VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 05
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA.......
"Ni muda wa kazi sasa. Uliniambia jana una mazungumzo binafsi na mimi. Nafikiri tutazungumza badae"
Sikuwa na namna zaidi ya kutoka ofisini kwa Sony.
Nilienda eneo langu la kazi kila nilipojitahidi kufanya kazi zangu akili yangu haikuwa sawa kabisa.
"Una nini leo Nice?" Sophia rafiki yangu na pia ni mfanya kazi mwenzangu aliniuliza.
"Nipo sawa"
"Nakufahamu lakini ila kama umeamua kunificha naamini ni jambo lako binafsi ila kuwa makini usiharibu kazi."
"Kiukweli simuelewi binamu".
"Manka?"
"Yeah"
"Yule ndugu yako hayupo sawa. Mala nyingi napokuja kwako kuna matendo naona anayafanya si sawa kabisa sema sijui ni namna gani mnaishi wenyewe nilichagua kunyamaza kimya nisiwafitinishe ndugu"
"Nitakueleza badae".
Tuliendelea na kazi. Majira ya saa nane mchana Manka alikuja kazini kwangu.
Kwakuwa mimi ni Secretary ilikuwa lazima apitie kwangu kama anataka kuonana na Sony.
" inaendeleaje?" Nilimuuliza kwa kujali ila alinijibu kwa mkato.
"Salama. Nataka kuonana na Sony.
"Kuna tatizo?" Nilimuuliza
"Mimi kuonana na Sony mpaka wewe ujue?, utaacha lini wivu wa kijinga wewe"
"Kumbuka mimi na wewe tupo vipi. Ni miiko mashemeji kuzoeana kupitiliza, alafu ujue kabisa unaongea na dada yako kwaiyo uwe na nidham.
"Unasemaje wewe. Ngoja sasa nikuonyeshe"
Manka aliyasema hayi na baada ya hapo alianza kulia kwa sauti huku anaugulia tumbo. Wafanya kazi wote walikusanyika eneo hilo.
"Kuna nini Nice?" Sophia aliniuliza.
"Sielewi ana shida gani na mimi. Huwezi amini sijamgusa hata ukucha tu"
Muda huo huo Sony alifika eneo hilo alimkimbilia Manka pale chini ni kama vile alikuwa amepagawa. Watu wote tulipigwa na butwaa.....
"Nini kimetokea?" Sony aliuliza na macho yake yalielekea kwangu. Kabda sijamjibu Manka alijibu.
"Nice amenipiga tumboni. Sijui kwanini ananitesa amesahau kama mama yangu na baba yake ni mtu na dada yake. Amekuwa katili sana kwangu". Manka aliongea huku anajiliza.
Sony aliniangalia kwa hasira, alimbeba Manka mikononi mwake. Wafanyakaza wakaachia njia wapita. Mie nilikuwa nimesimama kama mstimu jamani siamini nachokiona kabisa nilistuka tu nimesukumwa huko nikaenda kudondokea kiti.
Nilianza kuugulia maumivu ya tumbo.
"Pole Nice nashindwa hata niseme nini juu yako kipenzi" Sophia aliongea hayo huku ananifuta machozi.
Tunakuja kushtuka damu zinachuruzika miguuni mwangu.
Nilishika tumbo langu kwa uoga
"Una mimba?" Sophia aliniuliza. Kwa uoga niliokuwa nao maumivu yalizidi mala mbili yake. Sophia akiwa anashauriana na wafanya kazi wengine kunipeleka hospitali na wengi walikuwa wanaogopa kutoka kibarua kitaota nyasi.
Kwa mbali tulimuona kijana mmoja mtanashati anakuja eneo tulikuwepo.
Alitufikia pale alinitazama kwa huruma mie nikazima sikujua nini kiliendelea. Nilikuja kushtuka nilijikuta nipo hospitali pembeni yangu alikuwepo Sophia"
"Umeamka kipenzi. Unajisikiaje kwa sasa?"
"Naona nipo sawa. Vipi ulimpa taarifa Sony kuwa nipo hapa?"
"Siwezi kuzungumza nae chochote kwanza naanzaje na yeye ndiyo sababu ya wewe kuwa hapa"
"Niambie vipi kuhusu mimba yangu"
"Jambo la kumshuru MUNGU upo salama kabisa ila tumshukuru pia kijana yule kwa kutoa msaada kama si yeye kulikuwa na uwezekano mimba kuharibika"
"Nilishika tumbo langu nikaachia tabasamu ilhali ndani ya moyo wangu nina maumivu makali sana.
Majira ya jioni nilitoka hospitali niliongozana na Sophia mpaka nyumbani kwangu. Huko tuliwakuta Manka na Sony. Eti Sony wangu anambembeleza Manka ale chakula.
" Nyie watu mnawezaje kuondoka kazini bila ruhusa yangu?"
"Kwamba hata ningefia pale kazini ni sawa?, hivi Sony umepatwa na nini?"
"Punguza Jazba Nice, daktari alisema unatakiwa kuwa mtulivu kimwili hadi kiakili" Sophia alinitulia baada ya kuona nimeanza kupaniki.
Alinipeleka mpaka chumbani kwangu huko tuliweza kuongea mawili matatu.
"Nahisi kuchanganyikiwa mwenzio sielewi jamani" niliongea huku nalia.
"Usilie kipenzi jali kwanza afya yako kila kitu kitakuwa sawa ni jambo la muda tu".
" nisikuchoshe sana Sophia. Asante kwa msaada wako unaweza kwenda nyumbani kupumzika.
"Kama nisingekuwa mke wa mtu ningebaki na wewe leo hii. Ok acha niende ila naomba uwe mtulivu"
Sophia aliondoka, dakika chache tu Sony na Manka waliingia chumbani kwangu.
"Naomba nizungumze na wewe kwa uchache tu kabda sijaondoka kwasababu sihitaji umfanyie mwenzako vulugu. Safari hii utaionja polisi sitakuacha salama"
Sikumjibu zaidi ya kumtazama tu.
"Manka ni mjamxito na mimba ni yangu mimi. Baada ya kukwambia haya sitegemei kama utamfanya chochote kibaya sitokuelewa" Sony aliongea hayo bila ya aibu.
Nyie nilijikuta naangua kicheko huku nalia.............ITAENDELEA.........
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehemu