PENZI LA OMBA OMBA😍❤️😍❤️😍❤️ Sehemu ya 11
“hivi una shida gani wewe, kwanin I hutaki kuniona na mm ninafuraha, kwann hutaki mimi niwe na mahusiano lakin shureymu, nikaanza kulalamika…
“ mm sijakuzuia kuwa na mahusiano ila Yule mwanaume anaonekana kabisa ni muhuni ndio maana najitahidi kukuweka mbali nae, kwa maana asije kukuumiza bure, akasema shureymu…
“ muhuni!, embu nambie ulimuona wapi mpaka ukahisi ni muhuni, shureymu unajua kuwa muswaabu ananipenda sana, kwanini sasa unataka nimkatili mtu anaenipenda kiasi chote hicho, nikaanza kulalamika…
Shureymu akabana pua kisha akasema “ unajua kuwa muswaabu ananipenda sana, hivi wewe bnt unawajua wanaume vizur, yaan hapo ni unaona kama anakupenda kwa sababu hajalala na wewe, Ila akishalala na wewe ndio utaelewa ulikuwa na mwanaume wa aina gani, kwanza nasikia kichwa kinaniuma kanipashie maji ya moto uje kunikanda, akasema shureymu na sikumjibu, na wakat huo huo nikaenda jikoni na kupasha maji, kisha nikaenda kuchukua taulo na kuanza kumkanda, nikawa namkanda pale, alikuwa kama anasisimka flan, ila mm nilikuwa kimya namuwaza muswaabu wanu, na alijua kabisa kuwa sipo sawa, akawa kama anataka niwe sawa, ila tatizo lake sio muongea ji sana, kwa maana alikuwa kama anataman kunichekesha ila ndio hivyo niliweka ngumu nikawa sicheki kabisa, mwisho akanigeukia na kuniuliza “ una shida gani mama saidi...
“ kuna sehemu nataka niende, kama hutajal naomba unisaidie kukaa namtoto, nakuahidi kuwa sitachelewa kuerudi nikasema, nikashangaa shureymu kanyong’onyea kisha kwa sauti ya unyonge akasema “ haya nenda, nitakaa na mtoto kama unavyotaka…
Sikutaka hata kujiuliza mara mbili, kwa maana dakika hio hio nikajiandaa kisha nikatoka, kumbe nilikuwa namuacha shureymu katika hali mbaya ila sikuwa najua, basi nikaenda kukutana na muswaabu, aliponiona akawa na hasira sana , kisha akawa ananiuliza Yule ambae alisikika kwenye simu ni nani, na kwanini nilikiwa sipatikani….
“ naomba unisamehe kipenzi change, Yule ni kaka yangu, huwa hatakag kabisa niwe kwenye mahusiano, hata jana ulipopia simu yeye ndio aliizima na akaichukua, akisema kuwa nitaharibikiwa, ila mm nakupenda sana muswaabu, ndio maanan nimetorika nyumban ili nije kukuona, nikawa nasema…
Muswaabu akashusha pumzi kisha akasema “ haujui kiasi gani moyo wangu ulikuwa unauma, haujui kiasi gani sikuwa na raha, usirudie tena kunikalia kimya mamaa, kwa maana utaniua, yaan ulikuwa unaniteketeza kidogo kidogo salha wangu, akasema muswaabu…
Tulipana tukutane kwenye restaurant moja uchwara, maana ndio ilikua karibu na anapoishi, akasema tiutoke sasa out inayoeleweka, nikakubali, ila wakat tunatoka nikakutana na gari la shureymu nje, ila nikapuuza, nikahisi labda ni mtu mingine ila magari yanafanana tu, kwa maana sikuwa nafikiria kama anaweza kunifuata…
Basi tukaenda kwenye restaurant nyingine ilikuwa na hadhi flani hivi, yaan tukaagiza chakula tukawa tunakula na kutaniana,l yaan wakat wote tulikuwa tunacheka, ila sasa kuna muda nikasema nianalie nyuma, nikamuona mtoto kama wangu kanigeuzia mgngo, lakin namna alivyo na hata nguo alizovaa zilikuwa kama za mwanangu, alikuwa amekaa na kijana pemben yake, kuangalia viatu, nikashangaa naona viatu vya shureymu, “ kumbe kanifata? Nikajikuta naropoka…
“ nani tena huyo kipenzi change, akauliza muswaabu…n
“ kaka yangu kaamua kunifata mpaka huku, sasa shureymu akahisi tumemuona akaja na mwanangu mpaka kwenye meza ambayo nilikuwa nimekaa mm na muswaabu kisha akatusalimia na kuchukua kiti na kukaa…
“ salha ila siuliambiwa na mama kuwa ukae tu nusu saa, kwann umekaa na huyu boya wako masaa yote haya, akasema shureymu, nikashangaa kwann shreymu anaongea kana kwamba anataka kumkera muswaabu, na muswaabu akatabasamu kisha akasema “ shemu kwani hutaki mdogo wako awe na mume jaman, mm nampenda sana salha, na nasubiri ruhusa yake tu, ili niweze kumuoa, akasema muswaabu…
Shureymu akacheka kwa dharau kisha akasema “ ety kumuoa, unafikiri kuwa ndoa ni jamboa rahisi, au unahisi ndoa ni kama makalio kila mtu anayo, mwanaume mwenyewe una macho ya kurembua, una dimpos una mwanya, wewe ni mwanaume au ni pisi kali…
“ una sema nini wewe , akaongea muswaabu kwa ukali…
“ kwanza salha alikuambia kuwa alizalia shule, na huyu mtoto unaemuona ni wake, na hapo unavyomuona alikuwa anatakiwa awe kidato cha tano ila uhuni ukamponza akanzaa kabla ya umri wake, akasema shureymu, nikashangaa kwa nn anasema yote hayo na wakat anaujua ukweli wote…
“ salha embu nambie ukweli, huyu mtoto ni wakwako? Akauliza muswaabu…
“ naomba nikuambie kila kitu muswaabu, naomba tukae tuzungumze na nina uhakika utaelewa namna ambavyo nimempata huyu mtoto na sio kama kaka shureymu anavyosema, nikaanza kujitetea…
“ mahusiano yanakaribia kumaliza miezi mitano, kwann hukuniambia kuwa una mtoto salha, unajua nilikuwa nawaambia nn marafiki zangu, nilikuwa nawaambia kuwa naenda kuoa kabint kabikra kumbe umetumika kuliko maelezo, yaan kuanzia sasa mm na wewe basi, akasema muswaabu kisha akasimama na kutaka kupondoka, nikamshika mkono, kwa maana nilikuwa nataman kumsimulia kila ambalo nimelipitia kwenye maisha yangu, ila nikashangaa shureymu amenishika mkono kisha akasema “ embu tulia ww, unataka kumfata Yule boya wako badala ya kumbeba mwanao na twende nyumban…….
“ hivi shureymu una nini, kwann lakin unaniharibia kwa mwanaume ninaempenda, alafu embu nambie, ni kitu ani kilichokufanya mpaka ukanifata wewe na mtoto mpaka huku, nikaanza kulalamika…
“ kwasababu sikuwa namuamin mwanaume ambae ulikuwa nae, kwasababu sikuwa naamin kama ni mwema kwako, ndio maana nikaona nikufate, akaanza kujitetea shureymu…
“akiwa mwema au akiwa muovu wewe shida yako n inn, maana mm nampe…, kabla sijamalizia ninachotaka kuongea nikashangaa natulizwa na busu moja matata, na vile tulikuwa kwenye restaurant tukashangaa kila mtu aliekuwa pale anapiga makofi, hapo shureymu amenishika mm na mkono mmoja na mkono mwingine amemshika mtoto………..
…
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAAAAAAAA FULL
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni