PENZI LA OMBA OMBA😍❤️😍❤️😍❤️ Sehemu ya 08
Nilishangaa sana anashida gani, kwa maana alishasema mara kadhaa kuwa hawez kuwa na mahusiano na mimi na kila dakika ni warda, warda, sasa mbona yuko kama ananionea wivu hivi….
Bsikutaka kuendelea kujiuliza maswali sana, na badala yake nikaendelea na majukum yangu, na kwenye majira ya kama saa tisa mchana, nikashangaa mlango unagongwa kwenda kufungua, nashangaa nakutana na shureymu, aliponiona akanikumbatia kisha akasema “warda amekubali nimuoe, embu nipikie nile nishibe ili nikampropose warda wangu, nan ataman iwe surprise kwa maana sikuwah kufikiria kama mwanamke ambae nimemuangaikia sana, kama atakubali kuolewa na mimi….
Hata sikumjibu nikaingia jikoni kisha nikampikia, na mara baada ya kupika, nikamtengea, akala pale haraka haraka kisha akanambia niombee ile pete alioinunua, isije ikakataliwa, basi nikamuombea pale, kisha akaondoka zake…
Ila baada ya kama lisaa alirudi nyumban kwangu akiwa ameshikilia kile kibox cha pete, akaniangalia kisha akasema ‘ ni kweli nilitakiwa kumuacha warda, muda mrefu sana uliopita kbala hajazidi kuubabuwa moyo wangu, nikamsogelea na kumkumbatia kwa maana niliamini kuwa ni lazima atakuwa kwenye maumivu makali sana, nikashangaa shureymu anaanza kulia huku akisema “ nimemkuta akifanya mapenzi, yaan alikuwa anafanya mapenzi na mwanaume mwingine salha, moyo unaniuma sana, yaan mimi najiandaa kenda kumuoa yeye analala na mwanaume mwingine, na mwanaume mwenyewe ni mzee, sijui sote anatichuna au vipi, kwa maana angalau hata angekuwa kijana ningesema kuwa anamvuto kuliko mimi, ila ni mzeee, ni mzee mno salha, mungu wangu moyo wangu uliingia kwa gold digger, naumia sana, akawa anaendelea kulalamika shureymu na sikuwa na lakufanya zaidi ya kumbembeleza pale, nikamtoa mtoto kitandani kisha nikamuambia alale pale atulize moyo na akili yake, kweli akakubali na baada ya dakika chache akawa tayar ameshapitiwa na usingizi…..
Alikuja kuamka kama saa mbili usiku, nilikuwa tayar bimepika ila hata hakuweza kula ikabidi nianze kumpigia story za kuchekesha, kwa mara ya kwanza hakuwa anacheka ila baadae akachangamka, tukawa tunafurahi pale….
Siku hio hakutaka kuondoka kabisa nyumban kwangu, basi tukashinda tunapiga story, kwa maana sikuwa najiamin kulala na mwanaume chumba kimoja alafu msifanye kitu,basi tukapiga sory mpaka asubuh na kesho yake ilikyuwa ni jumapili, shureymu akataka tutoke out, hapo Yule mwanaume wangu nachart nae tu, maana nilimuambia kuwa naishi kwetu, hivyo kuna wakat nitakuwan siwez kuongera nae, alionekana kunielewa, ingawa alikuwa anaenda sana kuongea na simu zaidi ya kuchart….
Basi tulienda sehemu mbali mbali na shureymu pamoja na mtoto, mtoto alikuwa anampenda sana shureymu na wakat huo mwanangu tayar alikuwa ameshafika mwaka, na kila ambae alituona alijua kuwa mim I na shureymu ni wapenzi na wengine wakawa wanahisi kuwa sisi ni wanandoa na saidi ndio mtoto wetu…
Sasa muda wmini saidi alikuwa anashinda na mimi, yaan tunapika pamoja tunakula pamoja, yaan nyumban kwake alikuwa anenda kulala tu, basi maisha yetu yakawa yanaenda hivyo, na shureymu hakuwah kuonesha ishara zozote zile za kunitaka, ingawa nilikuwa nampenda, ila nikaamua na mimi kumchukulia kama kaka, na niweke mambo ya mapenzi pemben, na kweli alikuwa anakuja tunapika tunakula na maisha yetu yakawa yanaenda hivyo….
Siku moja nikawa nimekaa na shureymu nikaona simu ya shureymu inaita na aliekuwa anapiga alikuwa ni mama yake, akawa anaipokea kwa wasiwasi sana, nikawa namsikia mama yake akisema “ nilazima kati ya mwaka huu au mwakani uwe tayar umeshaoa, na uwe na mtoto, maana hata kama wewe ni mchapakazi kiasin gani, ila moja ya sharia ya kurithi makampuni ya baba yako ni kuwa umeoa, akasema mama yake shureymu kwa sauti ya ukali kidogo…..
“ sijampata sasa mwanamke wa kumuoa mama, kwa maana kama ningempata mwanamke yoyote ambae atakuwa tayar kuolewa na mimi basin ningeshamuoa, ila badpo sijapata, akawa anajitetea shureymu……
“unamiezi miwili, kama hujaoa nitakuoea mwanamke ninae mtaka mimi, akasema mama yake shureymu kisha akakata simu…
“ yaan mimi sijui natakiwa kupumulia wapi, kwa maana familia yangu inanisumbua, mapenzi yananisumbua, sasa sjui hata napaswa kukimbilia wapi, akawa anasema shureymu kwa sauti ya uonyonge…
“ sasa miezi miwili utampata nani, ila ndio uanze kupambana upate mwanamke ambae hata ikitokea la kutokea unajuwa kuna mtu wa kumpeleka mbele ya macho ya mama yako, nikasema…
“ sawa ngoja nipambane, akajibu shureymu
Sasa tukiwa pale si muswaabu akanipigia simu, nikaongea nae kwa dakika chache kwa maana alikuwa anataka kutoka na mimi, kwa sababu toka ile siku ya kwanz tuliyoonana hatujawah kuonana tena zaidi sana tulikuwa tunaongea tu…
Ikabidi nimuombe shureymu akae na mwanangu maana mm nataka kutoka, alikubali kwa sababu sio mara ya kwanza kukaa nae ikiwa sipo, basi shureymu akamchukua mtoto na kutoka nje ili nivae, na kweli siku hio nikavunja kabat, sasa wakat natoka nashangaa shureymu ananifata kisha akaniuliza kwa sauti ya ukali kuwa “ unaenda wapi?....
“ kukutana na mtu, kwani kuna shido, nikasema ..
“ mwanamke au mwanaume? Akauliza..
“ mwanaume ofcoz, Yule shemeji yako wa siku zile, nikasema…
Akaniangalia kwa hasira kisha akaniambia, haya nenda, mm hata sikumjali nikaupara zangu nimetoka huyo, nafika nje nikamkuta muswaabu akiwa amepaki gari ananisubiria…
Kumbe shureymu hakutaka kukaa kinyonge bana, si akaanza kunifuatilia, nay eye akamuita dereva wake na kumuagiza atufatilie, mm wakat huo sina kitu ninachokijua…
Basi tukafika sehemu moja ilikuwa ni tulivu sana, tukawa tumekaa tunapiga story, tukaagiza vinywaji na chakula, tukawa tunakula taratibu huku tunapiga story, na sio siri alikuwa ni mcheshi sana, kwa maana niliinjoy sana kampan yake, kumbe shureymu yuko maeneo yale, na kuna muda nikawa nasikia sauti kama ya mtoto wangu analia, ila nikawa najiambia kuwa ni mawazpm yang utu, kwa maana sikuamin kama shureymu anaweza kunifata…
Basi tukakaa pale tunaongea kwa karibu masaa manne, mpaka kagiza kakaanza kuingia, ndio muswaabu akawa anataka kunipeleka nyumban, na kweli alinipeleka mpaka nyumban kisha akaondoka zake, na akanambia kuwa ananipenda na hana shida atasubiria jibu langu hata kama ni baada ya muda gani, ila alikuwa anaamin kuwa nitamjibu vzr, basi nikamtoa hofu pale kisha tukaagana…
Ila sasa wakat naiia ndani nikashangaa nakutana na sura ya shureymu kanuna balaa, akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema ‘ mtoto kalala, kisha akawa anaondoka zake…
“ shida nini, mbona kama haupo sawa? Nikauliza…
Nikashangaa anacheka kwa dharau kisha akasema “ unavyoongea ni kama unanionea huruma, kisha akaondoka zake….
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni