JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 14
Mwandishi:lissa mwalla
Mmmh nilihisi utumbo unacheza, kwa nn haruhusiwi ndoa sasa? Au ameoa? Nilijiuliza sana, keanu akasema sijakuelewa kwa nn siruhusiwi kuoa sasa? Akasema kuna mashart katika kila kanisa ili ukamilike lazima uwe unahudhuria kanisani na kutambulika kama mkristo pia uwe unalipa zaka ww hufanyi hivo, ndio mana unakosa sifa za kufunga ndoaa, ukitaka ndoa anza kwanza kuwa unahudhuria kanisani pia unakipa zake kwa muda wa miezi sita mfululizo tukutizamie na hata kama hauishi hapa basi utaleta utambulisho wa kabisa unalohudhuria. Mmmh keanu alinitizama akasema sawa nimekuelewa. Tukasimama na kuondoka, keanu akasema nn tena hiki? Makanisa yameanza lini mashart magumu hiv? Nikasema kwani mara ya mwisho kanisani kwenda alikua ni lini? Akasema mmh kusema kweli ni kitambo sana, nikasema basi ndio hivo unatakiwa ufate. Akasema daaaah sawa bana kwa hio tuishi bila ndoa? Nikasema sijui sasa, akasema hapana tufunge hata ya serikali ili ww na kijacho muwe na haki hata kazini Kwangu au unasemaje wakati huo naendelea kuhudhuria kanisani kisha tuje tubariki. Sikuona kama ni wazo baya, akasema basi tutawashirikisha wazazi, nikasema sawa. Nililala siku mbili nikarudi kwa mama na baba nikawashirikisha hilo wakasema sawa ilimrafi ameshajulikana mengine tunawaachia ninyi, nikasema sawa. Nilimpa jibu mme nae akasema kwao wameelewa hivo tukaandikishe tu ndoa. Tukakubaliana tukaenda zetu kuandikisha .ilitangazwa siku 21 ndipo tukafunga ndoa yetu na kusherehekea katafrija kadogo tu kalikohusisha ndugu wa karibu sana na marafiki wa karibu. Kalikua na watu 30 tu waliokula na kunywa kwa gharama za keanu. Nilihamia dar sasa kwa keanu na kuanza maisha rasmi ya ndoa, keanu alikua ananijali kama kawaida yake na kunipenda sana. Graduation yangu ilifika
Nilifanyiwa party na kimimba changu nilipata chet changu na nilifanya vizuri snaa. Maisha ya ndoa yalikua matam kiasi kwamba nilikua nashangaa wanaosema ndoa ndoano sijui mana mm nilikua kama niko peponi, mme ananijali kila nitakacho napata, ananipetpet ananitoa out, nilipelekwa veta kusomea udereva miezi mitatu nikajua vizuri nikapewa gari hapo mimba ina miezi sana kuelekea nane. Niko kama Nina kazi vile navaa na vile naishi. Mimba ilipotimiza miezi nane mme wangu alipata uhamisho akahamishiwa tabora huko, hakupenda lkn hakua na naman. Aliomba yy atangulie akaandae mazingira ya mm na yy kuhamia huko, nikasema sawa hivo akaenda zake tabora huko. Alikua wiki tatu akasema. Sasa naweza kwenda mana ameshapata nyumba nzuri ya sisi kuishi. Yalikuja magari ya jeshi kwa ajili ya kutuahamisha nikafungashiea mizigo safari ya tabora ikaanza. Tulifika usiku lkn tulipokelewa na nyumba ilipangwa kama mchana vile ndio raha ya wanajeshi ukiwa na kacheo ww unatuma tu makuruta wanafanya kazi. Katika kufika mm sikuwa sawa kabisa nilikua nkmevimba sana mme wangu akasema ni hali ya mimba natakiwa kupumzika, sababu nae ni dokta wa wanawake nikamskiliza. Nilipumzika lkn kingine nikagundua sikuwa naskia mapigo ya mtoto kabisa wala alikua hachezi, mme wangu akasema inawezekana nae kachoka wewe pumzika. Nilipumzika Siku mbili mbili mfululizo simskii mtoto nikasema Hapana hii sio kawaida nikawambia keanu, nae akastuka akasema twende hospital. Nilijiandaa na kwenda hospital kupima Utra sound dokta alibadilika uso akawa na uso fln nilihisi kabisa kuna shida kubwa tena, nikasema kuna nn dokta? Akasema umeacha kumskia lini mtoto? Nikasema juzi nikivofika toka safari, akasema ahaa basi naomba mniskilize kwa makini itabidi tukushughulikie haraka mana mtoto amefia tumbon. Keanu akasema nn. Dokta akasema poleni aana ni hatari sana kwa mama inabidi leo tufanye hivo,mm. Niliangua kilio mana sikufikiria hayo kabisa. Keanu akasema naelewa mana mm Ni gyno pia basi anzeni. Nilichukuliwa pale nikiaa sielewi maskin nikapelekwa wodini nikadungaa sindano nikawekewa na dawa gani sijui huko chini,nilikaa lisaa limoja nikaanza skia maumiv ya kiuno na chini ya kitovu uwiii maikumiv makati yanakera nilihangaika na kulia sana sanaa dokta na manes walikuja nikapimwa nikachukuliwa na kupelekwa leba, nilijifungua mtoto aliefariki tayr niliumia sana moyo wangu. Nilisafishwa nikarudishwa wodini, nilikua nalia tu mana kitoto nilikiona ki bby boy kikubwa jmn sa kwa nn? Nilikua na maumiv yasioelezeka nilitaman hata kufa na mm. Mme wangu alikua faraja kwangu aliniambia nisiwaze tutapata wengi wengine wala nisiwe na shida. Aliwapigia nyumbn na kwao kueleza yalotokea wazazi waliskitika sana sana. Nilikaa hospital siku tatu nikichomwa madrip ya flagly na madawa menginr kuua infection nilipomaliza nikaruhusiwa nikarudi nyumbn nikiwa moyo wangu umevunjika sana. Sikuweza kua yule Mwenye furaha tena wala. Mwezi ulipita nklipata kazi hapohapo ajira kabisa ya serikali na nilipangiwa kituo cha afya mana tukipokua tunaishi haikua mjini ni kijijin fln japo pamechangamka sana. Sababu sikuwa mtu wa kujichanganya kitaa nilivornfa kurepory kazini nilikua kama mtu mpya kabisa. Niliriport na kuanza kazi sikutaka kabisa kuomba sijui ruhusa nijipange mana nilikua nikiwa nyumbn nawaza sana mwanangu. Nilifanya kazi mwezi mmoja mme wangu akaanaa wimbo wa kutaka mtoto, nikasema lkn mme wangu hospital si wameshaur nikae miezi sita ndipo nibebe mimba jmn? Akasema miezi Sita ya nn? Mm ndio mme wako na ni gyno Nakuambia sasa. Nikaona Kufanya mambo yawe mafupi nikakubali lkn nilikua natumia zangu kalenda. Mme aangu alianza kubadilika taratibu, alianza kuwa mnyaji sana ikifika weekend anakunywa kurudi usiku wa manane, nikaona hii inazidi nikamkalisha nikasema mme wangu hii tabia ya kurudi usiku wa manane mbona inakua kawaida sasa? Mm. Sipendezwi nayo. Akasema heee unataka niwe nawahi kurudi kufanya nn nyumbn sasa? Kama. Ww nimeshakuzoea nishacheza na ww sana ungekua na mtoto ningesema niwe nawahi kucheza na mtoto sasa nawahi nawahi nn? Umeanza gubu siku hizi bana sasa unahisi nakua wapi? Au hutaki hata niwe na marafiki? Aaaaghhhh akachukua funguo ya gari akaondoka. Nilijiskia vibaya yn mtoto wangu kafa ananitonesha? Nilihuzunika sana sikujua kiburi cha keanu kilitoka wapi.siku hio nilivomsema akaondoka mifa ya SAA nane usiku akatuma msg akasema najua unaona. Usumbufu mm kurudi usiku kukugongea sasa kuwa na amani lala funga milango yako mm sirudi. Uwiii yamekua hayo tena? Hapana nikapiga simu ikaita ikakata, nikapiga tena skapokea amelewa akasema Nini sasaa nikasema mme wangu naomba urudi mm siwezi kuchoka kukufungulia ww ni mme wangu keanu rudi. Akasema aaaahhh unamaneno mengi weweee mara nikaskia kay bana nachoka kukushikilia agana na huyo mwanamke wako twende tukatiane hukoo π³π³π³,alikua sauti ya kike keanu nae akakata simu.......
πππππππππππππππππππππππππππππππππ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni