kunijali , Denis alinihaidi kuwa atanipenda na kuniheshimu na kunifanya kuja kuwa mke bora kwake . Kidogo nikajikuta napata amani baada ya kusikia hivyo tukatakiana usiku ๐ mwema na Denis kila mtu akalala . Penzi jipya in town ๐, siku hiyo nililala usingizi ๐ mtamu sana hadi nilichelewa kuamka asubuhi๐ , mamkubwa alikuwa ameshaondoka kwa kuwa namba yake naijua nilimpigia simu ๐ฑ kumuuliza ameenda wapi . Simu iliita akapokea mamkubwa upo wapi nilimuuliza nimeenda kwenye biashara nimeona umechoka sana leo wewe pumzika tu nyumbani ๐ก leo. Sawa mamkubwa nilikata simu nikaenda kuoga kisha nikaenda kutafuta vitafunio ninywe chai njaa ilikuwa ishaanza kuniuma nikiwa narudi njiani simu yangu iliita kucheki jina ni Denis anapiga nilipokea chap . Aloh umeamkaje๐ค Denis aliniuliza , nimeamka salama sijui wewe ? niko poa nimepita hapo kijiweni sijakuona upo wapi ? nipo nyumbani ๐ก leo nimepumzika . Basi njoo tuonane leo upafahamu hata nyumbani ๐ก kwangu nikamjibu sawa, nikarudi nyumbani haraka nikaenda kujiandaa ili niende kwa baby nikamsalimie.
Alinielekeza kwake ni mbezi kwa Yusuph hivyo nikifika stendi nimwambie aje anichukue nikamjibu poa nikapanda daladala za mbezi nilivyofika tu nikampigia simu ๐ฑ kuwa nimefika nikashuka kwa kujiiba ili mamkubwa asinione nikashuka kule chini nikawa namsubiri Denis aje anichukue. Niliona gari ๐ lake nikamwambia nimemuona tayari nikaenda kupanda safari ya kelekea nyumbani ๐ก kwake ikaanza.
Sikai mbali sana ni karibu tu hapo Denis alivunja ukimya baada ya kuona nipo kimya muda wote, Anhaa sawa unaishi na nani ๐คniliamua kumuuliza maana unaweza kujikuta unaenda kupigwa huko kumbe mume wa mtu ๐. Naishi mwenyewe labda nikikuoa ndio tutakuwa wote unaogopa kufumaniwa nini ? Denis aliongea huku anacheka , ndio isijekuwa mume wa mtu . Hapana kuwa na amani upo peke yako japo niliwahi kuwa na mahusiano kipindi nipo chuo ila tukaachana vipi kuhusu wewe mahusiano yako๐ค Denis aliniuliza, sina mahusiano yoyoie na wala sijawahi kuwa nayo nilimjibu .
Kwahiyo unataka kuniambia kuwa wewe ni bikra hujawahi kuguswa na mwanaume ? Ndio , sawa nimefurahi kusikia hivyo tulifika kwenye nyumba ๐ก moja ilikuwa na geti akapiga honi geti lilifunguliwa tukaingia ndani, Karibu hapa ndio nyumbani kwangu na hii ni nyumba yangu , Asante tulishuka kwenye gari ๐ tukaingia ndani.
10
Ndani palikuwa pazuri nilifikia kukaa kwenye sofa yeye akaenda jikoni kuchukua juisi ๐ท kwenye friji alikuja na glasi mbili pamoja na chupa ya juisi, alimimina kwenye glasi akanikaribisha . Sasa niambie una mpango gani au unataka nini nikufanyie๐ค, nataka kuendelea na masomo yangu nilimjibu haraka haraka. Sawa si ulisema matokeo yako sio mazuri sana mimi nitakupeleka shule ya kulipia ukasome form five na six, Unasema kweli ? nilimuuliza Denis huku nikiwa sijaamini maneno yake aliyoniambia. Ndio sikudanganyi ila naomba muda wako tu mambo mengine niachie mimi, nilijikuta nimesimama kwa furaha nikaenda kumkumbatia Denis .
Na yeye hakupoteza muda akanikumbatia tukajikuta tumekumbatiana kwa sekunde kadhaa naona mtu ananisogelea kwenye lips ๐ zangu akaanza kuninyonya mate sikumzuia , alivyotaka kunishika maziwa nikarudi nyuma kidogo. Vipi mama Denis aliniuliza naogopa siko tayari kufanya hichi kitendo leo labda siku nyingine nilimjibu , Ok mimi nakusikiliza wewe unachosema ukiwa tayari utaniambia , kingine naomba tupime afya zetu ndipo tufanye mapenzi. Hilo ndilo linakupa hofu vipimo ninavyo twende tukajipime Denis alinishika mkono hadi chumbani kwake akaniambia nikae kitandani akaenda kabatini kwake akatoa vipimo akaniletea akavaa gloves kisha akafungua kipimo akanichoma sindano kidogo, pole mke wangu inauma kidogo alivuta damu kidogo kisha akapima na yeye akafanya hivyo hivyo kisha tukawa tunasubiri majibu.
Inaonekana unajua mambo ya hospitali sana ๐ค nilimuuliza Denis , Ndio mimi ni daktari nimesomea laboartory technician wow kazi nzuri nilitamani niwe daktari na mimi ila ndio hivyo tena, Usijali ndoto zako zitatimia tu tena unaonekana ni mtu mwenye akili sana ni vile tu haukuwa na uangalizi mzuri tu. Majibu naona yapo tayari tupo sawa wote siku ukiwa tayari utaniambia nakupenda โฅ๏ธ sana Nelly.
Sawa Denis hamna kitu cha kupika nikakupikie tule nilimuuliza, mara nyingi sishindagi nyumbani ๐ก hivyo kupika ni nadra sana ngoja niende sokoni nisubiri nakuja sasa hivi.Nilimsubiria hadi aliporudi akarudi na vitu vya kupika nikaingia jikoni kupika chakula kilipoiva niliandaa mezani nikamuita ili tule. Tulivyomaliza kula akawasha tv tukawa tunaangalia movie,tulishinda wote hadi jioni kisha akanirudisha nyumbani ๐ก. Kabla sijashuka akanipatia hela elfu ishirini , utaweka vocha hiyo. Asante nashukuru ๐ sana Denis uende salama kuwa makini barabarani unavyoendesha gari ๐.
Itaendeleaaaa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni