VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 12 ENDELEA........
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mama aliongea kwa uchungu mpaka alilia. Sony alipotaka kumuomba mama msamaha mama hakumpa nafasi hiyo aliondoka.
"Weww na Sony mna fahamiana?" Nilimuuliza Iron maana nilishangaa mbona Sony amenywea sana mbele ya Iron na namjua fika ana wivu kupita kiasi.
"Yeah tunafahamiana ni mtu wangu wa karibu"
"Kivipi?"
"Ebu malizia kula kwanza mama" Ilibidi niwe mpole. Baada ya kumaliza kula. Iron aliniomba nipumzike yeye alitoka nje ya wodi.
"Sijui naanzia wapi kumuambia". Mama aliongea.
"Haina haja ya kuwaza sana mama. Nice ni mtu mzima nafikili anaelewa kuwa mimba imetoka ila anahitaji uhakika tu".
Iron alikuwa sahihi. Nilifahamu vizuri kuwa mimba imeharibika ila nilitaka uhakika tu.
Kesho yake nilitoka hospitali, Iron alitupeleka mpaka nyumbani kwetu.
"Karibu mwanangu hapa ndo nyumbani" Mama alimlaki vizuri Iron.
Nilihakikishiwa kweli mimba imeharibika. Nilizipokea taarifa hizo japo moyo niliumia sana. Sikuwa na namna.
Siku hiyo tulishinda na Iron hapo nyumbani kwetu. Iron ni mwanaume na sunu jamani kwanza anajua kujali sana. Ana upendo na ana heshima sana.
"Wiki ijayo nitasafiri nitaludi baada ya miezi sita. Nimevutiwa sana na wewe Nice na bila hata kona kona niseme kweli nimetokea kukupenda"
Iron aliongea hayo bila ya kupindisha pindisha.
Nilinywea galfa. Mwanaume huyu nimefahamiana nae muda mchache tu lakini nimemzoea sana. Nafurahia sana na nahisi amani akiwa pembeni yangu.
"Mbona umenuna?"
"Amna nipo sawa tu"
"Upo tayari twende wote?"
"Naweza kusema ndiyo japo sina uhakika"
"Huenda una maswali mengi ya kuniuliza na mambo mengi ya kuniambia. Leo kuwa huru kuxungumza yote. Hii nafasi inaweza kuwa ya mwisho kwako"
"Kwanini unasema ya mwisho ni kwamba hutoludi tena Tanxania?"
"Noooo! Tanzania ni nyumbani. Mimi ni mtanzania Halisi mkataa kwao ni mtumwa mimi si mtumwa ndo maana napenda sana kuja nyumbani. Nimesema hivyo nikiwa na maana kwamba kuna kifo pia"
"Ni sawa". Iron alinipa uhuru wa kuzungumza na kumuuliza maswali. Swali la kwanza nilitaka kujua yeye na Sony wanafahamiana vipi.
Nilistaajabu baada ya kuniambia yeye ndo Ceo wa kampuni na sio Sony.
"Hii inawezekana vipi?"
"Hukuona bussness card yangu niliyokupa siku ile?" Iron aliniuliza.
Ndipo nilikumbuka. Siku ananipa bussness card yake baada ya kuondoka tu Sony aliichukua na kuiharibu"
"Sikufanikiwa kuisoma Bussness card Sony aliiharibu tena kwa Haraka zaidi.
"Huwa sipendi kujitokeza ndani ya kampuni kama Ceo huwa nakuja kishkaji tu ndo maana wafanyakazi hawanifahamu wanafahamu Sony ndiye mmiliki wa kampuni.
Aliniambiwa yeye ni Mtanzania ila amezaliwa nje ya nchi na amekulia huko ila anapenda sana Asili yake ndo maana hata lugha ya kiswahili anaongea kwa ufasaha kabisa.
Mama yake mzazi alishafariki dunia wamebaki na baba tu na wamezaliwa wawili tu yeye na mdogo wake wa kike.
Alimwambia mtu hakuna mtu asiyependa kwenda ulaya bhana. Mie huyu nilikubali kuondoka na Ironi.
Upande wa Sony na Manka
Sony alikuwa amejilaza chumbana ananiwaza mimi na kila tulichokifanya. Manka aliingia chumbani pia alipotaka kulala kifuani kwa Sony Sony alimzuia.
"Umeharibu mimba ya mwenzio makusudi kwanini?"
"Unaongea nini wewe?" Manka alijifanya kupaniki. Aiseee alishtukia karambwa kibao cha shavu ๐๐๐๐๐๐........ITAENDELEA..........
SHUKRANI โ Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehemu