JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 15
Mwandishi:lissa mwalla
Simu ilikatwa,nilichanganyikiwa,iv nimeskia kweli au ni mawenge yangu?keanu ananisaliti?yani maneno yake makavu yote aliyoniambia hayakua na maana sikuyajali kabisa nilijali mwanamke alieongea.nikasema hapana ngoja,nikapiga simu iliita ikakatwa,nilipiga tena ikakatwa,nikapiga tena safari hii ilipokelewa lkn nilikua naskia sauti za kimahaba sasa mwanamke anaguna kimahaba ni kama wanabusiana huku anasema twende chumbn banaa kay,nilisonya nilipatwa na hasira,bar zote pale nazijua nilitoka nje na kuwasha gari yangu sasa nikaanza safari,nilipita kila bara naangalia na nauliza sikumpata,nikawaza kuna bar moja ambayo ndio iko karibu na nyumbn niliidharau nikajua hawezi fanya hayo hapo jirani hivo nilianza kuangalia mbali kwanza na hakuepo kabisa.nikabishana na nafsi niende nyumbn au niende bar ile ya jirani?nikaona niende tu,nilinyoosha mpaka ile bar nilifika nikapak mbali kidogo gari yangu nikshuka na kuanza kutembea kuelekea ndani sasa.nikiwa natembea niliona magari matatu yamepaki kwa ndani hivi mana kuna sehemu ya kulala kwenye hio bar,akili ikanituma niende kwa ujirani niangalie kule ndani ya gati,nilienda heeee gari yam me wangu hii hapa,niliingia moja kwa moja hadi mlinzi hakuniona mana niliingia kama kishada,nilienda kwenye gari na lilikua tinted lkn nilihisi kabisa kulikua na watu mana lilikua linatikisika niligonga dirisha gari likawashwa kisha kioo kikafunguliwa na taa za ndani si zikawaza hivo nikajionea kabisa live bila chenga ni mme wangu Keanu kabisa mara nikamuona mdada ananyanyuka mmmh niliangalia uume wa mme wangu ulikua nje umeshikiliwa na Yule mdada aliekua amejichubua ila sugu za mikono nyeusiii,nikasema mme wangu ndio unayoshinda unayafanya haya huku?yule mwanamke akasema hee weee vipi kimekuleta nini huku si ungemsubir nyumbn wanawake wengine bana,nikasema pumbavu kelele siongeni na wewe Malaya kahabaaa wewe,akasema kama wewe sio kahaba mbona vitoto vinafia tumbon?si midaw aya kutolea mimb au umalaya mishahawa imejezana humo,acha tumzalie,nikasema kw aio unataka umzalie mme wangu kwa kumeza shahawa si dio?ameshindw ahata kukupeleka chumbn kila muda unang’ang’ania akupeleke upo tu humu looo ona aibu anaona haya kwenda na wewe ndani mana atakachokutana nacho ni pundamilia mchafu shetani wewe.yule mdada akasema Keanu hiv unamruhusu mke wako atukane watu hivo?kweli umerogwa kama watu wanavosema looo,mwanaume gani umezubaa kama uji wa mtama?mxxiiiiiiew nashuka zangu mie.keanu alimshika mkono kumzuia asishuke kisha akasema wewe mwanamke unafanya nn huku?aliniuliza mm,nikasema unaniuliza mm nimekufata wewe,akasema umenifata mm au ulikua kwenye mambo yako ndio umeona ujisafishe?nilimshangaa nikasema Keanu si nimeongea na ww hapa sasa hiv unaniambia mm hivo kweli?akasema nyumbn huli?siachi pesa?hulali vizuri imekupa kila kitu lkn umeanza kunifatafata bar si ndio?umenipanda kichwani eeh?toke nenda kwako haraka,sikuamin,ananifukuza mm au?nikasema Keanu unaongea na mm au unaonge ana mtu mwingine?yule mwanamke akacheka akasema heee kawa kiziwi mara hii,dada nendaaaaaa khaa.nilimtizama Keanu ambae alishuka kwenye gari akanisukumia pembeni nilipepesuka nikaangukia huko,akasema unaniskia?nasema ondoka hapa nitakuharibu sasa hivi,toka lini mke wa mtu akawa anahangaika bara usiku huu?unanitafuta mm ni mtoto mdogo si ndio?toka hapa nasema.sikuamin bdo Keanu aliniacha pale chini,akaingia garin namskia anasema bby tuondoke nikupeleke mahali kuzurii kuskiko na kiwingu sawa eeh tukibaki hapa kuna watu wanaweza choma lodge ya watu.mwanamke akacheka nikaona gari inaanza kurudi nyuma,nilisimama haraka na kusogea pembeni,walitoka getini kisha wakaondoka zao sikuamin macho yangu kilichotokea mm,kweli nimeachwa?nafanyiwa hivi na Keanu?nilikua kwenye mstuko hata machozi yalikua hayatoki,nilitembea nikikumbuka yote aliokua ananifanyia kuanzia mwanzo kipindi cha maua mpaka leo hii kanioa mapenzi yote yale kumbe mwishowe ni hivi?kisa sina mtoto au kuna kitu?nilijiuliza mambo mengi sana sikupata majibu.niliingia garini nikiwa nina ganzi mwilimzima sikuweza hata kuendesha maumivu yalivonizidi niliona kitu kinanikaba kooni nilijilaza kwenye usukani nikapiga keleleee kwa nguvu huku nikipigapiga usukani,nililia kama mwendawazimu kwa nguvu bahati nzuri ilikua ndani ya gari watu hawakuskia,nilikaa pale lisaa nikilia hasira zilishuka nikaona acha nirudi nyumbn,nilirudi nyumbn nilianz ahesabu masaa nikiskia hata paka kakatiza nje nachungulia najua ni yeye amerudi lkn hola,nilikesha macho kabisa na Keanu hakurudi wala.siku hio nilikua naingia kazini ilibidi nijitafakari kwanza,mm ni dokta ninatakiwa nitibu watu,wanakujaga wamama wana stress nawapa ushauri iwaje mm binafsi siwezi kujishauri nimekesha nikilia?keanu kweli anifanyie hivi?au pombe?au amerogwa?haya bana,nilisali nikaomba Mungu anipe uvumulivu.nilioga nikavaa zangu nikaenda kazini nikiwa na lundo la mawazo.kazini sikuwa na rafiki wala japo wote nilikua naongea nao nacheka nao vizuri lkn sikua na mtu wa kumwmabia mambo yangu,na vile mama alinikanya kuwa ndoa ni kuvumilia na matatizo ni kuyatatua mm na mme wangu sio na mtu wa tatu basi nikasema akirudi nitaongea nae labda atakua ameshajishusha.nilifanya kazi huku nikitizama sana simu yangu lkn hakunitafuta nilikua natafutwa na watu wengine tu,nilishinda pale mpaka muda wangu wa kazi uliisha saa 11 nikaondoka na kupitia sokon nikanunua vy akununua na kurudi nyumbn.,nilifika nikamkuta Keanu amekaa seblen tv iko on ila yeye anasoma gazeti,moyo wangu ulifanya paaa,hasira ilinikamata lkn nikakumbuka mwanaume hafokewi anaulizwa taratibu.nikasema habari za leo.akashusha gazeti akaniangalia akarudishi ana kuendelea kusoma,mm nilipita nikaedna chumbn nikaoga kisha nikatoka nikaingia jikon na kuanza kupika,nikiwa busy napika alikuja jikon akachukua maji akanywa kisha akaweka kikombe chake kwenye sink akatoka,sikuelewa yani amenikosea halafu ananuna yeye?nilishangaa,niliendelea kupika mara nikaskia anaonge ana simu anasema noo nimekaa tu hapa naangalia tv,nooo bana nakuja sasa hivi banaa …mmh anaondoka tena?ngoja nimuwahi tuongee,nilimfata seblen nikakuta ameshaenda chumbnn nilimfata huko huko,nikasema mme wangu nina maongezi na wewe,alinitizama akasema nani mme walko?nikasema sasa swali gani hilo?akasema nimeuliza mana humu ndani mm na wewe wote wanaume ndio mana tunashindana,nikasema sijakuelewa,aksema hujaelewa nn?ww si unataka tushindane humo mabar wewe,unanifata fata na kunidhalilisha mm kwa watu, na jana nilichofanya usije nilaumu nilifanya ili ujue mm ndio mwanaume,sikua na mpango kabisa wa kutembea na Yule dada ndio mana ulikua unaona kabisa sitaki kwenda nae chumbn lkn ww kujifanya umeniweka kiganjani ulinifedhehesha sna kukuonesha mm ni mwanaume ndio nikaona nikatembee nae sasa.mmh kweli haya anayoniambia?akaendelea ww ni mke wangu,nimekupa kila kitu,nakupenda na kukuthamini sana,sawa ninakunyw alkn nakunywa siku zote si narudi hapa?na hiv umewahi kuniuliza najiskiaje kw akupoteza mtoto?au unaona nachukulia poa tu?watu wengi wanakuwaza wewe na si mm kuniuliza najiskiaje,naumizwa sana na mengi sana.naumia navoambiwa umenishika,nakuogopa sijui nn ndio mana nikafanya yale yote,ww kwa nn unifate?ina mana ulikua huniamin?au sababu nimekuoa ww unafkir hakuna wanaonitamani?kama unamtafuta mbaya na adui yako aliesababisha mm nifanye nilichofanya jana kaangalie kwenye kioo utakae muona ndio huyo adui yako.aliongea mengi sana nikaona basi sababu mm ndio sababu ya yote acha niombe msamaha yaishe,nikasema mme wangu samahani sana nilikua sina nia mbaya kukufata ni vile niliskia kwenye simu sauti ya Yule dada.akasema ww unafkir wao hawatak kuolewa?au hawataki kuwa na mm?jitambue uko na mwanaume handsome,msomi na nina kazi nzuri na pesa kila mwanaume ana ndoto ya kuwa na mwanaume kama mm,na kila mwanamke anayeomba maombi ya kupata mme anapata picha yangu anataka kama mm.ww nimekuoa unahangaika nn?Nilizidi kuomba msamaha na kusema sitorudia tena mme wangu nimekosea samahani sana.akasema yameisha sawa nimekusamehe.nikasema asante mme wangu.akasema haya naenda onana na washkaji mara moja nakuja sasa hivi,niaksema sawa,aliondoka na gari lkn hakurudi tena siku hio,akarudi kesho yake akiwa na kitenge doti moja na keki kwenye kibahasha na mm sikwenda kazini siku hio,sikupendezwa kabisa na kulala kwake huko lkn sikusema chochote,akasema samahani mke wangu jana tulienda mji wa pili na rafiki zangu tukachelewa na tulilewa ikabidi kila mtu achukue chumba chake tulale,nikasema lkn ungenijulisha sasa mme wangu.akasema umeanza na wewe gubu nimeshakwambia nililewa sasa unataka ningetoaje taarifa?aaaaaaghhhh akatupa kile kitenge na kifungashio cha keki kwenye sofa akaenda zake chumbn.sikuelewa kabisa hizi tabia zake.ilikua kila siku anampya na safari zisizoisha kila akiwa na off.nilichoka sana na tabia zake.siku moja nilitoka kazini nilikua nasumbuliwa sana na tumbo hio siku,nilirudi nyumbn nikamkuta seblen,alivoniona kasem aehee bora umerudi vipi kwanza?nikasmea naumwa sana tumbo leo,akasema pole bora umekuja mana hapa nasafir naenda Dodoma muda huu na rafiki zangu.niaksema lkn mm naumwa,akasema wewe si umetoka hospitral na wewe si ni dokta sasa unaniambia mm nifanye nn?aaaaaaghhhhh,nilikwazika niaksema mme wangu hio safari yako ina umuhimu gani mpaka uniache mwenzio naumwa uondoke?akasema unasemaje wewe?unanidharau si ndio?alinisogelea akanishushia kipigo cha maana kisha aakaningia ndani akachukua lasket yake akatokomea zake.nililkia sana tena siku hio sikuwa haya na pesa kabisa nae hakuniachia hata mia.nililia nikanyamaza mwenyewe nikafunga zangu mlango mana niliamua kulala kabisa japo ilikua saa 10 jioni,niliingia chumbn taa zikawa haziwaki nikaenda jikon inawaka,mmh kuna nn?nikajaribu kuweka simu chaji nayo haiwaki nikaenda seblen nikwasha tv haiwaki jikon tu ndio kuko sawa.mmh kun shida gani?niliwaza.nikakumbuka kuna nes alikua anasumbuliwa na umeme akapata fundi wa kitaa tu akamsaidia hivo nikampigia akanipa namba akasema wasiliana na huyu fundi anaitwa Jeon.nikasema sawa.niliipiga ile simu akapokea kaka mmoja anaongea lafudhi ya kilugga hivi,mmh huyu ndio fundi kweli?ngoja nione.nikaongea nae anikamuelekeza akasema anapajua anakuja,nikasema sawa.nikamrudia nes alienipa namba nikasema wewe unauhakika huyo mtu ni fundi?akasema jeon?ni fundi sana tu na amesomea kabisa VETA aba vyeti vyake na anaduka la umeme pale chini kama unapajua wanapouza sana machungwa pale wamepanga na mafuta pale kuna duka la vifaa sio kuwa sana ila ndio yeye.nikasema mmh hata simujui ngoja aje.nikakata simu,baada ya kama dakika 10 niliskia pikipik inapaki mana mm sina geti kwangu pako tu.kabla hata sijachungulia niliskia hodi,nikaenda kufungua akaingia mkaka mmoja mrefu sio mweupeee na sio mweusi rangi ya kati amevaa prova na jeans yake na raba,yupo kati sio msafii na sio mchafu tupo na beg la mgongoni kuu kuu hivi,akasema mm ndo jeon fundi umeme nikasema karibu,akasema wapi pana shida?nikasema chumbn,akasema chumbn kwako?nikasema ndio,akasema mmmh ngoja kwanz,akapiga simu mahali,ikapokelewa nikaskia anasema dogo ebu njoo hapa nilipokuelekeza mara moja……..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni