*IN LOVE WITH YOU ZURI❣️❣️* *1-5*
*_________________________________________*
*SEHEMU YA : 01*
ANZA NAYO....
Ni katika jiji la Dar es salaam katika familia moja ya kitajiri sana, tunamuona binti mrembo, mrembo sana ambaye alikuwa na macho kama gololi na umbo namba nane lakini pia na nywele kama nywele za singa 😂🙌🏾
Binti huyu alikuwa mzuri acheni tu jamani, binti alikuwa anafanya usafi huku pembeni yake nilikuwepo mimi sasa jitu la miraba minne 😅 nimesimama namchungulia huyu binti namna anavyonikosha kila nikimuona tuu.
Wakati nikiwa pale nimejificha, mara tunamuona kijana mwingine anakuja sehemu ambayo alikuwepo yule binti mrembo
"Habari za asubuhi Zuri...??"
Yule kijana alimsalimia yule binti mrembo ambaye tumejua anaitwa Zuri, binti akatabasamu tabasamu murua ambalo lilimfanya azidi kuwa mrembo kisha akajibu
"Namshukuru mungu, vipi wewe..??"
"Niko poa, unapika nini Zuri..??"
Aliuliza yule kijana
"Kuna sausage hapa, chapati na masosojo mengi mengi kama unavyoona hapa "
"Wooooow, yani ninachokupendea Zuri unajua kupika walah, mumeo atakaekuja kukuoa atakuwa anaenjoy sana.."
Zuri aliishia kutabasamu tu, upande wangu wivu ulikuwa umenikaba mpaka koo, ikanibidi nijitokeze na kwenda huko jikoni maana nilishindwa kuvumilia kabisa
"Ethan umeshindwa kukaa kule seblen na kusubili msosi ukaiva, wewe unakuja mpaka jikoni kweli..??"
Niliongea baada ya kufika kule jikoni
"Ila Frank me nilishakwambia huo wivu wako sio mzuri kabisa et..."
Niliwahi na kumziba mdomo huyu dogo huwa anazingua kinoma, nilichofanya ni kuendelea kumziba huku nikiwa na wasiwasi sana
"Niachie basi we nae..."
Ethan alilalamika lakini sikuruhusu kabisa kumuachia maana anaweza kumwambia Zuri kama ninampenda kitu ambacho sitaki kabisa Zuri afahamu Yani mimi ni mwanaume muoga mno.
"Nini kinaendelea hapa, na wewe Frank kipi cha kumziba mwenzako mdomo??"
Wakati nikiwa nimemziba mdomo mara mama yetu akawa amefika mle jikoni, hapo nikamuachia kwanza Ethani kisha nikamfinya chini chini ili asiropoke 😂
"Asssssssh mama weee...."
Ethan alipiga ukelele wa maumivu na kusababisha mama ashtuke kidogo, wakati huo mimi nilikuwa namuangalia Zuri kwa jicho la kuibia ibia.
"Hivi nyie leo mmeamka na nini..??"
Mama aliuliza, muda huo nilikuwa namuangalia Zuri tu huyu binti mzuri walah muda huo yeye alikuwa busy na kupika huku akisikiliza namna mama na wanae wanavyobishana
"Haya potea sitaki kuwaona humu jikoni, watoto wa kiume asubuhi asubuhi jikoni yani hasara tupu..."
Mama alitutimua basi mimi nikaondoka zangu huku nikiwa namlaumu sana Ethan nilijua fika Zuri atakuwa ameelewa kile ambacho Ethan alizungumza
"Sasa kinachokuuma hapo ni nini??.."
Ethan aliniuliza baada ya kuona naumiza sana kichwa
"We hujui tu namna Zuri anavyoniheshimu, we unazani kama amesikia atanichukuliaje mimi..??"
"Sasa unashindwa nini kumwambia??"
"Ahh siwezi naogopa mno..."
"Tatizo lako Frank we nae ni muoga mno,harafu na wewe mda mwingine unanikera yani umekaaa kaa kama mwanamke bwana, yani unashindwa kumtongoza huyo tu yani Zuri tu ndio wa kukuumiza kichwa wewe...??"
Ethan alikuwa analalamika jamani mpaka jasho linamtoka..
"Sasa sikia me naenda kumwambia Zuri yote kabisa kama unampenda harafu tuone utafanyaje...??"
"Ethan jichanganyeeee, narudia tena jichanganyeee utanijua walah nakupiga naona tunapoelekea ni kukosana sasa.."
"Na mimi sitaki kusikia chochote kuhusu Zuri, yani sitaki ukiniambia sijui Zuri kafanyaje, nikamwambie yani mwisho leo, bora tuongee mambo mengine lakini sio Zuri..."
Nikaona huyu anijui ananiletea mambo meusi na mimi nikamjibu
"Fresh bana..."
Kisha nikatoka ndani, eeh jamani yaliyopo hapo juu ni cheka upasuke, anyway ngoja nijitambulishe kwanza kabla ya kuendelea na story yetu, Frank ndio jina langu halisi kabisa, niko na 25 years old.
Hapa nyumbani tumezaliwa watoto watatu na wote ni boys, harafu sasa sie wote ni mahandsome acha kabisa, sijisifii sana ila ni ukweli mtupu kama mnabisha nichek inbox nikuonyeshe nilivyo 😂😂
Upande wangu mimi ni mwanaume muoga mno, hapa ni miezi miwili tu toka nirudi Tanzania nimekuta mama ameajiri mdada wa kazi ndio huyu Zuri, sasa uzuri wa huyu mtoto wa kipemba unanichanyanga mimi..
Na kingine msichokijua kuhusu mimi yani mimi na wanawake bila bila, 😁 mimi bwana siwezi kumtongoza kabisa mwanamke, hapa mnavyoona nimejikuta nampenda tu Zuri
Na ni miezi miwili toka nirudi namfukuzia kinoma yani ila shida sasa ni aibu walah siwezi kumwambia Zuri kama ninampenda
Harafu kingine mimi bwana, ni aina ya wale wanaume ambao sio waongeaji sana yani mimi mpole mno na sijui kabisa mambo ya kwichi kwichi siyajui yani kifupi kijana wenu mimi bado bikra 😁
Msinicheke bana, 😂hebu tuendelee na Tulipoishia hayo mengine mtayajua huko mbele kwa mbele..
Basi kijana wenu nikatoka chumbani na kushuka mpaka sebleni ambako nilimkuta mdada mwingine wa kazi anaitwa Anita, Hapa nyumbani tuna wadada wa kazi wawili ambaye ni Zuri lakini pia na Anita.
Zuri kazi yake ni kupika tu harafu upande wa Anita yeye ni kuhakikisha nyumba inakuwa safi muda wote
"Habari za asubuhi kaka Frank..??"
Anita alinisalimia baada ya kuniona, nilichofanya ni kumpita kama simuoni na kuelekea nje, huku nikimuacha Anita ananiangalia kwa matamanio makubwa
Baada ya mimi kuondoka nje, punde anafika mama yangu na kumkuta Anita akiwa anajing'ata ng'ata kucha zake huku akiwa anaangalia nje.
"Na wewe cha kukufanya ung'ate vidole ni nini..??"
Mama alimuuliza Anita baada ya kumkuta ang'ata kucha zake
"Aah...nili...nilikuwa naangalia nje..??"
Anita alijibu huku akiwa anatetemeka
"Fanya usafi acha mambo ya kipumbavu.."
Mama alisema kisha akaondoka, jamani mama yangu ni mkali ila ni mpole, namaanisha kwamba mama yangu ni mkali ila ni mtu mzuri mwenye huruma yake mjini 😅...
Itaendelea..........
SEHEMU YA : 02
SONGA NAYO.....
Upande wangu baada ya kutoka nje nilienda kuingia kwenye gari langu na kuondoka pale nyumbani, kisa tu Ethan amekataa kumshirikisha mambo yangu kuhusu Zuri😂 So nimechukia na kuamua kuondoka kwa muda kidogo
Basi bwana huku ndani baada ya kuivisha chakula, waliandaa mezani na kwenda kuwaita watu mavyumbani mwao, baada ya muda kidogo waliweza kukusanyika mezani
Lakini mama alishangaa baada ya kutokuniona pale
"Frank yupo wapi mbona simuoni hapa..??"
Mama aliuliza
"Ameondoka kisa tulikuwa tunazungumza kuhusu jambo flan akachukia na kuondoka.."
Ethan alijibu huku akipeleka kikombe cha chai kinywani mwake
"Nyie watoto mtakuja kuniua jamani, hivi mnanitakia nini mimi enhee.."
Mama aliuliza lakini hakuna mtu aliyemjibu, upande wangu nilikuwa ndani ya hotel flan hivi nikipata kifungua kinywa, baada ya kumaliza kula nikalipia pesa pale na kuondoka zangu kwenda kwenye gari yangu kisha nikaondoka
Na kuamua kwenda kwa rafiki yangu flan hivi, huyu rafiki yangu ana maisha mazuri hata kwao pesa ipo so kijana alikuwa tajiri ila sio mimi 😅
Kwa uwezo wa mungu nilifika salama kabisa na kumkuta, akanikaribisha vizuri kabisa na kuandaa vinywaji juu ya meza kisha wakawasha game ya mpira wa miguu tukaanza kushindana pale ili mradi kupoteza muda.
Tulicheza sana tukifungana vya kutosha mpaka tukachoka na kuanza kupiga story nyingine sasa.
"Dah kuna kitu kinanitatiza sana broh.."
Nilianzisha mazungumzo ili niweze kupata ka ushauri kidogo niweze kumtongoza Zuri 😂🙌🏾
"Kitu gani tena..??"
"Ni kuhusu mdada wetu wa kazi, yani nimejikuta tu nampenda Zuri.."
Nilijikaza na kujieleza ila kwa upande mwingine nilikuwa naona sana aibu ila nilijikaza..😁
"Zuri ndio nani??.."
"Si yule mdada wetu mpya wa kazi ,ndio huyu ananichanganya kabisa akili yangu.."
"Sasa wewe unashindwa kumtongoza Zuri kweli??, harafu nini kuna rafiki yangu yule ambaye siku ile tulienda kwenye party yake si unamkumbuka??"
"Namkumbuka si Nancy yule...??"
"Enheee huyo huyo, huyo binti sasa anakuzimia kinoma usimuone vile tu yule binti ni pisi ya kwenda na kibaya zaidi karibia wanaume wengi wanamfukuzia ila hawajawahi kukubaliwa hata kwa bahati mbaya
Ila wewe umepata bahati ya kupendwa na yule binti so changamka ndugu yangu, na achana kabisa na huyo Zuri, kwanza mimi siwezi kudate na kijakazi yani siwezi Maana mimi na wao ni vitu viwili tofauti na sina hadhi ya kutoka na mskini mimi..."
"Wacha nikukimbie broh..."
Nilisema huku nikinyanyuka baada ya kuona Bruno anazingua kinoma 😔
"So umechukia au..??"
"Hapana bi mkubwa kanitumia message hapa kaniambia niende, basi acha niende kesho nayo tutakutana tuongee vizuri.."
Basi mwaya Bruno hakuwa na maneno mengi, alinisindikiza mpaka nje ambako niliingia kwenye gari langu na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Kwa uwezo wa mungu nilifika salama kabisa na kushuka kwenye gari yangu na kisha nikaingia ndani, picha linaanza nimefika seblen nikamkuta Zuri akiwa anaangalia TV ila kwa bahati mbaya alisinzia na kusababisha ile sketi yake ambayo alikuwa amevaa ifunuke kidogo
Na kuacha sehemu ndogo ya upaja wake kuwa wazi, mwanaume mimi nilibaki nikiuangalia tu huo upaja namna ulivyokuwa mweupe jamani jamani mzee baba akasimama pale pale 😂
Msinicheke jamani, ila si mnajua kabisa huyu binti mimi ninamzimia kinoma, basi bwana katika kujigeuza binti akawa ameamka na kuniona nikiwa nimeganda mlangoni namtazama
Akashtuka na kutengeneza sketi yake vizuri..
"Kaka Frank kumbe umerudi...??"
Zuri aliniuliza, nikajikaza na ukauzu wangu nikampita na kuelekea chumbani kwangu, nimefika huko moja haikaliki mbili yani nilikuwa natapa tapa na kusumbuka hii ni baada ya jamaa wangu kukakamaa sana mpaka nilikuwa naumia
Ikanibidi niingie bafuni kwanza, nimefika huko nikafungulia maji mpaka mwisho yakaanza kutililika kwenye mwili wangu, hapo kidogo nikapata unafuu na yule ndugu yangu aliweza kulala
Baada ya kumaliza kuoga nilipigilia mavazi yangu ya kushindia nikiwa nyumbani ila yalikuwa ya bei mbaya harafu mazuri na mavazi yangu ya kushindia huwa ni pensi mwanzo mwisho
Basi baada ya kumaliza kuvaa bila kusahahu earpods nikavaa zangu na kuelekea chumbani kwa kaka yangu Idress, Idress ni kaka yangu na ndie mtoto wa kwanza kuzaliwa nafuata mimi harafu anamalizia mcharuko Ethan
"Nakuona mume wa Zuri..."
Baada ya kuingia chumbani kwa kaka yangu, Idress akaanza mambo yake, nikacheka kwanza na kumtazama
"Oyaa taratibu basi, asije akasikia ujue.."
"😂 so unaogopa asijue, ila we Frank wewe sijui una nini yani Ethan huko aliko amemind vibaya mno kila muda analalamika eti unamcheleweshea kupata shemeji.."
"We umesahau akili za Ethan wewe, sema huyo dogo nae anazingua kinoma.."
"Kwanini..??"
"Ah si ile asubuhi alitaka kuongea na Zuri akiwa pale so nimechukia na kuamua kuondoka kwa muda, maana nina uhakika tu Zuri atakuwa amesikia hapo.."
"😂😂 we kijana wewe ni muoga walah sijawahi ona, na sijui huo uoga umeutoa wapi, hivi umeshawahi kufanya kweli wewe..??"
Idress aliniuliza, nikawa sijamuelewa
"Kufanya nini?? mbona sielewi..??"
"Eeh kweli nimejihakikishia alichoniambia Ethan ni ukweli, kwamba wewe bado bikra 😂😂"
"Sikia bro me natoka.."
Itaendelea..........
SEHEMU YA : 03
SONGA NAYO......
Nilisema huku nikinyanyuka kwa lengo la kuondoka
"Eeeh yamekuwa hayo tena..??"
"Sasa mambo gani hayo unaongelea..??"
Nilichukia, nilijua fika ananicheka kwa sababu tu sina mshipa wa kumwambia mwanamke kama nampenda
"Ah samahani bana Frank nilikuwa nakutania bana.."
"Fresh bana.."
Nilisema na kurudi nikakaa, na story zingine zikaendelea, upande wa huku chumbani kwa Zuri, Zuri baada ya kutoka pale sebleni alienda kuingia chumbani chumba ambacho wanatumia yeye na Anita
"Hivi Zuri yule Frank ni mzima kweli yule..??"
Anita alimuuliza Zuri baada ya kuingia chumbani
"Kwanini unasema hivyo..??"
"Yani me nashangaa Frank ni mwanaume wa tofauti sana na nduguze yani huyu sijawahi kabisa kumuona akiwa na mwanamke sasa sijui kama anasimamisha kweli...??"
"Anita muogope mungu ndugu yangu.."
"Kwamba unamtetea au vipi, ila hata wewe si unaona kabisa mtu ukimsalimia hajibu badala yake anakaa kimya tu yani ananikera mimi, bora hata angeitikia tu kuliko kutukalia kimya.."
Zuri alichofanya ni kuchukua shuka na kujifunika mpaka kichwani kisha akalala 😂 akimuacha Anita anaongea mwenyewe tu pale
Muda ulienda hatimae usiku nao ukaingia, kama kawaida ya Zuri akaingia jikoni kuandaa madiko diko ya usiku, upande wangu nilikuwa chumbani nimepumzika ila sasa mawazo yangu yalikuwa kwa zuri tu
Nikaona cha kufia nini acha niende huko huko jikoni, basi nikashuka mtoto wa kiume huyoo mpaka jikoni nikamkuta akiwa busy anapika
Nilienda kwa lengo la kuchukua maji ili niweze kumtazama usoni, lakini nilishangaa nikisukumwa kwa nguvu na mtu ambaye alikuwa nyuma yangu na kusababisha niende moja kwa moja mpaka alipo zuri na kujikuta tu nikipitisha mikono yangu kiunoni mwa Zuri na kumkumbatia kwa nyuma
Jambo ambalo lilimfanya Zuri aache kupika na kugeuza shingo akawa ananiangalia na mimi sasa nikabaki namtazama tu huku mikono nikiwa nimeipitisha vile vile 😊
"Heee ni macho yangu au naota..??"
Tulisikia sauti nyuma yetu ndio nikakurupuka na kumuachia Zuri, yule mtu ambaye alikuja jikoni alikuwa Anita na ndie aliyetushtua, jamani nilikuwa naona aibu kwa sababu tumefumwa nikiwa nimemkumbatia Zuri
Sio siri nikabaki nababaika pale kama sina akili nzuri 😅
"Aah am...am sorry Zuri.."
Nilisema na bila kusubiri nilitoka mle jikoni na kuelekea chumbani kwangu, nilikuwa naona aibu jamani nafika chumbani nikajitupia kitandani na muda huo huo akaingia Ethan na Idress wakiwa wanacheka sana
"😂walah Frank utaniua kwa kicheko.."
Alisema Idress huku akijizuia kucheka
"Acheni ujinga mnajua, najua kwamba ndio nyie mlionisukuma pale.."
"Sio mimi kabisa, Ethan wako ndio kakusukuma.."
"Ethan hivi una nini lakini..??"
"We sema tu umeenjoy basi, sasa cha kukufanya uchukie hapo ni nini..??"
Nikacheka kwanza, 😂 ila ukweli nilikuwa nasikia raha baada ya muda mrefu sana kumfukuzia Zuri hatimae leo nimeweza kumshika na kibaya zaidi nilimkumbatia, awee hii feeling wanaijua wale wanaume ambao wapo kama mimi
"😂 Ethan ila we noma.."
Nilisema huku nikikaa
"Si unamuona ee kumbe amesikia furaha ila anatuzoom tu.."
"Ah ila bana unajua me sijapenda kweli, harafu kibaya zaidi Anita ametufuma mle jikoni nikiwa nimekumbatia zuri we unajua Zuri anajisikiaje huko huenda hajapendezwa na hili jambo siku nyingine usirudie Ethan nitakuja nikupige.."
Nilisema kwa ukali kidogo
"Fresh bro, ila dah kila nikikumbuka nacheka tu harafu bana nilisahau kukwambia nilikuchukua photo.."
"Wee kweli..??"
"Kweli si unaona.."
Alisema Ethan huku akinionyesha, nyiee nilifurah kidogo nizimie yani hii furaha wanaijua tu wale wakaka wenye tabia kama yangu, nilichofanya hapo ni kuihamishia kwenye simu yangu kisha nikatulia zangu nikiwaza kesho asubuhi niamkie photoshop 😂...
SEHEMU YA: 04
SONGA NAYO.......
Basi story zingine ziliendelea, upande wa huku jikoni baada ya mimi kuondoka Anita akamsogelea Zuri akiwa kama haamini vile
"Mh imekuwaje tena hii..??"
Anita alimuuliza Zuri lakini Zuri alikuwa bize anapika tu
"Kwahiyo ule muda naongea kumbe ulikuwa unajua kabisa ila ukaamua kukaa kimya..??"
"Eeh Anita we umefuata nini huku jikoni??, kazi yako ni kufanya usafi au kuja kunipigia makelele ..??"
Zuri aliuliza kwa hasira, Anita akaamua kuondoka akimuacha Zuri akiwa amechukia sana, basi hatimae chakula kiliiva ila ndio hivyo sikuwa naweza kabisa kwenda sebleni
Na ratiba za hapa nyumbani hakuna mtu anaruhusiwa kulia chumbani yani wote ni kukaa sebleni, sasa nikaaa najiuliza namna ya kwenda huko
"Frank hebu twende bana, yani unakuwa kama mwanamke bwana.."
Ethan alizungumza
"Haya yote umeyataka wewe, kulikuwa na haja gani ya kunisukuma na huku unanijua kuwa nina mshipa wa aibu.."
Nilianza kumlalamikia sasa Ethan baada ya kuona uwezekano wa kwenda seblen ukiwa haupo
"Kwani atakufanya nini na ikiwa wewe ni boss wake, hebu twende basi.."
Idress nae alichangia, nikakataa wakaona cha kufia nini wakaja kunishika huku na huku na kuanza kutoka na mimi 😅 nilikuwa natumia nguvu yani napambana ila wapi walikuwa wamenishika kwa nguvu sana
Nilivutwa mpaka kwenye ngazi karibu labisa na sebleni, baada ya kufika hapo sasa ikabidi niwaombe nishuke mwenyewe
"Basi niachieni nashuka mwenyewe .."
"Sawa tunakuachia ila ukijaribu kutuletea hapa aibu zako namuita zuri hapahapa.."
Ikanibidi nishuke tu hivyo hivyo huku nikiwa nimeweka uso wa serious, basi tulifika mezani na kumkuta mama akiwa tayari kashafika so tukakaa
Muda wote nilikuwa nimeinamisha uso chini yani naona aibu kwa kweli, baada ya muda Anita na Zuri wakawa wamekuja pale wakiwa wamebeba hotpot za chakula
"Frank asubuhi ulienda wapi..??"
Mama aliniuliza muda huo Zuri na Anita wanatupakulia chakula, sikuweza kumjibu mama nikaa kimya
"Frank ai naongea na wewe au..??"
"Nilienda kwa Bruno.."
"Sasa kwanini hukuaga..??"
"Eeh mama kuna haja gani pale nikitaka hata kutoka kidogo tu mpaka nikuage, me ni mtu mzima mama na ninajielewa.."
"Sawa najua umekuwa ila unatakiwa kutoa taarifa pale unapotaka kutoka.."
"Sawa, am sorry mom..."
Nilimwambia mamaa, basi mama akatulia muda huo Zuri akawa amefika kwangu kwa lengo la kunipakulia lakini nkakataa na kumwambia tu aache nitapakua mwenyewe
Nyiee jicho nililotazamwa sio ka nchi hii, so nikamuacha tu akapakua kisha baada ya hapo akashika njia kuelekea chumbani mama akamsimamisha
"Kwahiyo leo huli au mwenzetu umefunga..??"
Mama alimuuliza Zuri
"Sijisikii kula, acha nikapumzike kidogo.."
"Lakini ungekula japo kidogo.."
"Nitakula kwa baadae.."
Alisema kisha akashika njia na kuondoka zake nikabaki namtazama tu mpaka akaishilia kabisa, hata mimi hamu ya kula ilikata pale pale nikawa mnyonge hatari....
Itaendelea........
SEHEMU YA : 05
SONGA NAYO......
Baada ya Zuri kuondoka nami nikamgeukia mama yangu, kisha nikazungumza
"Mama ongea na Zuri huenda anaumwa au hayupo sawa.."
"Mh..."
Anita aliguna nikageuka na kumkata jicho kali mpaka akanyanyuka mwenyewe na kwenda jikoni
"Mbona sielewi nyie, nini kinaendelea humu ndani..??"
Mama alituuliza
"Wala hakuna kitu mama, sema Anita ni mmbea sana sasa kulikuwa na haja gani ya kuguna pale ikiwa Frank anakuambia jambo la muhimu.."
Ethan alimjibu mama, muda huo mimi namuwaza Zuri wangu tu huko aliko hata chakula sikuwa nakula nilikuwa nakiangalia tu
"Basi nitazungumza nae.."
Alisema mama, hapo nikapumua kidogo kisha nikasimama kwa lengo la kuondoka lakini mama aliniita
"Unaenda wapi..??"
"Naenda kupumzika.."
Nilimjibu bila wasiwasi.
"Sahii tu umeshiba angalia hata chakula hakijaonekana kabisa kama kimeliwa.."
"Me nimeshiba mama bye.."
Nilizungumza na bila kusubiri nilielekea moja kwa moja chumbani kwangu, na kumuacha mama akiwa haelewi chochote
"Huyu ndugu yenu ana nini leo..??"
Mama aliwauliza Ethan na Idress baada ya mimi kuondoka pale seblen
"Sijui.."
Mama alibaki wakiwatazama vijana wake kama anawachora hivi, basi huku upande wangu baada ya kufika chumbani nikawa nakumbuka namna Zuri alivyoniangalia muda ule nikawa najisikia vibaya
"Inamaana Zuri mimi kosa langu nini mpaka uniangalie hivyo..??"
Nilikuwa najiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe walah mapenzi yanaweza kumfanya mtu akawa kichaa kabisa, ilinibidi tu nipande kitandani nipumzike lakini usingizi uligoma kabisa kuja
Hii ni kwamba Zuri hakuwa saw, ulipofika mda wa saa nne usiku uvumilivu ulinishinda ikabidi nitoke kwenda kule chumbani kwao wanapolala kwenda kumuona japo kidogo
Basi mwanaume nikatoka zangu na kuelekea huko chumba anachotumia Zuri lakini pia na Anita, baada ya kufika mlangoni nikijishauri nipige hodi mara mlango ukafunguliwa kwa kwa ndani
Nilishtuka baada ya kumuona mama yangu ndio anatoka humo, haraka haraka nikatunga uongo wa kumwambia maana mama yangu ni mtu wa maswali sana
"Enhee na wewe huku..??"
Mama aliuliza kwa sauti kidogo nikahofia huenda humo ndani watasikia, so nikamvuta mama mkuku mkuku na kuondoka maeneo yale
"Frank hebu niachie bana, unataka kuniua na huu uzee wanhu unanipeleka kama mwanajeshi bana.."
"Ni mazoezi hayo, ndio maana unazeeka vibaya kwa sababu hupendi kufanya mazoezi.."
"Hebu niache nipumue mimi, haya na kule chumbani kwa wadada wa kazi ulikuwa unafuata nini..??"
Eeeh 🙄 me nilijua amesahau bwana kumbe bado anakumbuka
"Aah nileienda tu kumsalimia Zuri, na kujua hali yake ipoje.."
Nilijitetea
"Hongera kwa kumjali, ila nikutahadharishe tu, zuri ni mke wa mtu.."
Nyieeeee mshtuko nilioupata sio wa nchi hii nikabaki kama nimemwagiwa na maji ya baridi na nisielewe chochote, hivi ulishawahi kupenda wewe??
Nakuuliza ulishawahi kama ambavyo nimependa mimi?? Na kufikia stage ambayo nimefikia mimi?? Guys sio rahisi mno kuamini lakini pia ni maumivu zaidi ya Maumivu maana mtu ambaye nampenda na ananifanya nakuwa chizi, harafu nakuja kuambiwa ameolewa
Macho yalinitoka jamani na kwa mbali machozi yalianza kunilenga lenga 😅 sema ilikuwa ni usiku na mwanga wa taa ulikuwa hafifu so mama hakuweza kabisa kuniona...
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni