BETWEEN SISTERS AND SECRET 3--4 Chapter 3 Mira aliingia ndani akafunga mlango
"Sikuwahi kufanya kitu kama hicho, kwanini unanifanyia hivi jamani? Ni Joel alinitongoza yeye mwenyewe na nilimkatalia."
Mia alianza kulia.
"Usiniletee uchuro hapo nje, kama unataka kulia nenda huko sio hapa. Na kama kipaji chako ni kulia basi nenda kalie misibani watakulipa."
Mira aliongea akiwa ndani.
Wapangaji wengine walimuonea huruma Mia. "Mia njoo huku."
Shufaa alimshika mkono Mia akaingia naye kwake chumba chake.
"Acha kulia basi, unajua utapata homa bure." Shufaa alijitahidi kumbembeleza Mia.
"Naumia sana Shufaa, sikuwahi kutetemeka. Dada yangu atanichukulia mimi kama takataka."
Mia alizidisha kulla.
"Acha basi kulia shoga yangu, achana naye. Huenda kuna mambo ya kazini yamsumbua,
ndomana anataka kumalizia hasira zake kwako."
"Natamani ingekuwa hivyo Shufaa, maana yangepita, lakini chuki yake haikuanza leo wala jana na sijui itaisha lini."
"Sasa utafanya nini kipenzi?"
"Nataka kuondoka, bora nirudi nyumbani siwezi
kuishi maisha ya kunyanyasika." Mia alifuta machozi, ni wazi aliamua kufanya
uamuzi.
"Bora iwe hivyo, maana hapa unateseka tu bure.
Ila nitakumiss sana Mia wangu."
Shufaa alivuta shavu la Mia. "Hata mimi nitakumiss sana."
Mia na Shufaa walikumbatiana.
Kama alivyopanga, Mia alisubiri Mira ameenda kazini, alichukua begi lake akaondoka.
"Babaa..."
Mia alimkimbilia mzee Charles akamkumbatia, "Mira mbona hakuniambia kama unarudi leo, au mmeshagombana tena?"
Mzee Charles alimuuliza Mia.
"Wala hatuwezi kugombana, nimeamua tu kurudi baba. Maisha ya kule sijayazoea hata kidogo." Mia alikaa kwenye mkeka.
"Ni sawa, kama hukupapenda kule unaweza kufanya biashara hapa hapa, nitakupa mtaji." Alisema mzee Charles.
"Asante sana baba, ndomana nakupendaga." Mia alifurahi sana, aliamua kuanza biashara ya kukaanga mihogo.
"Mia unajua hii kazi huendani nayo hata kidogo." Alisema Furaha rafiki wa Mia.
"Kazi ni kazi tu shoga yangu, ilimradi mkono uende kinywani. Nikianza kuchagua kazi
nitafanikiwa kweli?"
"Ngoja kwanza nikupe habari njema."
Furaha aliongea huku anakula mihogo.
"Mmmh, niambie shoga yangu, nakusikiliza."
Mia alikaa vizuri kumsikiliza Furaha.
"Kuna mama mmoja anataka mtu mwingine wa
kumuuzia duka lake la simu. Kama upo tayari tunaweza kwenda pamoja ukaanze kazi, hata
mimi nafanya kazi hapo hapo." "Unasema kweli Furaha?"
Mia alikuwa haamini hata kidogo.
"Kweli, sio utani. Kama upo tayari hata kesho tunaondoka, utaanza kazi yako mapema na
mshahara sio mdogo. Namuelewa sana mama G, sio mtu wa ahadi za uongo."
Alisema Furaha.
"Mimi nimekubali, lakini mpaka niongee na baba kwanza. Siwezi kufanya uamuzi mwenyewe." mimi
"Hakuna shida, mimi nitaongea na mama G asimpe nafasi mtu mwingine."
Mia hakutaka kuchelewa, alienda kumwambia baba yake kila kitu.
"Mimi siwezi kukukatalia mwanangu, lakini
nataka tu uwe muangalifu. Na kama ukishindwa rudi nyumbani, usijilazimishe kukaa kwenye miji ya watu."
Aliongea mzee Charles kwa msisitizo.
"Sawa baba, nimekuelewa na nakuahidi
nitakuwa salama, na kikitokea chochote ni lazima nikujuze."
Mia alifurahi sana.
Kesho yake asubuhi sana aliondoka pamoja na Furaha kuelekea Dar es Salaam.
"Mia... twende basi, usibaki kushangaa majengo, tutachelewa ujue."
Furaha alimvuta mkono wa Mia huku anacheka. "Heeh shoga kweli, Dar es Salaam sio Muheza, ona kulivyo na magorofa kila kona hadi shingo
inauma kwa kuangalia juu."
Mia aliongea huku macho yake yakitazama juu. "Sasa hapa bado utazidi kujionea vitu vya kila aina na vitakushangaza."
Furaha alimshika mkono Mia, wakaingia kwenye duka kubwa la simu lililoitwa NextGen Phones.
Walimkuta mwanamke mmoja wa makamu alikuwa amependeza sana na kulikuwa na
wafanyakazi wengine wawili.
Chapter 4
Waliingia kwenye duka kubwa la simu lililoitwa NextGen Phones. Walimkuta mwanamke mmoja wa makamu, alikuwa amependeza sana na
kulikuwa na wafanyakazi wengine wawili.
"Karibuni, wewe ndio Mia?" aliuliza Mama G. "Ndiyo, ni mimi. Shikamoo. Mia alijibu kwa heshima, alijikuta akitetemeka kwa hofu.
"Marahaba, una jina zuri kama wewe
mwenyewe. Hapa dukani kwangu sipendi uvivu wala uongo. Ukifanya kazi kwa bidii utafurahia, maana huwa sivunji ahadi zangu. Lakini ukiwa mvivu au muongo nitakufukuza kazi." Aliongea Mama G kwa msisitizo huku
akimuangalia Mia usoni. "Sawa boss, nimekuelewa vizuri." Mia alijibu kwa
sauti ya chini.
"Madam, Mia ni mpole na ana aibu kidogo, ila nikuhakikishie kuwa ni mchapakazi sana. Akikaa hapa kwa muda ataozea tu."
Furaha aliongea huku ameshika mkono wa Mia. Mia alitabasamu kwa aibu.
"Sawa, kesho unaanza kazi ila kwa leo Furaha atakuonyesha mazingira ya hapa dukani. Lakini
Mama G alimuangalia Mia akatabasamu.
kumbuka, hapa Dar kila mtu anahangaika kutafuta maisha. Usimuamini mtu yoyote, hata rafiki. Na hao wanaume ndo usiwaamini kabisa,
wengi ni waongo." Mia akatikisa kichwa.
"Nimekuelewa madam." Alijibu Mia kwa sauti yake ya upole.
"Sawa, nadhani tumeelewana na nimemaliza kuongea, mnaweza kwenda."
Mama G aliendelea kukagua duka.
"Mia twende huku nikuzungushe, unatakiwa. kujua simu zilizoka kwenye upande wako wa mauzo kwanzia aina ya simu, bei yake, matumizi yake na ubora wake kushinda aina nyingine ya simu ili kumshawishi mteja anunue." Furaha aliongea huku anamuonyesha Mia aina za simu.
"Kwahiyo mimi nitakuwa nauza upande huu peke yangu?" aliuliza Mia kwa hofu.
"Ndiyo, kila mfanyakazi ana upande wake.
Kwenye hili duka kama unavyoona kuna sehemu nne, na wafanyakazi wanatakiwa wanne. Kwahiyo kila mmoja ana sehemu yake."
"Duuh, mbona nimeanza kuogopa, nitaweza kwell?"
Mia aliongea huku anamuangalia Furaha usoni. "Usijali bhana, utaweza tu. Hata mimi nilikuwa
hivyo hivyo, lakini saizi kila kitu ni rahisi. Cha kufanya ni kuzingatia unachofundishwa."
"Sawa, nitazingatia."
Furaha alimuonyesha Mia kila kona ya duka, alimuelezea aina zote za simu atakazokuwa
anauza.
"Sasa tumemaliza upande wa dukani, twende nikakuonyeshe upande wa nyumba za wafanyakazi."
"Kumbe kuna hadi nyumba za wafanyakazi?" Mia alibaki mdomo wazi.
"Ndiyo, madam ni mtu mzuri sana. Anatujali kama watoto wake, ila ndo kama alivyosema, hapendi uongo, udokozi na uvivu. Ukimuudhi tu-
kazi huna."
Alisema Furaha.
"Nitajitahidi kufanya kazi vizuri." "Twende huku."
Furaha alimshika Mia mkono, walipanda daladala, hawakuchukua muda mrefu walishuka. "Tumefika."
Furaha alitoa funguo akafungua mlango. "Hee, hii ndo nyumba mnayoishi? Mbona ni nzuri sana."
Mia alianza kukagua kila kona.
"Kwa maisha anayoishi Mama G, hiki ni sawa na kibanda cha mlinzi shoga yangu, upo?"
Furaha alikaa kwenye kiti.
"Weee, usiniambie, natamani hata kuona hapo anapoishi."
Mia alienda kukaa pia.
"Utapajua tu hata usijali. Kila mwisho wa mwaka, wafanyakazi huwa tunaenda kwenye sherehe za mwisho wa mwaka, watu wanakuwa ni wengi sana siku hiyo."
"Wote ni wafanyakazi?β aliuliza Mia.
"Ndiyo. Mume wa Mama G. Mr. Maximilian, ni tajiri sana. Ana makampuni makubwa, kwahiyo
lazima wafanyakazi wawe wengi sana." "Mmmh, inaonekana familia yao wanajiweza sana, sio kama sisi."
"Hao ni wazazi tu, wana mali nyingine. Hivyo na ukija kwa watoto wao, kila mmoja ana kazi yake na anaingiza mabilioni ya pesa. Mtoto wao wa
kwanza ni Gavin, yeye ni daktari ana hospital yake binafsi-tena sio hivi vya uchochoroni, hospital haswaa. Wa pili ni Gael, yeye ni CEO wa kampuni ya Purenex, na wa tatu ni Gian, yeye ni
mwanamitindo maarufu." "Usiniambie, kumbe wenzetu wana maisha, sisi wengine tunasindikiza tu." "Ndo hivyo shoga yangu, na sisi tuhangaike.
kutafuta vimiambili mia mbili tulishe familia zetu, tusifanye mchezo. Njoo nikuonyeshe chumba." Furaha alienda kumuonyesha Mia chumba.
Kwa siku hiyo walipumzika, na kesho yake kazi Ilianza.
Mia alipata shida sana kuhudumia wateja, lakini alizoea. Ulipita mwezi mmoja Mia akiwa anafanya kazi kwenye duka la Mama G, wateja walimpenda kwa tabasamu na heshima yake. "Mia hadi nakuonea wivu, wateja wamekupenda kwa siku chache tu ulizokuwa hapa,"
Alisema Dora.
"Hata wewe pia wateja wako wanakupenda." Aliongea Mia huku anatabasamu.
"Mmmh, sisi tulichukua muda mrefu sana mpaka kuzoeleka na wateja."
Alisema Judith...
"Kila mtu na nyota yake bibi wee, usijifananishe na mwenzio."
Aliongea Furaha kwa utani, wote walicheka.
Siku moja, Mia alikuwa na wateja wengi sana. "Opps, nimemaliza sasa. Miguu yote inauma." Mia alikaa kwenye kiti chake.
"Inawezekanaje duka kubwa kama hili hamna mfumo wa risiti? Mnafanya kazi kwa kubahatisha si ndio?"
Mia alishtuliwa na sauti nzito ya kiume.
Mia aligeuka haraka, mapigo yake ya moyo yaliongezeka kwa kasi.
Mbele yake alisimama mwanaume mtanashati.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni