VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 04
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA.......
"Manka wewe wa kunijibu mie hivyo?"
"Kibaya kipi hapo si nimekuuliza tu"
"Ukiwa na maana?"
"Maana yangu ni kwamba kuzaa huzai. Bwana unae miaka miwili sasa ila hujawai shika mimba hata ya bahati mbaya kwa kisingizio cha kusema kwamba mpaka unioe. Wewe huyo ukiolewa sijui"
Nilishangazwa na kauli ngumu za Manka na alivuka mikapa mpaka kunitukana eti mie mgumba. Uvumilivu ilinishinda nilujikuta nampiga Manka. Nilimtembzea vibao vya maana.
"Unanipiga mimi, sasa ngoja nikuonyeshe" Manka aliyasema hayo na baada ya hapo alichukua simu yake.
Sikuwa na haja ya kuendelea kubaki chumbani kwake. Nililudi chumbani kwangu. Moyo wangu ulikuwa na maumivu makali nisingeweza kujizuia kulia. Nililia kwa uchungu haswaa.
"Mbona kama vile Manka amedhamilia kulisambalatisha penzi langu. Hapana Sony ni wangu sitokubali, huyu ni mwanaume wangu na naweza kusema ni mume wangu maana tayari ameshanitolea mahari na pete ya uchumba ipo kidoreni mwangu" niliyasema hayo huku naitazama pete ya uchumba niliyovalishwa na Sony mwezi mmoja tu uliopita.
Basi nikiwa nimejilaza kitandani kwangu mlango ukifunguliwa gafla aliingia Sony akiwa amefulu kwa hasira.
"Karibu baba watoto wangu". Nilimkaribisha kwa tabasamu ila tabasamu hilo niligeuka kuwa kilio.
Aiseee nilitembezewa mkongoto huo uwiiii!
" kwaajili ya Manka unanipiga mimi?" Nilimuuliza Sony baada ya kutosheka kunipiga.
"Na nitaendelea kukupiga mbwa wewe. Kwanini unampiga mwenzio na unajua anaumwa"
"Sikudhamilia kumpiga ila alinijibu vibaya na mimi pia nina moyo sio chuma, Sony mpenzi wangu mbona imekuwa hivyo. Hujali chochote kuhusu mimi. Hunipi muda wa kuongea wala kujitetea. Inamaana mimi huyu nimekuwa mbaya gafla tu kwako?"
"Usiku wa leo nilitegemea ungekuwa usiku wa pekee sana kwetu ila umekuwa usiku wenye maumivu sana kwangu. Kosa langu liko wapi eti?"
Namna nilivyokuwa naongea huku nalia Sony aliingiwa na roho ya huruma juu yangu. Niliona amelegeza nyuso zake ananitazama kwa huruma namna ninavyolia kwa uchungu.
Alinisogelea kwa ukaribu alinyanyua mkono wake anifute machozi ila kabda hajafanya hivyo Manka aliingia chumbani kwangu.
Alijifanya anaugulia tumbo. Sony alimkimbilia haraka.
"Unajisikiaje. Nikupeleke hospitali?".
" mbwa huyu ulifaa hata kumpeleka polisi" Manka aliongea hayo kwa hasira.
Sony alimtoa chumbani kwangu. Sikujua kuna nini kinaendelea kati ya Sony ma Manka.......
Kesho asubuhi niliamka nikajiandaa kwenda kazini nilipokuwa tayari nilipita chumbani kwa Manka kumjulia hali.
"Sony aliniambia nikwambie uniandalie chai kabda hujaenda kazini"
"Hivi ni kweli unaumwa?" Nilimuuliza Manka.
"Wewe unanionaje?" Alinijibu. Niliangalia saa yangu ya mkononi. Muda ulikuwa ushaenda. Sikuwa na namna niliingia jikoni nikabandika chai fast baada ya hapo nikaondoka.
Nafika kazini tu nikaitwa ba boss.
"Mbona hujamuandalia mwenzio chai na unajua kuwa anaumwa, kwaiyo kazi ni bora sana kuliko utu wa mtu tena ndugu yako" Nilipoingia ofisini tu kabda ya salamu kutoka kwa boss wangu ambaye ni Sony mchumba angu na mume wangu mtarajiwa.
"Kama chai mbona nimempikia Jamani"
"Bila kitafunwa?"
"Mkate upo" Nilimjibu.
"Kaendelee na kazi zako"
"Sony naomba nizungumze jambo moja hata kwa dakika moja". Niliona hiyo ndiyo nafasinya kumwambia Sony nina mimba yake...........ITAENDELEA..........
SIMULIZI :
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehemu